Brother Michuzi assalam alaykum,
baada ya salaam naomba uniweke ombi langu hili katika blog yako. Najua kwa niyaandikayo watatokea waosha vinywa na kusema watakayo hilo halinizuia kuleta ombi langu. kwani nategemea watatokea angalau watu wawili watatu watakaolewa lengo langu na kunipa muongoza na msaada ninaouhitaji.
Kwa Jina naitwa Simai Mohammed Ahmed (almaarufu Dr Balozi) nimekuja uk kipindi, naam nimekuja na nimepiga boksi. Hata hivyo pia nilijisomesha hadi kuweza kumaliza degree ya kwanza katika fani ya Computing mwishoni mwishoni mwa mwaka wa masomo wa mwaka jana.
Ni lengo langu kurudi nyumbani na kutafuta kazi huko nyumbani. Wengi wanijuao wamenipa pongezi na pia wamekuwa wakisema kuwa watu wenye taaluma kama yangu tanzania wanahitajika sana na kuna soko kubwa. hata hivyo kila nikiwaomba wanipatie details za kampuni kama vile za NGO na nyenginezo ambazo zinatangaza nafasi za IT wanashindwa kunipatia, pia nimeomba kama wanajua websites zinazotangaza nafasi za kazi pia wanashindwa, ndio hii leo nimeamua kuleta ombi langu hapa.
Kwa ufupi natafuta kazi katika fani IT ningelipenda zaidi kuwa katika line ya software development hata hivyo area yeyote ile sitoiwacha. ningelipendelea zaidi kufanya katika mashirika au makampuni yasiokuwa ya serikali.
Naomba yeyote yule mwenye kujua kampuni zinazotafuta wafanya kazi wa IT anijulishe. au kama kuna website ambayo ninaweza kuangalia nafasi za kazi naomba kupatiwa.
Pia ushauri wowote ule kwenu unakaribishwa, ila mmoja tu siutaki nao ni "BAKI HUKO ULIKO" kwa mimi nyumbani ni nyumbani, nimekuja kujiendeleza, nimefanikiwa kiasi naamini nitafanikiwa kujiendeleza kimaisha nikiwa tanzania. Nakusudia kuondoka huku mara tu visa yangu inapomalizika.
email yangu ni
shukrani nyote na hasa hasa brother michuzi kwa kukubali kuweka ombi langu katika blog yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Katembelee www.jamiiforums.com, jivinjari huko waweza pata kidogo kitu

    ReplyDelete
  2. jaribu
    naombakaziblogspot.com
    brightermonday.com
    kweli the last thing you need ni mtu kukwambia kaa huko huko mie pia nataka rudi the only thing nafanya mipango yangu taratibu ikifika time na tiket mkononi nawapigia watu simu hei am on my way to TZ kesho mwenye kutaka kuniaga anitafute:nakutakia maandalizi mema

    ReplyDelete
  3. Dr nakupongeza kwa uamuzi wako wa kurudi nyumbani. Kupata kazi TZ ni lazima uwe na links. Website sidhani kama zinasaidia sana,ila kuna makampuni kama raha.com, simbatech, vesl ltd, cats-net.com etc. Kama inawezekana tafuta professional qualification kama Oracle DBA, Oracle Developer etc. Huo ndio ushauri wangu. Good Luck!!!!!

    ReplyDelete
  4. Mimi naona ungeweka wazi ni programming language zipi ambazo una utaalamu nazo kwenye hiyo area yako ya software development.Na amini kama ni mtaalamu wa Java au microsoft languages(C#,visual basic n.k) pamoja server side language kama cgi,php kwenye web development na database ,kuna uwezekano mkubwa wa kupata kazi bongo,ila kama unacheza na C/C++ sikushauri urudi bongo,sababu hizi ni programming language zinazotumika zaidi kwenye high technology industries,language ambazo zipo close na assembly language(machine language) hivyo hazina nafasi kwenye nchi masikini kama bongo.

