
Poll yetu ya kwanza kabisa ya mtoto wa kiume atahiriwe akiwa na umri gani imefungwa rasmi tarehe 31 january. napenda kuwashkuru wale wote walioshiriki kupiga kura pale wanapoona ndio chaguo lao.
Hadi inafungwa poll hii ilipigiwa kura na watu 127.Matokeo ya Mtoto wa Kiume Atahiriwe Akiwa na Umri Gani? ndio haya.
Kabla ya Arobaini: 41 (32%)
40 hadi Miezi Sita: 33 (25%)
Chini ya Miaka 2: 25 (19%)
Zaidi ya Miaka 2: 13 (10%)
Atajua Mwenyewa Akishakua: 15 (11%)
*****
Kutahiri kwa wanaume ni kuondoa kwa ngozi ya mbele ya uume (govi). Utafiti wa mambo ya kale unaonyesha kuwa ilikua inafanywa tangu enzi za Misri ya Kale. Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinakadiria kuwa asilimia 30 ya wanaume wote duniani wametahiriwa, ambapo kati yao, asilimia 68 ni waislam.
Kuna utata mkubwa hasa kwenye nchi zilizoendelea kuhusu kutahiriwa. Wanaounga mkono wanasema kuwa maumivu ya kutahiriwa ni kidogo ukilinganisha na na faida za kiafya zinazotokana na kitendo hicho.
Wakati wanaopinga suala hilo wanadai kuwa lina madhara kiafya hasa katika kujamiiana, na wanasema linakiuka haki za binaadam linapofanywa kwa mtoto ambaye hashiriki kwenye maamuzi hayo.
Utafiti na WHO wanakubaliana kwamba kutahiri mtoto wa kiume kunapunguza kwa kiwango kikubwa uwezekano wa wanaume waliotahiriwa kuambukizwa virusi vya ukimwi.
*****
Kwa kweli nimekosa utafiti unaoonyesha lini ni vizuri kutahiri mtoto ingawa watu wengi pamoja na madaktari wanasema ni vyema kumtahiri mtoto akiwa mdogo ili kupunguza maumivu as mtoto mdogo anakuwa bado hajui maumivu, au kitaalam wanasema senses zake zinakuwa mbali, bado hazijawa fully formed, ingawa huko nchi zilizoendelea wanasema kwamba maumivu hayana tofauti kati ya mtoto na mkubwa.
Nikiwa mama wa mtoto wa kiume, na mtu ambaye kwa kiasi kikubwa nategemea sana ushauri wa kitaalamu kufanya maamuzi yaliyosahihi, wataalam hawajanisaidia kabisa katika suala hili, hivyo basi ntatumia tamaduni zetu kufanya ninaloona ni sahihi.
*****
Narudia tena kuwashukuru wote mlioshiriki.
Poll mpya inakuja soon
Poll mpya inakuja soon
bro michuzi hii mama na mwana imenikumbusha kopa kopa.
ReplyDeletesafi sana jiang,,,
ReplyDeleteofkoz mtahiri mtoto wa kiume akiwa bado mdogo tu akimaliza arobaini before ajafikisha mwaka..ni usafi kwanza,kupunguza maambukizi,na shape nzuri
maumivu yapo palepale.
umri mzuri wa kutahiri mtoto wakiume ni baada ya kukauka kitovu tu ambapo atakuwa na wiki mbili,huo ndio umri mzuri, hata kidonda hakizidi hata wiki kinakuwa kimepona akitoka arobaini amepona,hata wewe mzazi unakuwa umeshasahau na unaenjoy na mtoto wako.
ReplyDeletemandishi amesema sawa kuwa mila hii ilianzia misri, na ilikuwa utamaduni wa waabudu jua, lakini hajasema hawa % hawajatahiriwa wanaathirirka vipi, hizi mada nyingine ni uchokozi wa kidini. kutahiri mtoto hakuna faida yoyote zaidi ya kumnyanyasa, nani kakwambia kuwa halitaki govi. hospitali tunawatahiri wanapopata maambukizi tu, huu mwingine ni ushabiki,pia hii ya kuzuia ukimwi ni sawa na magonjwa ya zinaa.
