WHAT DOES THE TANZANIAN’S FUTURE HOLD?
By Charles Mukuru
With much gratitude to those who have expressed their concerns and ideas towards our nation’s direction; I take this opportunity neither competing with the rhetorical skills of Mr. Mashaka nor the business acumen of Dr. Shayo. I rather, would like to pursue a different perspective of what Mr. Mashaka and Dr. Shayo have articulated. I also thank brother Michuzi for his service to each and everyone who loves mtandao, thanks a lot.

Before going further, I have a full comprehension that what I am about to express will be hit from different angles. I welcome constructive ideas, negative and positive. To those who would rather criticize for the sake of criticizing; checking grammar, questioning my level education, even questioning my motive; I know you have nothing to do but criticize. So, go figure.

Much of Mr. Mashaka’s articles have pictured the would be or should have been Tanzania, conveying what ought to be done for our nation to be competitive or rather get out of poverty. Likewise, Dr. Shayo’s ideas capture the same thoughts; giving advices to Tanzanian investors, if we really have them. Without a doubt Mashaka and Shayo deserve a credit, particularly Mr. Mashaka who has written extensively through Michuzi's vehicle. Mashaka’s commitment goes beyond the call and above the duty for his educational ideas.

When discussing the Tanzanian road to economic prosperity; one can not ignore its political environment and the will of its government to implement policies. Without being too harsh to our government, it is clear that what we have in Tanzania is fully muddled. Given the lifespan of the government and its achievement; it is obvious that our future and our children’s future is uncertain..

My point is that not matter how good our policies are, if we do not have good governance nothing will be achieved. Without fair justice system, objective and purposeful parliament, corrupt free leaders, and long run visions we will be running cycles, gazing everywhere for who should take the blame.

Our justice system is questionable, we have vivid examples of people committing crimes and walking free based on how fat is their pocket. Without the rule of law I am not sure how one can attract investors used to equality regardless of their status or how much money they have. At the moment everybody feels like those involved with "ufisadi" are living large; we are told some are still serving in the ruling government. Meanwhile, the ruling party doesn't want to be associated with ufisadi; that ufisadi has nothing to do with the ruling party. I guess the English saying "When one falls in love ignores all the red flag" might explain this.

What about our parliament? This is another instrument that doesn't function to its fullest. Without being disrespectful, I am not sure if some members of the parliament have the intellectual capacity of not only writing a serious bill to be presented to their fellow parliamentarians, or understand the government's bill presented to them. Now, if the legislative body is weak who will regulate our rules of investments, environment, energy, education etc?

Those with the privilege of living in the western world have witnessed time and time again when someone is vying for higher office they lay down their vision for the next sometimes twenty to fifty years. They try to be specific on every vital policy affecting their constituencies such as transportation, education, defense, healthcare etc.. What about our leaders in Tanzania? Do our leaders take into consideration the need of long run policies? Just few days ago, our beloved president Kikwete asked about those days when all schools had same books regardless of what school they went to. Then someone has to wonder: What education policies did you run on Mr. President four years ago?


Granted, Mashaka, Shayo and every Tanzanian patriot, if we really need to have a discussion of where our country is heading; I believe we should start with the basics, In my view education should be ahead of every policy. The kind of education that will produce not only thinkers, but inquisitive, and creative minds.
However, we ought to acknowledge that major reforms are inevitable within our government for the betterment of the majority who are suffering. No matter how good our ideas are; without a springboard to stand on, we can not go anywhere. And, it is clear that you can not build economic prosperity out of political vacuum.


Mungu ibariki Tanzania
Mchangiaji anapatikana kupitia
chmukuru@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. Tupunguzieni huu wimbo wa Mashaka, kuna watu wengi wanaandika nyumbani ila tu kwa kuwa watu wa majuu hamsomi magazeti, basi inakuwa shida tupu. Hebu nendeni zenu na Mashaka sijui Shayo.

    ReplyDelete
  2. MICHUZI NAKUOMBA WAANZISHIE AO MABWANA MTANDAO WAO WA KIINGLISHI,NAJA WENGI WETU ATUJUI WANACHOJADILI

    ReplyDelete
  3. No you are wrong about parliament. The quality of our parliament is improving. Witness the boldness and confidence of the Zitos, Mwakyembes, Slaas, Kimaros Manyanyas and others. Never before have we had parliament force the resignation of a PM and cabinet ministers on a single issue. Ofcourse the executive has not gone far enough in prosecuting the Richmond case. But Parliament (the legislature) is certainly getting bolder, more confident and assertive.It is moving in the right direction and we must give credit where credit is due.Our parliamentarians have been very brave indeed because they have also been iunder considerable fisadi pressure and threats but they have been very brave and patriotic.

    ReplyDelete
  4. inaniudhi, inanikera na inanisikitisha kwa kuwa kumetokea watu kwa malengo ya kujifaharisha au kuwa na uchungu wa uzawa na utanzania wao wameamua kuanzisha mjadala huu. kinachoniuma, kunikera na kunisikitisha ni lugha waitumiayo, kusema kweli wengi wetu nikiwemo mimi mwenyewe kiimglishi kinatupiga chenga, sasa kama huu mjadala ni kwa ajili ya manufaa ya tanzania na watanzania kwa nini wachangiaji hawaandiki kwa lugha ya taifa? hilindili lilonifanya niseme wameanzisha mjadala huu kwa madhumuni ya kujifaharisha, kujionyesha kuwa wanajua kiingilishi, wanafikiri nje ya boksi na mwisho ni lengo lao kubwa kujijengea profile zao tu. hawana lengo la kusisimua watanzania kuimarisha maisha na maslahi ya nchi yetu. Nachukizwa zaidi pale baada ya kuandika mlolongo wote kwa lugha ngeni kwetu eti wanamaliza kwa MUNGU IBARIKI TANZANIA, kwa nini wasiseme na hilo kwa kiingilishi si wanaona kishwahili sio lugha nzuri?

