BWAWA LA MAINI HOOOI JIONI HII!!
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya,
Hivi karibuni umezibania meseji zangu mbili, tafadhali kwa hisani yako hii usiiweke kapuni, ni breking nyuzi hasa!Mzee mzima BWAWA LA MAINI leo ameendeshwa mchakamchaka vibaya mno, na hatimaye kupigwa bao 1 kwa nunge huko katika uwanja wa Watani wa jadi Everton!
Pambano lilikuwa na mvuto wa aina yake, na ziliposalia dakika 15 hivi za muda wa kawaida, kwa sisi wenye macho tukakaa tayari tayari kutoa pole kwa wapenda bwawa la maini, kwani tukaona tu dalili za mtu kuadhirika, pale mchezaji Lucas alipotolewa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kutumia nguvu zaidi ya akili.
Huyo Torres leo alikuwa mrenda mtupu usio hata na chumvi, hakufurukuta kabiiisa kwa Jagielka.Gerrard alikuwa na dakika 15 tu uwanjani, akatulia nje, majeruhi.Sijui jijini Liverpool leo kukoje, wadau wa huko tumegeeni umbea!
Mheshimiwa pole sana, maana kufungwa na mtani wa jadi si unajua kunavyouma?Si bora basi msingemuuza Robbie Keane?Ndio yamekuwa ya mgema hayo, akisifiwa tembo hulitia maji.
Isingekuwa vibaya Mheshimiwa ukafatilia pambano na kuujulisha umma laivu, maana mpambano ulikuwa mkubwa ule, umetikisa hapa Ukerewe kila pembe.Haya, wapenda bwawa la maini sijui mna lipi la kutwambia leo, maana hamshindwi na la kusema nyinyi!
Ahsante,
Mdau Leicester
----------------------------------
Mdau wa Leicester
Asante kwa ujumbe mreeeeeeeeefu na matumizi ya nguvu nyiiiiiiingi katika kuuleta. Ila kumbuka bahari haikauki na maji hupwa na kujaa. Sema usemalo lakini bado tupo
-Michuzi


We Michuzi inamaana hujui tofauti ya bwawa na bahari, hilo lenu ni bwawa la maini, sasa utasemaje bahari haikauki? kwa taarifa yako bwawa hukauka na ndo maana tunakosa umeme mara kwa mara kwa bwawa la mtera kukauka ama kupungua maji.
ReplyDeleteDuh, yap, oh nooooooooo, yap yap yap, ebwanaeeeeeeeeeeeeee, MANUTD EKSIPRESI YUA SELFU!
Kibajaj!!!!!!!!!
watu wanasema bwawa tukifungwa hatuji humu ila mie na wenzangu najuwa tunakuja humu MAnchester united wakifungwa huwa ndio hatuwaoni siku hizi wameenza kutokea tena.
ReplyDeleteUkweli tu huo Turudi kwenye Everton Sio Siri kipigo kile kinauma sana Tena Saaaaaaaaana kimeniuma Sajala nimeendakulala ukitegemea Everton hatunao tena mpaka Msimu ujao mungu akipenda mbali kweli. Huyo Keane katika watu wameeona bora aende mie nimo pia, Keane hafai kabisa Pamoja na Lucas, Keane Wanasema hajapata nafasi nafasi gani apewe? ukiniambia mtu hajapewa nafasi Liverpoolfc ni Babel huyo ndio anatakiwa kuwa mbele kule na Torres, Benitez kachemsha kutoleta Winger wa Kulia. Najuwa watu watasemakuhusu SG kuumia ndio Mwisho wa LFC. Steven Gerrard kweli ni muokozi wa Liverpool ila si anayechezesha Liverpool anayechezesha ni Alonso, Steven Gerrard yeye anaifanya timu isikikate Tamaa kuwapa wenzake nguvu Ambayo ndio nasema Man U wanatuzidi hapo wachezaji wao wamekaa sana kwenye Timu na kuwa na HAsira na Uchungu na timu Liverpool ni wachache ni Reina,Carra,Srktel,Alonso na Torres BAsi Kuyt sababu anajituma LAzima timu iwe na machungu ya ushindi Liverpool siioni Kushinda ubingwa ni wa Man u ila tutaenda hivyohivyo kiubishi mie simlaumu sana Benitez na laumu wachezaji. Benitez kweli anakosea Ubadilishaji ila Liverpool Bila benitez sioni. na watu wawache kumlaumu Benitez kuhusu Keane.
Liverpoolfc Machungu ya Everton tunakuja kuwamalizia Man U, Man U na Chelsea zinajulikana Timu ya GB wengi Liverpoolfc isingekuwa na SG ingezidi kupondwa na Media wanamuonea tu Benitez. ila nawapa Man U heshima yao Arsenal na Chelsea wao utumbo tu. Bosingwa anaachiwa vipi yule?. Lampard angekuwa Mgeni sio muengereza naye asingeachiwa, ndomana SG hakupewa Red.
Michuzi na wenzako wa LooserFool polen sana.
ReplyDeleteIn fwakiti ze gemu waz so nice kwa kweli,esipeshiali pale alipoumia Gerrard maana Uwanja ulifurahia kujua kuwa huyo ndio alikuwa mwiba kwao.hata hivyo ilionekana kweli maana liver walicheza vibaya na kuonyesha kuwa Gerrard iz the injini ofu ze timu.
Poleni sana na ndo the Game hiyo.sasa Premier na Champs league mtaweza kweli kuchukua??
MKONO MTUPU HAULABWI JAMANI oooh,mnatoka pakavu tena kama msimu muliopita.
Everton Hoyeeee,jamaa wamebana kweli mechi 5 zilizopita,Droo 2 na Liver,Droo na Arsenal,Kashinda Jana isipokuwa Man u tuu alishindwa kiduuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuchu