CHAMA CHA MAPINDUZI
TAWI LA MAREKANI
Linapenda kuwakaribisha Wanachama,
Wakereketwa na Watanzania wote popote pale mlipo
katika sherehe za kuadhimisha miaka 32ya
kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
TAWI LA MAREKANI
Linapenda kuwakaribisha Wanachama,
Wakereketwa na Watanzania wote popote pale mlipo
katika sherehe za kuadhimisha miaka 32ya
kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Zitakazofanyika
Houston - Texas,
siku ya Jumamosi tarehe 07 mwezi wa 02 saa Mbili kamili usiku,
katika ukumbi wa Safari.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na;
Zainab Janguo: 832 206 6277
Miraji Malewa: 832 741 4452
Michael Ndejembi. 713 384 4567.
Wote mnakaribishwa: Vinywaji, Vyakula na muziki bure!
siku ya Jumamosi tarehe 07 mwezi wa 02 saa Mbili kamili usiku,
katika ukumbi wa Safari.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na;
Zainab Janguo: 832 206 6277
Miraji Malewa: 832 741 4452
Michael Ndejembi. 713 384 4567.
Wote mnakaribishwa: Vinywaji, Vyakula na muziki bure!
Zainab Janguo,
Katibu Mwenezi,
CCM-Marekani.


Sasa nakubaliana na wale waliosema saa nyingine mapinduzi ya kijeshi ni muhimu.
ReplyDeleteWatoto wa mafisadi vinganganizi kama nini. Wazee wao wamekula nchi mpaka wamechoka na wao kupewa maisha mazuri lakini bado haitoshi ni lazima na wao wale kivyao. Janguo familia nzima imekuwapo US hakuna hata mmoja aliyekuwa na uwezo hata wa kufaulu kuingia chuo wanafurahia matunda ya baba zao kuwa na nafasi na connections kubwa serekalini. Wanaoumia kusomea TZ ni watoto wa walala hoi wenye uwezo zaidi kielimu lakini ndiyo hivyo masikini. Na ndivyo hivyo wanavyofanya mafisadi kama ni Balali, Chege au wengineo wanahitaji hizi connections na accounts ili kuweza weka mahela yao. Nchi yoote imeliwa kama ni Kiwira Coal Mine, Mramba na mwenzake, EPA, Tanesco, Zombe na mengineyo mengi ambayo yanahitaji kusafishwa.
ReplyDeleteCCM ina pesa hizo za kuchota na ina uwezo wa kutumia watu kama Michael Ndejembi kujipenyeza inapotaka. Naomba watanzania wenzangu wa USA tuungane kuweka stop kwa huu ujinga wa wachache kula nchi.
same crap different day!!
ReplyDeleteD_money
hahahaha ebola naona imefika mpaka H-Town sasa!
ReplyDeleteNyie kina Janguo na Ndejembi mnaweza kutueleza kuhusu hilo tawi la marekani ya wapi? Nijuavyo mimi kuna majimbo 50 na hii ndio mara ya kwanza kusikia TAWI LA CCM Marekani. Au ndio MAPROMOOOO?
ReplyDeleteLazima niwapigie simu U.S. Immigration and Customs Enforcement (ICE), kwa yeyote atakayetokea kwenye hafla hiyo na hana makaratasi atakiona cha mtema kuni, na kwa wale wengine wote watakaotokea kwenye hiyo sherehe yao uchwara ambao wanajua walipata makaratasi kwa kuoa ndoa feki nanyi nawatahadharisha kabisa, tusionane wabaya and I MEAN IT. Tumeshasema hatuitaki CCM hapa MAREKANI, iishie huko huko kwa WAPORIPORI wa UK. Sasa hivi napigia watu wengine simu ili nao wapige simu ICE. Hii ni tahadhari nawapa mapema wote mnaotaka kuhudhuria huo ujinga
ReplyDeleteTanzania ya pili Afrika kwa kuwa na wanawake wengi wenye VVU wanaojifungua
ReplyDelete2009-02-02 17:18:40
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya wanawake wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), wanaojifungua kila mwaka.
Hayo yamesemwa na Naibu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Hasmik Egian, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la makala zinazohusu Mpango wa Kuzuia Maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (PMTCT).
Shindano hilo liliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Ukimwi Nchini (AJAAT) na kufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).
Bi. Hasmik amefafanua kuwa nchi ya Afrika Kusini ndio inayoshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanawake wenye VVU wanaojifungua kila mwaka.
