mwimbaji wa nyimbo za harakati na injili vicky kamata akighani wakati wa sherehe hizo
msanii frank mfalila akifanya vituzzz vyake
mdau akinunua chupa ya kilaji katika mnada wa kuchangisha pesa kutunisha mfuko wa tawi

picha ya pamoja ya meza kuu na wasanii waliotumbuiza
wadau wakiserebuka
ukumbi ukifurika wakereketwa
ccm juu!
sebene la nguvu lilichapwa
Maadhimisho ya miaka 32 tangu kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika London UK
tarehe 07/02/2009 yalifana sana na kuhudhuriwa na Watanzania pamoja na
wageni wa Mataifa mbalimbali.
Katika Sherehe hiyo, walikuwepo wasanii
wengi kama Francia Chengula kutoka Tanzania, Arua Boi kutoka Uganda,
Frank Mfalila kutoka Tanzania, Vicky Kamata kutoka Tanzania. Live Band
ilitumbuiza Wageni akiwemo Mgeni Rasmi ambae ni Mlezi wa Tawi la CCM
London UK Ndugu Shariff Maajar.
Ndugu Maajar aliwashukuru wageni wote
kwa kuhudhuria na pia aliwashukuru waandishi wa habari na Viongozi wa
Tawi na Mashina ya CCM London UK kwa kuweza kuandaa shughuli hii
muhimu.
Pia Ndugu Maajar alijitolea Vinywaji ambavyo vilinadiwa ili kusaidia
mfuko wa Chama Cha Mapinduzi London UK, ambapo zaidi ya paundi mia
tatu £300 zilipatikana na kwenda kwenye mfuko wa CCM London UK.

Katika sherehe hizo Katibu wa Tawi la CCM London UK, Ndugu Susan Mzee
aliomba dakika moja ya utulivu ya kumuombea Mtanzania mwenzetu Bi
Laura Dausen Munis-Mesaque aliyefariki dunia tarehe 02/02/2009 huko
mjini London.
Katibu wa Tawi aliwashukuru wageni wote waalikwa kwa
ushirikiano wao katika kujumuika kwa pamoja kusheherekea sherehe hizo
za kuzaliwa kwa CCM, Katibu wa Tawi pia aliunga mkono na kumpongeza
Mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa hatua
zote alizochukua katika kushughulikia sakata la watu waliochota fedha
Benki Kuu (BOT) kinyume cha sheria na kuahidi kuwa CCM London UK
itahakikisha kuwa hakutakuwa na Viongozi ambao watatumia nafasi zao
kwa manufaa yao wenyewe.

Pia Mwenyekiti wa Tawi la CCM London Ndugu Maina Owino aliunga mkono
kupinga mauaji ya Albino Tanzania, na pia kuwahimiza Watanzania
watilie mkazo kuezeka Tanzania kwenye sekta ya Kilimo ili kuendeleza
Kilimo nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Tumefurahishwa na sherehe inaonekana ilikuwa nzuri sana lakini katika maelezo pamekosekana historia kidogo kuzaliwa kwake na waasisi wake walikuwa ni viongozi gani wengi hatulielewe wasisi wake wakuu ni akina nani baada ya mwalimu tunaomba maelezo zaidi

    ReplyDelete
  2. Sasa jamani, mnada wote huo paundi 300 tu? au imekosewa kuandikwa?

    ReplyDelete
  3. Upumbavu mtupu, leo ndio nimeamini watu wa UK asilimia kubwa wana akili mgando, hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu ambaye anaweza kuhudhuria sherehe za CCM na kushangilia uchafu wa Kifisadi unaofanywa na hiki chama.

    Michuzi najua hutotoa hii comment kutokana na wewe kuwa ni kada na mpambe mkubwa wa hiki chama. Lakini Message Sent.

    ReplyDelete
  4. Nawaona vijana wa Kawele Mutimwana a.k.a fingerprinter (ana aina ya pekee ya upigaji gitaa)ndani ya bendi ya Congolese& Tanzanians makazi ya East London, Uingereza wakishambulia jukwaa kwa sebene, Kweli 'Kwenu Ni Kwenu Tu' wimbo wa Kawele akikumbuka Bongo.

    Pichani kulia namuona mtoto ya Kinondoni Moses, zamani alikuwa Muungano Group viwanja vya Vijana Social Club Kinondoni, akiimba jukwaani na wenzake, jamaa huyu pia mkali kwa acrobatics, Tupatupa wa Muungano (Mzee Small& Tupatupa) mnatukumbusha nyumbani.

