Habari yako kaka Michuzi
Nilikuwa napenda kuchangia mada katika blogu yetu tukufu
katika pita pita zangu nilikutana na makala hii kwenye website ya nifahamishe.com iliyotolewa na MWAJABE KIZIGINA nimeipenda kwakweli kwakuwa inanigusa mimi pia ni Graduate na bado hadi sasa bado nahangaika kutafuta kazi nikipewa majibu hayo hayo Naomba uirushe kwenye blogu yetu wadau watoe maoni yao nini kifanyike

MDAU JANET
-----------------------------------------------------------------------------

Wiki hii nakuja na mada tofauti kidogo inayohusu new graduates. Kutokana na matatizo yaliyokumba soko la dunia kila sehemu utakayoenda kuomba kazi utakuta wanataka mtu mwenye atleast uzoefu wa miaka miwili.

Tukijaribu kuziangalia nchi zilizopo bara la Afrika, matatizo ya uchumi yapo tangu enzi na enzi. Of course si kila nchi ya Afrika ina matatizo ya kiuchumi ila nyingi hali yake ya kiuchumi si nzuri. Sasa hali imezidi kuwa mbaya kwa sababu hata nchi zinazotoa misaada Afrika na zenyewe masoko yao ya nje yameathirika kwa kiasi kikubwa.
Kwa sababu hii makampuni mengi badala ya kuajiri wafanyakazi yanapunguza wafanyakazi kutoka kazini. Yapo baadhi ya makampuni machache ambayo still hali yao haijabadilika sana almost ipo the same.
Mbaya ni kwamba kama ni new graduate na ukaenda kuomba kazi wanasema uwe na uzoefu usiopungua miaka 2 au labda uwe na refa atakaye kuunganishia kazi. Sasa kama kila sehemu inahitaji uzoefu, je, itakuwaje kwa vijana wetu ambao ndio wamemaliza na wanataka kuanza kazi??

Wakati nilipokuwa naumiza kichwa changu kuhusu nini cha kufanya nikapata mdau mmoja ambaye na yeye ameshapoteza muda wake mwingi kutafuta kazi kila sehemu na kuniambia kuwa cha moto anakiona. Hivyo akaniambia kuwa angalau vingeazishwa vyuo au makampuni maalumu kwa ajili ya kuwapa new graduates experience.
Ni vigumu kupata organization au company katikati ya tatizo hili la uchumi likachukua new graduates na kuanza kumtrain na kumlipa for 6 months for free. Ndio maana kupunguza unnecessary expenses wanachukua mtu mwenye experience ili aingie straight kazini.

Nini kifanyike? Hatuwezi kuwaacha vijana bila kazi, na hatuna marefa wa kuwasaidia vijana wetu waingie kazini. Na economic crisis hatujui itaisha lini. Kama super power zinaathirika basi sisi waafrika ndo tunaumia zaidi. Nini kifanyike?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. usitumie neno "tukufu" wewe hii web ina utukufu gani

    ReplyDelete
  2. Mimi mchango wangu ni mdogo sana lakini ninaamini utakuwa na impact kubwa.

    Dhana 'TEGEMEZI' ifutwe na isitumike katika kumchakato mzima wa kufikiria nini cha kufanya.

    Ukianza na kufikiria kuwa vijana watapata wapi kazi, basi umeshaweka utegemezi ndani yake kwa maana kuwa wategemee kufanya kazi mahali ambapo papo.

    Jambo la kufanya ni kuwa, for the time being wajaribu kukaa chini kila mmoja wao afikirie kama yeye binafsi anaweza kufanya nini katika mazingira aliyokuwa nayo sasa. Si lazima afanye kazi au shughuli ambayo ni relevant na shule yake, no as long as alikwenda shule na amepata elimu basi afikirie afanye nini. Mambo ya kufanya ni mengi sana let them waumize vichwa lili nchi iendelee.