    ReplyDelete
  5. I think you forgot to mention another arm of the government which is not functioning well...the judiciary. The current Liumba saga is evident to this

    ReplyDelete
  6. wait a minute!!!!!!!! where did you plagarize this,let me do my homework and get back to you,i swear on my mothers grave i have read this somewhere

    ReplyDelete
  7. Education is the cornerstone to the future we are building. We need an enabling education, one to make the capabilities of our children boundless. All the developed countries have developed because of the capabilities that are opened by the education they have had.

    elimu yetu nyumbani bado utata, mwisho wa mwaka waziri anakuja na statistics za wasichana wangapi wamepasi na wangapi wamefeli without any roadmap or radical proposed changes for the way forward. u think we'll ever get there????

    i doubt..........

    ReplyDelete
  8. This is on of the brilliant post I have ever seen at this board. Mukuru you have nailed it, I dont have anything to add. Those of us who read the rhetorics of Mashaka and co..we knew that they were trying to export what they see in western world directly to our poor African countries.

    Bila kuwa na viongozi wawajibikaji...hatuwezi kwenda popote. Rule of law is the foremost requirement for any progress.

    I can assure kwa Tanzania tulivyo na viongozi wetu wa sasa WALIOCHOKA NA WALA RUSHWA.....hata TUNGEPEWA STIMULUS YA OBAMA YA $$Billion 700..ZITAISHIA KWENYE ACCOUNT HUKO MAJUU! Hatuna viongozi tuna watu ambao wana interests na matumbo yao..

    AGAIN THANKS MUKURU FOR SEEING WHAT OUR WASOMI IGNORED.

    Tanzania mwizi wa kuku anachomwa moto na mwizi wa billions za serikali anateuliwa kwenye nafasi za uongozi! Halafu watu wanakuja na kelele za credit crunch? My foot! Ndo maana akina Mashaka wakiongea..wengine tunakaa kimya kwa sababu tunajua kabisa..ni political science perse..ambayo haitekelezeki katika dunia halisi.

    Sana sana viongozi wataitumia hii credit crunch kuhalalisha uzembe na wizi wao dhidi yetu wananchi.

    ReplyDelete
  9. To mr kikuru, i think you've been overseas for a long time but i tell you what?? you are out of touch with our country my friend and i don't even know where are you getting the informations from, the only area that i must admit to be crooked is jurdicial system but mr president and parliament they've been doing a such a superb job to get us out of povert, disease and ignorance. Mahakimu ndo noma kama walivyomwachia Liumba aka vigari vyekundu.

    ReplyDelete
  10. Kwa maoni yangu naona mahakama ndiyo iliyoooooooza sanaaaa ukilinganisha na mihimili mingine ya dola. Nasema haya kwa sababu mahakama ndiyo mahali pekee ambapo mtu anaweza kupata haki zake kwa hiyo ndiyo sehemu inayohitaji uadilifu wa hali ya juu sanaaaa ili haki itendeke lakini kwa nchi yetu mahakama zimekuwa vichaka vya watenda maovu, majambazi, mafisadi n.k. Majaji na mahakimu wamekuwa sehemu ya kunyang'anya watu haki zao badala ya kuwa sehmu ya kutoa haki. Kimsingi wezi, mafisadi n.k wanafahamika, mbinu za wizi zinafamika lakini kwa sababu watumishi wa mahakama wanatanguliza rushwa badala ya maadili ya kazi zao na hivyo kufanya wahudumu wengi kuwekwa mifukoni na wenye pesa. Tuanze kwa kupiga kelele kwa wahudumu wabovu wa mahakama ili tulinusuru hili taifa

    ReplyDelete
  11. Jadili mambo yako kichwani mwako, achana na akina Shayo na Mashaka. Tumia akili zako, msituletee watu wenye attention seeking syndrome.

    ReplyDelete
  12. hawa kwani zamani walikuwa wapi hawa kina mashaka???au ni hio economy crisis ndio imewafanya wamekuwa jobless sasa kazi kutujazia mgazeti wa maneno tu hapa bloguni,mi nachangia tu lkn sina muda wa kusoma walichoandika nikishaona naingia humu nachangia wakome

    ReplyDelete
  13. Mapungufu tuliyonayo kila kukicha!! Toeni basi mapendekezo, hiyo elimu itakayotukomboa ni ipi na ni kwa namna gani? Hiyo justice system ni ipi na inakujaje? Wabunge wanawakilisha wananchi na hiyo serious bill inapaswa kutoka kwa wananchi. Unayoongelea wewe ni ipi tuwafikishie wakaiwasilishe? Unaongelea westerners na policies wakati wanagombea, hivi hujui kuwa wanasiasa wetu hufanya hayo? Hujui kitu kinaitwa ilani ya uchaguzi? Reforms unazotaka ni zipi? Mbaya zilizopo ni zipi? Mimi sidhani kama tuna mapungufu makubwa saaana katika 'policies' au katika sheria zetu, au katika 'policies', tatizo ni watu tu kutokuwa na uwajibikaji, kutokujali, ubinafsi n.k. Wanaokemea wizi, ufisadi n.k, wako nje, mara wanapopata nafasi tu ....wizi mtupu?

    ReplyDelete
  14. mashaka na shayo wanajadiliwa sana kwa sababu wanakuna vichwa sana

    wanaandika vya maana, akili zao zimetulia ndo maana kila mtu ili hoja zake zichambuliwe na wasomi, lazima mashaka atajwe. hongera wadau, naona kasi inazidi kuwa kubwa mwisho siyo mbali 2015. mashaka kaza buti mzee tunakuaminia

    ReplyDelete
  15. The first commentator is right and Mukuru is again wrong and uninformed. It is not just parliament which has shown positive growth and signs of maturing. The media has been critical,vibrant, perceptive, informative and deeply analytical- the Swahili print media which Mashaka perhaps does not read. In this regard Mwana Halisi, Raia Mwema stand out and the likes of Saed Kubenea and Johnson Mbwambo are highly creditable columnists in Swahili. Moreover, we have had much better quality articles from the likes of Jenerali Ulimwengu on the development problems and prospects of Tanzania. Ofcourse there have been some negative trends recently of newspapaers being launched as scurrilous attack to assasinate the characters of targeted pubic figures; but in this I submit it is not just the media that is to blame but the regulator must also share the blame in subjecting the public to such low levels of filthy journalism and ad hominem arguments that distract the public from the critical issues of our time.

    P.S I am a lingo-phile and I would not discredit anyone simply because they had written in one language or another. But once one decides to express themselves in one language they should show respect for the language and its readers and do their utmost to observe the language's rules: Mukuru has some way to go in this respect with respect to the English language.
    Tuendeleze libeneke.

