Mbunge wa Nyamagana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Lawrence Masha
(shoto) akiteta na Mbunge wa Karatu na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mh. Dr.Wilbroad Slaa, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. utazania wanasema:
    masha: wewe mh. slaa nyamaza dili tule wote. mkwanja mkubwa mzee.
    slaa: hapana sikuachii kwa hili.....

    ReplyDelete
  2. Masha dalili ya mvua ni mawingu baba. Umekwisha

    ReplyDelete
  3. halafu picha ya pili masha anasema kama huniachii kweli nitakupiga ngumi...

    ReplyDelete
  4. Eeh taratibu..., siyo baada ya hapo Slaa utuambie kuwa yameisha!!

    ReplyDelete
  5. hahaha lakini hii picha ya chini kama anasema vile (ok )mambo powa nusu kwa nusu mkuu ila hapo juu alikuwa haja kubali unaona hapo anameza mate wewe pesa kitu mbaya hapo wesha kamilisha deal hayo ndo mambo ukila peke yako kibarua kitaota majani hehehehe

    ReplyDelete
  6. This Boy looks very Stubborn just from the direction his finger is pointing!Kaota Mapembe!Kipo anacho jiaminia au siyo!

    ReplyDelete
  7. BRO Michu mimi sina cha zaidi kwani picha inajieleza yenyewe ni aina gani ya mazungumzo yanayoendelea. Ila tu napenda kumpa hongera huyu bwana aliyepiga picha hizi ni picha nzuri sana zipo so clear huyu jamaa anamiliki kamera nzuri sana. Ukiangalia katika blogs zooote picha zenye viwango kama hizi zinahesabika nyingi ni ilimradi picha tu zimejaa ukuungu.
    Mpe hongera zake huyu bwana.
    Mdau

    ReplyDelete
  8. Picha nzuri sana. Pamoja na yaliyosemwa na wachangiaji mimi binafsi hakuna kinochonipa faraja ninapoona kuwa bado kuna waheshimiwa wanaoweza kuvaa suti yetu maridhawa ya kitanzania: simple and comfortable, badala ya kung'ang'ania ile uniform aliyokuwa akieneza bw gwb kama wamisionari walivyokuwa wakieneza injili

    ReplyDelete
  9. Hello Anon at 2;47 Masha is not stubborn ila ana confindence ya kisomi kama aliyo nayo Slaa. Kwa hiyo hapo ngoma draw. Mimi naishangaa serikali kwa nini haimkamati Slaa kukutwa na dokezo nyeti ambalo lilinyofolewa kutoka file la siri. Hivi ni mchezo gani unaochezwa? Mbona sielewi?

    ReplyDelete
  10. Picha ya chini....Dr. Slaa anatafakari bado hajakubali...kama anasema "we gijana usinizuge hapa...."

    ReplyDelete
  11. Walianza kwa kunyoosheana vidole lakini Masha kanyoosha kwa msisitizo zaidi. Picha ya pili Slaa anataka kukimbia maana kidole kimekuwa sumbwi.

    ReplyDelete
  12. hiyo wizara aliyopewa Mh.Masha naona ni very sensitive.Mh huyo nafkiri angefit kama wizara za maliasili na n.k lakini sio hapo.

    ReplyDelete
  13. Wewe Patrick ni kibaraka, unamuabudu Masha wewe. Ana usomi gani? hebu muulize. Ni msomi kwako kama watu wa jamaa fulani humu kwenye blogu wanavyomuona.

    ReplyDelete
  14. wewe patrick wacha wendawazimu
    file la siri ndio nini
    kwa nini mikataba ifanywe siri....
    watu wanatakiwa wajue mkataba umesainiwa kivipi...
    kila nchi kuna wissle blower...
    watu wanauchungu na nchi yao ndio maana wanampa slaa nyeti kwa ajili wanaona inaliwa unazani kila mtu anapenda nchi iliwe

    ReplyDelete
  15. Dk. Slaa hatarini

    2009-02-06 16:18:48
    Na Khalfan Said, Dodoma


    Mbunge wa Karatu (CHADEMA), Dokta Wilbroad Slaa yuko katika mashaka makubwa kufuatia kitendo cha watu wasiofahamika, kuingia kwenye chumba cha hoteli anayoishi mjini hapa na kutegesha mitambo inayosadikiwa kuwa ni ya kunasa mazungumzo yake.

