Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa amefanya uamuzi kuwa makao makuu ya Serikali mjini Dodoma sasa yatajengwa katika eneo la Chamwino, baada ya eneo lililokuwa limetengwa awali kwa ujenzi huo katika eneo la Chimwaga, kutolewa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), chuo kikubwa zaidi cha umma nchini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa amefanya uamuzi kuwa makao makuu ya Serikali mjini Dodoma sasa yatajengwa katika eneo la Chamwino, baada ya eneo lililokuwa limetengwa awali kwa ujenzi huo katika eneo la Chimwaga, kutolewa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), chuo kikubwa zaidi cha umma nchini.
Rais Kikwete pia ameutaka uongozi wa chuo hicho cha UDOM kuelekeza nguvu zaidi katika kufundisha wataalam zaidi wa shahada kubwa zaidi za Uzamili na Uzamivu, badala ya kushikilia kufundisha watu kwa ajili ya kupata shahada la kwanza tu.
Rais Kikwete ameelekeza hayo wakati alipotembelea UDOM, ili kujionea maendeleo ya wa chuo hicho, ikiwa ni mara yake ya kwanza kutembelea chuo hicho tokea alipokwenda kukagua ujenzi wa chuo hicho Agosti 2, 2007.
Akizungumza na jumuia ya wanachuo baada kumaliza kutembelea chuo hicho na kukagua ujenzi wake, Rais Kikwete amesema kuwa ameamua kuwa sasa makao makuu ya Serikali yatajengwa katika eneo linalozunguka Ikulu Ndogo ya Chamwino, baada ya kuwa ametoa eneo la awali la ujenzi wa makao makuu hayo kwa ujenzi wa UDOM.
“Kuna sababu mbili za kufanya hivyo. Moja ni kwamba eneo hili sasa tumelitokea kwa ajili ya ujenzi wa chuo hiki maridadi na cha kupendekeza kabisa. Hata kabla ya ujenzi kumalizika, nyie mnajionea kinachovutia,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“ Pili ni kwamba Rais hawezi kufanya kazi ya kusafiri mwendo mrefu kiasi hiki kati ya makazi yake ya Chamwino na ofisi yake kwenye eneo hilo la Chimwaga,” Rais Kikwete amewaambia wanajumuia hao.
Inakisiwa kuwa kuna umbali wa kiasi cha kilomita 35 kutoka Chamwino kwenda mjini Dodoma. Hivyo, safari ya kutoka Chamwino kwenda Chimwaga na kurudi ni kiasi cha kilomita 70.
Rais Kikwete amewaambia wanajumuia hao wa UDOM kuwa ameshangazwa kweli kweli na hatua ya ujenzi wa Chuo hiki. “Nimepata faraja kubwa moyoni mwangu. Naamini kuwa baada ya ujenzi, eneo hili litakuwa moja ya maeneo ya kuvutia zaidi nchini, na wala sisemi maeneo ya vyuo viku, bali majengo yote.”
Rais Kikwete pia amewaelezea wanajumuia hiyo jinsi wazo la kuanzisha chuo hicho lilivyozaliwa, kwa sababu uamuzi wa kuanzisha chuo hicho ulikuwa uamuzi binafsi wa Rais Kikwete, na wala hilo halikuwa sehemu ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM, mwaka 2005.
Amesema kuwa aliamua kuanzia chuo hicho kwenye Jengo la Chimwaga lililokuwa mali ya Chama cha Mapinduzi kwa sababu jengo lilikuwa halitumiki ipasavyo. “Unajua tulikuwa tunalitumia jengo hili mara moja ama mara mbili kwa miaka mitano. Kama mkikumbuka hili jengo ndilo lilikuwa limetumike kwa ajili ya Bunge. Ni jengo kubwa sana hili na lilifaa kabisa kuanzia chuo hiki.”
Rais Kikwete ametumia zaidi ya saa mbili kutembelea ujenzi wa chuo hicho ambacho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi kiasi cha 40,000 kwa wakati mmoja.
