Mkuu Michuzi,
Hongera kwa kulipigia debe suala la maeneo ya kupumzikia na maeneo ya wazi kwa ajili ya michezo.Tatizo hili limekuwa sugu kwa sababu madiwani hawajui kazi yao.
Natoa pendekezo jitihada za makusudi zifanyike katika kuishirikisha sekta binafsi katika kuyaendeleza maeneo haya.
Kwa kuanzia,kunaweza kukawepo na mkakati wakuanzisha kitu kama Adopt a Park ambapo makampuni yatajitolea,kwa kuanzia kama kuchukua eneo la kidongo chekundu na kupatengeneza na kuwa eneo mrua kwa ajili ya mapumziko na viwanja vya michezo.
Makampuni yanaweza kukubaliana na watu wa jiji ili baada ya matengezo ya eneo hilo wakaweka matangazo yao bure katika eneo hilo.Michuzi kama Vodacom inatoa karibu mil 300 kwa ajili ya miss Tanzania,nadhani kama kuna uhamasishaji kuhusu ili mambo yatawezekana.
Huku nilipo watu na makampuni mbalimbali yanatoa sana kwa jamii zinazowazunguka.Tuanze na hili,wanasiasa waelimishwe na media itumike sana kushikia bango suala hili.
Naomba kuwakilisha,
Mdau-Houston,
Texas.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Namshukuru sana mdau wa Houston, ni wazo zuri na linatekelezeka. Binafsi naona tatizo la kuwa na madiwani mbumbumbu limesababishwa na sisi jamii kwa kuwa tuliwachagua kwa kura zetu. Uchaguzi ujao tubadilike, tujitokeze kwa wingi kuwania nafasi hizo na kuchagua watu watakaoleta msukumo chanya katika kubadilisha mazingira yetu. Madiwani wasioenda shule, hawana upeo, hawajui nini maana ya bustani na wanagombania kugawa maeneo ya wazi, tutarajie nini? Tunavuna tulichopanda.

    ReplyDelete
  2. Hilo mbona linawezekana na nadhani pale Moshi kuna eneo linatunzwa na Kampuni moja ya IPP kama sijakosea. Ni ubunifu tu viongozi wetu. Tatizo la Tanzania viongozi wengi hawana malengo ya kazi (pango kazi)na ndiyo maana kila siku wanakuwa watu wa kuzima moto tu na kufanya viongozi wa juu wafikiri kwa ajili ya maeneo yao. Nawaomba wananchi wenzangu wakati wa uchaguzi tuchague viongozi kwa kuangalia mpango kazi wa kiongozi kwa ajili ya eneo atakaloliongoza na siyo ilani ya chama chake pekee kwani ilani ya chama ni jumla sana na mara nyingi hailezi mikakati ya kufikia malengo

    ReplyDelete
  3. Nimearifiwa kuwa Mkuu wa Wilaya Ilala kwa kushirikiana na ofisi ya Makamu wa Rais na kurugenzi ya mazingira watawakutanisha wadau kama hao aliowataja annon wa saa 11.52 hapo juu, ili kufanikisha hilo wazo kwa nia ya kuwa na a green city angalau maeneo ya Ilala. Ni kweli kuwategemea madiwani hao wasiokuwa na upeo ni kazi ya bure. Mwakani wasomi tujitokeze kugombea udiwani ili tuliosoma tuchaguliwe. La sivyo ni kuwa na mfumo tofauti wa jiji la dar au wizara ya jiji la daressalaam.

    ReplyDelete
  4. Dah!
    Sijui wadau tuanzie wapi, kwa maana kuna mambo mengi ambayo kinadharia yanawezekana, na yanafanyika katika jamii za wenzetu, lakini kwetu hayawezekani kabisa.
    Na hili ni mojawapo.f
    Si nia yangu huivunja moyo jamii yangu iliyonilea na kunisaidia kuwa hivi nilivyo, lakini ukweli ni kwamba tukubali wadau kuwa tuna kazi pevu ya kuelimishana hadi tuweze kuwa na mwelekeo. Bahati mbaya tumekosa uoni au niseme upeo. Na hata kwa mfano mradi huu ukibinafsishwa, bado tuna vikwazo kibaaao vutavyourudisha nyuma, urasimu, rushwa, miundombinu na vingine vingi.
    Kwa kifupi jamii yetu imejaa uvundo, na tuna kazi pevu ya kuiletea mabadiliko.
    Ahsante

    ReplyDelete
  5. Pia watanzania tunatakiwa tubadilike tuwe wapenda usafi tusitupe takataka ovyo, pia beaches/fukwe zetu ziboreshwe, ziwe safi kama kuna uwezekano ziwe zinafagiliwa na jiji kwa kuajiri vibarua wa kufagia, hii kitu inafanyika mahali pengi sana duniani, maeeneo ya Asia ya kusini fukwe zao ufagiliwa kila siku na hupendeza na hata wakati mwingine wanaongeza mchanga pale ulipopunguwa, pia maeneo ya visiwa vya Amerika ya kusini/Caribbean/West Indies Islands pia hufanya hivyo na huvutia sana watalii wa ndani na nje, kupumzisha mwili baada ya kazi za wiki ni muhimu sana kwa afya njema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...