    Taarifa zilizothibitishwa na Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Bw. Salum Msangi zimedai kuwa, jana mishale ya saa 5:00 usiku, kitu kimoja cheusi kilikutwa kwenye chaga ya kitanda cha mbunge huyo wa Karatu.

    Amesema mbunge huyo amefikia kwenye chumba namba 201 kilicho ghorofa ya kwanza ya hoteli ya Fifty Six.

    Licha ya Dk. Slaa, afande Msangi amesema kuwa kifaa kama hicho pia kimekutwa kwenye chaga ya kitanda cha mbunge wa Konde (CUF), Dk.Taarab Ali Taarab, ambaye naye amefikia chumba namba 202 kwenye hoteli hiyo hiyo.

    Gazeti hili ambalo liilifika eneo la tukio kiasi cha dakika 15 baada ya polisi kuwasili mahala hapo, lilikuta maafisa kadhaa wa polisi kutoka kitengo cha upelelezi mkoa wakifanya uchunguzi wao.

    Walionekana wakimhoji Dk. Slaa ambaye alikuwa na wabunge wenzake wa upinzani, wakiwemo Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini), Halima Mdee (Viti Maalum), John Mwera (Tarime) na Grace Kihwelu (Viti Maalum).

    Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dodoma (RCO), Salum Msangi, amesema ni kweli polisi wamekuta kifaa cheusi kikiwa kimenatishwa kwenye chaga chini ya godoro la kitanda cha Dk. Slaa, ndani ya chumba chumba namba 201.

    ``Kifaa hivyo tulikuta kinatoa mwanga mwekundu kama kimulimuli…pia kifaa kama hicho tulikikuta sehemu inayofanana na hiyo kwenye kitanda cha Mheshimiwa Dk.Taarab Ali Taarab (CUF), chumba namba 202,`` alisema.

    Akieleza zaidi tukio hilo, afande Msangi amesema kuwa baada ya kupelekewa taarifa mishale ya saa 5:00 usiku wa Alhamisi, walifika hotelini hapo na kufanya uchunguzi ili kujua kifaa hicho ni cha aina gani.

    ``Hadi sasa bado hatujajua ni kitu gani hasa... lakini uchunguzi wetu wa awali unaonyesha kuwa si bomu,`` akasema.

    ``Tunachukua vitu hivi na tutavipeleka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa uchunguzi zaidi,`` akasema mkuu huyo wa upelelezi.

    Pia aliwaambia waandishi wa habari kuwa hadi wanakamilisha kazi ya uchunguzi na mahojiano kwenye mishale ya 7:45 usiku, hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kwamba uchunguzi zaidi wa polisi utaanza mara moja.

    Katika hatua nyingine, afande Msangi amesema kuwa polisi imechukua chupa yenye mvinyo, ambayo inadaiwa kufikishwa mapokezi na mtu asiyejulikana aliyedai ni mzigo wa Dk. Slaa.

    Amesema juzi, mtu aliyejitambulisha kuwa ni mgeni wa Dk. Slaa, aliacha mzigo huo aliodai kuwa amemletea kama zawadi.

    ``Pia chupa hii yenye mvinyo tumeikuta ikiwa na vijitundu vidogo kwenye mfuniko... tumeichukua na tutaipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili afanye uchunguzi wa kimaabara na kujua kama kulikuwa na kitu chochote cha kudhuru,`` akasema.

    Akizungumzia tukio hilo, Dk. Slaa amesema jana asubuhi wakati akishiriki mkutano wa wabunge na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Beno Ndulu, alipigiwa simu na mtu mmoja, aliyemtahadharisha kuwa kuna kitu kimefungwa ndani ya chumba chake na kwamba akifika chumbani humo, awe makini.

