Matokeo ya mtihani kidato cha nne mwaka 2008 yanaonyesha kuwa kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa asilimia 10.13. Wanafunzi wengi wamefanya vizuri kwenye Kiswahili (aslimia 81.59) na wengi wamefeli basic mathematics (waliofaulu somo hili ni asilimia 24.33 tu).
Shule zinazoongoza kama kawaida ni za binafsi huku senminari zikionekana kufanya vema zaidi. shule kumi bora zenye watahiniwa 30 au zaidi
1. St Francis Girls (Mbeya) 2. Marian Girls (Pwani)
3. St Joseph-Kilocha Seminary (Iringa)
4. Uru Seminary (Kilimanjaro)
5. Dungunyi Seminary (Singida)
6. Anwarite Girls (Kilimanjaro)
7. St Mary Goreti (Kilimanjaro)
8. Feza Boys (dar es Salaam)
9. Don Bosco Seminary (Iringa)
Shule 10 bora zenye watahiniwa chini ya 35
1. Scolastica (Kilimanjaro)
2. Feza Girls (Dar)
3. Brookebond (Iringa)
4. Bethelsabas Girls (Iringa)
5. Maua Seminary (Kilimanjaro)
6. Rubya Seminary (Kagera)
7. St Marys Junior Seminary (Pwani)
8. Katoke Seminary (Kagera)
9. Kilomeni (Kilimanjaro)
10. St Carolus (Singida)
Shule 10 za mwisho zenye watahiniwa 35 au zaidi
1. Selembala (Morogoro)
2. Kilindi (Pemba)
3. Ngwachani (Pemba)
4. Michiga (Mtwara)
5. Ummussalama (Pwani)
6. Chunyu (Dodoma)
7 Busi (Dodoma)
8. Uondwe (Pemba)
9. Nala (Dodoma)
10. Maawal (Tanga)
Shule 10 za mwisho zenye watahinwia chini ya 35
1. Juhudi Academy (Zanzibar)
2. Mima (Dodoma)
3. Selenge (Singida)
4. Kijini (Zanzibar)
5. Kwamkoro (tanga)
6. kwala (Pwani)
7. Mtende (Zanzibar)
8. Ng'hoboko (Shinyanga)
9. Mbuzini (Pemba)
10. Mwadui Technical (Shinyanga)
Matokeo zaidi nenda
au
www. matokeo.necta.go.tz


Nikiangalia hapo naona shule za PEMBA na ZANZIBAR zinajitokeza kwa wingi MWISHO MWISHO... sijui hasa kama wazazi/walezi hawatilii mkazo katika hii ELIMU DUNIA na kuweka uzito katika ILIMU AHERA ambayo haina nafasi katika CV wakati wa kuomba kazi n.k
ReplyDeleteTUSAIDIANE MAWAZO wadau, kwamba nini kifanyike hapa visiwani.
Huko pemba na dodoma kunahitaji gear up. Shule zao nyingi za mwisho
ReplyDeleteNa kingine nimeona shule zenye majina ya ajabu ajabu zinachemsha sana.
Kweli majina ya ajabu yanaweza kuwa ndo sababu ya kudororesha matokeo duh ebu yangalieni haya majina eti SELEMBALA KILINDI NGWACHANI MICHIGA UMMUSSALAMA CHUNYU BUSI
ReplyDeleteUONDWE NALA MAAWAL MWADUI JUHUDI MIMA SELENGE KIJINI KWAMKORO
KWALA MTENDE NG’HOBOKO MBUZINI
Zanzibar mnatuangusha!! Karume, ni aje na yule mhindi wako waziri wa elimu? Du, kumbe wapemba vipi jameni yaheee!
ReplyDeleteWazanzibari bonyeeeeee kizenj kabisa, acheni kupiga domo na siasa za chuki ndugu zangu wekeni msisitizo ktk kitabu
ReplyDeleteMichuzi kuna t-shirts naona zimevaliwa sana sijui wana print wapi zina maandishi mazuri ya art nzuri sana zimeandikwa MCHAGA MJANJA naomba madau anaejua anijulishe
ReplyDeleteOh my God.. Bro michu leo ni siku mbaya sana kwangu Mdau wa Dodoma,¨
ReplyDeletekatika hiyo list yoote yaani nimetinga nyavuni mara 4 (Bottom 10). Kazi kubwa inahitajika kufanyika sana huko kwetu, hongerani wadau wa Iringa na Kilimanjaro mambo yenu sio mabaya.
Mdau wa Dodoma
wapemba darasani kwa kuchemka hamjambo nakumbuka nilisoma primary mbuyuni sasa pale kuna wapemba wanaishi wengi maeneo ya namanga wazazi wao wakiwa wafanya biashara ukisikia tu majina ya wapemba yanaitwa ujue sifuri hizo.du wapemba mnatia aibu yakhee
ReplyDeleteNa mimi najua wapemba kwa shule wako juu. Hasa wale wa enzi ya mwl. Kwanza wanasoma masomo magumu kuliko unavyoweza ku imagine. kwa mfano makamu wa rais wote wa2, Dr. Omari na Dr Shain. wamepiga nondo si mchezo. Acha udaktari wa heshima wa JK, Dr Shain and PhD kwenye wa ma-BioChemistry na manini sijui!.
