Ndege iliyombeba Rais Hu Jintao wa China na ujumbe wake ikiruka katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo asubuhi baada ya Rais huyo kumaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini Tanzania
JK akimtabulisha mwanaye Khalfan Kikwete(8) kwa Rais Hu Jintao wa China muda mfupi kabla ya Rais huyo kutoa mhadhara katika ukumbi wa Diamond Jubilee leo asubuhi jijini Dar es Salaam.Baadaye Rais huyo aliondoka nchini baada ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu.Rais Hu Jintao amwaga sera ya China kwa Afrika
Na Mwandishi Maalum
RAIS Hu Jintao wa Jamhuri ya Watu wa China, leo, Jumatatu, Februari 16, 2009, ametangaza Sera Mpya ya China kwa Afrika ikiwamo Tanzania, ikiwa ni kilele cha ziara yake ya siku tatu yenye mafanikio makubwa katika Tanzania.
RAIS Hu Jintao wa Jamhuri ya Watu wa China, leo, Jumatatu, Februari 16, 2009, ametangaza Sera Mpya ya China kwa Afrika ikiwamo Tanzania, ikiwa ni kilele cha ziara yake ya siku tatu yenye mafanikio makubwa katika Tanzania.
Rais Jintao ametangaza Sera hiyo katika hotuba muhimu aliyoitoa mbele ya viongozi wa Serikali za Tanzania na China, wanasiasa, wanafunzi wa sekondari na vyuo vikuu, wafanyabiashara na wawakilishi wa jumuia ya Wachina katika Tanzania kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee mjini Dar Es Salaam.
Akitangaza Sera hiyo mpya ya China kwa Afrika ikiwamo Tanzania, Rais huyo ameimwagia sifa nyingi Tanzania, akipongeza uhusiano kati ya Tanzania na China, uhusiano ambao umedumishwa na kuimarishwa kwa miaka 45 iliyopitwa.
Akizungumza mbele ya mwenyeji wake, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye amemtambulisha mgeni wake kwa hadhara hiyo, Rais Jintao amesema: “Tanzania ni asili ya Binadamu, kisiwa cha amani katika Afrika, mfano usiokuwa na kifani wa uhusiano kati ya China na Afrika, na mfano halisi wa uhusiano kati ya nchi zinazoendelea za Kusini.”
“Kama isemavyo methali ya Kichina, ‘hakuna lolote linaloweza kuwatenga watu wenye shabaha na azma moja, hata milima na bahari haziwezi. Kwa miaka 45 tokea Tanzania na China kuanzisha uhusiano rasmi wa kibalozi wananchi wa nchi hizi mbili wameshirikiana katika mengi. Katika miaka ya 1950 na 1960 tulisimama bega kwa bega kutafuta uhuru.
Watanzania ni marafiki wa kweli, ni marafiki wa kudumu, ni marafiki wa kuaminika, na siku zote tutabakia marafiki na wananchi wa Tanzania na Waafrika wote,” amesema Rais Jintao.
Amesema kuwa katika miaka ya karibuni uhusiano wa Afrika na China umeimarika zaidi kwa kuongezeka kwa mahusiano ya mara kwa mara ya kisiasa, kuongezeka kwa shughuli za uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili, na thamani ya biashara kati ya Afrika na China kufikia kiasi cha dola za Marekani bilioni moja mwaka jana, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya uhusiano kati ya pande hizo.
Ametaja baadhi ya miradi mikubwa ambayo China imegharimia katika Afrika kuwa ni pamoja na ujenzi wa Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) ambayo yanajengwa mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Jintao ametangaza kuwa Sera hiyo mpya ya China kwa Afrika itaongozwa na misingi mikuu sita ambayo ni pamoja na kutaka Afrika na China kuimarisha mshikamano ili kwa pamoja kuweza kukabiliana na changamoto za kiuchumi ambazo zinaikabili dunia kwa sasa.
Katika msingi huu, Rais Jintao ameihakikishia Afrika kuwa nchi hiyo haitapunguza misaada yao kwa Afrika pamoja na hali mbaya ya kiuchumi duniani, akiongoza kuwa, kwa hakika, China itaongeza kiwango cha misaada kwa Afrika, itapanua biashara na Afrika na kuongeza uwekezaji katika bara hilo kwa kadri nafasi inavyoruhusu.
Msingi wa pili, Rais Jintao amesema ni kuongeza kiwango cha kuaminiana na kuimarisha mahusiano ya kisiasa na maelewano ya jadi.
Katika hili, Rais Jintao amesema kuwa China itaendelea kushiriki na kuchangia katika shughuli za kulinda amani katika maeneo mbali mbali ya Afrika yanayohitaji kuungwa mkono kwa namna hiyo.
