Hongera kwa blog yako nzuri kaka Michuzi lakini hivi karibuni blog yako imekuwa ikitoa habari zisizojenga taifa letu badala yake imekuwa kusifiana eti Fulani ameoa, Fulani alikuwa beach jana, Fulani katika pozi la ufukwe n.k wakati kuna mambo ya muhimu katika taifa letu yanaendelea hususani bunge la Jamhuri ya Muungano.
Wakati naanza kuisoma blog yako nilikutana na habari muhimu sana kuhusu Kagoda hivyo nikavutiwa sana blog na kunifanya kuwa mmoja kati ya wasomaji wa blog yako kila siku lakini kwa sasa nachelea kusema imekuwa ya kihuni.
WAZO LA LEO: NAKUOMBA UBADILIKE SANA KURUDISHA HESHIMA YA HAPO AWALI
Mdau Magesa Lucas


We mdau Luka acha bana Misoup yuko juu mie namkubali bana anapiga kona zote habagui bani. Lakini kaka misoup bwawa la maini vipi mbona mnatuangusha kaka
ReplyDeleteNdugu Magesa Lukas kwa niaba ya bwana Michuzi ninaomba nikujibu hoja yako. Hoja yako ni nzuri kama kweli wewe ni msomaji wa blog hii ukifuatilia kwa undani kuna habari zote za mchanganyiko nyingi zipo kwenye blog hii. Ni kazi yako kutafuta habari zaidi kwa vyanzo vingine vya habari. Tunahitaji habari mbali mbali mchanganyiko za what is going on with the current gorverment and entertainments at the same time zote ni habari muhimu kwa jamii ya watanzania hasa walio nje ya nchi. Binafsi ninafurahi ninapoona picha za mitaa ya bongo na jinsi jiji lilivyobadilika. Kwahiyo usilalamike chochote unachokisoma kifurahie na ni wajibu wako kutuma habari kwa bwana Michuzi na yupo tayari kuzituma hewani baada ya kuzihakiki. Asante kwa hoja yako bwana Magesa.
ReplyDeleteSPM
Magesa kweli umechoka ndugu yangu.
ReplyDeleteKAMA UNATAKA WEBSITE YA KUFUATILIA YOTE ULIYOYATAJA NENDA WWW.JAMIIFORUMS.COM.
Otherwise unamsumbua Michuzi bure. Hii blog ni ya kujifurahisha tuu. Hii siyo blog ya ma-intellectual.. Watu wengine bwana..hivi wewe Michuzi unamlipa? unataka akuwekee mambo ya maana? You are just a sorry mind! Unalipia?
Anyway sina la zaidi..nenda kasome Jammii forums, labda utagundua kwamba kuna wenye akili wenzako wanaotaka mambo serious as you want!
WABONGO TUSIPENDE VITU VYA MTELEMKO SANA! ITS NOT GOOD! Michuzi humlipi wala hujamuajili...let him do what he wants with his blog...
