kocha wa taifa stars marcio maximo akiwa na meneja wa timu hiyo na mchezaji wa zamani wa taifa stars leonard tasso mukebezi (shoto) na kocha msaidizi ambaye pia alikuwa kipa namba moja wa taifa stars ali bushiri siku moja kabla ya kuelekea ivory coast.


Na Florian Kaijage, Abidjan

Taifa Stars leo inashuka katika dimba la Felix Houphet Boigny jijini hapa kuwakabiri Simba wa Teranga, Senegal katika mchezo wa fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani(Chan) huku ikizungukwa na hisia za kulipa kisasi kwa Taifa Stars.

Mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya pili ikitanguliwa na ya ile ya ufunguzi kati ya wenyeji Ivory Coast na Zambia itachezwa saa moja usiku kwa saa za hapa sawa na saa nne za usiku za Afrika Mashariki.

Ni kisasi kwa hasa kwa Taifa Stars kwa sababu March 24, 2007 Stars ilichapwa mabao 4-0 mjini Dakar wakati wa kampeni za kufuzu kwa fainali za Afrika zilizofanyika 2008 huko Ghana na katika mchezo wa marejeanp jijini Mwanza Stars iliwakosa Senegal kwa kulazimishwa sare ya 1-1 Juni 2 2007 jijini Mwanza.
Nizar Khalfan alifunga bao la dakika ya 17 lakini Demba Ba akaisawazishia Senegal zikisalia dakika 17 mpira kumalizika, mbele ya mashabiki zaidi ya 20,000 akiwemo Rais Jakaaya Kikwete.

Wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza cha Stars walioshiriki michezo hiyo miwili bado wapo kama vile Shadrack Nsajigwa, Salum Swed, Nizar, Haruna Moshi, Athuman Idd Shabaan Nditi, Henry Joseph toufauti na Senegal ambayo wachezaji we ngi wa kikosi cha kwanza wanasakata kandanda barani Ulaya.

Na ifahamike kuwa hicho kipigo cha mabao 4-0 ndicho kikubwa zaidi kwa Stars tangu Maximo aanze kibaru cha kuinoa timu hiyo Agosti 2006.

Hata hivyo Stars inashuka dimbani bila viungo wake wawili Athumani Idd ambaye Maximo anasema hayuko fiti asilimia 100 na Kigi Makasi mwenye kadi mbili za njano huku Godfrey Bonny ambaye alikuwa akisumbuliwa na tumbo akianza, inatarajia kushuka ikiwa na lengo moja tu la kuibuka na ushindi.

Stars ilikuwa ya kwanza kutua katika mji wa Abidjan kwa fainali hizo za kwanza na wachezaji wake wameonesha kuwa na ari ya mchezo hasa kutokana na mazoezi waliyoyafanya wakichekelea hali ya hewa inayofana na ya Dar es salaam kutoka na nyuzi nyoto kufikia sentigrade 29.

Mbrazili Maximo alisema:’kushinda mchezo wa kwanza ni muhimu mno ili kupandisha ari na hamasa ambayo tayari iko juu miongoni mwa wachezaji wangu’.

‘Tanzania sasa inaapanda kufanikiwa kushiriki mashindano makubwa baada ya miaka 29 kieleelzo kuwa nchi iko katika mwelekeo wa kuwa moja ya miamba ya soka sote tinawajibika kuonesha kuwa kufuzu kwetu kwa fainali hizi haikutokea kwa bahati bali kazi kubwa ilifanyika’ alisema Maximo ambaye meci ya leo itakuwa ni 42 kwake kuongoza timu ya Taifa.

Kulingana na mazoezi ambayo yamekuwa yakifanyika tangu timu kuwasili hapa Abidjan ukiondoa wachezaji ambao hawawezi kushiriki mchezo wa leo ni dhahiri kuwa kikosi kitakuwa kama ifuatavyo:

Shaaban Dihile, Nsajigwa, Juma Jabu, Swed, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Geofrey Bonny, Henry Joseph Nizar, Haruna, Jerson Tegete na Mrisho Ngasa.

Mchezaji chipukizi Mwinyi Kazimoto aliyevaa jezi ya Stars kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Zimbabwe anatarajia kuwapo katika benchi la wachezaji wa akiba pamoja na Deo Munishi, Kevin Yondani Nurdin Bakari Mussa Hassan Mgosi, Abdi Kassim na Amir Maftah.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mungu ibariki Tanzania, wabariki wachezaji wetu wacheze kwa moyo wote, wawe makini wanapokuwa na mpira na wanapolinda goli, wabariki makocha wetu waweze kutoa mafunzo ya hekima kipindi chote cha dakika tisini, wabariki waamuzi wa mchezo, wachezeshe kwa haki bila kujali tofauti zozote. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Taifa Stars.

    ReplyDelete
  2. Aaaaaaaaaaaaaa MIMI nilishaga kata tamaa na mambo ya mipira hapo bongo tangu Mzee Ruksa alipo comferm kuwa sisi ni kichwa cha mwendawazimu hivyo hata aje Bekham kufundisha mimi walaaaa siko huko labda BRO MICHU NIFANYIE KANSELINGI

    ReplyDelete
  3. Kila la kheri taifa Stars. Watanzania popote pale tulipo dunia tupo nyuma nyenu kwa kuwa kazi mnayoifanya ina mchango mkubwa sana katika kuitangaza nchi yetu. Ninawaombea mshinde ikiwezekana mechi zote ili mrudi na ushindi nyumbani.

    Mdau
    France

    ReplyDelete
  4. Utabiri wa hakika:
    Taifa Stars 2 Senegal 1
    Stars watatangulia 1 na Senegal kurudisha, lakini kuonyesha ukomavu Stars ita ongeza bao la pili na ushindi ktk kipindi cha pili.

    Mdau
    Njozi za Kweli
    Abijdan.

    ReplyDelete
  5. kila la heri "Staz". Tunawatakia mafanikio mema.

    Mh. Balozi tunaomba update pindi utakapozipata! Nasikia mechi iko live EATV

    ReplyDelete
  6. Mbeba maboski Marekani hapa. Msaada tutani.
    Kuna mtu anajua naweza kuiona vipi hii mechi live au hata delayed, kwenye luninga au streaming online?

    ReplyDelete
  7. Kwa mdau hapo juu. Nadhani tunaweza kuiona mechi live online kupitia websites mbili so far. Ila tatizo moja ni ya kiirabu na nyingine ni kireno. Nimefikia hapo katika kutafuta ila sioni sehemu inayosema bonyeza kwani mie kiarabu na kireno not reachable. Sasa kama kuna mdau anareach hizo lugha aendelee na atupe ufafanuzi. Nazo ni (ART Sport 3) na (TV Mozambique). links are:
    http://www.artonline.tv/sports/SportsPrograms.aspx?ChannelID=92

    http://www.tvm.co.mz/


    Mdau hadji helper.

    ReplyDelete
  8. LEONARD TASSO MUKEBEZI NI WA SIKU NYINGI LAKINI BADO ANAONEKANA KIJANA, LISHE BORA HIYO, SI UNAJUWA TENA BUKOBA KWA MATOKE NA SAMAKI.

    ReplyDelete
  9. heheh kocha wetu mark shimo ana miguu ya kushoto yote kwikwikwikwi asivae bukta noma mark shimoo

    ReplyDelete
  10. mpeni timu ali bush

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...