    ReplyDelete
  5. kaka michuzi inabidi uweke sherehe zilizofanyika Houston maana kuna watu walisema watawatumia immigration wawafate, tupe data kaka

    ReplyDelete
  6. Ish! Vicky Kamata na nyimbo za injili tangu lini?Taratibu jamani!

    ReplyDelete
  7. Ndugu zangu Watanzania na wanaopigania haki na usawa,lazima tukubali ya kwamba kulalamika kwetu hakutasaidia kama hatutaunganisha nguvu zetu.Sawa C.C.M WAMEBORONGA,Je Wapinzani tuko tayari kupata mtu anayekubalika na vyama vyote ili asimamishwe kupambana na C.C.M?
    Mabadilko yote yanataka watu wajitoe na kinachosumbua ni umaskini,ufinyu wa mawazo,ubinafsi na kukosa ushirikiano.Tukubali udhaifu ndipo tutashinda,tumekuwa adui wa maendeleo bila kujua.

    ReplyDelete
  8. Wadau naomba mnisaidie, kama mtu anajua kuwa chama cha Labour, au conservative party. (Vyama vya siasa Uingereza). Vina matawi yao hapa Tanzania, naomba anifahamishe ofisi zao zilipo, nina shida muhimu sana. Au kama vya UK havipo hata kama vipo vile vya US kama Democrat na Republican, tafadhali nifahamisheni ndugu zangu.
    Mdau
    Dar

    ReplyDelete
  9. Jamani, kwa uoni wangu mdogo,mnapokuwa nje ondoeni tofauti za kivyama. Lengo liwe moja kuijenga Tanzania moja. Sasa mko nje, mimi CCM, mimi CUF, je miye nisiye na chama nitasemaje?
    Jingine viongozi wa serikali mnapotembelea maeneo, na nia kikuhutubia wananchi, lakini nashangaa, mambo ya chama yanaingilia kati, je kama sipendi chama tawala ina maana nisihudhurie? Nafikiri kuwe na mpaka, mambo ya kiserikali ni yakiserikali na mambo ya chama yapewe muda wake, sijui ni sawa/
    m3

    ReplyDelete
  10. hahahahaha hehehehehe wewe Mdau wa Dar hapo Anon wa 8:56AM unaetafuta matawi ya vyama vya UK conservative na Labour huko bongo umenifurahisa sana na Uzushi wako hehehe very clever. Lakini poa yaani when you put it that way, msg delivered kabisa. Na mimi ni mwanachama wa CCM huku tena ni mpenda siasa mno nilichukulia kadi yangu huku huku UK sema for the first time leo ndio mtu (wewe) amepoint out kitu ambacho kimeniingia kwenye bichwa langu na umenifanya nione sense ya hii situation tena bila ya kukashifu wala kutukana mtu asante sana Mungu akubariki na nimekuelewa kiundani,na ninashukuru kwa kunifungua kichwa mana nilikuwa napagawa vilevile na mimi. Na Kuanzia sasa kwa kweli nitakaa na kadi yangu nyumbani bila ya kuhudhuria sherehe zozote za chama Ugenini huku labda nikirudi bongo. In short it makes sense, kwa nini nchi huru or a Sovereign Country with a Democratic Government ikafungue matawi nchi za Ugenini ? Kwani sisi tumekuwa Wakimbizi au Somalia isiyo na Serikali ? Kweli tumepotea sema ndio hivyo its a free world and people can do what they want even if it means making no sense or having no purpose at all. CCM Oyeee Na Kidumu Chama cha Mappinduzi.

    ReplyDelete
  11. I am tired of hearing about the CCM branch in London. It is not my intention to persuade anybody to not belong to CCM.

    I do not belong to any political party, neither do i hate CCM as a political party, but the truth is i hate the hypocrisy that exist among its members, including high ranking figures.

    It should be noted that, there is small group of people with their personal interest,trying to pull others to become members of CCM .To me this sounds silly and shameful as Tanzanians living in London should have been in front line to talk about the true democracy as they live in a highly democratic country. It would have been exciting to hear about Tanzanians living in the UK to discuss about matters of National interests and more importantly to support people like Dk Slaa who is trying to rescue the country from the deadly disease of corruption that includes high ranking figures from CCM.

    However it should be noted that this sort of dirty shit does not include all Tanzanians in London.