Rais Jintao amesema kuwa msingi wa tatu ni kuongeza kiwango cha ushirikiano wa utendaji wa kiuchumi na biashara kwa misingi ya nipe nikupe na kwa manufaa ya pande zote mbili.
Amesema katika hili, China itaendelea kuimarisha biashara na Afrika, kutilia maanani mahitaji ya Afrika kwa kadri ya uwezo wake, na kuchukua hatua za upendeleo kuruhusu bidhaa za Afrika kuingizwa katika China.
Rais Jintao amesema kuwa msingi wa nne umuhimu wa kupanuliwa kwa mahusiano kati ya watu wa Afrika na wa China na kuongeza mahusiano ya kiutamaduni baina ya watu wa pande hizo mbili.
Katika hili, Rais Jintao amesisistiza kuwekwa msisitizo maalum maeneo ya utamaduni, elimu, afya, michezo, utalii na maeneo mengine.
Pia amesisitiza haja na hoja ya kujenga mahusiano kati ya vijana na wanawake pamoja na taasisi zisizokuwa za kiserikali, vyombo vya habari na maeneo mengine ya kiutamaduni.
Tano, amesema kuwa nchi za Afrika na China lazima zifanye kazi kwa pamoja na kuongeza ushirikiano katika masuala ya kimataifa.
Amesisitiza kuwa China itaimarisha uhusiano wake na Afrika katika Umoja wa Mataifa, katika Shirika la Biashara Duniani (WTO) na taasisi nyingine za kimataifa.
Rais Jintao pia amesema kuwa chini ya msingi huu, China itashirikiana zaidi na Afrika katika kupambana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa duniani, masuala ya usalama wa chakula, jitihada za kuondoa umasikini na maendeleo kwa jumla.
Msingi wa sita na wa mwisho ni kutaka ongezeko la ushirikiano na kwa pamoja Afrika na China kuendeleza ushirikiano kupitia katika taasisi ya Forum on China-Africa.
Mara baada ya hotuba yake hiyo muhimu, Rais Jintao ameondoka nchini kuelekea Mauritius ikiwa ni nchi yake ya tano na mwisho kuitembelea katika ziara yake ya Afrika.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar Es Salaam, Rais Jintao ameagwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete na maofisa wa Serikali za Tanzania na China.


South African man nabbed in Addis with drugs destined for Tanzania
ReplyDeleteETHIOPIAN security officials on Saturday arrested a South African national with over 70 capsules of suspected narcotics inside his stomach, reportedly destined for Tanzania.
This latest arrest occurred just days after the reported deaths of two Tanzanian nationals who were also found with illegal drug capsules in their stomachs.
The two Tanzanians - Yahya Abdulkadir and Yosuf Said - died over the past fortnight after undergoing medical treatment in an Addis Ababa hospital.
According to Ethiopian police, more than 77 drug capsules were found in the stomach of the South African man who was travelling from Dubai to Tanzania aboard Ethiopian Airlines.
The arrested man is reported to be safe and receiving medical treatment at the Ethiopian Federal Police Hospital.
He is said to have been apprehended at the Bole International Airport in Addis Ababa by members of the Airport Drug Control Division.
’’The individual was admitted to hospital after he was found to have this huge amount of drug capsules inside his stomach. The capsules were taken out of his stomach with medical treatment,’’ a police spokesman said.
Last week, Malaysian police arrested three people, including a Tanzanian national, with narcotics worth more than 500m/-.
Media reports from Kuala Lumpur described the drugs haul as the biggest narcotics police bust in more than three years.
Authorities in Dar es Salaam have said they were unaware of the reported deaths of the two Tanzanians in Addis Ababa.
According to THISDAY finding, possibly hundreds of Tanzanian youths are being recruited by local drug barons to smuggle narcotics to and from the country.
The so-called drug ’mules’ are usually persuaded to swallow often more than a hundred packets containing cocaine and other types of drugs, as a means of escaping grinding poverty.
They are never warned that they could end up in prison, or worse that they would die if just one of the packets burst in their stomachs.
The high-risk enterprise involves swallowing narcotics wrapped in condoms, latex gloves, and the like.
It is estimated that hundreds of Tanzanian couriers are currently involved in drug trafficking activities.
Dar es Salaam-based couriers using the Tanzania-China route often pose as legitimate traders as they carry out their smuggling errands.
source: Thisday.
Mh. JK
ReplyDeleteNakupongeza na nakushukuru kwa uungwana wako wa kuwaalika viongozi wa upinzani katika hafla kama hizo.
Umeonesha siasa ni ushindani wa fikra na hoja na sio fani ya chuki binafsi.
Mungu akubariki na akujaalie hekima zaidi.