Mdau Magesa, pamoja na maudhui maridhawa kwenye "wazo la Leo",naomba nitofautiane nawe. Kumbuka kwamba hii ni "Blog" na kila mwenye blog huwa anaiandika (au ana-post) vitu ambavyo aidha ameamua au amelazimika maudhui yake yawe, kibiashara ama kimtindo. Kimtindo: Kaka Michuzi pamoja na kuwa muadhishi kielimu, kitaaluma ni mpiga picha (tuvumiliane kwenye "kielimu" na "kitaaluma". Kuna tofauti!), therefore ni jambo la busara (wen gine wataita "no brainer") kama blog yake ikitawaliwa na picha na ujumbe mfupi, as compared to other options. Ukiingia jamii forums (www.jamiiforums.com) utaona maudhui tofauti ya ku-debate,"www.globalpublishers.com" -kwa maudhui ya stori za jioni,www.mjengwa.blogspot.com kwa maudhui ya yaliyojiri mikoani, www.bongoradio.com na mwanakijiji.podomatic.com kwa maudhui ya radio za kwenye Internet (audio/video Syndicated download via web feeds) nakadhalika nakadhalika. Nitakuunga mkono however, kama hoja yako itakuwa ni kumuomba aongeze link za vyombo vingine vya habari au umma ambazo watumiaji wanaweza kuzifikia maana, takwimu zinaonyesha Blog ya Michuzi inatembelewa zaidi kuliko nyingine. Naomba niwakilishe. Kibiashara: Angalia maudhui ya matangazo ambayo Michuzi anayapata…Sponsors wake wanatarget traffic ya watu wanaoperuzi picha. Sponsor wake ni makampuni ya Simu na Bia, i.e. watu wa huduma. Naomba niwakilishe. Kaka YEnu
ReplyDeleteMKUU WA NANIHII, HUYU JAMAA NAFIKIRI NI MNAFIKI. HUO UHUNI ANAOUSEMA NI UPI HALAFU BADO ANASIFIA. HUYU SIO MTUMIAJI WA BLOG HII KWANI HATA HIYO MSAADA TUTANI ALIYOTUMIA SIO LOGO YA KUBEBA UJUMBE WAKE. KISHA ANATAKIWA ASEME HIYO INAYOUPIKU BAADA YA KUPOTEZA UMAARUFU NI IPI.
ReplyDeleteSHABIKI LA BWAWA.. NA MAUMIVU YOTE ULIYONAYO, TAFADHARI USICHUKUE USHAURI HUU, KWANI GLOB HII HAICHOSHI KUSOMA SABABU YA KUWA NA MTIRILIKO USIOKISIWA, NAMAANA MCHANGANYIKO. NAFIKIRI HUYO BLOGER AMEKUNJWA KIMPUMU.SAMAHANI LAKINI.
Wewe kasome gazeti la uhuru ,Mzalendo utapata habari za chama na serikali tuu ,UMU MAMBO MCHANGANYIKO
ReplyDeleteBwana Lucas mawazo yako sio mabaya lakini hii ni blog ya jamii. Do u know what that means??
ReplyDeleteMdau namba 6
Mh mkuu wa wilaya ya nanihii, Nakupongeza kwa kuwa na upeo mpana mno kimawazo kuweza hata kuposti akina nanihii kama huyu jamaa! Hivi wewe ni nani wakuweza kuamua nini watu wasome na ni nini UHUNI, JE UNAJUA KUNA BLOG NGAPI ZA KISWAHILI(ZA NYUMBANI)Unaanza kuleta malalamiko yasio na msingi, kwa nini usianzishe BLOG yako isiyo ya kihuni na ukaandika habari za maana, HII KAMA ANAVYOSEMA MHE MKUU WA NANIHII NI BARZA, NA BARZA INAKUWA NA MAZUNGUMZO TOFAUTI, SI LAZIMA KILA SIKU TUZUNGUMZIE BUNGE TU. WADAU HUJA HAPA KUPATA HABARI PAMOJA NA BURUDANI IKIWA HARUSI, AKINA CHIBILITI(UKO WAPI MDAU) DEBATE ZA KINA MASHAKA, JK NA PIRIKA ZA NCHI, FUTBOLI,NA MATUKIO YA MITAANI, KWA TAARIFA YAKO TUKO MBIONI KUTAFUTA MDAU WA MILIONI SITA, HEBU NENDA ANZISHA BLOGU YAKO YA BUNGE NA BORING LIFE YAKO NA UONE LINI UTAFIKIA MDAU WA MILIONI SITA!!! TUPISHE TUSTAREHE BARAZANI KWETU!!!
ReplyDeleteKIP DHE GUD WAK MHESHIMIWA, SISI TUPO NAWE DAIMA, FOR US ANY NYUUUUZ IS A GUD NYUUUUZ!!!