    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  12. ukisikia wizi wakimachomacho ndio huo,

    ReplyDelete
  13. The notion behind all this is for a good course! To bring Watanzania in London together, now that we got the exposure of morden politics and all that, may be these folks could actually take advantage of such gatherings to challenge the wannabe future leaders. Regardless of one's political inclination, establishing a dialogue on ongoing issues back home is a way forward. Once in a while such meetings (CCM LONDON) get visits by top officials, I personally thinks we should grab the opportunity to air our corcern. Ofcourse, will they care? But that dont matter that much, small communities like that should groom future leaders, create passion for the country for those soo far away. Well, you see, bureaucrats, individualism 'umaarufu na sifa za kijinga', the same all bull-shit from home wakaleta UK. This should be different, WaTZ waliopo abroad trying to make some sense. It takes some few committed WANANCHI to change a country. Noone is born to do it, and some one gat to start somewhere! This coulda been a good platform, a one you wouldn't necessarily get back home

    ReplyDelete
  14. Two Tanzanian drug traffickers die of overdose in Ethiopia

    By ARGAW ASHINE, NATION CorrespondentPosted Tuesday, February 10 2009 at 19:37

    Addis Ababa, Tuesday

    Two suspected Tanzanian drug traffickers have in the last two weeks died in the Ethiopian capital Addis Ababa of overdose.

    The two, Yahya Abdulkadir and Yosuf Said had been arrested by Ethiopian police after they collapsed while on board two separate Ethiopian airline flights from Tanzania to China and China to Tanzania via Addis Ababa.

    Some of the heroin pellets ingested by the suspects burst in their stomachs resulting in their deaths.

    They collapsed in the air planes and were rushed to different hospitals in Addis Ababa where they were in admitted.

    Hospital sources told the Nation in Addis Ababa that more than 109 drug capsules were found in the stomach of one of the suspected drug traffickers travelling from Tanzania to China on an Ethiopian Airlines plane two weeks ago.

    He died last week after intensive medical care in Addis Ababa.

    Dr Behailu Haile, medical Director of Hayat hospital in Addis said doctors found a bunch of capsules containing around 15 grammes of heroin each in the suspect’s stomach. The other Tanzanian also arrested during his trip from China to Tanzania via Addis Ababa died yesterday while trying to smuggle drug pellets.

    They burst in his stomach.

    Doctors said more than 42 drug capsules were found in his stomach. Seventeen pellets were surgically removed before he died on Monday.

    www.nation.co.ke

    ReplyDelete
  15. matiya
    i have read your comment and to be honest they cannot pass without my comment.I am suprised by your contradictory view when you bully us to support Dr Slaa on his war on the graft.When you look into that picture is not CCM london on the right path?they have never bullied us to join or support them and they might be interested in national affairs hence establishment of the branches abroad.It does not need rocket science to know that these guys are true wananchi's as they spend their meagre time and resources to participate on national or CCM matters whilst living abroad.
    Yes London is one of democracy centres but we cannot leave Tanzania aside.Tanzania democracy is good example of changing african political arena.
    tanzanians abroad have been vocal for long time against anyform of ufisadi back home so am very surprised by your comment that we might be narrow minded!You should never be tired of hearing about CCM in London try to bring some positive ideas which can help to solve main pressing issues like poverty,disease,infrastructure,ignorance.killing of innocent people like albinos and commend CCM under guidance of Kikwete on the war against graft and all the positive things they are doing.
    Ngoko Bhuka Kanoda

    ReplyDelete
  16. HIVI HUU MRADI WA NGUO ZA KIJANI NA NJANO NI WA NANI!

    ReplyDelete
  17. upumbavu mtupu huu watuwengine wakiona hawapati umarufu wanatafuta umaarufu wa kinguvu sasa wameingia na design mpya ya kuendesha magari makubwa da inatia huruma wakati huko afrika hata kibanda hawana na ndugu zao wamechoka sasa wewe wazungu wenyewe wana fedha na magari makubwa wanayaogopa kwasababu insurance yake ni kubwa sasa wewena kazi ya kuosha wazee na ccm itakulipia kodi watuwengine bwana sifa zikikuzidi unatibua upumbavu kweli huu.

