mkutano wa mawaziri wa fedha, magavana wa benki kuu wa nchi za Afrika na Shirika la Fedha Duniani (IMF), wataokutana kesho kujadili jinsi ya kuliepusha bara hilo na madhara ya mgogoro wa kiuchumi unaoendelea duniani.
Mkutano huo wa siku mbili, utaofunguliwa na JK, utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dar. Pamoja na mambo mengine, pia utajadili mafanikio na upungufu uliowahi kutokea katika uhusiano kati ya nchi za Afrika na IMF.
Katika maboresho ya uhusiano huo, washiriki ambao ni pamoja na watungaji wa sera mbalimbali za uchumi, wawakilishi wa sekta binafsi na wa asasi za kiraia wapatao 300, watajadili mafanikio ya baadhi ya nchi zilizoonyesha ukuaji wa uchumi katika muongo mmoja uliopita, ili yatumike kuweka malengo ya pamoja ya uhusiano mpya kati ya Afrika na IMF.
Aidha katika mkutano huo uliodhaminiwa na kampuni na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, ikiwemo Kampuni ya magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers (TSN), inayochapisha Daily News, Sunday News, HabariLeo na HabariLeo Jumapili, washiriki hao pia watajadili jinsi ya kupunguza umasikini kwa kuboresha miundombinu, kilimo, elimu, afya na kuongeza wigo wa shughuli za kiuchumi.
Jumla ya mada 36 zitawasilishwa na watoa mada mbalimbali akiwemo Rais Kikwete, Rais mstaafu wa Botswana, Festus Mogae, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha-Rose Migiro, Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Dominique Kahn na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB), Ngozi Lweala.
IMF husaidia nchi zilizoendelea na zinazoendelea kutekeleza sera za uchumi na fedha kwa kufanya uangalizi wa karibu wa utekelezaji wa sera hizo, kutoa msaada wa kiufundi na mikopo kwa nchi zinazokabiliana na hali ngumu ya kifedha.
wadau kama mnavyosema, nadhani jon mashaka na dr. shayo wangealikwa kwenye midahalo kama haya kwa sababu wasomi wengi wa watanzania ni watu wa kuboronga hata hawa maprofesa wetu ni maji tu
ReplyDeletehawa vijana wameonyesha kubobea kwao katika maswala ya uchumi ya kidunia, ukizingatia mashaka anafanya kazi katika soko la hisa la marekani na shayo naye ni mtaalamu mkubwa nayeshauri nchi nyingi.
kwa hiyo serikali yetu ingetafuta namna ya kuwashirikisha ili tuone pande zote za bongo, majuu kutoka kwa wataalamu wetu.
hivi hawa waandaaji nina uhakika wamewaalika wakina mashaka na shayo kwani wale vijana ndio taifa letu la kesho. kura tunawapa.