Nakubaliana na mtoa mada. Two years back, in a day ulikuwa unaweza kutumia even one hour in the site. That was caused by hot issues/debates zilizokuwa zinatolewa huku. Lakini sasa imekuwa kama notice boards za shule,matangazo ya mikutano,disco etc. Naona michu should look back and think of doing something.
ReplyDeleteNdugu Michuzi,
ReplyDeleteNaomba nitumie nafasi hii kuweka mawazo yangu kuhusu blog ya jamii.Ni wazo zuri kuendeleza Libeneke kwa kuweka burudani za kila aina kwenye blog hii, lakini ninaonelea tuwe serious kidogo ili blog hii inayosomwa na Watanzania wengi itoe changamoto na mijadala hai ya kutatua matatizo ya jamii ya Kitanzania kama Umaskini, maradhi, elimu duni,namna ya kuboresha maisha ya mjini na vijijini n.k, pamoja na Libeneke la burudani kama ilivyosasa.
Mwisho bwana Michuzi nakupongeza kwa ubunifu wako na kazi nzuri ya keundeleza blog ya Jamii.
Mdau USA.
Watu wengine bwana.. kama hii blog haijengi taifa sasa wewe unatafuta nini hapa? Ukitaka mambo ya Kagoda kuna blog zaidi ya mia zinazungumzia mambo hayo. Kuna website nyingi tu zinazungumzia hayo mambo nenda mwanakijiji.com na utaelekezwa kwa kwenda.
ReplyDeleteMwanakijiji, sangara huyo mvue amejileta mwenyewe kwenye nyavu.
Mdau Magesa Lucas you are asking for it huh?
ReplyDeleteJust wait for "wadau" to pounce on you....
Watakuja sasa hivi utawasikia.
IT'S TRUE MICHU' I WAS ABOUT TO TELL YOU. MIMI NILIIFANYA HII BLOG KAMA MBADALA WA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI LAKINI NIMEGUNDUA NAKOSEA SANA KWANI WAKATI MWINGINE KUNAKUWA NA ISHU KUBWA YA KITAIFA INAKUWA INAENDELEA, HUIBANDIKI PENGINE KUTOKANA NA WOGA WA KUFUNGIWA HII BLOG AU KWA INTEREST ZAKO KAKA MICHU. TUNAOMBA HABARI ZA MSINGI KWA JAMII NZIMA KAKA MICHUZI.
ReplyDeleteVINGINEVYO NAOMBA NIKATIE KILA LA KHERI KATIKA KULIPELEKA MBELE LIBENEKE.
Bwana Magesa!
ReplyDeleteNavielewa mimi hii ni blog ya jamii; na ktk jamii kuna mambo mengi; siasa, biashara(uchum),burudani n.k . Sioni tatizo la bwana michuzi nadhani anajaribu kuwapa wadau wa aina zote na hivyo kuwa blog ya jamii kweli kweli, na sio blog ya watu wa type flan tu, kwa mfano wanasiasa.
Ndugu, Magesa Lucas,
ReplyDeleteSijui kama unaelewa maana ya Jamii.
Katika jamii kuna furaha,sherehe, harusi, na mambo mbalimbali ya kufurahia maisha. Bila kusahau kuna machungu pia, tusiyoweza kuyazuia, kama misiba,kuugua, kuibiwa, ujambazi, ajali, kuanguka kimaisha nk. Mambo hayo machache niliyo andika bila shaka yatakupa uelewa kidogo. Hali kadhalika katika jamii kuna burudani, yaani starehe na michezo. Hiyo ndio jamii yetu. Hata hivyo Balozi michuzi amekuwa akiandika habari zote pamoja na siasa.Ushauri wa bure kwako. kuna blog nyingi za siasa unaweza kujiunga uanachama, au pia unaweza kuanzisha blog yako, nasi hapa katika jamii tukakusaidia kiufundi kama utahitaji msaada.
Mzalendo Halisi
Huyu Bw.Luka ninahisi akili ZIMEMRUKA kama jina lake lilivyo.