    ReplyDelete
  5. ILI MRADI HUTAKI USHAURI WA "BAKI HUKO" NAFIKIRI USHAURI WA "NJOO NYUMBANI HATA KAMA HAKUNA NAFASI" UTAKUWA THE BEST. NAHISI WEWE ULIKUWA HUTAKI USHAURI BALI UNASANII.

    Ilikuwa uombe ushauri halafu baadaye uchekeche mwenyewe, usidhani hata wasiorudi bongo ni wajinga.

    BILA KUFUATA USHAURI WAKO, NINGEKUSHAURI UFANYE KAZI SEHEMU YEYOTE UIPATAPO, KUMBUKA GLOBALIZATION.

    ReplyDelete
  6. We siye jamaa aliyeandika kiingereza mbofu mbofu waki fulani? Umejirekebisha na kuja kwa kiswahili sasa hivi.

    Kwa taarifa hiyo huihitaji ushauri maana huna options nyingi, una option moja tuu, kurudi nyumbani.

    ReplyDelete
  7. KWA USHAURI WANGU BONYEA KTK KUDEVELOP POINT OF SALE SOFTWARE BONGO BADO BADO KAMA UNAWEZA UNAJICHEBA KIVAKO UNAFUNGUA KAMPUNI YAKO KWANI NIMEFANYA UCHUNGUZI MAKAMPUNI MENGI HASA MAHOTELI SOFTWARE ZAO NI KUTOKA SAUZ SIDHANI KAMA KUNA LOCAL DEALER TZ JARIBU KUIFANYIA UCHUNGUZI NA WEWE KIVAKO VAKO MIE SIKU SI NYINGI NITARUDI BONGO PIA KIMTINDO HUO NAVUTA NGUVU TU NIMEPOTEZA MUDA SANA NJE EKA 14 SI MCHEZO INABIDI NIRUDISHE MAJESHI KWA MAANDALIZI YALIOKOMAA

    ReplyDelete
  8. Kama unaweza basi usirudi Bongo kwa sasa bali fanya masters. Naona hivi sasa bongo ina watu wengi ambao wana degree moja ya IT kwa ni kuna vyuo kibao tu vya IT. Sasa naona utakuja kusota kwa kipindi tu. Soma zaidi kabla ya kurudi.

    ReplyDelete
  9. Sijui una skills gani katika software development lakini ushauri wangu ni huu, bongo kutafuta kazi kama alivyosema wa huko juu sharti uwe bongo na uwe na connection, bongo haiko that developed kupost kazi kwenye websites hivi sasa. Lakini kinachonishangaza ni hiki kwanini haswa unataka kurudi bongo na hiyo taaluma uliyonayo. Sisemi kwamba ubaki huko "forever" lakini kwa mfano marekani even though uchumi ni mmbaya watu ambao wanafanya web design wanalipwa at least $40000 na software development depending on language unayojua from out of college to senior or lead developer ni kuanzia $40000 mpaka $120000 depending na experience na knowledge na ni katika fani ambayo siku zinavyo zidi kwenda the whole world inatafuta watu wenye hizo knowledge hivyo mimi binafsi ningekushauri badala ya kwenda kufanya kazi bongo nenda bongo kwa likizo lakini tumia muda wako kuwa sponsored work permit katika first world countries as a software engineer kama vile usa, canada, huko uliko uk, germany and many other european countries zinatafuta sana software engineers fanya kazi kwa muda utakaoweza huku uksave hela zako kisha amua na hizo hela kama wataka kurudi bongo kufungua business au wataka kuendelea kukaa huko. Hivyo ndivyo wahindi na wasia wanafanya wamejazana wengi wanafanya kazi kwenye IT kwa kuwa sponsored (kwa vile nina ujuzi na marekani) H1Bs and greencards as software engineers halafu wanafanya contract work najua wapo pia canada na nchi nyinginezo ila wahindi wamefunika maana wao wamekuwa wengi kiasi cha sasa hivi wanafanya computer work from india kwa kuwa outsourced na kwa hela yao wakikconvert mfano wanavyolipwa katika dollar kwa hela yao sasa hivi wanaishi maisha mazuri sana huko india ndiyo sababu nchi yao uchumi unaanza kuja juu. Ushauri wa mwisho katika IT lazima ujiendeleze kila kukicha, language mpya ikitoka "be on top of it learn it" hivyo utakuwa unaexperience katika platform na language nyingi na chance ya kupata kazi inaongezeka software development sio nyanja ya kubaki na ulichosomea shule maana teknologia inakuwa kila siku na language zinaongezeka na opportunity pia mfano tu mdogo kama ulisoma C/C++/C# shuleni au sasa hivi microsoft imeshatoka na c# 3.0 hivyo kuna makampuni bado yako nyuma yenye kazi watatafuta wenye kujua c++ au c# 2.0 na kuna wengine wanataka mambo ya silverlight yaliyotoka mwaka jana so sharti ujue c#3.0 kwa ushauri naona nimetoa mwingi wa kutosha Good Luck

