CHAMA CHA MAPINDUZI

TAWI LA LONDON

SHEREHE YA KUZALIWA KWA

Chama Cha Mapinduzi (CCM)


Wanachama Wote - C C M
Wakereketwa Wote - C C M
Watanzania Wote
Tarehe: 07/02/2009 Saa: 12 jioni Hadi Saa 5 usiku

WAPI:
115 Hertford Road
Edmonton
London
N9 7EN

Watanzania ambao wangependa kujiandikisha Uanachama wa CCM, mnaombwa kuleta picha zenu za passport size mbili na paundi kumi na tano (paundi tatu kwa kadi, halafu paundi kumi na mbili kwa ada ya uanachama ya mwaka mzima).

Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na:
Tinno Msei - 07949000736
Wencheslous Ikumla- 07825253375
Moses Katega - 07728616029
Wote Mnakaribishwa – Kutakuwa na Vinywaji, Vitafunio, Live Band, na mengineyo Baada ya Shughuli Zote.
Kiingilio – BURE!!!

-- Susan Mzee
Katibu wa Tawi
CCM - London
Uingereza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hivi na baridi yote hii, ma-barafu yaliyoyolala barabarani, kigugumizi cha hali ya uchumi, na mambo mengine yote, kweli niache shifti zangu za kubeba ma-box nije kwenye kuzaliwa kwa CCM!!.

    Inanishangaza sana kuona watu wanapoteza mudakwa ajili ya kuja kusherehekea kuzaliwa kwa chama ambacho umri wake ni mkubwa zaidi yahao wanaoitisha hafla yenyewe.....

    ReplyDelete
  2. CCM Oyee. Nimeshaandaa shati langu la Kijani safi kabisa. Hii sherehe niliimiss mwaka jana nilisikia ilifana sana. Nyie wabebe mabox ambao hamna weekends off mnaweza kubaki kwenye shift, sisi tunaopenda kujichanganya na wenzetu tuende huko tukaangalie mambo yanavyokwenda. Jamani hii ni Sherehe siyo Kikao wala Semina na ni bure . Hongereni wana CCM kwa hili kwa kweli mnajitahidi kwa kuhamasisha Watanzania wote na hamna ubaguzi nani aje nani asije.

    CCM Oyee

    ReplyDelete
  3. Nawashauri mtafute njia nyingine ya kuwaunganisha Watanzania UK badala ya kuwagawa kwa gharama ya kujipendekeza kwa viongozi wa Chama na Serikali ya Tanzania. Hacheni unafiki,hii haiwezi kuwasaidia Watanzania kwa namna yoyote!!!

    ReplyDelete
  4. Huu wimbo CCM, ni kejeli kwetu watanzania tunaoishi Uingereza.

    Kama kuna haja ya kuwa na matawi ya CCM hapa Mama [Great Britain], kwanini serikali haitaki kuruhusu tushiriki kupiga kura za uchaguzi wa rais na wabunge?

    Lakini pia, mtu wajiuliza swali.Hivi hizi harakati za wana CCM wa Uingereza ni kwa manufaa ya nani?

    Ningeunga mkono kama zingeanzishwa charity za kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mashuleni, ujenzi wa shule na tiba kwa wagonjwa kule nyumbani Tanzania.Lakini hii kelele ya CCM ni kupotezeana muda, after all CCM haitakufa kwa kukosa wanachama London.

    ReplyDelete
  5. ccm london ni mbinu za kujipendekeza kwa viongozi......

    na matawi yote ya ccm uingereza yapo kinyume na sheria kwa ajili wanatakiwa wapate kibali cha kufungua tawi la siasa za tz ndani ya uingereza (where is the legality?). hata marekani ambao ni maswaiba hawana matawi kila mji kama nyinyi mlivyo.... wao wana umoja ambao ni email tu na sio matawi kila mji ambayo hayana umuhimu wowote.

    ReplyDelete
  6. NAONA MTU YA UK INA MDA MZURI MCHAFU YAANI KWELI MNAPATA MUDA WA KUFANYA HAYO MAMBO?HERI NENDE STRIP CLUB

    ReplyDelete
  7. CCM chama kizuri sana,kadi ninayo.Leo tarehe 5 tunatimiza miaka 32!Hapa TZ pamepooza kweli hakuna shamrashamra kama zamani bwana.

    ReplyDelete
  8. watz bwana eti ccm UK ni kujipendekeza kwa viongozi kwani kuna tatizo gani kujipendekeza?we kama hutaki kujipendekeza endelea na mbinu zako zingine sio lazima uandike humu.kwani hao viongozi wa sasa wa ccm huko tz walijipendekeza kwa nani?

    ReplyDelete
  9. kama nyumbani sherehe imepooza iweje leo inje ya nchi ambapo chama akijazaliwa ipendeze msitupotezehe muda acheni keherehere chenu kama mna inaipenda kwanini msiende kusherekea nyumbani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...