    ReplyDelete
  16. Wewe unashangaa nini, hujui mashaka ni chakula cha Msenene.
    Mashaka ni chakula cha masenene yenye minofu, wkimuona ni kama vile wameona nyama ile NONO

    Wengine wanakimbia na visu wengine na mapanga na hasira. Wivu dhidi ya mashaka, sijui nitauhitaje. Ila jama,
    Kijana anatuhamasisha sioni sababu ya kumuonea wivu kiasi hicho.

    Asante kaka kujumuika na kundi la wataalamu wetu Dr Shayo na Jon Mashaka. Orodha yetu ya 2015 inakamilika

    ReplyDelete
  17. BARUA YA WAZI

    Ndugu Mashaka pamoja na wenzako wote, hususan Dr. Shayo, January , Mokes Gama, na Charles Mukuru.

    Pamoja na wadau wengine, naungana kuwapongeza kuanza kujadili maswala muhimu kwa uwazi na undani kuhusu taifa letu.

    Vijana, tuna imani kubwa kwamba ukomboziw a taifa letu upo mikononi mwenu. Tunawaomba mjifunze kutokana na vitimbi vinavyoendelea katika nchi yetu. Mwaka 2015 siyo mbali.

    Mashaka, umekuwa mhamasishaji mkubwa sana, umewaamsha vijana wa kitanzania na sasa tunaona matunda ya kazi yako. Tunaomba muungane, msilumbane

    Tunawaomba mje na mkakati madhubuti ili mwaka huo uwe mwaka utakaokuwa na manufaa na tena kumbukumbu katika bara la Africa kwamba vijana waliamua kutumia ujuzi walionao kwa kuliokoa taifa.

    Tumechoka na UFISADI. Tumechoka na ufisadi kwenye mahakama zetu, tumechoka na ufisadi ndani ofisi za zerikali, tumechoka na Ufisadi kila sehemu. Wananchi wanakufa, walimu wnachapwa viboko, raia hawana hata chakula, huku mengine yanatoa mabillioni ya Bond.

    Vijana, kura tutawapa, tunawaomba muungane, ili mjadili hatima ya Tanzania baada ya Kikwete, 2015. Wanachadema ndo wale wale, wasitupige changa la macho, inabidi mjitayarishe kutuongoza.

    Mashaka, Wakusanye wenzio, mlete hata na US-Blogger, mkae pamoja wote ili mjadili ni nini hatima ya Tanzania baada ya Kikwete. Tafadhalini sana UCHUNGU tunao. Tumechoka na hawa viongozi ambao wamekuwa madarakani miaka nenda rudi, tumechoka na UFISADI


    Mungu Awabariki,
    Mungu na Aibariki Tanzania

    Mollel Nendio
    Arusha.

    ReplyDelete
  18. MICHUZI NIMEKUWA NIKIWASOMA AKINA MASHAKA. SHAYO NA HUYO TENA MUKURU
    KWANI HAWA WATU HAJUI KISWAHILI?NI NANI ATAKAYE KUJA NA KUKITANUA KISWAHILI CHETU, MZUNGU LEO AKIANZA KUONGEA KISWAHILI HAO WAKINA MASHAKA WATAANZA KUANDIKA KISWAHILI KAMA LENGO LENU NI KUELIMISHA UMMA KWA NINI MSITUMIE LUGHA AMBAYO HAO UNAO WAELEZA WATAELEWA, ILA KAMA UNAWAELEZA MATAIFA MENGINE NA SIO WATANZANIA BASI ENDELEA NA HICHO KINGEREZA NA NINAVYO ANDIKA HIVI SIO KUSEMA NINAWACHUKIA MASHAKA NA HAO WENZAKE NINAHESHIMU WANACHO ANDIKA,PIA KAKA MICHUZI NAOMBA UWAPE UJUMBE.

    ReplyDelete
  19. You sound like Mashaka.

    Sidhani kama kuainisha matatizo ni kuanzisha discussion. Why is it mtu ukitaka kuleta mada lazima ulauuuuumuuuuu vyombo vilivopo??? Inanikera sana hasa mchangiaji anapokuwa mtu asieishi ndani ya Tanzania.

    Corruption iko kila mahali, angalia nyumbani kwa Obama, Chicago. Gavana alikuwa impeached, na wa kabla yake na wakabla yake wako jela. Angalia fitna na misallocation ya funds za Bush kuanzisha vita Iraq na camps kama Guantanamo. Hivo sio bongo tu kuna upuuzi. Ndo dunia ilivo na itakavokuwa.

    Mi naona kitu pekee kitakachoweza tufanya tupige hatua ni kuzalisha kwa ziada for export. Kujenga viwanda na kuexport products. Vingine ni vyote ni vitu vya kawaida tu havita kaa viishe.

    ReplyDelete
  20. Justinian F Rweyemamu. (1981). The formulation of an industrial strategy for Tanzania. Africa development. Vol. 6(1):5-18

    ReplyDelete
  21. I will totally agree with you on the issue of education. Education is key for the future of the country Tz Gov need to invest heavilly in education. IT IS SHAME TO SEE MPAKA SASA HIVI KUNA MIGOMO UNIVERSITY OF DARESALAAM. EDUCATION IS KEY FOR INNOVATION. We need to put some kind of requirement in the law that require for every member of bunge kuwa na at least bachelor degree. We are tired with yes men in the bunge.