    ReplyDelete


  10. Mkuu wewe umesoma IT; tafuta kazi ki-IT..!!

    www.eThinkTankTz.org

    http://www.radarrecruitment.com/

    ReplyDelete
  11. Wewe Annoy wa: Tarehe February 24, 2009 12:48 AM.

    Umeshakaa nje miaka 14 halafu bado unajipanga kurudisha majesho bongo...!! Unachekesha...wewe sio wa kurudi bongo.

    ReplyDelete
  12. ndio alakh huko ughaibuni kuna dhambi nyingi saana. njoo hapa bongo ni kama maka au jerusalemu.

    we umefanya kosa gani huko mpaka unapachukia hivyo? au unataka kusingizia ubaguzi?kama unabaguliwa huko basi hutapona dunia yoote.

    tena tuu una diploma, bado hujasoma vizuri, fanya degree za juu.

    ReplyDelete
  13. Km hujawahi toka Bongo unatamani kutoka. Kama ulikwishatoka na kukaa nje unatamani kurudi. Ndo binadamu tulivyo. Kwa hiyo wakati unawaza kuzamia meli uende nje, mwache yule aliyeyaonja maisha ya nje na kuona machungu yake arudi Tz. Usimshangae. Ana experience zote mbili - ya nje na ya Tz. Yuko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kulinganisha na kufanya uchaguzi. Wee si experience yako si ya Tz tu? Huna kingine cha kulinganisha zaidi ya kuota tu kwamba nje ni pazuri.

    ReplyDelete
  14. Hongera kwa kuamua kurudi nyumbani bila kutaka ushauri mwengine wowote zaidi ya huo.
    Mimi nakushauri rudi haraka kabla JK hajamaliza muda wake wa kuongoza nchi na ukifika tu uombe kazi serikalini haraka. IT serikalini inalipa sana.
    Huko hakuna mshahara mikubwa(nadhani pia huuhitaji kwani nia yako ni kujenga nchi), ila utakutana na mtandao wa mafisadi ambao wanakula nchi hata kama hawajakwenda kazini.
    Utapata fursa ya kula posho nyingi za kazi za kwelikweli na za kifisadifisadi ili mradi hutaadhirika kimaisha.
    Pia kumbuka kuwa sisi wenye level hiyo ya elimu kwa sasa hapa Bongo tupo wengi sana ingawa hatujalitosheleza taifa.
    Karibu kijiweni.

    ReplyDelete
  15. ulaya ikushinde ndo ukaweze bongo??baki humuhumu kachukuwe nvq level 3 ya care utajiendeleza kimaisha huku. juu kazi zipo na hazina ushindani na wazawa. najua huu ushauri huutaki but it will make you think again.IT in 5 to 10yrs haina soko utajikuta kama fundi wa redio with no time.

    ReplyDelete
  16. My Experience

    If you attempt to come back in Tanzania make sure you are either very compentent enough and good/maltilingual computer programmer or make sure you have a connection/god father otherwise prepare to safer until you regret why you decided to return back ...sorry sikutishi ila upo uwezekano wa kupata kazi kama huna hayo mawili niliyoyataja lakini guarantee sio kubwa.

