JK na mama Salma Kikwete wakiwafariji ndugu na jamaa za marehemu Jeremiah Ullaya,mwenyekiti mstaafu wa CCM wilaya ya Iringa mjini wakati wa ibada ya kumuombea marehemku iliyofanyika katika kanisa la hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar leo mchana.Akizungumza wakati wa ibada hiyo Rais Kikwete alisema alimfahamu marehemu na kwamba aliwahi kushirikiana naye kwa karibu katika kutekeleza majukumu ya Chama Cha Mapinduzi
JK na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa mwenyekiti mstaafu wa CCM wa wilaya ya Iringa mjini Marehemu Jeremiah Ullaya aliyefariki jijinji Dar hivi karibuni.Ibada ya kumuaga marehemu ilifanyika katika kanisa la Hospitali ya Taifa Muhimbili leo mchana.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Poleni sana wafiwa. Mungu awawezeshe na kuwapa nguvu. Kufiwa na mume au mzazi ni jambo zito mno.

    ReplyDelete
  2. RIP Mzee wetu, nilifanya kazi na marehemu akiwa chairman wa Board ya Iringa girls.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu popote mlipo na wakazi wote wa Iringa Mjini.Rambirambi za pekee zimfikie Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa kwa msiba huu mkubwa.Ndugu yetu Jeremiah Ullaya atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya mji wa Iringa na mkoa mzima kwa ujumla na kwa Taifa zima.Tuko nanyi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi makubwa.Sisi tulimpenda,lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi!Kazi yake haina makosa.Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi,amina!

    ReplyDelete
  4. Poleni wafiwa. Je wanaundungu na Ben Ullaya?

    ReplyDelete
  5. Namjibu Anonymous wa Feb 20,5:37pm hawana undugu na Ben Ulaya, unamtafuta?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...