    Hata hivyo, Dk. Slaa anasema hakuipa uzito sana taarifa ya mtu huyo ambaye hakumtaja jina ingawa wanafahamiana na hivyo akaendelea na kikao hicho.

    ``Lakini nilipofika kwenye chumba changu, kabla ya kulala nikaanza kupekua huku na huko... kweli nilikuta kifaa kidogo cheusi kikiwa kimenasishwa kwenye chaga, chini ya godoro. Baada ya kuona hivyo, nilikwenda chumba cha jirani yangu ambako ni kwa Mheshimiwa Dk.Taarab na kumjulisha. Naye kwa tahadhari, akaanza kupekua na akakuta kitu kama hicho,`` akasema.

    Akasema baada ya kuona hivyo, alimpigia simu Katibu wa Bunge, Dk. Kashilila, ili kumjulisha juu ya tukio hilo.

    Akasema kuwa naye (Dk. Kashilila), kwa haraka akaagiza Afisa Usalama wa Bunge kufika eneo hilo .

    ``Baada ya muda walifika polisi na tukawaonyesha... na wao wakachunguza kabla ya kuvinasua vitu hivyo,`` akasema Dk. Slaa mbele ya waandishi wa habari, maafisa wa polisi na wabunge wengine.

    Mbunge huyo ambaye mara kadhaa amesimama kidete kufichua uovu mbalimbali Serikalini, alisema yeye bado yuko imara na hatishiki na hali iliyomkuta, kwani sio mara ya kwanza kukumbwa na mambo yanayoashiria kumtishia maisha.

    Amesema yeye ana imani na jeshi la polisi na ana uhakika kuwa uchunguzi wao, utatoa picha halisi ya kwamba kifaa hicho kiliwekwa kwa malengo gani.

    ``Nilipata kusikia huko nyuma kuwa watu wanaweza kufungiwa vifaa vya kunasa sauti kwa siri, sasa siwezi kujua kama kweli kifaa hiki nacho kiliwekwa kwa malengo hayo,`` akasema mbunge huyo.

    Akielezea kuhusu kutumiwa mvinyo unaodhaniwa kuwa na sumu, mbunge huyo amesema juzi Februari 4, alipotoka bungeni, alifika mapokezi hotelini hapo na kuelezwa na mhudumu kuwa kuna mzigo wake ameletewa na ndugu yake.

    Akasema alipouona na kuufungua ili kujua ni mzigo gani, akakuta ni chupa ya mvinyo, lakini kilichomshangaza ni kukuta chupa hiyo ikiwa na vijitundu vidogo na ndipo hapo akawaambia wahudumu waendelee kuitunza.

    ``Sasa leo nilipokutana na mambo haya, nikawaeleza wahudumu wanipatie na ile chupa ili niwakabidhi polisi kwa sababu vitu hivi vinatia shaka,`` akaongeza.

    Kwa upande wake, mbunge wa Konde, Dk.Taarab Ali Taarab, yeye alisema baada ya kuingia chumbani kwake, kamwe hakuwa na taarifa yoyote juu ya vitu alivyowekewa.

    Akasema alikuja kustuka pale alipogongewa na mbunge mwenzake na kuelezwa juu ya kilichojiri chumbani kwake, hivyo akaamua kuchukua tahadhari kwa kupekua na ndipo alipokuta na yeye kawekewa kifaa kama hicho.

    SOURCE: Alasiri

    ReplyDelete
  16. masha mi nakupendaga....

    ReplyDelete
  17. Jehovah tufikishe salama,,,
    ila nasema ivi hakuna confidential files ya wizi wa aina yoyote kwakweli,acha Slaa apate mavituz yote ayo na siku "akifa" mambo yaanaanikwa hadharani.

    anyway

    ReplyDelete
  18. Dr Slaa, Tarab bugged?

    2009-02-07 12:03:05
    By Lusekelo Philemon, Dodoma

    Unidentified people are alleged to have secretly placed a gadget looking like a tape recorder under the bed used by Karatu MP, Dr. Wilbroad Slaa, at Hotel Fiftysix, here in Dodoma.