    ReplyDelete
  3. Nachangia kama ifuatavyo: kwa maisha yetu ya Africa mtu anapomaliza shule lazima ahitaji kazi.Kwani bila kazi hata pata msingi wa kuweza kufanya hicho ambacho si tegemezi.Huyu mtu bila pesa ya mtaji au vifaa hataweza kufanya lolote.Ukiangalia mifumo ya mikopo ktk nchi yetu ina mfeva mtu mwenye pesa.Bank au Makampuni binafsi yakukopesha hayawezi kumpa mkopo kwani mtu huyu hana security yeyote.Na watu binafsi waliopiga hatua hawana utamaduni wa KUTOA PUSH Kwa vijana hata kidogo.Nakumba nilipo graduate sikutaka kufanya kazi.Niliamuakum aproach tajiri mmoja kwa mkopo nikiwa na business plan.Aliniambia kama sina fixed asset yeyote ile nimkabidhi VYETI vyangu vyote yaani msingi mpaka university.Hapo tulishindwana,kwani sikua tayari kwa hilo.Lakini baada ya mwezi niliona wazo langu la Biashara akilifanyia kazi yeye mwenyewe.Sikuwa na jinsi wala umiliki wa kisheria.Kwa hiyo ndugu yangu huyu graduate lazima atahitaji kazi,Lasivyo awe ametoka kwenye Familia zenye hewa ya kutosha.Ahsanteni.

    ReplyDelete
  4. bongo bila kupigiwa pande hupati kazi ya maana
    watoto wa wakubwa wamepigiwa pande wamejazana BOT wakati wengi wao ni bomu hawana elimu yeyote

    ReplyDelete
  5. Kusoma ni Investment kama investments zingine.Unapoanza kusoma inabidi ujue kitega uchumi hicho kitalipa au hakilipi.Huwezi kusoma tu kama pimbi pori eti unatarajia usiyemjua aje akuajiri.Soma ukijua utaenda wapi ukimaliza.

    Mfano kuna kijana mmoja Iringa mtoto wa mkulima maskini wa kijijini wa kigiriki kule Nzihi mkoani Iringa.Yeye alisomea chuo kikuu cha Dar es salaam Geology.Alipomaliza tu chuo kikuu alikataa kuajiriwa akaenda shambani kijijini kwa baba yake na kuanza kuitumia elimu yake ya Geology kuchimba maji na kuyafunga kwenye chupa na kuyauza.Maji hayo ni yale ya chapa Africa .Ambayo yameenea maeneo kibao Tanzania.

    Tatizo naliona hasa liko kwenye Carrier selection watanzania wengi husoma tu kama vichaa hawajui ku-panga mbeleni wanataka waishie wapi.Mtu anasoma tu kwa kuwa bodi ya mikopo inakopesha au kuna mfadhili wa kusomesha basi anasoma tu kama chizi ukimuuliza ukimaliza kusoma wapi utakuwa anakutazama usoni kama mjusi alifiwa na mkwewe.

    Watu waelekezwe kuwa wawe makini kuchagua nini wanataka kusoma ili wawe nani na wapi baadaye vinginevyo tutaendelea kuwa na mibwege inayolia kazi hakuna baada ya kumaliza vidigrii vyao uchwara visivyo na soko mjini wala kijijini.

    Na vyuo navyo vikome kutoa vidgrii visivyokuwa na masoko iko siku wasiona kazi watavishtaki kula hela zao za ada kwa kuwasomesha kozi uchwara zisizo na ajira.

    ReplyDelete
  6. Anony wa juu hapo unakuwa kama hujasoma bongo!
    Unajua fika kwamba Tanzania chuo kikuu huwapangia watu kitu cha kusoma wakati mwingine unaomba kusoma computer engineering wao wanakutupa ukasomee uhandisi wa maji au madini
    sasa hapo utamlaamu mwanafunzi hakuchagua topic nzuri ya kusoma?

    ReplyDelete
  7. ukweli lazima usemwe, staili ya masomo tegemezi kwa style za kizungu lazima ifike mwisho.watu wamekalili kupata maksi nyingi darasani klakini wambie wabuni kufanya nini baada ya shule hakuna kitu, Afrika bado chance za maendeleo ni nyingi sana, lakini uzembe wa kufikiri na utumwa wa mawazo wa kupenda rahisi ndo unawatesa graduates, dunia kwa sasa inawabana ,lazima tubadiri mitaala yetu.SOMA MAKALA ZA GENERALI ULIMWENGU, KTK RAIA MWEMA KWA WIKI NNE UTAFAHAMU ANAONGELEA NINI.

    ReplyDelete
  8. SOMA AINA YA ELIMU ULIYOPATA TOKA GAZETI LA RAIA MWEMA, GENERALI ULIMWENGU , UTPATA PICHA YA ULICHONACHO KICHWANI. MABADIRIKO NI LAZIMA ,AZAWAIZI TUTAENDELEA KUWA WATUMWA WA AKILI.