ReplyDeleteKwanza kabisa utuombe radhi hapa jamvini kwa kutuita sisi ni wahuni.. kwa kauli yako kuwa blog imekuwa ya KIHUNI.
Wewe ndiye Muhuni kwa kutokuwa na uelewa wa mambo yaendavyo katika Media stuffs.. kwani hizo Hot News kama za kina Kagoda(kwa upeo wako) haziwezi kutokea kila siku inayokucha.
Chukua mfanowa CNN, BBC n.k za huku juu nazo hukosa habari kwa nyakati fulani na kutuonesha habari hizo hizo ambazo wewe uliyerukwa unahisi ni za kipuuzi.
Tembea uone na usiwe mvivu wa akili kutafuta habari unazozitaka toka vyanzo nyingine mpaka usibiri MICHUZI akuletee humu jamvini..
Tatizo lako naliona umezoea dezo dezo hivyo unasubilia slope ya michuzi kupata habari bure bure, nenda uka Subscribe kwenye paid site upate unachokitaka.
Tutolee UPUUZI wako wewe mtu uliyelukwa :((
JAMANI NI WAZO LAKE UYU ANNON,,,NA KAULIZWA MICHUZI SO MICHU NDO WA KUAMUA VIPI!!
ReplyDeleteOFKOZ KUNA BLOG NYIIINGI TU ZINA VITU "SERIOUS ALWAYS" ILA MTU PALE ROHO YAKO INAPENDA,SO MICHU SIKILIZA THEN UTAONA
ofkoz vile vipicha vya watu sijui bethidei,barafu,pozi la nini sijui vinakera sana!!
ANYWAY
ANZISHENI YENU..TUACHENI NA MICHUZI WETU NA BLOG YETU....PUMBAFU
ReplyDeleteBwana Lucas kama wanavyoandika wadau wengine hii blog ni jamii na inagusa kila pembe ya jamii. Kwa kuona picha ya mtu whether ni beach ama harusi you never know you can meet a long lost friend na kumcontact tena! sijui hili unalielewa - sio kwamba ni picha tu bali blog hii inawezesha watu kuwasiliana pia! Siku nyingine uwe makini na maneno unayotumia - 'Kihuni' maana yake nini? I doubt hata kama unajua!!! We tuache na blog yetu and go an find another blog where you can read what you want better still unaweza anzisha yako na uweke unachotaka! Kaka Michu Big Up na kazi nzuri unayofanya and keep it up!
ReplyDeleteLUCAS,
ReplyDeleteWazo lako la kupenda na kuchagua unachotaka ni uhuru wa msingi. Lakini pia huwezi kuchagua unachotaka pasipo wajibu. Je, wewe una uhuru kiasi gani wa kumiliki mawazo ya wasomaji wote humu, hadi uwachagulie watu vya kusoma? Bila shaka kama Michuzi kachemsha wengi wangelalamika, ila ni wewe tu peke yako. Napata shaka.
Pili, hata kama unapendelea habari za Kagoda au Bunge zaidi, kwanini usipendekeze kama ombi? Kwani ungeambiwa ni mwisho wa dunia? Yaani wewe unalazimisha hata hujaheshimu wasomaji wengine. Wazo lako lilikuwa zuri lakini umeshaharibu kabisaaaaaa!
Site hii ni kama tu magazeti yalivyo mengi pale DAR, unachagua usome unalotaka. Kuna udaku, siasa, maisha, uchumi, na mambo ya Kimataifa. Sasa wewe leo, uwaambie gazeti la Mtanzania waandike kama RAIA MWEMA, nk. wapi na wapi?
Afterall, mimi naona unapingana na kazi ya hii BLOG.
Nanukuu: "....... zisizojenga taifa letu badala yake imekuwa kusifiana eti Fulani ameoa, Fulani alikuwa beach jana, Fulani katika pozi la ufukwe n.k wakati kuna mambo ya muhimu katika taifa letu yanaendelea hususani bunge la Jamhuri ya Muungano......".