    ReplyDelete
  18. Naona watu wameanza kuingilia maisha ya watu na siyo Chama. All this ni wivu wa watu wchache against wapenda maendeleo. Siku zote mpenda maendeleo lazima atapingwa tu. Naona hawa wapinzani wangefurahi sana kama Hii CCM ingekuwa na watoto wa Vigogo tu na Viongozi wenye kuangalia maslahi yao na kuburuza wanachama wake. Watanzania sijui msaidiweje. Huyo Dr Slaa mwenyewe CV yake inasema alikuwa Katibu wa CCM huko Itali miaka ya nyuma, leo mnamtukuza. CUF walishafungua Tawi huku 1995, hamsemi chochote. Hebu tuache personal issues za watu mara kuendesha magari, mara sijui nini, kwani mtu anakula kwako? Ongeleeni mambo ya kimsingi kama Hawa Viongozi ni kweli wanasimamia kile walichoahidi etc na sio kuangalia huyu Kiongozi kavaa nini, anafanya kazi gani na anakula wapi.

    Hebu tuelimikeni kidogo, maana hizi porojo hazitupeleki pooote. Kama siyo Mwana CCM, kajiunge na Tanzania Association na uache kupiga makelele.

    ReplyDelete
  19. KWA ANONY HAPO JUU. HUJAELEWEKA! HAPA TATIZO NI MAGARI MAKUBWA AU JINSI WALIVYOYAPATA NA KUYA'MAINTAIN'! KAMA WAMEVUJA JASHO KWA NJIA YOYOTE HALALI BASI WANASTAHILI KUTUMIA MAPATO YAO KWA JINSI WANAVYOPENDA. KAMA WAMECHURUZISHA ISIVYOHALALI BASI HAPO UNA 'ISSUE'! NA USINIAMBIE KUHUSU WAZUNGU, WAO SIYO 'STANDARD MEASURE' YA JINSI YA BINADAMU NA MATUMIZI HALALI YA VIPATO VYAO! WENGI WAO WANAENDESHA 'ANTIQUE' WANAYAITA 'CLASSIC' ILI KUKWEPA KULIPA ROAD TAX! PETA MWANANGU KAMA UNA NAFASI YA 'HUMMER' WE UNGURUMISHA TU! SASA WOTE TUKIENDESHA ROVER NA KIWANDA KILISHAKUFA NANI ATAENDESHA HAYO MA'LINCOLN' NA MA'FORD F150'?

    ReplyDelete
  20. Ningefurahi iwapo hao wana-CCM wangenielimisha kuhusu duku duku zangu ambazo nimeezieleza hapa.

    ReplyDelete
  21. Kwa kukusaidia tu wewe mwenye dukuduku na Matawi ya nje kama yataleta mvurugano. Ngoja na mimi nikuulize swali. Tangu CCM imefungua Matawi ya nje, ni miaka miwili imepita sasa. Naomba unipe evidence ni wapi wana CCM wameleta mvurugano hasa katika kipindi hiki cha matatizo nyumbani. Nipe ufafanuzi ni jinsi gani wana CCM wanaharibu amani na jinsi gani wanawabagua wasio Wanachama. Watanzania tumesahau Demokrasia ya mtu jamani. Kila mtu anayo haki ya kufuata kile anachokipenda awe ndani au nje ya nchi. Kwani ni wapi wana CCM wamesema wao sio Watanzania. Na kama navyoelewa ni kuwa Wana CCM ndiyo waliokuwa mstari wa mbele kuunganisha Watanzania wote kwenye shida na raha.
    CCM ni Chama Tawala. Mbona hawa wana CUF na wengineo hamwahujumu kwa kuunga mkono hivyo Vyama? Tatizo ni nini? Kama unachukia CCM kwa matatizo yake usichukie wanachamawake, kemea maovu, kama Wana CCM hapa wanavyofanya pia. Yote hii ya kuanzisha Matawi ni katika kutafuta better CCM for the benefit of all Tanzanians.
    CCM inaongoza Watanzania kule nyumbani, sasa kuna tatizo gani kuwa mwanachama wake? Wote tusipokuwa na Chama nani atachukua nchi??? Lazima kuwe na chama ili Kiongozi apatikane. Kuwahujumu wana CCM walio nje eti wasipractice uanachama wao ni kuwanyima haki yao ya kimsingi kabisa.
    Angalia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lina vyama mbalimbali lakini nia yao ni moja, kujenga nchi, kwa nini sisi wa nje tusiige mfano wao?

    Nadhani nimekujibu swali lako

    ReplyDelete
  22. Kwa wasomaji wa blogu yetu hii, napenda kusema kuwa huwa ninajitambulisha kwa jina, kwa heshima kwenu, mjue ni nani anayeongea. Sielewi kwa nini nisijitambulishe. Pamoja na duku duku nilizotoa katika makala niliyotaja hapo juu, nawaombeni, kwa nia njema, mpitie pia makala hii hapa na nitashukuru kuelimishwa zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...