    ReplyDelete
  9. Bwana Reformed SINAMAKOSA,

    Kwani wewe uliona hatari gani kuweka vyeti vyako kama bondi? Si unajiamini na biz plan yako bwana?

    Na pili vyeti kitu gani bwana? Mtu hawezi kukuibia elimu yako wala vyeti. Wewe ungebaki na copy na barua/mkataba unaoonesha kwa nini huna originos.

    Au ungebaki na certified copies of orijinos.

    Kifupi wewe hukuwa tayari kwa ujasiriamali .. ulikuwa unawaza "sasa hapa ikitokea nafasi ya kazi itakuwaje?"

    Yaani hata ingekuwa mimi kitendo cha kushindwa kuniamini na kitu kidogo kama vyeti wakati mimi niko tayari kukuamini na pesa zangu nilizotoleamachozi, jasho na damu... kwa kweli nisingekufinance.

    That guy was good.

    Nenda benki uone kama watachukua vyeti kama collateral.

    Banks are stupid my friend. Nenda hata na signed contract ya tenda hawakupi mkopo ng'o! mpaka uwape hati za nyumba.

    Wake up my friend, and start thinking much wider.

    ====

    PS wewe mdau wa February 06, 2009 2:55 PM umenikera sana hata neno "career" unashindwa ku-spell!

    ReplyDelete
  10. Bwana Reformed SINAMAKOSA,

    Kwani wewe uliona hatari gani kuweka vyeti vyako kama bondi? Si unajiamini na biz plan yako bwana?

    Na pili vyeti kitu gani bwana? Mtu hawezi kukuibia elimu yako wala vyeti. Wewe ungebaki na copy na barua/mkataba unaoonesha kwa nini huna originos.

    Au ungebaki na certified copies of orijinos.

    Kifupi wewe hukuwa tayari kwa ujasiriamali .. ulikuwa unawaza "sasa hapa ikitokea nafasi ya kazi itakuwaje?"

    Yaani hata ingekuwa mimi kitendo cha kushindwa kuniamini na kitu kidogo kama vyeti wakati mimi niko tayari kukuamini na pesa zangu nilizotoleamachozi, jasho na damu... kwa kweli nisingekufinance.

    That guy was good.

    Nenda benki uone kama watachukua vyeti kama collateral.

    Banks are stupid my friend. Nenda hata na signed contract ya tenda hawakupi mkopo ng'o! mpaka uwape hati za nyumba.

    Wake up my friend, and start thinking much wider.

    ====

    PS wewe mdau wa February 06, 2009 2:55 PM umenikera sana hata neno "career" unashindwa ku-spell!

    ReplyDelete
  11. nilijua tu tutafika hapa siku moja. asilimia 90 ya vijana wanao kuja kusoma hapa ukerewe wanakuja soma biashara au uchumi ninachoulizaga siku zote ni kwamba ? hakuna kazi nyingine tofauti na hizi za uchumi? muziki? bwana mifugo? kilimo? cammon guyz amkeni mie mtoto wangu anachukuwa digrii ya vichaa na target ni mirembe hana upinzani

    ReplyDelete
  12. Hili tatizo lipo sehemu nyingi. Kuna mdau mmoja alikumbwa na matatizo kama hayo akiwa na cheti chake. Alisomea fani ya usanifu majengo aka architecture katika chuo kikuu kimoja mashuhuri Marekani, nadhani ilikuwa Rutgers au Syracuse. Bodi yao ya mikopo ilimkopesha mahela mengi maana ilikuwa haina mambo ya tunahisi baba yako tajiri hatukupi hela na pia chuo alichosoma kilikuwa cha pesa nyingi na fani aliyochagua ilikuwa inaonekana ndio keki ya moto. Baada ya kuhaha uwanja mzima kama Athuman Iddi Chuji ndani ya Taifa Stars alijikuta madeni yanaongezeka, mishahara anayopata ni ya kubahatisha pale anapopata kazi na riba za mikopo zinazidi kumkandamiza. Alifanya ubunifu wake wa mwisho kwa kuamua kunadi cheti chake ndani ya ebay.com. Aliweka bayana kwamba hata ukinunua cheti hicho hutatambulika kama msanifu majengo wala nini lakini ameamua kukiuza kwa kuwa kinamtia hasira na hataki kukiona tena. Haikuweza kufahamika mara moja mnada huu uliishia wapi lakini chuo kikuu chake kilijaribu kumsihi abadili uamuzi wake kwa kuchelea kuadhiriwa bila shaka.

