Home
Unlabelled
kwa mtaji huu, tunahitaji kukaza buti zaidi...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
kaka misupu siku hizi marafiki zangu wananiita minimo kwa kupinga uwezo wa maximo,lakini habari ndio hiyo!tunapigishwa makitaimu na mbrazil mjanja ila mwisho wa siku tutakuwa hooi bin taaban........Kiwango kile kile kila siku...hii hata Jamhuri kiwelu angeweza kufanya. TUWAIGE WAKENYA,WATANI ZETU WANAJALI VYAO SIO KAMA SISI NDIO SABABU WAMEJIJENGEA UWEZO HATA RAIS WA USA WAO!!
ReplyDeleteKwakweli sioni matokeo ya ajabu au ya tofauti na nchi nyingine zenye makocha wazalendo. Hii timu ipewe mzalendo na apewe fungu na benefits anazopewa MINIMO tuone kama hata chart halitakaa top 60. Makocha waliopita hawakupewa mishiko na support ya aina hii anayopewa MINIMO=MAXIMO. Mkataba ukiisha tujaribu kuwa na kocha mzalendo anayeaminika, kama Mziray hivi tuone matokeo.
ReplyDeleteMontenegro, Georgia na El Salvador haziwezi kuwa na mpira mdogo zaidi ya Tanzania na Cape verde.
ReplyDeleteHivyo taarifa hii haielezi hali halisi ya kiwango cha ubora wa kutandaza kabumbu.
Jana Spain ili ilaza England mbili mtungi. kiwango cha England ktk mchezo huo kilifanana na Taifa Stars. Lakini kwa ajili ya kelele nyingi kushabikia kandanda la England ndio maana inawekwa juu ktk msimamo wa FIFA.
Pia timu ya Ecuador XI iliifunga England (vijana1) hii juzi ya kina Ashley Young, Huddlestone, Cambell n.k 3-2. Hiyo England (vijana!) imesheheni wachezaji wazoefu wa first eleven ktk ManUTD, Aston Villa, Tottenham n.k
Maximo ni mkali, tuombe mechi na England, na hakika tutawatoa jasho la mwaka. Hata hivyo najua England itakacha kuikabili Taifa Stars ili isiadhiriwe na nchi 'ndogo' na kupelekea England kuteremshwa ktk msimamo wa FIFA.
Hivyo nchi nyingi ziko 'selective' ktk michezo ya kirafiki ili kulinda nafasi zao FIFA, lakini msimamo wa FIFA hauonyeshi hali halisi. Si tunakumbuka Senegal ya kina El-Hadj Diouf ilivyo ziadhiri nchi kubwa world cup.
Hivyo Taifa Stars msibabaike na 'rankings' za FIFA, wala hizi propaganda za wasiompenda Maximo na Tanzania. Taifa Stars nendeni kifua mbele Ivory Coast mkanyoe watu.
Mdau
Jijini London.
Ni ubwege kumpa mziray ukocha wa timu ya taifa mtu ambae vilabu tu hakuna kinamchotaka na pia mziray sio kocha wa ufundi kama maximo (technician)mziray yeye ni wa viungo tu (physical tranner)hana mbinu za kichezo zaidi ya stamina tu.msiwe mnaropokwa kama mliokunywa maji ya chooni vile.WACHEZAJI MNAOMLETEA MAXIMO STARS MLIWAANDAA TANGIA WAKIWA WADOGO???AU MNABWABWAJA TU???MAXIMO ANA KIBARUA KIGUMU MNO KUINOA STARS BINAFSI NINGESHAURI AONGEZEWE MSHAHARA NA MARUPURUPU.WACHEZAJI WA TIMU ZINAZOFANYA VIZURI NI MATUNDA YA MIPANGO YA MUDA MREFU YA NCHI ZAO KATIKA KUWAENDELEZA VIJANA WADOGO TANGIA MASHULENI SASA LEO MASTAR WETU WA BONGO NI WACHEZAJI WALIOKUSANYWA KWENYE VIJIWE VYA BANGI TU MTAANI NA NDIO WACHEZAJI TULIONAO HAO TZ.TUTAMLAUMU BURE MAXIMO TATIZO NI LA NCHI HAINA MIPANGO KWA FUTURE GENERATION.LEO HII HATA ALETWE FERGUSON BONGO LAZIMA ACHAGUE WACHEZAJI WALIOOKOTEZWA VIJIWENI TU UNATEGEMEA NN HAPO???TUELEKEZE NGUVU ZETU KWA VIZAZI VIJAVYO NDIO SOLUTION PEKEE ILIOBAKIA.MI NAONGEA HAPA NIKIWA KAMA MCHEZAJI NILIEPATA KUCHEZEA TAIFA STARS NA MOJA YA TIMU AMBAYO HUYO MZIRAY AMEPATA KUIFUNDISHA, NA VILE VILE NI MIONGONI MWA HAO WACHEZAJI WA KUOKOTEZA MITAANI TU VIJIWENI.
