HABARI,
POLE NA MAJUKUMU YAKO YA KILA SIKU YA KULIJENGA TAIFA.
MIMI NI MDAU WA BLOG YETU HII YA JAMII,
POLE NA MAJUKUMU YAKO YA KILA SIKU YA KULIJENGA TAIFA.
MIMI NI MDAU WA BLOG YETU HII YA JAMII,
. NINAOMBA KUTAFUTA WATANZANIA,WAKENYA AU WAGANDA WANAOJUA KUZUNGUMZA KISWAHILI WAWE NI WANAFUNZI AU WANAISHI HAPA SOUTH KOREA.
NIMEFIKA KIPINDI MPAKA NASHINDWA KUZUNGUMZA KISWAHILI KUTOKANA NA MAZINGIRA YA LUGHA HAPA SOUTH KOREA.
NINAOMBA KWA WAHUSIKA NILIOWATAJA TUWASILIANE KWA EMAIL;
jackbjackdo@yahoo.co.uk
NIMEFIKA KIPINDI MPAKA NASHINDWA KUZUNGUMZA KISWAHILI KUTOKANA NA MAZINGIRA YA LUGHA HAPA SOUTH KOREA.
NINAOMBA KWA WAHUSIKA NILIOWATAJA TUWASILIANE KWA EMAIL;
jackbjackdo@yahoo.co.uk
AU
karibu sana south korea, mimi ni mdau naishi hapa muda mrefu ila kiswahili sisahau, tatizo haujasema uko south korea mji gani
ReplyDeleteila inaonekana wewe ni mshamba kidogo
wewe unayetaka waswahili si uangalie ze comedy za kibongo? au wakina kingwendu wapo kwenye youtube ili usisahau kiswahili? au unataka kujitangaza kuwa uko south korea? yaani wewe ndio wakuja kweli
ReplyDeleteKwanza sema km ni mwanaume au mwanamke.
ReplyDeleteYani wabongo nyie mafala sana kwani mtu kuulizia watanzania wenzake ni vibaya?au mnaleta majungu tu hapa?nyie ndo washamba kwani mtu kusema yupo south korea kwani kawambia yupo mbinguni tayari?anyway mdau uliyeomba kuwajua watanzania nitakutumia email then utajua zaidi.
ReplyDeleteJamani huyu mdau sio mshamba sema tuu ameweka bayana tatizo lake la kuto-ongea kiswahili si mshamba ila inatakiwa tumpe ushauri maana hatujui katokea wapi hapa tanzania kuna wengine wanatokea KIGOMA-KASURU KAMA VIJIJI VYA MKWIVANGA, MANG'UDANGA na kapata zali la nje kupitia taasi binafisi sasa utakuta mtu kama huyo kiswahili mdomoni hakimo rafudhi na kila kitu ni kiha na huko korea hawaongei kiha ni kikorea sasa mdau kiingereza hajui huyu, na kiswahili anajua lakini cha kiha,kikorea atakuwa anajua ila kinampa shida mdau sasa bora ajifunze kishwahili tuu ndio maana anatafuta wadau wenzake wa kiswahili, mimi namuomba atafute na aulize maana huko Korea vijana wa kitanzania si wengi.
ReplyDeleteMimi Mdau wenu
Issa Bin Jini-Ujiji-Kigoma
haya ndio matatizo ya watanzania tuliopo nje, mtu anatafuta watanzania ili aweze kujuana nao mtu anamkandia na kumwita mshamba. hebu niambieni ni kwa kipimo gani ameweza kumwita mwenzake mshamba?
ReplyDeletewewe mweka maoni wa February 18, 2009 10:54 AM tafuta la kufanya bwana. mtu anatafuta watu wa kujuana nao huko aliko wewe unasema atizame youtube na utumbo mwengine hivo atazungumza nao vipi hao? mtu anatafuta watanzania ili ajuane nao kuna uzima na ugonjwa kuna kufikwa na matatizo, uongo mbaya ukiwepo nje kujuwana na wananchi wenzako kuna manufaa mengi.
ReplyDeleteJambo zuri sana kutafuta wajamaa wa kitanzania na majirani zetu unapokuwa nje ya nchi, kwani hujui litakalokufika, pia kuna mambo mengi utasoma au kujuwa haraka kuhusu hapo ulipo kupitia kwa wenzio, kwa hilo nakupongeza. ila usizidishe chumvi bwana, mtu hasau lugha yake kwa kukosa kuzungumza na watu kwa kipindi.
ReplyDeletewabongo mpokeeni mwenzenu na maswala ya uzushi tuyaache
ReplyDeletemdau netherlands
Mimi nipo seoul email yangu gquest80@gmail.com
ReplyDeletewabongo wengine bwana na wewe huko south korea umefuata nini haswa utueleze nchi yenyewe nzima wananchi kama wanajeshi kazi moja tuu huko kutengeneza silaha kali!tehetetehe. Hamia zako ukerewe na Dumila (by the way bro Michu dumila ni wapi vile nimesahau ?) kuna wabongo kama karanga vile nakiswahili nje nje barabarani kama kariakoo ndio mana na majungu yamezidi tunaendelza libeneke.Raha iliyoje
ReplyDeleteNaona waosha vinywa wengine wameshindwa kumuelewa huyu bwana sio kama hajui kiswahili ila amekaa mudaz mrefu bila kuongea kiswahili hio ndio tatizo lake amtu asiyejua kiswahili asingeweza kuandika kama alivoandika hapo ana maana kiswa chake kitapotea au vp mdau mpeni tafuuu jamaa walioko huko
ReplyDeletemichu mi nashauri humu itungwe sheria mtu asiiingie kuchangia kama ana njaa kama hao wanaomwita mwenzao mshamba sidhani kama wamekula na hata kama wamekula basi itakuwa ni lishe duni tu nyie hamuoni wanaokulaga magengeni kwa mama ntilie wanavyoropokwaga?nenda kwenye restaurant inayouza msosi wa maana kama utakuta watu wakizozana au kelele,mdau nafuu uwatafute wakenya kuliko waganda hapa ninapoishi mm waganda hawajui kabisa kiswahili hawa jamaa yaani siwaelewi kabisa ujue.misosi ya mabarabarani inawadatisha wabongo sio lazima upate kipindupindu tu hata kuropokwa kunachangiwa na hio misosi yenu ya hamira,mtu una jero unataka mama wa watu akujazie msahani top, hehehe kwanini asikutilie hamira kesho kwenye ubwabwa ili zikatoka pleti nyingi na mkapata kujaziwa nyie kajambanane sasa mkishakula ubwabwa wenu uliokosewakosewa vipimo huko mnaingia michuziblog kuchangia.