    ReplyDelete
  13. KWA WALE WANAOSOMA ILI WAAJIRIWE, CHA KUFANYA BAADA YA KUMALIZA MASOMO ILIKUEPUKA KUDAIWA YEARS OF EXPERIENCE NI KUOMBA KATIKA MASHIRIKA KUFANYA KAZI KWA KUJITOLEA KWA BURE BILA MALIPO KATIKA FANI YAKO AT LEAST KWA MWAKA I MEAN INTERNSHIP.

    PIA UTAMADUNI WA TANZANIA WA BAADHI YA WAAJIRI WA SEHEMU AMBAZO SI TECHNICAL SANA KUTAKA WATU WALIO NA SIFA EXACTLY NDO WAWAAJIRI NI MTINDO WA KIZAMANI WA KIKOLONI HATA WAKOLONI WENYEWE WAMEACHA, NAKUBALIANI KUNA KAZI NI LAZIMA MTU AWE AMEISOMEA KWA MFANO DAKITARI WA BINADAMU I LAZIMA ASOMEE FANI HIYO. LAKINI KUNA KAZI KWA MFANO KUWA MFANYAKAZI WA BENKI SI LAZIMA USOMEE MAMBO YA BENKI NIMEONA HUKU ULAYA WATU KIBAO WAMESOMA DEGREE ZA HISTORY NA WAKAENDA BENKI NA KUTOKEA KUWA BANKER WAZURI SANA, HATA UHASIBU HUKU SI LAZIMA USOMEE UHASIBU, KUNA WATU WANAINGIA NA DEGREE ZA CHEMISTRY KATIKA FANI YA UHASIBU WANAKULIA HUKO MPAKA WANAKUWA WAHASIBU WAZURI, WATANGAZAJI WA TV NA RADIO SI LAZIMA USOMEE KUNA WATU WENGI WAMESOMA HISTORY DEGREE NA NI BROADCASTER WAZURI SANA WA AINA HIYO WAKO WENGI SANA KATIKA BBC NA KWINGINEKO, WANAAMINI MTU YOYOTE AMBAYE AMEWEZA KUFAULU KIWANGO CHA DEGREE ANAWEZA KUFANYA KAZI YOYOTE ILE AMBAYO SI TECHNICAL SANA. PIA WATANZANIA WAJARIBU KUJIAJIRI WENYE KUFANYA KITU CHOCHOTE KILE SI LAZIMA ULICHOSOMA. NA KWENDA UNIVERSITY SOMETIMES IS NOT NECESSARY UNAWEZA KUFANIKIWA MAISHA KWA AKILI ZA KAWAIDA TU, NIMEONA MTOTO WA SECONDARY TU ANA KAMPUNI YA KUUZA SAMANI ZA MAOFISI KAMPUNI KUBWA TU ALIPATA HATA TENDER ZA KUUZA VIFAA WHITE HOUSE NA NI WA CHINI YA MIAKA 20 NI UBUNIFU TU. NIMEONA MTOTO WA MIAKA 16 KAWA TAJIRI KWA KUFUNGUWA WEBSITE TU NA KUPATA PESA KIBAO KUPITIA WATU WANAOTUMIA WE YAKE, NIMEONA MTOTO DIRECTOR WA KAMPUNI YAKE YA KUUZA MADAWA.

    ReplyDelete
  14. MIMI NINAUNGANA NA HUYO BWANA ALIETOA COMMENT YA KWANZA KUHUSU HUYU BWANA ALIYESEMA BLOG TUKUFU HII NI BLOGY YA JAMII SAWA LAKINI SIO TUKUFU MTUKUFU NI MUNGU TU ANGALIA SANA HILO NENO UNAVYO LITUMIA HATA RAIS MKAPA ALIISHA KATAA ASIITWE MTUKUFU KWASABABU ANAJUA YEYE SIO MTUKUFU ILA BWANA MUNGU SASA ITAKUA BLOGY, PLSEEEE