    ReplyDelete
  22. JAMANI MNALALAMIKA WATU KUTUMIA ENGLISH KWA NINI? MIMI BINAFSI SIWAELEWI! NAWASHANGAA, KWANI NI DHAMBI KUIJUWA LUGHA YA WATU WENGINE? BASI KAMA KI-ENGLISH HAKITAKIWI TANZANIA SASA YA NINI KITUMIKE MASHULENI, VYUO VIKUU KWENYE MASOMO YOTE NA MAOFISINI TENA HADI ZA SERIKALI BASI SERIKALI NDO YA KULAUMIWA JUU YA HILO SI HAWA WAANDISHI, KWA MANTIKI HIYO BASI PIA SERIKALI HAJUWI KITU KIFANYACHO KWA NINI WAENDELEE KUTUMIA ENGLISH MASHULENI NA MAOFISINI? NI HIYO SERIKALI MNAYOISIFIA HAINA AKILI SIYO KUTUMIA ENGLISH? HAMNA POINT ON THAT, YOU ARE JUST COVERING
    YOUSELF WITH A SHEEP ATTIRE WHILE YOU ARE LEOPARDS, NI KWAMBA MKO POLITICALLY COREECT HAMTAKI KUWA OPEN KWAMBA MNAKERWA NA HAWA JAMAA KU-MASTER ENGLISH,WHICH IS A LANGUAGE THAT COMMONLY AND WIDELY USED AND ACCEPTABLE IN OUR COUNTRY INCLUDING YOUR GOOD GOVERNMENT, IS IT MAD BY USING ENGLISH? NOW COMING TO THE MADA/DISCUSSION ITSELF NI KWAMBA IMEENDA SHULE, BUNGE KUPIGA KELELE JUU YA UFISADI NA KUMVUA MADARAKA WAZIRI MKUU SI DALILI YA KUWA LIMEBADILIKA NI BADO BOVU, KWA WALE WENYE UMRI WA KUTOSHA NA KUKUMBUKA MAMBO HATA WAKATI WA BUNGE MOJA LA CCM 1960s - 1990s WABUNGE WALIKUWA NA MBWEMBWE HIZO HIZO KAMA MNAKUMBUKA AKINDA NANDONDE MBUNGE WA TATAHIMBA NEWALA, MTWARA ALIKUWA MKALI KUPITA HATA HAWA SASA, KAMA MNAKUMUKA AKINA DODO WA ARUSHA KIBOKO YA NYERERE THE SAME, OUR PARLIAMENT LACKS PRINCIPLES OF CONDUCTING THEIR BUSINESS, IT IS INCREDIBLE BEHIND THE GOVERNMENT CURTAIN HALIKO HURU KAMA MNAVYOFIKIRIA NA HII INATOKANA NA SYSTEM YA MANAGEMENT NA KATIBA YETU, MSIDANGANYIKE NA KELELE ZA AKINA ZITO, WANAPALILIA FUTURE YAO KWA KUWA RHETORIC KUPALILIA KURA ZA WATANZANIA MBUMBUMBU WHO CAN NOT EVEN ANALYSE SIMPLE THINGS, HASA WA VIJIJINI. TUNAHITAJI MABADILIKO MAKUBWA SANA ILI KUWA COMPLETELY WHAT WE NEED TO BE, TUONE UKWELI BADALA YA KUSIFIA THINGS SIMPLY BECAUSE YOU LOVE SOMEONE IN A PARTICULAR POSITION, A COUNTRY IS BIG THAN INDIVIDUALS, STOP THAT BLINDENESS. THIS IS OUR COUNTRY IF WE WANNA GO ON AS OTHER PEOPLE OUTSIDE THERE WE HAVE TO BE BOLD AND SWIFTLY IN OUR ACTIONS. NCHI ZA ASIA YA KUSINI WAKATI TUNAPATA UHURU ZILIKUWA CHINI KULIKO SISI IN TERMS OF EVERYTHING INCLUDING EDUCATION SASA WAMETUPITA KWA MBALI SANA. WE NEED TO CHANGE OUR BIG PICTURE AND THINK OUTSIDE THE BOX HOLISTICALLY

    ReplyDelete
  23. Nanukuu.."Due to these harsh economic conditions and world ression, cargill Tanzania Ltd, has no alternative but to close down all operations in TANZANIA"(Cargill,2009).

    John Mashaka alisema watanzania wenzangu tujiandae kwa hili janga,linakuja huko!!. Was Mashaka right or Wrong?
    Nanukuu..."most regrettably the decision has necessitated terminating the services of all our TNZANIAN employees"(Cargill,2009).

    Beno Ndulu alisema msiwe na wasiwasi Tanzania haitaathirika na huu msukosuko wa kiuchumi.Was Ndulu wrong or right?.

    mashaka heshima kwako, utabiri wako umefika

    Hahahaaa....hawa ndio wataalam wetu tunaowategemea Tanzania.
    Mkuu wa nanihii...Nawasilisha

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  24. mashaka, wakusanye wenzio kama wadau wanavyosema ili mlete mabadiliko, wanaosemwa ni january na dr. shayo, hawa ndio watu serious ambao wtaifaa nchi.

    ReplyDelete
  25. michu, tunaomba ufungue upya zile atiko z genius rhetoric masta, jon mashaka, nadhani sasa hivi watu watazielewa
    ni kweli kabisa aliyoyasema yanakuwa kweli.

    ReplyDelete
  26. I know michuzi does not like my coments buts but this is another sH** from the same stream known as masha ka if ur real soni just criticise on whats are written with "waandishi wa TZ" maana wengi kwenye uchambuzi wana tafiti vitu but not mashaka coz we know who da he** is mashaka,,if u can write something then andika something that has been said by Tanzanian legents like Chachage Chachage other wise ur another peace of crap bro/sisy

    ReplyDelete
  27. @ Mollel Nendio

    Good job son, for your open later. We definately need young, smart, energetic and focused vijana kama hawa for our young, growing nation.
    Hopefully wamekusoma na kukuelewa.

    Keep up the good job!

    ReplyDelete
  28. Kama nawezekana naomba niwasaidie kitu kimoja nyie wote na mashaka,

    Producers of primary products (Agriculture products) have no voice because of one thing that is the change in prices cant have effects on the the amount of good to be sold in the market"

    Kwa mfano tuseme "bei ya tumbaku ikishuka haiwezi kumfanya mvuta sigara avute zaidi endapo amezoe kuvuta pakti mbili za spotsman"

    ni kitu kile kile kwa mtu anaelima pamba, mpunga, mahindi ya "BONDO" nk,

    "Prebisch anasema ili nchi iendelee ni lazima iende industrialisation"

    ukiangalia nchi zilizoendelea hadi kufikia hapo ziliwekeza kwenye viwanda na "Viwanda nje Mbadala""Import substitution Industries"

    Tatizo lililokua linakwamisha mambo kama hayo ni "Corruption" tunamshukulu Kikwete kwa kuwafikisha waliokua wanakwamisha juhudi hizo (Mramba and the type

    Kilichopo kwa sasa ni kuongeza juhudi katika iMPORT SUBSTITUTION na pia tuondoe udhalim, ubadhilifu na ufisadi basi,

    Desert Eagle, Born in Geita educated in Tarime and I real like Ja rule and 2pac ni mchango tu wadau tuchambue kwa maslahi ya taifa

    ReplyDelete
  29. ndugu wadau
    kwa kweli nimeamini kuwa vijana wa kitanzania waliopata nafasi ya kujua mambo wameanza kuwa chimbuko la kuleta muamko mpya katika kizazi kipya cha Tanzania.