``Idadi hii ni kubwa mno na ndio maana UNICEF imeamua kusaidia katika jitihada zinazolenga kupunguza maambukizi mapya kwa kutumia kila njia ikiwemo kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Tanzania,``akasema kabla ya kuongeza:
``Bila ya kuwa na mpango wa kupunguza maambukizi, inakadiriwa kila mwaka watoto 45,000 watazaliwa wakiwa wameambukizwa VVU,``.
Akizungumzia kuhusiana na huduma ya PMTCT, amesema huduma hiyo inafika katika vituo vya afya karibu kwa asilimia 50 na kwamba ni asilimia 43 tu ya wanawake ndio waliopata huduma hiyo katika kipindi cha mwaka jana.
Pia akasema ni asilimia 33 ya idadi ya wanawake wajawazito 127,000 wanaoishi na VVU tu walipata dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi mwaka jana.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa AJAAT, Bw. Saimon Kivamwo amesema waandishi wa habari 15 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wameibuka washindi katika shindano hilo.
Hata hivyo akasema katika mchujo wa awali waligundua kuwa baadhi ya waandishi waliwasilisha makala zinazohusiana na mambo mengine ya afya na hivyo kubakia na makala 20 tu.
Amesema shindano hilo lilianza Septemba mwaka jana na lilitakiwa kumalizika Desemba mwaka jana, lakini walilazimika kuongeza muda ili kutoa nafasi kwa waandishi wengi zaidi kushiriki katika shindano hilo.
``Lengo ni kuwapa motisha waandishi kuandika habari za kina kuhusu mpango huu na hivyo kuwakinga watoto na maambukizi ya VVU kutoka kwa mama,``akasema Bw. Kivamwo
hhhhhaaaa hilo tawi mlilifungua lini nyie wezi.....naona mlifungua chini ya uvungu wa kitanda ati tawi la ccm marekani....ni nyie wenyewe tu mnalolijua.....sigh......
ReplyDeleteMbona hayo majina yaliyotajwa yamekaa kifisadifisadi? Do you think watu wenye akili zao wanaweza kusikiliza wito wa kwenda kusikiliza hotuba za watu wenye damu za kifisadi? Oh my Goodness!!!
ReplyDeletejamani hamjalazimwishwa kwenda so kama hupendi usiende acheni maneno yasiyo na maana
ReplyDeleteGavana Balali aliiba, Kukimbilia US Kufariki na kuzikwa Marekani, yaani mwili wake wala hukuonekana, huo ndio ufisadi uliokomaa.
ReplyDeleteJamani kama hatutaki kwenda musiende..Kama nyie munaipenda Tanzania mungeenda nyumbani kufanya mambo sio munabana hapa hapa marekani...munasema kina Janguo hawajasoma uzushi mtupo watoto wana degree na wengine wanachukuwa Masters...Nyie ma HATER'S munayenu bwana...we ukiangalia umezaliwa ndani ya CCM mpaka umekuja Marekani CCM ilikuwa inatawala...!!! watu tunatia maguu kwenye sherehe hizo za CCM kama kawa unataka kumtisha nani bwana??? Mkubwa hatishiwi NYAU...we mwenyewe unaishia kimchongo muuza mapupu wewe!!! Ebwana mimi kama Mdau wa H-TOWN jumamosi kama kawa tunasherekea kwa fujo kama wachawi munayenu mukalale...!!!WATOTO WA DOGO WANGA MUNA BANA MPAKA KIVULI...!!!
ReplyDeleteHivi kuna mtu kasikia US au UK wamefungua tawi la chama cha siasa Tanzania au kokote duniani? Nyie watanzania mnaofungua matawi nchi za watu mna agenda gani na ni kwanini? Tunaomba mtufafanulie tafadhali
ReplyDeleteWote mnakaribishwa: Vinywaji, Vyakula na muziki bure!
ReplyDeleteTHERE IS NO SUCH A THING LIKE FREE LUNCH IN AMERICA!..............
AND WITH THIS GREAT RECESSION.....JEEZE
FYI, Nime-confirm na watu wa ICE. Watatia timu ukumbini kukamata mtu zisizo na karatasi za kueleweka. Halafu mrudishwe nyumbani then tuone jinsi SISIEM itakavyowasaidia kuwapatia maisha bora kwenu nyote... Michuzi, tega sikio kesho upate update za watu waliokamatwa mkutanoni.
ReplyDeleteMMECHAGULIWA NA NANI NYINYI WEZI WAKUBWA???? MGOMO MPAKA UCHAGUZI UFANYIKE.
ReplyDeleteheeeee heeee ati wana degree na master....walizifanyia jela?
ReplyDelete