ReplyDeleteHapo mchezaji wa kuokotezwa kijiweni umenena. Zamani ulikuwa ukiangalia CV za wachezaji unakuta walishindana katika Umishumta, Umisseta (Salvatory Edward, Abubakar Kombo nk), Shimivuta (Lawrence Mwalusako, Benjamin Magadula), Michezo ya majeshi taifa (kipa John Bosco) ambako walikuwa wanapata miongozo ya kuwasaidia. Leo Maximo anawafundisha wachezaji wa taifa kupiga freekick na krosi kwa sababu hawana misingi mizuri. Wachezaji wanakosa fundamentals ndio maana analazimika kuweka kambi ya timu ya muda mrefu. Kwa mchezaji aliye kamili katika mambo ya msingi anaweza kuingia kambini kufanya mazoezi ya tactics na strategies kwa ajili ya mechi ijayo akiwa na timu ya taifa. Hata klabu zetu nyingi unakuta zinacheza formation ile ile kila siku, ukimwambia mchezaji abadilike kutoka kuwa namba 10 wa 4-4-2 kuwa namba 10 wa 4-2-3-1 unamtafuta lawama.
ReplyDeleteTuimarishe klabu zetu na maandalizi katika ngazi za chini za chipukizi tutengeneze wachezaji walio tayari. Baada ya hapo tutakuwa tumejitengenezea uhalali wa kulaani hatua zilizopigwa na kocha wa taifa kama hazituridhishi.
Hii jeuri tuliyo nayo ya kupiga kelele hizi inasahau jambo moja: Zimbabwe ilikuwa inatupa homa enzi za kina Stanley Ndunduma. Sasa hivi tunaenda uwanjani tukitegemea ushindi. Hiyo ni hatua kwenda mbele. Tusisahau vilevile kwamba kina Grobbelar na Mwaruwari wametokea Zimbabwe. Sisi tuna mchezaji wa kitanzania aliyewahi kutwaa kombe lolote la hadhi ya Champion's League duniani? Mzimbabwe Grobbelar alifanya hivyo akiwa na Liverpool.
Date::2/12/2009
ReplyDeleteZimbabwe wadai Eto'o ndiye aliyewapa siri za Taifa Stars
Na Ibrahim Bakari
KATIBU Mkuu wa Chama cha Soka Zimbabwe, ZIFA, Henrietta Rushwaya amesema alipata salaam za ukali wa timu ya Tanzania, Taifa Stars alipokutana na mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Etoío mjini Nairobi.
Akizungumza katika mahojiano maalum jana, Rushwaya ambaye ni mwanamama alisema: ''Tulikuwa Kenya kwa mechi za kufuzu Kombe la Dunia na Cameroon walikuwa njiani wakitoka Tanzania na walifika hoteli tuliyofikia.''
''Nilikuwa na mazungumzo na Samuel Eto'o, nikamuuliza vipi huko Tanzania, akasema Tanzania ni timu ngumu na wametoka suluhu.
ìAliniambia hakutarajia kama Tanzania ingewawekea ngumu kwa sababu walikuwa wanajua wanashinda kwa sababu walisheheni mastaa wa dunia.î
Timu hizo zilitoka 0-0 mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2010, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja Mkuu wa Tanzania.
Rushwaya alisema Tanzania ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika Fainali za Afrika kutokana na kuonyesha kiwango cha hali ya juu kisoka tofauti na alivyokuwa akiisikia.
''Niliwaambia hata wachezaji wangu kuwa Tanzania si ile ya zamani na ndiyo maana tulicheza kwa tahadhari,'' alisema.
Alisema: ''Haya ni mabadiliko ya soka Afrika, timu nyingi za Afrika zimeanza kuinuka, zamani ilikuwa Nigeria, Cameroon, Ghana lakini mabadiliko yanaonekana.''
Aliwasifu wachezaji wawili wa Stars kuwa wanatumia akili na wanaweza kucheza soka popote dunia. ''Nimefurahishwa na yule mwenye jezi namba nane na nahodha, kweli wamecheza vizuri na popote wanaweza kusimama.''
Katika mchezo huo wa juzi wa Tanzania na Zimbabwe ulioisha kwa suluhu, mshambuaji wa Stars, Mrisho Ngassa ndiye alityevaa jezi namba nane wakati nahodha alikuwa Shadrack Nsajigwa.
Katibu huyo alisema kuwa ana imani Tanzania itafanya vizuri kwa kuwa ina wachezaji wake karibu wote kwa muda mrefu isipokuwa timu yake imeondokewa na wachezaji sita muhimu.
''Nina matumaini hafifu, wale sita walioifikisha timu fainali wameondoka, mmoja amekwenda Poland, mwingine Finland na mwingine Ubelgiji wakati wachezaji wetu watatu wamejiunga na klabu za Denmark...uwezekano ni mdogo kwa wao kujiunga na sisi,'' alisema.
source: www.mwananchi.co.tz
I dont believe in FIFA rankings. Can some one agree with china being placed one place behind Tz, i.e. 104, this is impossible. China wanapiga mpira bwana na wana proffesionals kibao km vile Park wa MAN U, etc. So these FIFA rankings are nosense.
ReplyDelete