    Dr Shayo, Mashaka na wengine wote wenye nia njema wanajua kuwa huwezi kubadilisha Tanzania kwa siku moja, ila katika kila jamii ni lazima wawepo watu ambao ni chanzo cha kuleta mtazamo mpya.

    Mtakumbuka kama mpo wale waliosaoma kajitabu kinaitwa "Animal farm" haka kajitabu kanaonyesha ni kwa jinsi gani hawa akina Dr. Shayo na Msahaka wameamua kuwaamsha watanzanania wenzao.

    Kupanga safu ya 20015 si hoja, tunataka watu wenye nia njema kuweka majadiliano yenye manufaa kwa kizazi cha Tanzania. Dr. Shayo na Msahaka wameweka taifa mbele kwanza kwani wamegundua kuwa kwa vile huwezi kupigana na wale wachache wabovu , jiunge nao ili kuleta mabadiliko.

    Hongera Dr. Shayo, Hongera Mashaka kwa kutoa mwamko mpya ndiyo maana hata sasa wasomaji walio wengi wanafikia kiasi cha kumlinganisha Dr. Shayo na Prof. Ndulu ambaye alikiri kuwa matatizo ya kiuchumi hayataadhiri Tanzania, yetu macho wenye nia njema wakisema mnaona wanacheza tuuuu, mafisadi wakiiba mnawalinda.
    Kazi kwenu

    ReplyDelete
  30. Kwanza kabisa naanza kwa kumpongeza ndugu mukuru kwa mada yake nzuri ,ingawaje baadhi ya watu wamekosa cha kusema na kuamua kuikashifu. jamani ndugu zangu watanzania lazima tukuwe au kukomaa ki akili hasa katika karne hizi. Tumekuwa na tabia ya kuogopa au kuchukia ukweli unapowekwa hadharani na yeyote yule atakaye simama na kusema ukweli watu humshambulia kwa kila hali. Mimi naungana 100% na hoja za ndugu Mukuru kwani yalioandikwa ni ukweli mtupu na ndio dawa kwa donda ndugu linalotukabili nchini. Mara usuluhisho wa hayo ukipatikana basi nchi yetu itakuwa mfano mzuri kwa wote dunia ukizingatia tulikotoka.
    Ndugu zangu hata kama lugha haipandi basi usighadhibike na kuleta kasha zisizo na maana . Na zaidi ya hapo kwa wanaopinga au kutoa kauli chafu kwa lugha aliyoitumia ndugu mukuru; lugha hiyo na official nchini na naomba niwakumbushe kuwa serikali ya tanzania ina lugha mbili ambazo ni swahili na English, ambazo kila hufundisha kila kona ya nchi kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.
    Mungu Ibariki tanzania na watu wake wote.

    ReplyDelete
  31. ili swala la mashaka linakuja kama vile utabiri. mashaka alitushauri lakini wajuaji wenye midomo saba walisema kwamba tanzania haiwezi kukumbwa na misukosuko na haya sasa yameanza

    swala ka kagil ni nyeti. watu wanaojiita wajumi na chupi ndani ya apartment zao huko texas, muandika uharo a.ka mchumi wa texas midomo mikubwa yalijifanya aha, hakuna shida, sasa tanzania imeanza kupunga kutokana na kufungwa ka haya makampuni, semeni sasa.

    kumbafu, mnatuchafulia hali ya hewa na usenene. bwana shayo na mashaka asanteni sana. tunaona sasa mliyokuwa mkiandika yanatokeaa kweli