    Habari ndio HIYO

    ReplyDelete
  17. SOMA HII STATISTICS HALAFU UPEMBUE WEWE MWENYEWE.

    1. CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KINATOA WATU WANAOMALIZA FANI YA IT/COMPUTER ZAIDI YA 100 KILA MWAKA

    CHUO KIKUU MZUMBE KINATOA WATU WANAOMALIZA FANI YA IT/COMPUTER ZAIDI YA 100 KILA MWAKA

    TAASISI YA TECHNOLOJIA YA DAR ES SALAAM KINATOA WATU WANAOMALIZA FANI YA IT/COMPUTER ZAIDI YA 80 KILA MWAKA

    CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA KINATOA WATU WANAOMALIZA FANI YA IT/COMPUTER ZAIDI YA 100 KILA MWAKA

    ARUSHA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY KINATOA WATU WANAOMALIZA FANI YA IT/COMPUTER ZAIDI YA 100 KILA MWAKA

    ST. JOSEPH COLLEGE OF ENGINEERING KINATOA WATU WANAOMALIZA FANI YA IT/COMPUTER ZAIDI YA 70 KILA MWAKA

    RUAHA UNIVERSITY KINATOA WATU WANAOMALIZA FANI YA IT/COMPUTER ZAIDI YA 50 KILA MWAKA

    ACHA VYUO MBALI MBALI VYA WAHINDI NA VILE VILE KUNA WALE WANAOMALIZA KATIKA VYUO VYA JIRANI KAMA KENYA, UGANDA(E.G KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY, MAKERERE ETC)

    KWA HIYO TAKRIBANI WATU ZAIDI YA MIA NNE WANAMALIZA MASOMO KATIKA FANI YA IT/COMPUTER KILA MWAKA NA HAWA WOTE WANATAFUTA KAZI.

    JEE HAPO WE UNAONAJE?

    ReplyDelete
  18. IT ya bongo imejikita mno kwenye networking.ingawa software ipo kiasi,we njoo tu unaweza kupata kazi lakini pia inategemea na mno na links,otherwise yaweza kukuchukua mda kidogo kupata.InshaAllah utafanikiiwa

    ReplyDelete
  19. hahahahahaaaa kwi kwi kwi,jamani michu umu bloguni kuna wehu na vichaa adi RAHA!!u make my day.ona izo ushauriz
    kijana rudi tu home kazi kwa fani yako na ivi umetokea kwa wabeba box?utapata tuuu fatilia izo link watu wamekupa

    ReplyDelete
  20. WATU WA UK NAONA WANAANZA KURUDI NYUMBANI KWA KASI SANA, SIO HUYU PEKE YAKE KUNA JAMAA KIBAO WENGINE WAMESHATUA KABISA JIJINI WAKISIKILIZIA KAZI YEYOTE ITAKAYOPATIKANA. NAJUA MAMBO YA RECESSION NA HII GLOBAL FINANCIAL CRISIS NDIO BAADHI YA SABABU LAKINI PIA JAMAA WAMEANZA KUTIGHT SANA MAMBO YA KAZI HUKO. NI WENGU TU WANAMAWAZO KAMA YAKO YA KUTAKA KURUDI LAKINI NIKUPONGEZE TU KWA UJASIRI NA KUAMUA KUWEKA WAZI KWENYE BLOG YA JAMII. RUDI TU MKUU KAZI UTAPATA JUU KWA JUU.

    ReplyDelete
  21. SHALOOM WAPENDWA....Naomba msimpatie chanel.....ATAKUJA KUTUTAMBIA SANA HUYU....SI MNAELEWA FANI ALIYONAYO INAVYOLIPA!....achaneni naye kabisa.....HAYA TUENDELEZENI LIBENEKE LA MAJUNGU......NAWAPENDENI SANA....MBARIKIWE

    ReplyDelete
  22. wewe mchangiaji wa February 24, 2009 12:36 AM, ni wapi pale aliposema kuwa wasiorudi nyumbani ni wajinga? hebu soma vizuri kwanza alichokiandika na baadae ndio ulete comments zako, unajuwa ule msemo "asiyejuwa kusoma ni mjinga mkubwa mno"? usidhani ni kutojuwa kusoma kilichoandikwa ni kusoma na kuelewa kilichoandikwa.