ReplyDeletesababu nyingine za utototni hazina msingi wowote ziadi ya udini usio wa lazima.
Kwanza nafurahi sana kuwa kuna mada hii ya kutahiriwa. Kwa maoni yangu mimi binafsi watoto watahiriwe wakiwa na umri kati ya miaka 13 mpaka 15 na hii iwe ni sehemu ya mitaala (curriculum) ya elimu yetu. Hii hoja ya maumivu kwangu mimi binafsi hii si ya msingi. Maumivu ni sehemu ya maisha yetu, kuzaa kuna maumivu, kufa pia ni maumivu. Kung'oa jino maumivu na kuvunja ungo pia ni maumivu. Maumivu ya kutahiriwa ni kitu kidogo sana ukifananisha na maumivu mengine ya kimaisha.
ReplyDeletebinafsi nimetahiriwa lkn sioni kama kuna umuhimu wa kumsababishia mtoto maumivu kwa kumtahiri.KUTAHIRI NI MILA ZA KALE HAKUSAIDII LOLOTE SISHAURI KABISA MTOTO ATAHIRIWE MUNGU HAJATUUMBA TUTAHIRIANE NDIO MAANA TUNAZALIWA NA NGOZI ZETU KUTAHIRI IS JUST A MAN PLAN"
ReplyDeletesi vyem kiutahii watoto wadogo ni bora kuanzia miaka 15 na kuendelea.
ReplyDeleteMie naona bora iwe kama Wamasai unatahiriwa ukiwa na akili na wanakuangalia kama utalia au la kama kipimo cha uwezo wako wa kuhimili maumivu na ukakamavu. Pia ukitahiriwa ukiwa mkubwa unakua na heshima na mwili wako kwani unaweza pia hata kuchelewa kuanza ngono kwa kuogopa kuonesha govi kwa mabinti hiyo itakusaidia kuepukana na STIs kiulaini kabisa... Ni mtazamo wangu na uzoefu waku kwani binafsi nilitahiriwa nikiwa form four baada ya mabinti kuanza kunicheka ingawa ulikua ni unyanyasaji na matkeo ya mapokeo mabaya...na sasa nipo US watu kibao wana magovi yao na hakuna anayewashangaa kwani ni kitu ambacho mtu anaamua mwenyewe.
ReplyDeleteASANTE KAKA MISUPU KWA NAFASI.
Naomba kuwasilisha
Unconfirmed- yes even for chinese is a such a new customs for them, said(un-cited) in the year 2007 all who are above 15years are uncircumsed in bilief of circumcised boy/man have abnormal dick(penis) size!
ReplyDelete"kubalehe kuna maumivu na maumivu mengine maishani"hahahaaa teh teh
ReplyDeletesasa tueleweje
Biblia inasema watu watahiriwe,mnakumbuka ibrahimu na watu wake wooote ilibidi watahiriwe watolewe magovi yao?
jamani mkatahiri kwanza zinapendeza sana...
....ni mila tuu na desturi za watu lakini sijui kama kuna faida yeyote ya kutahili,nimetahiriwa lakini ingekuwa choice yangu wala nisingetahili,nipo US na watu wengi sana hawajatahiriwa na maisha yanaendelea kama kawaida na hakuna mtu atakushangaa hujatahiriwa,haya mambo kila mtu aamue kivyake na Daktari wake kwa jinsi anavyoona,hakuna sababu ya kuweka umri wa mtu kutahili au ulazima wa kutahili
ReplyDeleteni uzuri mtoto kutahiriwa akiwa mdogo ktk kipindi cha arubaini lkn mkubwa hupata maumivu makali kwani huwa anajitonesha mara kwa mara.
ReplyDeleteMtoto ni vizuri atahiriwe akiwa mchanga. Mie ni muuguzi na hosipitalini kwetu tunatahiri watoto wenye siku mbili. Hao watoto wanabahatika kupewa dawa ya maumivu. Dawa inapakwa karibu na uume na nyngine ni ya kunywa. Hii inasaidia sana maumivu.
ReplyDelete