Akipata maelekezo kuhusu maendeleo ya ujenzi na masomo katika Chuo hicho ambacho tayari kina wanafunzi wapatao 7,000 kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Kikura, Rais Kikwete ameutaka uongozi wa chuo hicho kubadilisha fikra na kuelekeza nguvu kubwa zaidi katika kukifanya chuo hicho Kituo cha Ubunifu kwa kutoa wasomi wengi zaidi wa shahaha za Uzamili na Uzamivu.
“Kwa kuchukua wanafunzi wachache wa shahada hizo za juu, na wakati mwingine kwa kuongozwa tu na hisia zetu, tunaweza kabisa kuwa tunadumaza maendeleo ya taifa,” amesema Rais Kikwete, akitolewa mfano wa uzoefu wake katika Chuo cha Kenyatta cha Nairobi, ambacho mwishoni mwa mwaka uliopita, kilimtunukia shahada ya heshima za Uzamivu.


JK anapiga stori na madenti au anaongea na waandishi wa habari? Manake naona hao wanaomsikiliza wako bize sana kumfotoa.
ReplyDeleteTeknolojia ya simu imekuja na mambo mengi sana...hapo naona vijana wa UDOM badala ya kumsikiliza JK wanakazana kumpiga picha na kamera za kwenye simu...Resolution ya hizo picha ni very pooor yaani ingefaa hao vijana wamtazame na kumsikiliza live badala ya kumchukua picha!! Kulikoni hawa viongozi wetu wanatembelea vyuo vikuu vyote except UDSM?
ReplyDeleteChuo kikuu cha university of dodoma ndio nini????????????yale yale barabara ya morogoro road.Andikeni Lugha sanifu jamani Blog ni kama online newspaper sasa kama lugha ndio hiyo kweli tutafika tena habari ikiwa inatolewa na mhariri?
ReplyDeletehivi hakuna jumba lamikutano akaa na hao wanafunzi na kuongea hapo naona si muafaka.
ReplyDeletebig up JK,hiki chuo ni heshima ulojiwekea katika maisha yako,kama mkapa alivyoamua kujenga uwanja wa mpira,wewe umeamua kuwekeza kwenye elimu,hakuna kama elimu,hiki chuo ni kikubwa na cha kisasa,ni ukombozi mkubwa kwa watanzania,kutoka na asilimia kubwa kuishia form 4.tunakuomba kipindi chako cha pili utujengee chuo kingine kimoja cha maana kama hiki au zaidi ya hicho bkwenye mikoa iliyokuwa haina chuo,kama vile tanga lindi sumbawanga au mtwara.ni hayo tu mheshimia President
ReplyDeleteMmmh,mmenyoosha simu zenu mnampiga picha manake leo kawa mzuri kesho wa kwanza kumponda.Nafkiri hakukuwa na umuhimu wa kumpiga picha mna watu kibao katika familia wa kuwapiga picha na kuweka kwenye simu zenu.
ReplyDeleteWadau,
ReplyDeletemimi ni mbumbumbu wa utaalamu wa snepu, lakini nikiri kwamba picha hii imeleta mvuto wa ajabu ndani ya hisia zangu.
Imenivutia hasa, zaidi huo mjengo huko nyuma.
Pia nimevutiwa na namna Rais wetu alivyo mwepesi kujichanganya na kupenda kuonekana mtu wa kawaida tu kama wengine.
Ni jambo la kutia moyo linaloendana na wakati.
Anony 5.52PM Karibu Kijijini! Tumeshachoka kuwakaribisha wageni humu.Well lugha ya humu we soma alafu iache kama ilivyo ni vijimambo vya humu tu wadau wote wanatambua hilo hivyo kama unataka kusahihisha watu lugha fungua blog yako.Kwanza kama si mgeni wewe unamjua Chibiriti?Kama humjui basi pia huwezi jua vionjo vya blog hii na lugha ya wadau hivyo uliza na usikurupuke.
ReplyDeletecameraphones kibao, je hapakuwa na viatu size 10? teh teh....teh!
ReplyDeleteSitta’s NO to issues under probe
ReplyDelete2009-02-05 11:00:19
By Lusekelo Philemon, Dodoma
National Assembly Speaker Samwel Sitta yesterday barred Members of Parliament from discussing issues related to the Radar purchase and National Identity Cards project scandals.