Kwa taarifa yako blog hii inaganya kazi kama vile uwanja wa Fasihi. Fasihi kazi zake huwa ni:
1) KUELIMISHA
2) KUBURUDISHA
3) KUONYA
4) KUELEZEA UTAMADUNI WA JAMII
5) KUSAHIHISHA NK.
Sasa wewe, watu kuoana ni upuuzi? Kwenda beach ni upuuzi? Wengine tunahitaji kuona mambo ya Bongo yanavyotokea yakiwemo haya, unayoita upuuzi. Mimi Kagoda sihitaji, nahitaji tu siku rais akiwawajibisha hao, au nisikie wananchi wa mkoa fulani sasa wanapata barabara.
Mawazo yangu,
Mdau United States of America.
MDAU LUCAS YUPO SAHIHI KABISA MICHUZI NAAMINI WEE MWENYEWE NI MWELEWA NA UTAYAFANYIA KAZI MAWAZO YAKE,JAMANI LUCAS HAJAMLAZIMISHA MICHUZI ILA AMETOA USHAURI WAKE TU AMBAO PIA BAADHI YA WADAU KAMA SISI TUMEUUNGA MKONO NA BINAFSI NILIKUWA MBIONI KUMWAMBIA MICHUZI KUHUSU HILO.WABONGO TUNA MENGI YA KUONGELEA KATIKA KIPINDI HIKI CHA UKWASI ULIOIKUMBA DUNIA NINI KIFANYIKE,EBU TUJARIBU TU KUFIKIRIA WAKATI HAMNA HUO UKWASI BONGO TAYARI TULIKUWA TAABANI NDIO UKWASI USHAIVAMIA DUNIA KWELI TUTAPONA SIE??TUSIJITIE KUYAAHIRISHA MATATIZO YETU KWA KUTUNDIKA PICHA ZA MTOTO KALALA KWENYE BARAFU WHAT IS SNOW??KWELI BURUDANI SIO MBAYA LKN KUNA UTOTO UTOTO MWINGI SANA SIKUHIZI.NATAMANI KAMA WATUMIAJI WA INTERNET WASIZIDI KUONGEZEKA BONGO MANAAKE ITAKUWA NI KERO SASA VURUGU MECHI KAMA UWANJA WA FISI BORA TUBAKIE WACHACHE TU.
ReplyDeletedah, kidogo nitukane lakini kwa heshima ya kaka mithupu nakustahi bwana luka.
ReplyDeletelabda uka-research nini maana ya blog na umuhimu na matumizi yake.
nuff said.....
Mdau Luka kweli umerukwa
ReplyDeleteSisi humu tunaingia kupata vitu hivyo wewe unavyoona vya kipuuzi.
pumbafu mkubwa wewe kwa kukosa adabu!
michu endelea na moto huu huu wala usimsikilize mdau huyu aliyerukwa
TUTAENDELEA KUJIMWAGA TU HAPA HAPA WALA HUKO UNAKOTAKA TWENDE HATUTAENDA
Mheshimiwa,
ReplyDeleteInawezekana una habari unazopenda kusoma na hivyo misupu hakidhi haja yako. Natoa suggestions kwako:
1. Anzisha blog yako, weka nyuzi zote unazoona zinakufurahisha na uzisome mwenyewe.
2. Endelea kusoma Blog ya michuzi ila uchambue kile unachoona kina make sense. Nina uhakika hata ukisoma majira, uhuru au mzalendo utakuta habari za watu kuoana. Kila mtu ana haja yake kwenye gazeti, we can never have the same interests.
3. Interests zako haziwezi kudictate dunia nzima, we ni sehemu ya dunia.
Hii ni globu ya Mkuu wa Nanihii na sote tunatambua alivyo mlevi wa taswira. Tunategemea itawaliwe na taswira. Hiyo ndiyo sababu watu imebidi wakubali awe anaanika matokeo mazuri ya bwawa la maini na kumtania kidogo pale mambo yanapowaendea kombo.
