Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Mustafa Mkulo (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IFM) anayeshughulikia Afrika Samuel Itan (katikati) na Mshauri wa Mkurugenzi huyo Ahmed Ndyeshobola (kushoto) kuhusu maandalizi ya Mkutano wa IMF na Afrika utakaohudhuriwa na Mawaziri wa Fedha na Magavana kutoka Nchi zote za Afrika utakaofanyika Nchini tarehe 10 – 11 mwezi wa tatu mwaka huu . Washiriki kutoka Zambia, Misri, Cameroon, Senegal, IMF na wenyeji Tanzania walishiriki mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Brother Michu kazi nzuri sana.Ila nimecheka sana kwa sababu kuna sehemu kweye picha hii badala ya IMF umesema IFM,nimefurahi sana kwa sababu you sent me all the way back to 1998.
    We were in daladala,jamaa mmoja(mzalendo)akaanza kuongea kwa sauti mle kwenye akilaani masharti magumu ya IMF mikopo kwa nchi masikini.Akasema kwa sauti,"tena hao IMF wana chuo chao hapa kinaitwa IFM,bora waje wakitoe,haiwezekani wawe na chuo chao hapa halafu wanatufanyia mambo kama haya".Watu tulivunjika mbavu mle kwenye daladala.

    MDAU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...