Sitta announced the decision after Ole MP, Bakar Shamis Faki posed a supplementary question to the Finance and Economic Affairs deputy minister Jeremiah Sumari, on whether the implementation of the two projects followed the Public Procurement Act procedures.
The Speaker stood up and told the house that the two issues were under investigation, hence it wouldn`t be fair for the National Assembly to discuss them.
``These two issues are under investigation. It is not proper to discuss them here. Let`s leave the responsible organs to work on them,`` he said.
Responding to the basic question, Sumari said the government was looking into the possibilities of improving the procurement system.
He also said the government would soon make amendments on the legal issues related to the procurement system so as to give the Public Procurement Regulatory Authority (PPRA) teeth.
``This will give PPRA a mandate to punish those who go against the public procurement Act,`` he said.
Minister Sumari also underscored the need to have e-procurement in government departments, saying the move would improve services offered by PPRA.
He said presently many government departments were not connected to the e-procurement system, which links them with PPRA as well as business people in the Private Sector.
In his basic question MP Faki had wanted to know the
government position on improving procurement system in the country.
Meanwhile, Sitta said it is strictly prohibited for chairpersons of the Parliamentary committees to reveal issues discussed in the committee chambers to the press.
He issued the directive after the question and answer session yesterday, saying there was a growing tendency for leaders and members of those committees to reveal details of the discussed issues to media practitioners.
Sitta said the move preempts the National Assembly as the issues were supposed to be first tabled in Parliament before being made public.
``There are some MPs who have a tendency of briefing media people on what transpired in their chambers. This is contrary to parliamentary standing orders. I ask them to stop doing so,`` he said.
His statement comes at a time when Home Affairs Minister Lawrence Masha is meeting the Parliamentary Committee on Defense and Foreign Affairs, over the multi-billion shilling national ID cards project.
Media was not allowed into the committee meeting hearing the controversy surrounding the USD 152m national identity cards project.
Last week, Prime Minister Mizengo Pinda confirmed that he was aware of the controversy.
He however called for patience on the part of MPs while the project`s tender process continues.
According to Pinda, one major weakness in the tendering process was the unexplained loss of documents from folio number 47 at the Ministry of Home Affairs, which contains important information on the project.
This, he said, had resulted in much of the information being leaked.
Reliable sources have intimated that differences have recently come to the fore between Masha and State House Chief Secretary Philemon Luhanjo over the way the tender process is being handled.
Initially, the home affairs ministerial tender board had sought to float a restricted tender, but the government ordered the tender process to be made public to avoid loopholes for corruption and other wrongdoings.
It has now come to light that Masha last year complained formally to premier Pinda that Chief Secretary Luhanjo instructed the permanent secretary in the home affairs ministry to report directly to the Cabinet on the implementation of the tender process, without informing him (Masha) as minister.
It is understood that the minister`s argument was that he would be the one forced to shoulder political responsibility should anything go wrong within the ministry.
The chief secretary, who operates from State House, is secretary to the Cabinet and responsible for ensuring that all important government decisions are implemented.
According to our sources, Masha also told Pinda that he had received complaints from one of the bidders for the tender, Sagem Securite, and summoned the home affairs PS to Dodoma last November for discussions on the matter.
A total of 54 companies initially submitted bids for the tender to supply the ID cards.A special government evaluation committee then picked 21 of the bidders for the pre-qualification stage.
Out of these, 16 bidders were found to be `substantially responsive,` while five bidders were given `conditional pre-qualification.`
The tender board later came up with a shortlist of eight companies, excluding Sagem Securite, out of those recommended by the evaluation committee.
SOURCE: Guardian
Hayo ndiyo maendeleo,tukifanikiwa kuwa na vyuo vikuu vya uhakika mikoa 15 italipa sana.
ReplyDeleteKingine inabidi tuanze kuwatumia wasomi kwenye ubunifu.
Magari ya Nyumbu yameishia wapi? kwani hatuwezi kuwa na kiwanda kinachotengeneza nyumbu za mfano wa BMW au Scania na zikatumiwa badala ya kuagizia mikoko kutoka nchi za nje kama Japani ambayo ni hatari kwa mazingira yetu .
Tuwaandae wasomi na tuwaandalie mazingira ya kufanyia kazi pindi wanapohitimu.
Asante