ReplyDeletewewe anon unayesema watu wa kigoma hawajui kiswahili koma kabisa, usisababishe watu wakachafua hali ya hewa kwa kiha humu,, mi nahakika hata wewe mwanyewe kiswahili hukijui kabisa mfano kigoma hakuna sehemu inayoitwa KASURU NI KASULU, so acha kujifanya mjuaji sana, na pia kuzunguzia hayo ni ukabila... yaani bado tu unaishi karne ya 16 ???
ReplyDeletetehe tehe tehe! ha ha ha! wabongo bwana! ndio maana napenda kuingia blog ya mithupu kila siku.. kwani maneno yao yananifurahisha saaaana na kunivunja mbavu... hata kama siku nzima nilikuwa nimenuna kwa kazi ngumu za kubeba box na kitabu..
ReplyDeleteTehe tehe tehe!
nicheki mimi hapa mimi nipo seoul email yangu ni fortunese4@yahoo.com
ReplyDeletena wewe uliyesema huku watu wako kama wanajeshi usiongee vitu usivojua hapa ni south korea na sio noth korea na kwa taarifa yako wabongo tunaoishi hapa ni makini kinoma tunasevu na kularaha pamoko na hapa jukuna mabo ya kimbea mbea kama nchi zingine zenye wabongo wengi.
Asikwambie mtu Korea iko juu sasa wewe mdau unae sema ovyo juu ya KOREA njoo uone huku huingii kama unaenda zako china au Nigeria huku wako juu , ki technology, Ki- uchumi tena kuliko hata nchi maarufu za ulaya kwa kifupi wako kwenye Boom na si reccesion we ponda sisi twala raha mustarehe
ReplyDeleteMdau South Korea
nafikiri huyu ndugu anatafuta company, sasa wanaomuita mshamba ni hawaelewi hali,,,kama umeshakaa nje utajua, kuna upweke na ukiwa, sometimes unahitaji mtu uongee naye kikwenu,mpike ugali mle wote, mtie story za bongo,,basi tu mtu ujisikie furaha na faraja....
ReplyDeletena unaweza kuta mgeni bado hajakaa sana huyu...mliko korea jamani mpeni mwenzenu contacts mpeane company IKIBIDI NA KWA KUHESHIMIANA....
sasa kaka mimi niko nje ya nchi huu mwaka wa 11, ushauri wa bure:hao unaowatafuta, ukiwapata basi iwe ni kupeana company,kushirikiana kwa yale ya lazima TU na zaidi ni kuheshimiana BASI!!ukiwazoea saaaaaana, mkaanza kuunda magenge na ushoga/undugu feki..yatakuja yakutokee puani, utajuta kuwatafuta,,utazushiwa umetongoza mpenzi wa mtu, utasemwa umekopa haujalipa, utasemwa kwenu masikini we unabadilisha raba mtoni,utaambiwa kwako kumejaa furniture za mitumba,utapelekwa bar utasakiziwa kwa wakorea huko upate makaratasi n.k ndio kawaida ya huku nje wabongo wengi wakishaanza kuwa karibu too much,,,unafiki ni mwingi mno, imefikia hatua watu wakienda bongo likizo wanarudi na mizizi kuanza kurogana ili watu wasiendelee n.k so sisemi ni kila nchi huku nje wanafanya hivyo, ila nasema kwa experience yangu na mengi niliyoyasikia toka nchi kadhaa,so uwe careful ndugu yangu,,,fanya kilichokuleta huko,,mazowea ya too much angalia sana yanaweza yakaja kukucost,,sababu kuwa ni kuwa asilimia karibu 99 ya wabongo wanaokaa nje(too long and for no good reason) wako frustrated teh teh teh,,,we haya weee, yangu ndio haya,,UTAKUJA KUNIKUMBUKA....
Ciao,
dada lao.
Itachukua miaka mingi sana kwa sisi Watanganyika kubadilika na kupiga hatua ya kimaendeleo.
ReplyDeleteYaani mtu kaweka e-mail address yake lakini watu bado wanakandia kwenye blog badala ya kuwasiliana nae yeye mwenyewe...kazi ipo!
Mnyama Mbaya
kama ni mwanaume basi bila shaka atakuwa anatafuta dem.....WIZI MTUPU
ReplyDeleteSOUTH KOREA WAPIIIIIIIIIIIIII?NAWE
ReplyDeleteKAA ZUZU?SEMA UKO WAPI WATU WAKUTAFUTE ALAAAA!!
anyway south korea zipo sehemu kibao wabongo wapo tu na english waongea tuu
sema kama uko maswekeni uko mayb itakua ngumu sana
ila jamani Busan ule mji?si mchezo,sio fulugu mechi za seoul