    ReplyDelete
  32. Watanzania wenzangu,
    Napenda kutoa maoni yangu machache ambayo yatalenga maoni yaliyotolewa na wadau wengi hapo. Kuna wengi wamekuwa wakikandia maandishi ya kiingereza. Nataka niwakumbushe tu kuwa kwenye dunia ya leo, hata China, China, Mexico, Brazil wote hao wanajifunza kingereza. Sisi watanzania tusipojifunza kingereza, tukamate wapi? Tusidanganyike na maoni ya kizamani, dunia imekuwa kijiji tayari na wanakijiji walioko kwenye dunia ya leo wanaongea Kingereza, kama hatutaki itabidi tutafute ulimwengu wetu. Magembe kuna siku alisema hilo akaonekana muovu, lakini alikuwa sahihi. Ila kwa vile kuna watu hawapendi kuambiwa ukweli, basi wakampinga sana Magembe. Shauri yenu, watoto wa vigogo ambao wanakipigia debe Kiswahili kila siku wanasoma shule za English medium huko nje ya nchi. Wanachotaka ni kuwa sisi watoto wetu wasijue Kingereza ila watoto wao waje kuendelea kutawala watoto wetu. Kiswahili ni muhimu, lakini Kingereza baba! Nawashauri wale wasioweza kukisoma, wakajifunze.
    Pili, kuna watu they are just critical. Leo tunasema kuwa judiciary kumeoza kuliko kwingine because of the current incidence ya Liumba. Lakini kwangu sioni mahali paliposawa hata kidogo. Na napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza sana Dr. Kitine kwa sababu ndio ukweli wenyewe, nchi inaendeshwa kiholela. You cannot tell the direction of the country. That is the fact. Huwezi kulisifu bunge kwa sababu ya wabunge watano akina Zito. Wabunge pale wako zaidi ya 300, sasa what is 5 in more than 300?
    Ninachosema mimi ni kuwa Tanzania haina dira, viongozi wana mawazo ya kizamani sana. na ninawaambieni mambo yatakuwa magumu sana hapo baadae kwa sababu ninachoona ni kuzima moto tu. Hivi kweli ni ulize yafuatayo?
    SWALI 1. Kuna haja ya kuingiza mchele kutoka nje? Kuna haja ya kufikiria njaa wakati Mungu anatupatia mvua ambayo tukiitumia kwa mwaka mmoja tunaweza kuvuna vyakuala vya kutusaidia miaka hata mitano ijayo?Bongo ukienda dukani unakuta maziwa yanayotoka Zimbabwe, Kenya, lakini Tanzania ni nchi ya Tatu Africa kwa kuwa na mifugo mingi.
    SWALI2. Kuna haja ya Dar es Salaam kuwa na foleni wakati watu wanaoishi ni kiduchu tu. Unaweza ukasema kuwa bongo tuko wengi, lakini kwa vile hujasikia mji kama Mexico wenye watu zaidi ya milioni 25
    SWALI3. Kuna haja ya kuona wanafunzi wanafukuzwa eti kwa sababu ya kubaguliwa kwenye kupewa mkopo na serekali. Hao wanafunzi wote wanatumia shillingi ngapi? Mafisadi wametumia ngapi?
    Ningeuliza mashwali mengi.
    Lakini kwa mtazamo wangu: TANZANIA HAINA FUTURE,
    Sababu: Serekalini hakuna watu wanaofikiria mbele. Sijaona hata mmoja na hata akiwepo anapata frustration na kuacha kazi. Nasema hakuna kitengo cha serekali hata kimoja excel. Hii ni kwa sababu kila mtu anafanya rutine duties na mambo ya ndio mzee kama jeshini. Mkubwa amesema. Na suala hili limetoka kuanzia shule za primary. Watanzania hawaandaliwi kuwa creative. Na akiwa creative kidogo atapigwa madongo na wenzake ile mbaya. Ndio hapa unaona watu wanamwandama aliyeandaa makala hii na wengineo waliokwisha andaa makala zilizopita. Hizo ndio zetu watanzania. Hakuna shirika hata moja linalomilikiwa na serekali litakalobaki, yote yatakufa kwa sababu ya mambo kama hayo. Ndio maana mimi wakati mwingine nasema bora tu mamiradi yanayoanzishwa na wageni Tanzania, pamoja na kuwa sisi watanzania tunahitaji ajira, tuwaache wageni tu waajiriwe ili at least tuwe na uzalishaji wa maana hapa kwetu, kwa sababu kazi hatuwezi. Kama unabisha niulize. Nitakuambia mahali watu wanapofanyakazi. Bongo hatufanyi kazi kabisa.
    Sababu ya pili: Kulindana wakubwa. Itakuwa kama ufalme sasa. Nikuambie, Sula la mtu kama Chenge, JK anajua kabisa kuwa jamaa alishiriki kwenye ufisadi. Lakini hata kumkemea, hakuna. Je, kwa staili hii ufisadi utaisha. Unajua athari za ufisadi ni mbaya kuliko watu wanavyofikiria. Ni ufisadi ndio unafanya hata watu wasifanyekazi. Mtu anajisemea, why worry? Baba yangu atalipua bomu nitapata ada ya kwenda kusomea ulaya. Au, hata nikipata maksi ndogo, baba yangu ni mkubwa bwana, atawaambia mabosi serekalini wanichukue, mimi si ninavutia wanaume, nikienda kwa bosi wa kampuni fulani bora nina cheti, hata ni kibaya kiasi gain, nikimwonyesha huu mwanya tu, si atakubali. Kwa maana hiyo, tuna watendaji wabovu serekalini. Kwa sababu ya kulindana. Tunaogopana, hakuna kuambiana ukweli. Watu kama akina makamba wanaongea wanachotaka. JK alete shida tu, Tanga hapati kura mwaka 2010. Obama hata kabla hajaapishwa kuwa raisi, alishamwambia gavana wa ilinois ajiuzulu. Yule jamaa akakataa, je yuko madarakani sasa? Kama hatuwezi kusema ukweli ni kulindana tu, shauri yetu. Yaani tuna risk maisha yetu kwa sababu ya kulindana. Ni kama unampa mtu asiyeweza kuendesha gari kazi ya kukuendesha kwa sababu unasema, kijana hana kazi bwana, ngoja aniendeshe. Unamlinda, lakini anakupeleka shimoni.
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  33. Kweli rushwa, ufisadi na wizi wa kura, msigano wa maslahi na kashifa kama hizo si matatizo ya Tanzania peke yake. Soma "A 'fraud' bigger than Madoff" jinsi wakubwa wa kijeshi wa marekani wanavyotumbua Iraq
    kwenye website ya The Independent ya UK, kumbuka Bush 'alivyoshinda' kipindi cha kwanza na rafu alizocheza kipindi cha pili 'akashinda' tena; kumbuka Watergate na jinsi Nixon alivyosamehewa; elewa Vice President Cheney wa Marekani alikuwa ni mwenye hisa wa makampuni makubwa yaliyopewa zabuni ya kutoa huduma na vifaa nchini Iraq,familia ya Bush ni wafanyabiashara wakubwa wa mafuta na ndicho wengine wanacho hisi kilimsababisha Bush kuanza vita ya Iraq, Bwana Mills- mume wa waziri mmoja katika baraza la Blair- na rushwa aliyohongwa na Berlusconi na kesi nyingi nyingine. Kweli dawa ni mihimili yote kufanya kazi yake. Mimi naona mwanga iwapo na sisi wanachi tutachagua watu wenye msimamo tunapokuwa na fursa hiyo, kama tutakataa rushwa na vijipilau wakati wa uchaguzi, kama tutawaambia wazi wale tunaowachagua kwamba tunataka watetee maslahi yetu na ya taifa siyo ya chama chao katika bunge na serikali.Tatizo ni letu sote na si la CCM tu, rushwa na kutokuwa na principles ni tatizo la kitaifa, hakuna chama kisafi (vinginevyo kwa nini Chadema warithishane kiukoo, anatoka baba mkwe kwenye uongozi anaingia mkwe, kwa nini kina uchagauchaga mwingi, kwa nini byama vingine vina udiniudini kwa nini vingine vina ukanad wa ziwa??). Mimi naona mwanga hasa katika bunge la sasa tunahitai kina Mwakyembe na wenzake ambao watatetea maslahi ya taifa bila woga na hata kama ndani ya chama chake CCM ataitwa CHADEMA. Tunawahitaji kina Zitto zaidi na kina Ole Sendeka.Lakini jukumu la kwanza ni la kila mtanzania: usiwe mwoga kutetea haki yako, kataa rushwa (kwa mfano: komaa na trafic barabarani; dai haki usitoe rushwa kuharakisha maombi yako ya paspoti; kataa vijipilau vya wakati wa uchaguzi, wengine wanasema kula pilau alafu kapige kura unavyotaka, lakini mimi nasema kataa wajue it does not work na masinia ya pilau yawadodee). Sasa watanzania mko tayari kwa kazi yote hii? Kazi ni kubwa kataeni vijicionvenience vya rushwa kuharakisha mambo yenu. Mko tayari????