Kila ninapomuona Bosi wa IMF akitua Darisalama huwa natetemeka na kuingiwa na hofu kubwa!Naogopa,sijui safri hii nchi yetu itapigwa mnada kwa matajiri duniani?Sijui tutanyang'anywa hiki na kile kwa kushindwa kulipa madeni ya BENKI YA DUNIA NA IMF katika muda na wakati uliotakiwa?Sijui wamekuja tukopesha mikopo mingine zaidi ambayo haikuwemo akilini wetu?Kwa kweli huwa napata wasiwasi mkubwa sana.Nikimuona tu Bosi wa IMF mara moja hukumbuka kiwango chetu cha UTEGEMEZI kwa nchi za nje;hukumbuka KIWANGO CHA MADENI YA NJE ambayo Tanzania imesha kopa na inadaiwa na mataifa ya nje!Huwa nakumbuka jinsi watoto na wajukuu zetu watakavyo kabiliwa na mzigo mkubwa sana wa madeni ya nje pindi wao watakapo kuwa watu wazima na watakao endesha nchi yao, sisi sote tuliopo sasa tukiwa hatupo tena duniani!Napata huzuni kubwa sana ninapo fikiria kwamba nchi yetu hivi sasa ni tegemezi zaidi na masikini zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 30 iliyopita!Na kwamba hatuwezi kubuni wala kufikiria mradi wowote ule wa maendeleo bila ya kwanza kufikiria MFADHILI ATATOKA WAPI?Sijui safari hii tutakuwa na nini cha kumweleza Bosi wa IMF?Kwamba uchumi wetu umekua kwa kasi sana;umaskini umepungua sana;kipato cha watanzania kimeboreka zaidi;kwamba tanzania sasa inauza zaidi nchi za nje kuliko inavyo nunua kutoka nje!Kwamba nchi yetu kwa sasa ina maProfesa wengi sana katika nyanja mbalimbali za uchumi na kwamba tatizo letu sugu ni UHABA TU WA FEDHA ZA KIGENI!Nadhani atatuelewa.Lugha yetu ni rahisi sana kutabirika itahusu somo gani!Kabla hujaomba,utajibiwa," well actually the IMF and the WORLD BANK" knowing the circumstances prevailing in Africa,the Global Economic Slump Notwithstanding,had already set aside some 5.5 Trillion Dollars for the Tanzanian Cause!This coming year all efforts should be directed at elliminating POVERTY completely!Right?".Then the entire Bandwagon would hyme unanimously with a resounding "YES SIR".If you have never been to Danganyika then this is it!The IMF Boss has come to Danganyika to learn how to run the prestigious IMF in the light of newly emerging global challenges!Manzese Mpo?
ReplyDeleteNilipoiona hii picha harakaharaka nilidhani wanapandisha kwenye ngazi za mahakama ya kisutu....Akili yangu iko mbele dakika kadhaa!!Samahani wadau
ReplyDeletembona prof.mukandala anaonekana amenywea mbele ya huyo mzungu?
ReplyDeletewatanzania tujiamini mbele ya hawa watu. vingenevyo watatuburuza.
mapenzi yangu ni non-verbal communication. Michuzi, ninakusukuru sana kwa sababu picha zako zinanipatia data ya kutosha kuhusu mwenendo wa non-verbal communication katika mageuzi ya kiuchumi na kisiasa. angalia wabongo na suti za ulaya na suti ya mtemi wa imf. hapa kuna makala kamili ya uchambuzi. tafadhali endeleza libeneke!!
ReplyDeleteDo amakweli lisemwalo lipo. Shayo na mashaka walipoanza kuyazungumza haya mambo ya kutikisika kwa uchumi wa dunia na adhari zake wengi wa wasomaji waliwaona kama vijana waliopotea vile.
ReplyDeleteSasa yale waliosema yanatokea. Hapa kuna haja ya kujiamini na kuwa wakali .Dr shayo aliwahi kutoa tahadhari kwa kuwapatia baadhi ya waheshimiwa tena wa nazi za juu hapa Tanzania kitabu kilichokuwa kinaitwa "Economic hitman"
Sasa sijui kama waliopewa walisoma au walifanya mapambo.
Ukweli ni kuwa hawa vijana wetu wamefanikiwa kuona upande wa pili wa shilingi, ndiyo maana wanakuwa na machungu na taifa letu.
Cha msingi tu ni wahusika kuweka kautaratibu ka kuwatumia hawa wataalamu, kwani Taifa litanufaika.
Mimi nikiwa kama kiongozi katika wamu ya nne ya J.Kikwete ni mmoja nilinufaika na hicho kajitabu. Nililetewa ofisini na kuambiwa mzee zawadi toka kwa kijana wenu.
Dr shayo sikupata nafasi ya kuonana na wewe ila taarifa nilizonazo ni kuwa Cabinet Ministers wasiopungua 13 walipewa hako kajitabu.
Jamani mnataka mchango wa namna gani?