Man arrested for smuggling drugs
ReplyDeleteSaturday, 24 January 2009
The first man this year smuggling as much as 1.06 kilograms into Macau was arrested by the Judiciary Police on Thursday, after arriving in the SAR through the Macau International Airport.
The 30 year old man originally from Nigeria confessed to have digested as many as 91 capsules weighing 1.06 kilos of drugs in the Malaysian capital of Kuala Lumpur, a day before getting on a flight to Macau.
Police received a tip-off of the man's arrival and were waiting for him at the airport. According to the police, the man also confessed he would be passing the drugs on to another man originally from Tanzania in exchange for 1,000 US dollars, around 8,000 patacas.
The second man was caught carrying as much as 4,000 US dollars, around 24,000 patacas, and confessed to having come from Hong Kong to collect the drugs.
Police believe the drugs with a street value of more than a million patacas was for sale in Hong Kong.
The number of individuals who have been arrested for smuggling drugs into Macau has reached 17 since October last year alone.
Macau
South Africa
ReplyDeleteSix Nigerians and one Tanzanian national were arrested in Rustenburg for prostitution and drug trafficking on Sunday, North West police said.
Spokesperson Senior Superintendent Tumi Golding said police were involved in a three day crime intelligence operation.
"The men are alleged to bring girls aged between 16 and 25 from all over the country to Rustenburg. They then sell them for money and feed them drugs."
"About R60 000 worth of drugs and three cars were seized during the police raid. Several of the girls have been taken in for questioning," she said.
The seven men are expected to appear in the Rustenburg Magistrates court on Monday on charges of prostitution and drug trafficking - Sapa
www.iolco.za
that is not south african he just hapen to use south africa passport he is man from east or west of africa habari ndo hio
ReplyDeleteMheshimiwa JK sasa amemrithisha na mwanawe tabia mbaya ya kutia mkono mfukoni wakati akisalimiana au kizungumza na watu. hii si tabia nzuri kabisa.
ReplyDeleteamaah hebu toa mkono kwa mufuko kijana au unawaiga taifa starz haha enzi hizo nilivokuwa mtoto hizi ndo zilikuwa zangu kila saa mkono kwa mufuko mgeni akiondoka hehehe nikichapo tu
ReplyDeleteNimeipenda hiyo picha JK ANAONEKANA YUKO PROUD NA MTOTO WAKE ! nA MTOTO KAMA WATOTO WENGINE WA KITANZANIA ANA AIBU KITU AMBACHO SIO KIZURI KWANI LACK OF CONFIDENCE.
ReplyDeleteKwa nini wachina wasitupende kwani tunawasaidia kununua mavifaa yao yaliyopitwa na wakati.Angalia midenge ya jeshi yalivyo ya zamani hariruki mpaka iwe na crew watano kwenye pilots' cabin...Sina uhakika ila mengi yalishaanguka tayari.
ReplyDeleteIt is always wise to be a fanatic but not a fool...!Urafiki gani huu wa kuumizana?
Michuzi,mimi nina maoni tofauti kidogo na hawa wachina.Kama kweli wako serious na sisi wangetusaidia kutujengea hata viwanda viwili au vitatu vya kisasa hapa nchini.Wao wako mbali sana kwenye teknolojia,wangetujengea hata kiwanda cha kuunda ,say,nguo za kisasa au computers,au cha kutengeneza matrekta halafu wakatoa training kwa wanasayansi wetu.Hiyo ungekuwa msaada mkubwa kwani tungekuwa na ajira kwa watanzani.Okay,wametusaidia uwanja wa Taifa,barabara na miundombino kibao.Ila naongelea SEKTA YA VIWANDA.Nchi haiwezi kuendelea bila viwanda.Ni wajanja hawa jamaa,huyu rais anatafuta soko la bidhaa za china Africa.Hakuna kitu hapo.Write it down.
ReplyDeleteninakubaliana na huyo jamaa anayesema hawa wachina wanatafuta soko la kuuza bidhaa zao hapa afrika. ni kwanini hawatusaidii kwenye teknolojia ili na sisi tuendelee mbele. kwanini wanataka kutusaidia kwa vitu vile ambavyo havitatusaidia kuondoa umasikini. hii inamaanisha wanataka tubaki waombaji siku zote. ninishangaa kusoma magazeti yetu ya kisema eti wachina wamemwaga mabilioni tanzania. jamani pesa walizotoa ni $21million. hizi ni pesa kidogo sana. infact watanzania walio nje ya nchi wanapeleka kiasi kikubwa cha pesa nyumbani kuliko hicho. hao jamma hakuna lolote. hii ndio maana nchi kama kenya hawajali na kunyenyekea sana misaada.
ReplyDelete