    ReplyDelete
  34. "John Mashaka alisema watanzania wenzangu tujiandae kwa hili janga,linakuja huko!!. Was Mashaka right or Wrong?"

    Kikwete alishasema hali ya uchumi itakuwa mbaya.

    Mashaka alisema thamani ya mchango wa kilimo ni mkubwa kuliko sekta yoyote akawa proven wrong kwa sababu utalii ndio sekta inayoongoza.Hakujua hata sekta inayoongoza, wapi atoe uwezo wa kutabiri. Asiyejua la leo atajua la kesho?

    ReplyDelete
  35. wee anymous hapo juu, naona unatumia makalio yako kufikiri badala ya akili.

    mashaka alituonya kwamba tujitayarishie ugumu wa maisha na makampuni ya kigeni yanayoajiri watanzania kufunga milango yetu, leo Cargil yameanza kufunga, sasa babu yako ataawajiri hao waliopunguzwa kazi au utawapeleka wapi?

    nadhani ww ni us blogger vinginevyo una ukaribu naye. hii ni hatari kwa uchumi wetu kwa hiyo sioni ubishi wako huko wapi. ni yale yale aliyotuonyea ndo yanatokea,kwa hiyo hata na wewe jitayarishe, funga mkanda, hali ngumu inakuijia hata na wewe huko kwenye utalii, subiria tu

    mashaka leo tunakuaminia, kwa sababu wale wanaobisha ushauri wako, imekuja kubainika kwamba hawana alternative ya kutupa. asante na ubarikiwe

    mchumi wa Dar

    ReplyDelete
  36. Rais matarajiwa Mh. Mashaka, busara zako sasa tunaziona, heshima kwako mkuu, ila tunaomba atiko zaidi.samahani sana kwa usenene wetu, ni upeo mdogo tulionao ndo maana tumekuwa na akili finyu ya kukujadili badala ya kujadili mada ulizotuletea.hali inakuwa mbaya duniani, tunaamini sasa kwamba uchumi wa dunia unalekea pabaya

    ReplyDelete
  37. watanzania tuna roho za korosho kweli. huyu mtoto alitushauri vizuri sana, lakini yale yale UJUAJI wetu.........haya

    ReplyDelete
  38. Ndugu wadau
    Si kwamba ninapingana na waliotangulia ila hapa nami ninataka kutoa mchango wangu kwa hawa vijana ambao wameamua kuanza kuonjesha njia ya wapi taifa la Tanzania linakwenda.

    Mashaka na kilimo Dr. shao na biashara. Vingine vyote vimo ndani ya michango ya hawa jamaa.

    Mimi siyo kuwa ninawapigia debe hawa vijana waliojitokeza ila ninaamini kuwa wapo jinana wengi tu tena nafikiri wenye uwezo wa kuwapita hawa ila tatizo ni kuwa ni waoga.

    Imefika kipindi mkuu wa nchi akubali kuwa mawazo ya kuleta baadhi ya mabadiliko fulani lazma yatoke nje. Ziundwapo kamati muhimu lazima wajue kuwa vinaja hawa wale walioko nyumbani wakishirikiana na wale walioko nje wenye nia njema na taifa la Tanzania wanaweza kutoa changamoto mpya.

    Mimi siyo kuwa ninampigia kifua mtu ka dr. shayo, ila kwa kweli kuna kitu kimoja amekifanya ambacho, bila kujua alikuwa anamuunga mkono ndoto ya swahiba wake Mashaka.

    Mwishoni mwa mwaka 2006 nilikutana na Dr. shayo nikiwa katika safari zangu za kibiashara jijini London. Katika mazungumzo akaniambia akikuwa anafanya utafiti wa ni kwa namna gani wanunuzi wa bidhaa hapo UK na EU ambao wanamakao yao makuu jijini london wangeweza kuagiza bidhaa moja kwa moja kwa wakulima wa Tanzania. Kutokana na maongezi ya shayo alikuwa haoni sababu Kenya wanunue matunda Tanzania, then wao ati ndiyo wayauze kwa kampuni ambayo ndiyo itaiuzia masupermarket.
    Kwa kweli sikumuelewa Dr shayo kwani niliona kama ni kitu ambacho hakiwezekani, Ila baadaya ya haya malumbano ambayo yamejitokeza kwenye hii blog, na baada ya kumcimbua zaidi kwenye google ndiyo hapo nikapata fahamu kuwa alijua kuwa ukiwaunganisha wanunuzi na wakulima, kwa kiasi fulani bidhaa za tanzania zitaanza kuonekana huko nje.

    Alichonifurahisha zaidi ni pale aliponionyesha statistics au Data za kwa namna gani Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa zake nje kwa takribani miaka 15 iliyopita.

    Takwimu kama hizi zilikuwa hazionyeshi tuu kuwa tanzania tumeuza nini na wapi, ila zilikuwa zinalinganisha ushinani kati ya Tanzania, Kenya, Uganda, Malawi, Zambia, DRC, Burundi na Rwanda.

    Mimi siyo mchumi, ila ninaelewa kuwa takwimu kama hizi ni silaha tosha ya kuwezesha wizara kusika kujua ni wapi pa kuborehsa na ni wapi kwa kutilia mkazo.

    sioni ni kwa nini Msumbiji waweze kuuza kwa mfano pilipili, Avacado katika supermaket za UK, Ugerumani, nk na Tanzania tunashindwa.
    Nafikiri baada ya hawa wachache kuanza kufikiria vitu kama hivi, ingekuwa busara wakashirikiswa katika kubuni mbinu za kuwasaida watu wetu wawe na mtizamo wa kukubali ukweli.

