Anuani ya alipokuwa akiishi ni
42 Caine Rd,
Hanbary Road,
W3 8RE.
Marehemu Laura alifariki nyumbani kwake alfajiri na chanzo halisi cha kifo bado kinafanyiwa uchunguzi wa kitaalamu (Autopsy). Marehemu ameacha watoto wanne.
Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kupelekwa kilimanjaro kwa mazishi inafanywa.
Familia ya Munis inachukua fursa hii kuomba michango ya hali na mali ili kusafirisha mwili wa marehemu kwa mazishi. Watanzania, ndugu, jamaa na marafiki tunaombwa kutoa rambirambi zetu kwa kuwafariji wafiwa. Akaunti maalum kwa ajili ya kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu na mipango ya mazishi kwa ujumla imefunguliwa
Lloyds TSB.
Name on account:
Sidi Kikenya (UK) 07932438234
Abubakari Faraji
---------------------------------------------------------------
Kupitia Blog ya jamii, familia ya Munis ilitoa ombi la michango ya hali na mali kutoka kwa Watanzania, ndugu, jamaa na marafiki, ili kusafirisha mwili wa marehemu Laura kutoka London kupelekwa Kilimanjaro kwa mazishi.
Sisi marafiki wa mdogo wake marehemu (Viola Dausen) tunaoishi Houston, tumeitikia wito huo kwa kuandaa harambee ya kuchangia gharama za kusafirisha mwili wa marehemu dada yake. Tunapenda kuwakaribisha ndugu, jamaa, marafiki na jumuia ya watanzania wanaoishi Houston katika harambee.
Itafanyika Jumapili tarehe 8, kuanzia saa 11 jioni mpaka saa 3 usiku, katika ukumbi wa Woodlake Community.
Anwani ni
2200 Tanglewilde,
Houston,
Texas 77063.
Tunatanguliza shukurani na karibuni.



JAPO SITOI MCHANGO LAKINI HIZO ACC. ZA LEO MBONA NYINGI SIO KAMA ZA POST YA JANA, AU NDO KUSEMA WALE WENGINE PESA ISIENDE KULE, AU HAWA WAPYA NDO WAAMINIFU. POLENI WAFIWA,SIE HUKU BONGO TUPO HOI.
ReplyDeleteNaomba kujibu swali la mdau kuhusu account zilizofunguliwa London na ile ya awali ya USA. Wale walioko USA wanaweza kutuma kirahisi kwa account ya awali ambayo imefunguliwa na dada mwingine wa marehemu Viola na hii ya sasa ni juhudi za msingi za ndugu, jamaa na marafiki wa Uingereza na sehemu nyingine za Ulaya. Edina Dausen Munisi ni mdogo wa marehemu na Heri NTIMIZI ni watu waliokua pamoja na marehemu tangu enzi hizo za Kijitonyama. Kwa KIFUPI, HAWA WOTE WANA mapenzi mema ya kufanya kila liwalo kufikisha mwili wa marehemu Dar Es Salaam na baadaye kwa mazishi Kilimanjaro. Tunaomba sana ushirikiano wa dhati na siyo utani msibani ambao haujengi. Tunawasiliana kwa karibu sana ili kufanikisha msiba huu wa ghafla na pigo kubwa kwa familia.
ReplyDeleteWatanzania wa Houston na vitongoji vyake tujitokeze kwa wingi jumapili ili kuwapa pole Viola Dausen Munisi na Peter Munisi watakaokuwepo pamoja nasi. Hiki ni kipindi kigumu sana kwa familia ya Munisi baada ya kuondokewa na binti yao mkubwa.
ReplyDeleteKwa ninavyoelewa account tofauti ni kwa ajili ya kurahisisha utumaji wa fedha. Unaweza ukawa unaishi sehemu ambapo banki moja inapatikana au miongoni mwa hao waliotajwa ambao wote ni ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa Marehemu ukapenda kutuma kwa Edina Munisi au Herry Ntimizi. Tunafanya kazi kwa karibu UK na USA; NIA NA MADHUMUNI KUFIKISHA MWILI WA MAREHEMU LAURA NYUMBANI KWA WAZAZI WAKE, na kuagwa kwa heshima zote na kuzikwa Machamu. Tunaomba ushirikiano na siyo utani bwege msibani.
ReplyDeletePoleni Kwa Msiba Laura RIP
ReplyDeleteNaelewa hali ya maisha ni ngumu sna hapa UK (with credit crunch bite almost in every pocket) Kutoa ni moyo, tuwasaidie waliofiwa mchango £10 kwa kila mtanzania aliyeko UK utasaidia kumfikisha marehemu Laura nyumbani. Marehemu ameacha watoto wanne je hawatapenda kwenda kumwaga mama yao??