
Habari bwana Michu?
Nimetuma picha hiyo kuonyesha moja ya vivuko cha pundamilia vilivyopo katika barabara zetu. Hii ni ile iliyopo mbele ya jengo la Millenium towers, Kijitonyama, ambayo imewekwa yapata miezi saba hivi iliyopita ila ilianza kufutika ikiwa na miezi mitatu hivi.
Najiuliza waliopaka walifanya makusudi ili warudie kupewa tenda hiyo mara kwa mara? Au rangi haiendani na lami? Kinachotisha ni kwamba madereva wasiotumia barabara hii hawawezi kufahamu kama hapa kuna zebra cross kwa kuwa imefutikafutika.
Na ni hatari kwa wavukaji kama unavyoona katika mojawapo ya picha hizo mtu akivuka na gari mbele yake inaendelea kwenda. Je, mpaka agongwe mtu wao hapa ndo watawajibika? Ama mpaka afanye ziara mheshimiwa fulani kukagua barabara ndo zitapakwa upya? Au tusubiri mapaka ifutike kabisa ndo mpakaji apate sababu ya kuomba tenda nyingine?
Nisaidieni majibu jamani?
GM (Trafic wa polisi jamii)


MAKOSA YANAYOFANYWA TANZANIA NI KWAMBA WANAPAKA RANGI YA KAWAIDA YA NYUMBA, SI HIVYO KINACHOTAKIWA KUTUMIKA NI AINA YA LAMI NYEUPE NZITO KAMA MATOPE INABANDIKWA IKIWA NA MOTO NA MASHINE MAALUMU - NAJUWA WATU WATAKUJA NA KUNISHAMBULA LAMI NI NYUSI! HAIWEZI KUWA NYEUPE! NENO LAMI HALINA MAANA YA RANGI, LAMI INWEZA KUWA NA RANGI YOYOTE ILE. KATIKA BARABATA NCHI ZA WATU HUTUMIA LAMI YA NJANO NA NYEUPE KUWEKA ALAMA TOFAUTI KATIKA BARABARA ZAO
ReplyDeleteALIEPAKA ZEBRA HANA MAKOSA NDUGU YANGU GM. TATIZO BONGO HAKUNA VIWANGO. BAHATI MBAYA WATENDAJI WETU WABISHI....HUO MCHANGA PEMBEZONI (SHOULDERS) UNAONDOA RANGI ZOTE.... INABIDI (MAINJINIA) WAGUSHI TEKNOLOGIA YA THEMOPLASTIKI AU PRIFOMD TEPU, NDIO ITAKAA ZAIDI KIDOGO.
ReplyDeletePIA BONGO HATUNA TABIA YA MATENGENEZO YA MARA KWA MARA.
SASA GM UNASHANGAA ZEBRA, MBONA MISTARI INAYOTENGANISHA NJIA ZA MAGARI IMEFUTIKA KARIBU BARAX2 ZOOTE TANZANIA NAKUFANYA UENDESHAJI MVUA IKINYESHA AU USIKU KUWA HATARI ZAIDI.
USHAURI WANGU ZEBRA ZOTE ZIJENGWE KWA VITOFALI BADALA YA KUPAKA RANGI BILA KUKUMBUKA KURUDISHIA BAADA YA MIEZI 3
zebra zote ziwekwe kwenye matuta bumps ili madereva wakifika kwenye zebra wapunguze mwendo watake wasitake mana wataonea huruma magari yao kuingia kwenye bump,sidhani kama wataona huruma gari zao kuingia damu ya binadamu lakini bumps wanaziheshimia sana,
ReplyDeletekwahiyo mji mzima uwekwe bumps na zebra paint juu yake kwisha kazi.
ZeBRA za Vitofali zitasaidia. Hizi za rangi hata kama inaonekana vipi, madereva hawajali
ReplyDeletekwa mtazamo wangu inaonyesha rangi ya "nyumba" inayopakwa hapo ni bei rahisi zaidi ya rangi ya "lami nyeupe" sasa kutokana na hilo ina maana hapo kuna ziada inabaki baada ya kununua na kupaka hiyo rangi yanyumba. Na kama ujuaavyo watendaji wetu hii "ziada" ndo panga lenyewe la kujikimu na ugumu wa maisha.
ReplyDeleteKwa kifupi watendaji wetu na viongozi kwa ujumla hawana discipline na kazi zao kama tuonavyo nchi zilizoendelea. mimi nadhani ili tuendelee tuna haja ya ya viongozi/watendaji kuiga mazuri ya nchi zilizofanikiwa kwa faida ya wananchi wote.
mdauz JPN
wanapaka kwa brashi lile la kawaida kabisa!!
ReplyDeleteyani mdau asante kwa hii newz,,,
SASA APO K'NYAMA KUVUKA NI HATARI KAMA SI KIFO SASA IVI HAPAFAI KABISA APO,YANI NILIRUDI JUZI TU APA ROAD IMEPANUKA NOW NJIA MBILI(4)KUVUKA HAPAFAI,yani unaomba uruma ya driver kwa kujirusha katikati ya road ili upishwe,TENA NI ENEO LENYE WAKAZI WEEENGI SANA NA LAZIMA UVUKE KUFATA KITUO AU APO MILLENIUM TOWER,,,
MAGARI YANAPEPERUKA KAMA FORMULA ONE RACE APO!!!
SIJUI ITAKUAJE MANA BEFORE TU NI ROAD YENYE AJALI NYIINGI SANA
Aah! yaani huko kufutika sio issue. Mimi nilikuwa huko wakati ikiwa bado inaonekana na nilikwoswa koswa mara kadhaa kugongwa na magari yaendayo kama ndege ya chini. Nashukuru mtoto wa mwenyeji wangu aliyenishika mkono. Hakuna tofauti kuwa na kivuko au bila, tena kivuko ni hatari zaidi maana utaamini kwamba madereva wanajua ni kivuko na watasimama. Kuvuka barabara huko nyumbani, sharti mguu niponye.
ReplyDelete