    Dr. Kitine watakupiga vita sana ila hali ndiyo hiyo. Nchi inaoza kufikia kiasi cha kuibiwa kwa nyaraka njeti za Serikali! Nani asiyejua kuwa File original la EPA liliuzwa kwa 20,000,000? na halipo Tanzania? Anayekuwa na wasiwasi Muulizeni Gavana kama baada ya kuteuliwa aliwahi kuiona? Haya ndiyo mambo ambayo yanaiozehsa nchi. Badala ya kufikiruia ni wapi tunalipeleka taifa tunafikiria ni kwa jinsi gani ya kulindana.
    Haya mwee yetu macho....
    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  39. jamaa aloleta hii amekopi article yote! si maneno wala mawazo yake kabisa

    ReplyDelete
  40. wwe unayesema amekopy na ku paste the entire article, tuamie ameukopi wapi.

    haya majitu mapumbavu ndiyo yanayorudisha nchi yetu nyuma. kaoge ili usafishe mwili wako mchafu, jinamizi

    mashaka hoyeee,
    shayo hoyeee

    ReplyDelete
  41. ndugu zangu tuache usenene, kama unafikiri Mukuru ka-copy sehemu basi tupe evidence?
    kwasababu jamaa mtalaam basi tunasema kagezea sehemu. Kwanini hatuamini kwamba tunaweza

    ReplyDelete
  42. Hi, nimesoma haya aliyosema Aloyce Kimaro, haya wajameni kiswahili mnachotaka ndiyo hicho makosa kibao. Je sasa tutumie kiarabu? mnataka kiswahili hamuwezi kuandika kitu cha maana, haya weeee kazi kwenu mnaodai eti wachangiaji waandike kwa kiswahili

    ReplyDelete
  43. mimi nimeona nita fsiri hii habari ili kila mtu aelewe ni kwa kifupi. zipo aya 10
    aya 1. kamsifia mashaka na dr shayo

    aya 2. yuko tiyari kwa watu kuchangia mjadala huu na kumkosoa yenye maana.

    aya 3. sifia mashaka na dr shayo

    aya 4. ukiwa unaongelea uchumi wa TZ uwezi ukaweka kando hali ya siasa na serikali kutekeleza sera zake. bila kuiponda sana serikali, ukiangalia mda wa serikali na mafanikio yake, utajua ya kwamba maisha yetu na watoto wetu ya siku zijazo hayaeleweki.

    aya 5. point yangu hata kama ukiwa na sera nzuri kama uongozi ni mbovu ni bure. bila kuwa mahakama yenye nguvu, viongozi wasio mafisadi na mikakati ya mda mrefu ni sawa na bure.

    aya 6. mahakama zetu hazina mpango watu wanafanya makosa lakini hawakamatwi bila utawala wa sheria ni bure. wawekezaji wanavutiwa na nchi zenye utawala bora wa sheria. sasa kila mtu anawaona mafisadi wakitembea bila matatizo yoyote, wengine wana nyazifa mbalimbali CCM, lakini CCM wanajidai hawausiki na ufisadi/mafisadi na wakati wapo mafisadi kibao ndani ya CCM. Mzungu anasema ukipenda dalili zote za hatari unajidai huzioni.

    aya 7. Bunge letu ni zohofu, bila kuwadharau, baazi ya wabunge hawawezi kuwakilisha mswada bungeni au kuuwelewa mswada ulio wakilisha na serekali. kama bunge ni dhaifu kiasi hicho nani atasimamia sheria za uwekezaji, mazingira, nishati na elimu.

    aya 8. mlio kaa nje mmeona watu wakitoa ilani zao za uchaguzi, wakichambua nini watafanya kwa undani, je viongozi wetu? rais kikwete alisema anakumbuka enzi zile za nyerere ata ukienda shule gani unakuta vitabu ni vilevile elimu iko sambamba nchi zima, vipi leo kumetokea nini? rais aliuliza.
    je huyu rais sera yake ya elimu katika uchaguzi uliopita ilikuwa nini?

    aya 9. sifa kwa mashaka na shayo

    aya 10. lazima tukubali mabadiliko makubwa yanahitajika TZ, hata kama mawazo mazuri kiasi gani ni bure.

    sababu ya kutafsiri nimeona watu wengi ni mashabiki hawaelewi kitu kinachoandikwa kwa ajili ya lugha inayotumika, samahani simtukani mtu.

    maoni binafsi
    hamna solution iliyotolewa, hamna jipya, kila mtu anjua ulichooandika na ameshasikia kabla lakini walikuwa tu hawaelewi kiingereza.
    wakina zito na wezake wanne wa chadema wanajitahidi kutatua matatizo hayo.

    ufumbuzi wa tatizo.
    step 1. wananchi wa TZ hususan wa dar wamelala.... kinachohitajika kwanza wabunge wa upinzani wakifike angalau 100. Mabadiliko yanaanzia mji mkuu, na mji mkuu wetu wote ni CCM na wananchi wamelala. Pigieni kura Upizani ili muondoe MONOPOLY. PUNGUZENI MAJORITY YA WABUNGE CCM 2010. KURA TU NDIO ZINAZOHITAJIKA

    mdau uk

    ReplyDelete
  44. Kweli nyie wote Ze Komedy. Ai dont riali andastend yua problem. As e mata of fakt yu a ol ze komedy and ai wana mek it klia tu yuu all stop ze shit. I think it mek sens tu kuit zis kaind of diskashen manake kila mtu anajifanya mjerumani na wengine wajapan. Itakuwa vema mjadala kuhusu tanzania ukifanywa kwa lugha mbalimbali na watakaopenda kifaransa waandike kifaransa na kirusi waandike kirusi na kiitaliano waandike kiitaliano. Wanajua kingereza tu watanyamaza na wanajua kiswahili tu watakimbia.Huo ndio uzalendo.

    ReplyDelete
  45. Jamani nisaidieni,nimeitafuta sana hii Novel ya Charles Mukuru - Wither Tanzania : A Discussion,katika Bookshops zetu sikuipata!Jamaa mmoja akanidokeza inapatikana maduka ya Kariakoo,nikaenda lakini sikuipata!Please help me,This guy is a Super-talented Time-Waster!Lakini mbona hampatikani katika serious blogs za Marekani na Uingereza?Fixi sana nyie!

    ReplyDelete
  46. mbavu zangu,,,,annons nyie?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...