Eti International Monitary Fund IMF)! Pamoja na makao yao makuu kuwa Washington DC, wameacha pesa yote ya wananchi marekani imeliwa na wajanja wa Wall Street. Where the hell were they when American economy was falling apart?? Kaeni macho kina Mukandala, hawa watu wana lugha nzuri sana wanapotafuta lakini wakishapata tunakuwa kichekesho. Sasa hivi China na Marekani wana vita baridi; Tanzania ndiyo uwanja wa mapambano, tofauti tu sasa hivi we do it with a smiling face :) - sijui hata nisemeje ili mpate kunielewa... "Sikio la kufa halisikii dawa"!
ReplyDeletei think what anynony hapo juu anachokizungumzia is true. mashaka wrote extensively on things we should prepare for, but many of us ignored, and ridiculed him, now we are seeig the same problem he talked about. mm wala sishangai, haya ndo ubongo. majungu
ReplyDeletehebu mnieleweshe, hapa wabongo wanapewa ka msaada au ndo hivyo tena?
@anon 5:19pm
ReplyDeleteLOL!, funny!
Uchumbuzi wa undani wa IMF unapatikana katika blog ya taifaletu.blogspot.com huko wamekuwa exposed. Ukweli ni kwamba Watanzania wengi hamjui nini maana ya IMF... Mtembelee january Mkamba uone jinsi uchambuzi ulivyofanywa
ReplyDeleteannon wa #3 juu
ReplyDeleteso do I khaaaa,nilitaka nijue kulikoni kisutu tena??
hahahaaaaaa
Hongera mashaka
ReplyDeleteHongera Dr. Shayo
Hongera January
Tanzania shamba la BIBI
Tukae macho!
Nyie Watanzania wenye elimu ndogo acheni vituko. Mashaka na Shayo hawakusema lolote la maana na jipya. Wao walipiga debe tu mambo ambayo kila mtu alikuwa anasema. Shayo aliweka msururu wa mambo ambayo hayamo Tanzania, kwa mfano alisema diversification of investments, kitu ambacho hakina maana kwa Tanzania. Tanzania watu hawa-save pesa zao, hajui investments wala nini. Alikuwa anaongea mambo ya vitabuni tu. Mashaka yeye alifululiza na mambo ya kushauri eti watu wakienda kufungua akaunti benki waulize kuhusu bima za pesa zao wanazoweka benki. Tanzania hatuna kitu kama hiki ambacho Marekani na Ulaya ukifungua akaunti unatakiwa kupewa maelezo. Yeye alikuwa anatoa utatuzi wa mambo ya Marekani huko aliko kwa watu walioko Tanzania. Na isitoshe ilikuwa ni mambo ya kwenye vipeperushi vya mabenki ya Marekani. Zaidi ya hapo hakuna kitu.
ReplyDeleteJamani msifikiri uchumi ni kuimba mambo ya vitabuni na kurejea data zilizofanyiwa kazi na wengine tu. Hawa vijana wanachojua ni kitu cha kawaida tu, huyu Mashaka hafanyi kazi Wall Street. Muulizeni kwa nini kwenye makala zake huwa hasemi yuko wapi? Anakaa North Carolina, hata New York usikute hakujui.
Kama hamjui mambo kaeni kimya.
Nakuunga mkono kaka, hawa vijana wanatia aibu na comment zao. Hamna lolote. Kufanya kazi Wall Street pia sio hoja ya kutetemekea hata kama wangekuwa Ma CEO wa Goldman Sachs. CEO wa Gold man Sachs wa zamani alikuwa waziri wa fedha wa marekani na kavurunda mambo vilevile ndio itakuwa makarani. Waal Street kitu gani Wabongo wengine acheni inferority complex mtu akikaa Wall Street au akiwa mkuu wa IMF sio mungu.Rais pia sio mungu.Believe in yourself. Sio vibaya kumsifia mtu lakini sifa zingine na comment zingine zinaendekeza inferiority complex kuhusu mnaowajua mi siwajui hao.Toa hoja yako kwa kujiamini usipapatikie mtu. Hoja hata ukiandika kindengereko ni burudani.
ReplyDelete