    ReplyDelete
  23. sijibu waosha vinywa wote ila huyu wa February 24, 2009 10:17 AM kaa na ushauri wako wa nvq care assistance bahati mbaya sitaki kufanya kazi ya BBC (Brish Bum Cleaner)

    simai

    ReplyDelete
  24. Naomba kumjibu mchangiaji mjinga sana wa February 24, 2009 12:39 AM, hivyo uasemaje hana options akiwa huku? anazo option tele ikiwa pamoja na kijiendeleza zaidi na kutafuta work experience huku huku. Pia anaweza kabisa kujiripuwa, anaweza kirahisi kujipatia karatasi za kuishi kwa kudanganya lakini yeye kama alivyosema hataki kukaa anataka kurudi nyumbani.

    wacha chuki binafsi, kwa kuwa wewe hukufika nje sio sababu ya kuwa na chuki a walio nje na kuwapaka ubaya mtupu. si kosa letu kuwa wewe umeshindwa kutoka na kuja nje, kama unataka kuja ongeza ujanja wako. chuki za moyo zitakuu kabla ya wakati wako.

    ReplyDelete
  25. wewe annon wa February 24, 2009 3:14 AM umesoma vizuri post hii? jamaa amesema anayo degree ya kwanza wewe unamwambia eti bado hakusoma sana eti ana diploma, au kwa kwako degree ya kwanza ni diploma? tena ni wapi aliposema kama anakuchukia uk au kusingizia ubaguzi? mbona unakuwa mzushi kiasi hiki? hivi kwa nini watanzania hatuwi wastaarabu, mtu kauliza suali kama huna jibu ya nini kuanzisha maudhi?

    ReplyDelete
  26. mwacheni mwenzenu arudi kukaa nje nikujiengezea umaskinini tu mwisho wake anafia gerezani mungu amnusuru na ampe nguvu ya kuja kuanza maisha mapya

    ReplyDelete
  27. wewe mtowa takwimu za wanafunzi wahitimu wa IT/COMPUTER nakuuliza kama ni idadi hiyo wako wapi hawa? mbona hatuwaoni? mbona tunahangaika mpaka tunawatafuta kutoka nchi za jirani? wangapi kati ya hao wanaomaliza wanaondoka na first or second class? la muhimu zaidi narudia mbona hatuwaoni? makazin wamejaa wenye vyeti vya vichochoroni tele!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  28. dah watu wengine jamani utadhani wanaishi katikati ya janga na hawaoni lolote ila kilichowazunguka, hebu angalieni mtu kajikaza na kupoteza muda wake hapa analeta data za wahitimu wa vyuo mbali mbali na kumaliza na suali sasa hii imekaaje. is he real? kila mwaka kunapatikana wahitiumu katika vyuo vyote wa fani mbali mbali na mbona wanapata kazi? mbona ameshindwa kutueleza ni idadi gani ya wahitimu wa fani nyengine huwa wanatafuta kazi kila mwaka? ni kasumba tu na kumtia wasi wasi dogo asirudi nyumbani.

    ReplyDelete
  29. Hivi alikuwa anaomba ushauri wa "arudi au asirudi?" au aliomba msaada wa sehemu ya kutafuta kazi? Maana inaonyesha "kurudi au kubaki" kwake si tatizo kwa sababu ameshaamua kurudi haina mjadala.

    muonesheni chaneli sio kujadili "kurudi au kubaki"