ReplyDeleteNadhani kuna haja ya kuangalia tena hoja za Sidelinig-Pemba.
Mdau Kiwoso UK
wachaga wasijidanganye kuwa matokeo yao yale, shule zao ni madaraja ya watoto wa dar na arusha, baada ya zao la kahawa kuanguka , wamebaki na shule za kata, hata mie wanangu wanne wapo katika hizo bora ,lakini sio mchaga,so hiyo dhana ya mchaga mjanja, sawa na wanyakyusa mbeya au mazaramo marian ,bagamoyo wajisifie.pole ndo tanzania ya leo.
ReplyDeleteWe unayejiita Hussein acha ujinga, inahusu nini suala la kuzingatia dini na kufeli masomo ya shule. Mpuuzi nini huoni hizo shule ziloongoza z ni za kikanisa, sijui st, Mary Goreti? kwani huko hawafundishwi dini pia? Toa sababu inayoeleweka sio kulete gumzo lisilo na maana. Kama hujui hiyo feza ni ya Waturuki na ni Waislamu pia? sasa mbona husemi? toa sababu zenye uzito kwenye mzani sio lelemama!
ReplyDeleteWabongo acheni ujinga, jina la shule linahusiana nini na kufeli? Au hamkusoma nini? Muhimu ni mitala inayotumiwa na uwezo wa walimu na wanafunzi wenyewe. Kama huna la kuchangia si usome makala tu na ikupite? Watu wengine bwana? pumba tu!
ReplyDeleteHakuna uhusiano wowote kati ya IQ au uwezo wa kuelewa mambo kielimu na kabila au sehemu. Suhula na mazingira ni miongoni mwa mambo yanayochangia mtu akawa hana akili na mwingine akawa mwenye akili. Uchunguzi unaonyesha kuwa, karibu binaadamu wote wanazaliwa na uwezo sawa wa kiakili au kutofautia kidogo lakini mazingira walokulia na elimu wanayopewa huchangia katika kukua kwa akili na vipaji vyao. Zamani tulikuwa tumezoea nadharia kuwa mzungu ana akili na mwafrika ni goigoi, lakini muda ulivyopita na tukatoka katika ujima tumeona wote ni sawa na hata wazungu wanaweza kuwa wajinga. Sioni sababu ya Wapemba kuambiwa hawana akili kwa kuwa shule zao zimebaki nyuma katika matokeo, wala wachaga hawastahiki kusifiwa kwa kuwa shule za Kilimanjaro zimeongoza katika matokeo. Shule hizo nyingi ni za watu binafsi, na wanaosoma humo wengi wao si wanafunzi kutoka mkoa wa Kilimajaro. Na shule za pemba nyingi ni za serikali. Nina hakika kuna shule za binafsi huko pemba zilizofaulisha vizuri, na kwa namna hiyo hiyo kuna shule nyigi moshi za serikali zilizofelisha. Watanzania inabidi tuache kujadili mambo bila kuzingatia ukweli wenyewe kwani sasa ni zama za kusema jambo bila kupayuka tu kwa kutokutumia data zenye nguvu.
ReplyDeleteNawakilisha
Mdau Uajemi.
Hongera sana kanisa katoliki, kwani shule zenu za seminari na zinginezo zinaendelea kutesa kielimu Bongo.
ReplyDeleteMasista wa Holy Cross hongereni kwa sana, Shule yenu ya Mtakatifu Anwarite imefanya vizuri ile mbaya.
ReplyDeletehongereni sana nyie mliofaulu na shule zilizofanya vizuri. nikiangalia ninaona shule zilizofanya vizuri ni zile za makanisa na za mikoa ya kilimanjaro. kwakweli haya makanisa hupata misaada mingi kutoka makanisa ya nje kuwawezesha kuendesha shule zao kwa hali ya juu kuliko shule za serikali. walimu wa shule zao huwa na elimu bora na wanafunzi wao huwa na tabia nzuri. inasikitisha kuona jinsi shule nyingi zilivyo fanya vibaya. kwakweli hapa tanzania hatuwezi kuongea juu ya shule fulani kuwa na matokeo mazuri wakati walio faulu nchini ni chini ya asilimia 30. ukiangalia list ya matokeo ya mtihani wa kidato cha 4 unaona failed failed nyingi sana na passed ni chache sana. hii inatisha sana. serikali ni lazima iwe makini sana juu ya elimu. shule zetu zimejaa walimu ma mbumbu. wenyewe hao walimu wana kiwango cha chini sana cha elimu ukifananisha na walimu wa nchi jirani. ni vigumu kuibadilisha hii syestem kwa muda mfupi kwasababu tulikuwa na ujamaa kwa miaka mingi lakini we can start somewhere.
ReplyDeleteJamani KIFUNGILO ni aje tena??....au imesahaulika??
ReplyDelete