    ReplyDelete
  15. Ni suala la kusikitisha sana. mwaka huu naona watanzania zaidi ya 10,000 watamaliza vyuo vikuu, lakini sijaona ajira 10,000. Huko ughabuni ndio mambo ni mazito ajabu. Na mambo yao yakiwa mazito, ya kwetu ni kiama kabisa. Si unaona GTV ya uingereza, pale naona wafanyakazi wa GTV bongo wote watakuwa wanaenda kufikiria mahali pengine. Sasa makampuni mangapi bongo ni ya wageni, karibu bank zote, usije ukataja bank ya watu wa Zanzibar au ya watu wa Mwanga au ya watu wa Dar es Salaam. Hizo ni wajukuu wa benki, na wala sio bank. Nitajie Backlays, NBC, CRDB, CITI, STANDARDCHATTERED nk
    Ninachoona hapa ni mfumo mbaya wa elimu ambao unamfanya mtu akitoka chuo kikuu aombe kazi. Kwanza, napenda kukujulisha kuwa chuo kikuu ni degree chache sana wanafunzi wanafundishwa kufanya kazi. So, hata kama mimi ningekuwa na kampuni, I would not take risk, sitaajiri mtu asiye na uzoefu unless I foresee potential in him. Na ya masaa mawili au hata siku nzima inaweza isinihakikishie kuwa jamaa kazi anaweza. Niandikishane na mkataba na mtu mwenye degree ya uhasibu wakati hajawahi kuwa mhasibu, and these universities of ours. Mtu mwenyewe huenda alidesa ndio akamaliza kozi yake, au alitoa vitu kwa maprofessor wakamfaulisha, alafu mimi nimpe kazi hivi hivi? No way!
    So, tunaweza tukafanya mawili, tukabadilisha mfumo wa elimu kabisa uwe practicak oriented ili kusiwe na matatizo kuwa mtu hana ajira. Kwa mfano, wanafunzi wawe na mwaka mzima wa practical training wakiwa chuoni. Wawe attached kwenye makampuni kwa mwaka mzima. By so doing, those companies would have cheap labour for a year, which is a big deal to them. This is a long term na inahitaji muda kwa sababu hata hayo makampuni yako wapi? Kila kitu bongo kinatoka nje ya nchi. Nadhani hata toilet papers zinatoka nje ya nchi. Kwa maana hiyo, kila kitu tunachozalisha tunapeleka nje indirect. Yaani, ukifua, ukienda haja kubwa, ukipiga mswaki na ukifanya consumption ya kila kitu unawapa watu wa nje utajiri.
    Kingine, hicho kinawezekana, ni suala la kuwashauri wanafunzi wakiwa tangia secondary kuwa wajue hakuna ajira kwao. Waelekezwe kufanya maamuzi mazuri ya career wanazotaka kulingana na talents walizo nazo. Tanzania na Africa kwa ujumla ni mahali ambapo mtu anachagua kozi ya kusoma chuo kikuu wakati hajui kuwa yeye anapenda nini. Mwingine kwa vile rafiki yake alimwambia, ukisoma international relation utatembea nchi nyingi, anachagua international relations. Tell me the future of international relations graduates, si mpaka baba yako awe waziri wa mambo ya nje. Even an engineer can be a diplomat! Tatizo bongo hata hakuna wataalamu wa kuwashauri vijana kuhusu career, na sio career tu, hata hayo mambo mengine yanayohusu ushauri hayana wataalamu. Watu wanafanya ushauri nasaha bila utaalamu wa kutosha.
    Mwanafunzi akianza tu mwaka wa mwisho wa masomo, aangalie mahali pakwenda. Kazi zipo nyingi tu, ni vile watu wanapenda ubosi. Kweli nikienda shamba siwi tajiri mara moja??? Sasa ukulima tumewaachia watu wasio na elimu na ndio maana wanavuna kidogo,ufugaji tumewaachia wamasai, wana ng’ombe wengi, lakini maziwa kidogo, nyama mbovu. Kuku tumewaachia watu wanaofanya bila elimu ya kuku. Wataalamu wanaomaliza kilimo pale SUA wanataka waajiriwe Dar es Salaam. Kwa mtaji huo, tutendelea kusema tu, he Botswana imeendelea, sisi ng’o. the time has come to set aside childish things!

    ReplyDelete
  16. Mimi naona kuna kitu kimoja ambacho vyuo na makampuni yanatakiwa yalazimishwe kufanya au yachangie kwa hiari yao wenyewe.Yawe yanatoa internship kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho kufanya kazi kwa kadri ya mwaka mzima na iwe ni mojawapo ya kigezo cha kumaliza shule na pia mara nyingi kama hapo mahali unapofanyia intership wakipenda utendaji wako baada ya wao kukufundisha basi watakuajiri au la itakuwa ni mojawapo ya reference na experience.Au kingine ni mwanafunzi kujitolea kwenye kampuni kufanya kazi bure kwa masaa 5 au 6 kwa kipindi ambacho huna kitu cha kufanya bila ya malipo ili upate uzoefu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...