    ReplyDelete
  30. HIVI MNAJUA KAMA KUKAA ULAYA LAZIMA VIBALI VYA KUISHI VIWE SAWA?????
    Au MNAROPOKA TU ABAKI ULAYA, KAMA PEPA ZISHAKATAA LAZIMA ARUDI KWAO, EBO. HALAF WE MCHAMBA WAZEEITAJI NVQ3 YA KULEA VIBIBI VINAVYOKUTEMEA MATE NA KUKUMWAGIA CHAI KILA SIKU??? UNAENDA KAZINI UNA HASIRA UKIRUDI UNA HASIRA, NDIO MAANA UNAISHI KINYUME NYUME< MWENZIO ANA DEGREE YA IT UNAMWAMBIA AKASOME ELIMU YA WATU WAJINGA?? NVQ3 UNAONA UMESOOMA, ANGALIA NATURE YA KAZI UNAYOMSHAURI MWENZIO< KUSUKUMA HOIST NA KUCHAMBA VIZEE AMBAVYO HATA MAMA YAKO MZAZI AKIUMWA UTALETA POZI, MWEHUKABISA WEWE,
    MICHUZI uSIBANIE HII.... MANAAKE JAMAA KANICHEFUA ILE MBAYA.
    KAMA NDIO KAZI ZENU ZA 13k P/A UNAONA MAISHA USHAYATOA NA KULETA FRUSTRATION ZAKO HUMU, UMECHELEWA KWELI....
    BACK TO MTAKA USHAURI, NAKUSHAURI UENDE KWANZA BONGO LIKIZO KAMA UNA MUDA WA KUBAKI HAPA UK KWENYE PASS YAKO, KAFANYE RESEARCH YA KUTOSHA, NA APPLY KAZI NYINGI SANAA, INSHAALLAH ZITAITIKA TU... USIOGOPE MAISHA, LAKINI USIONDOKE KAMA HUNA MPANGO NA KUPEWA HABARI ZA REDIO MBAO.
    NAMUUNGA MKONO ANON ALIYETOA TAKWIMU KWAMBA WAHITIMU WA VYUO VIKUU KILA MWAKA WANAONGEZEKA, SASA UMEJIANDAAJE?
    MWISHO KABISA, HOW GOOD ARE YOU IN SOFTWARE DEV??? PANUA MAWAZO, UNAWEZA UKAWA YOUR OWN BOSS KAMA UNAMIPANGO MADHUBUTI NA UJUZI WA KUTOSHA.

    ALL THE BEST.

    MDAU UK.

    ReplyDelete
  31. rudi kwa vile nyumbani lakini kazi ni taabu hata kama una PhD JIANDAE KUTOA RUSHWA AU KAMA UNA NDUGU WA KUKUSHIKA MKONO OTHERWISE UTASOTA, KURUDI NI LAZIMA KWA VILE HUKO SI KWENU, NYUMBANI NI NYUMBANI TU

    ReplyDelete
  32. Aliyetoa takwimu za wahitimu wa vyuo vyetu amekushauri vizuri ili uweze kufanya tathmini ya job market and how much you can survive the compentition.

    Be prepared kupata some sort of negativity,.... things are not so straight forward as you might think.
    Otherwise kama unaweza kupata documents zitakazokuwezesha kuishi huko basi endelea kuishi huko ...ila kama visa yako haikuruhusu kuishi huko basi fikiria na fanya uamuzi haraka.

    usiache muda upite ukiwe na blank CV space .... yaani namaanisha mtu akiuliza kuanzia muda huu mpaka muda huu ulikuwa unafanya nini? basi atleast upate cha kujibu

    ReplyDelete
  33. jaribu hii!!
    Job Title : Computer Management Assistant

    Source : http://tanzania.usembassy.gov/job_opp5.html

    Requirements : College degree or host country academic equivalent, in the fields of computer science, information systems management or equivalent.

    Job Description : Service, Maintenance and Support Maintain DNS, NFS, DHCP, Back up, Scan mail, E-mail system, Web mail, SQL, FTP, Proxy and proprietary services for all staff clients. Ensure secure operation of all servers and services though the use of security and encryption tools such as SSH, SSL, IPSec and through extensive staff training and documentation. Provides desktop support for all office workstations, Monitors system logs and activity on all servers, Administrate, verifies and restore from backups. Replace defective hardware on clients and servers as necessary.

    Apply To : Human Resources Section

    Full Address : American Embassy, P.O. Box 9123, Dar es Salaam

    Closing Date : 6/Mar/2009
    bensam- Ar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...