ReplyDeleteWakati huo huoa ameamua kuifanya iwe globu ya jamii. Habari nzito kabla haijatoka sehemu nyingine yoyote mtandaoni tunaipata kwanza kwenye globu ya jamii.
Ukumbuke ni mambo mangapi yanaendelea katika jamii? Kuna mambo ya maana na ya kipuuzi, yote hayo ndiyo yanayofanya jamii iwe jamii. Mfano kuna picha moja ilinifurahisha ilipata kutoka humu ya foleni zetu Dar. Kuna makutano yalikutanisha magari mbalimbali yamebanana shaghalabaghala hakuna anayeenda popote. Kichwa cha habari ile kilikuwa usenene. Utasema sio jambo la maana hilo?
Am sorry to say this,huyu bwana Magesa kama hajatumwa basi ng'ombe wake hawajarudi zizini "Michuzi" bring the same issues every now and then,afterall what you take as stupidity might have significant advantage to the other fellows.
ReplyDeleteHey hey my fellow Tanzanians,huyu Michuzi tumekalia kumsifia tu kila siku,Oooooooooooooh unatupasha,Ooooooooooooooh unatukumbusha nyumbani,Ooooooooooh sijui nini.Hasa nyie nduguzetu mliopo huku "majuu",sijaona hata sikumoja mtu akasema,Michuzi hebu nipe particulars zako ili kesho uende WESTERN UNION ukakinge,Kijana anahangaika huyu tangu miaka ile.Na hata sasahivi ukikutana naye utamwona yupo bize ilimradi tu kutimiza malengo hayo ya kuwapasha habari halafu leo wewe MAGESA unataka kuleta habari zako.Umeniudhi!!,Sijui nkutukane?anyway,next time ukirudia nnakutukana,shenzy taip!
MDAU
Masomoni majuu.
na mimi jomba chilingi bado chijachema kitu. nimekaa ndomo kimya. wewe kama wataka blogu yenye vitu unavyotaka si uanzishe yakwako angalia nani atakuja kukaa kusoma ati saa zima.
ReplyDeletewewe MDAU,Masomoni majuu.
ReplyDeleteShukrani siyo lazima western union. Hebu niambie ni wadau wangapi wakishuka bongo wanampelekea zawadi kaka michuzi? Kama wewe hufanyi basi wenzio tunafanya. Ni wabongo wangapi wakishuka bongo kufunga ndoa wanamtafuta michuzi na kumpa tenga? Kama wewe hufanyi basi wenzio tunafanya. Ni kivipi michuzi angeweza kupata wadhamini kwenye hii blog ya jamii kama hakuna watu wanayoiangalia? Ni kivipi angeweza kuwa balozi wa zain bila hii blogu. Nafuu umeamua kwenda shule.
Magesa leo umechokoza nyuki, ngoja zikuumeeeee mpaka. ni hivi magesa humu kuna vichwa vya kila aina vinaperuzi humu na kila mtu anaeingia hapa jamvini huwa ana upeo na burudani na matakwa yake, sasa kwa siku nyingine huwa kuna matukio ya utashi wa mwenzako m.f huo uloutoa wa mavazi, vyakula, mpira, bunge, kipanya, elimu hata hina na tamaduni za wengine na nk nk, sasa hebu usiwe mbinafsi kwamba kila siku walete khabari za bunge na dr slaa na kagoda tuuuuuu acha kila nafsi iridhike hapa, almuradi theutamu haipo hapa sisi poa tuu we subiri siku ya agenda unazopendelea soma kisha mezea kwa zile tunazopenda sisi mf. mavazi vyakula kilimo miti maua mbali na wale wachumi wakemia wahandisi nk. nk.
ReplyDeleteushauri wa bure: Usiwe mbinafsi, tazama na jifunze wengine wanapenda nini? pole sana.