    A similar equipment, black in colour, was found under the bed used by Konde legislator on the ticket of CUF, Dr. Ali Tarab Ali.

    Dr. Slaa, a lawmaker with the opposition Chadema, was staying in room number 201 at the hotel, while Dr. Tarab was in room number 202, both on the first floor of the hotel which is very close to the oval chamber of Tanzania `s National Assembly.

    Dr Slaa and then Dr Tarab discovered the equipment under their beds on Thursday night at around 11pm.

    Police confirmed the incident, saying they have taken away the said equipment for thorough investigation of what they termed a rare incident in Tanzania`s political history.

    Regional Criminal Officer (RCO) Salum Msangi, told reporters here that the two gadgets were switched on.

    ``We have taken the two electronic appliances for investigation and we interrogated the two MPs on the matter,`` he said, adding that initial investigations show that the two appliances have nothing to do with bombs.

    The RCO also said so far no one has been arrested in connection with the incident.

    He however said that information technology (IT) experts from police headquarters were expected in Dodoma today for a thorough investigation into the scientific use of the equipment.

    According to Msangi, police have also taken one bottle of wine which was left at the hotel`s reception by an unknown person.

    The reports said that the said person arrived at the hotel carrying the bottle of wine and identified himself as a guest of Dr. Slaa, and sa ying the wine was a gift for the Karatu MP.

    ``We have taken the bottle for further investigation after noting its cover had some small holes punched in it. We are planning to take it to the chief chemist for laboratory tests,`` he said.

    He added that the aim was to establish whether the wine was meant to harm the Chadema MP.

    Dr. Slaa told reporters that while attending the MPs seminar, someone phoned to caution him that there was something strange under his bed.

    ``I didn`t take the issue very seriously, and proceeded with the meeting. Thereafter when I returned to the hotel I decided to make an inspection and found the gadget under my bed,`` he said, declining to mention the name of the person who tipped him.

    He said that he informed his colleague MP, Dr. Tarab and together they also inspected his room and found similar equipment under the bed.

    Dr. Slaa then contacted the Clerk of the National Assembly, Dr Thomas Kashililah and informed him on the matter.

    Kashililah informed security officials and police to take up the issue.

    The Karatu MP has been in the forefront in unearthing different scandals related to grand corruption in the country, such as that of Richmond and Bank of Tanzania (BoT) External Payment Arrears (EPA) scam, among others.

    The MP said he would not be deterred by the incident, pledging that he would continue to unearth evils within the government cycles, without fear.

    The outspoken politician also said he had faith in the police force in working on the matter and revealing the truth.

    On the wine, the MP said on February 4, this year he was told that there was a gift for him at the reception.

    After opening it he found that it was a bottle of wine, but was shocked to see that the cover of the bottle had some small holes punched in it.

    For his part, Konde lawmaker Dr. Tarab, said that he was shocked by the incident.

    The incident was also witnessed by MPs Zitto Kabwe (Kigoma North), Grace Kiwelu (Special Seats), John Mwera (Tarime) and Halima Mdee.

    * SOURCE: Guardian

    ReplyDelete
  19. Perfect Camera Angle...

    MOtoMOto.

    ReplyDelete
  20. This is Absolute Cowardice!An Outspoken Member of Parliament of Dr.Slaa's stature could never be suspected to be a Sabotuer!Yeye siyo mpiga majungu au mtu wa fitna!Angeweza kabisa kubakia kimya bungeni kama angekuwa na tabia hiyo na bado akatimiza alivyokusudia.Lakini ameamua kuwa mkweli na mcha Mungu!Daima Mhalifu ni mtu Mwoga Sana tena sana hata angekuwa na utajiri kiasi gani au madaraka makubwa kiasi gani!Pindi pale anapobainika na ukweli wake kuwekwa hadharani!In every rich there is a crime!Mungu atakulinda Dr.slaa.Kazi uliokwisha ifanya ni kubwa sana,haiwezi kulinganishwa na thamani yoyote ya fedha!Moto uliouwasha kamwe hakuna atakaye weza kuuzima!Time will tell!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...