mdau hassan twaha ally na mai waifu wake mwanaidi ali araba wakikata keki kwenye mnuso wao wa nguvu ubungo plaza usiku wa kuamkia leo
bwana harusi akiwa na trupu zima la familia yake
bi harusi akimeremeta na trupu la familia yake
mbunifu wa mitindo aliyetengeneza mavazi ya maharusi alikuwepo kwenye rusha roho kinondoni usiku wa kuamkia jana
shughuli ni pilau. hapo bado ndizi tu, hassan na mai waifu wake walisahau kuagiza, ah!





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. asa we supu ulijua kuna shughuli kwanini hukubeba ndizi mfukoni?siku ingine ukumbuke mzee

    ReplyDelete
  2. Du! Bro kwa minuso nakuaminia. Ninauhakika hilo sinia lazima ulilimaliza...Hahahha.God bless u ili uendelee kutuletea news


    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  3. Du Michuzi Kiwavi Utamaliza Hiko Kisinia Kweli Mkuu??

    ReplyDelete
  4. big up maharusi!mmependeza, kila la heri ktk maisha!

    ReplyDelete
  5. The Rise and Fall of the Ze Utamu

    Wakati magazeti Binafsi yanaanza yalionekana ni Tishio kwa tabaka fulani, Chama tawala kikawa kinayaita magazeti hayo kuwa yanatumiwa na wapinzani na kuwa ni mali ya vyama vya Upinzani.

    Nakumbuka Gazeti la MAJIRA mara kadhaa lilipata msuko suko wa kufungiwa, Komandoo mpaka aliapa kuwa Majira haitagusa uso wa aridhi ya Zanzibar. Na hicho ndicho kisa kiliifanya Majira iende Online.

    Majira walipoandika kuwa mshahara wa mawaziri ni shilingi Milioni tisa Serikali ikaiita hiyo ni habari ya uchochezi, wakaifungia Majira na wananchi tukaiiunga mkono. Lakini Machoni mwa wenye Masirahi ilionekana ni gazeti la wahuni na la kichochezi.

    Ilikuwa hivyo hivyo hata kwa redio, wakaweka mpaka sheria kuwa zisitangaze zaidi ya mikoa 5. Leo hii MAJIRA na Hizi redio wanaheshima kubwa sana kwa jamii yote serikali mpaka Kijijini, maana sasa tunasikia BBC, Sauti ya Ujerumani, VoA, N.k Mapaka Kijijini kateroro Bukoba, kwasababu ya hizi redio.

    Vijana walipoanza kuimba nyimbo za kufoka foka na kuvalia suruali matakoni, wakaitwa wahuni na nyimbo zao zikaitwa nyimbo za wahuni, mara za vijana. Kila Mtu akisikia hizo nyimbo anaita Uhuni mtupu, hata maproducer maarufu akina Mster J. wakaitwa wahuni. Leo hii ukitaka kituo chako cha redio kisikilizwe basi usipige Bongo Flava. wameiita Bongo Falava kwani wanautambulisha kuwa ni mziki wa bongoland na wa wabongo na unaohitaji ubongo kuuimba, na kuusikiliza hata kuuelewa. Mambo huwa yanaenda yanageuka.

    Eric Shigongo alipoaanza magazeti yake alisemwa sana, watu wakayaita magazeti ya Mia mia, mara ya udaku mara ya mitaani, wakatafuta kila namna ya kutaka kuyaua,. Leo yapo hewani, Eric anaalikwa katika dhifa kubwa kubwa na anapewa nafasi kubwa sana. Hadithi zake zinasomwa na kila mtu, mpaka sasa watu wanataka Eric awashauri wasomaji wake kuwa waache kusoma Hadithi zake wasome Vitabu vya shule maana ametukamata, sawa sawa, si wakubwa kwa wadogo, wasomi na maimunas.

    Wakaja jamaa na Forum za mtandaoni, mafano ni hii moja iliyokuwa maarufu sana, JAMBOFORUMS. Ikawa inaandika habari za siasa, kukiwa na kablanda kadogo kawe ni tetesi hakajathibishwa, au iwe ni habari iliyotokea mchana kweupe, iwe na ushahidi iwe imefanywa kisiri siri wanaiianika wenyewe wanaiita Jamvini.

    Tabaka la watu waliookuwa wanashambuliwa na mtandao huu wakaja juu, tukasikia mpaka Bungeni wabunge wanashambuliana kuwa hizo ni habari za kwenye internet. Wakajaribu kuifanya Jamii ya watanzania iamini kuwa Internet sio source nzuri ya habari, kuwa internet ni sehemu ya porojo ambako huwezi pata jambo la maana. Wakasema kuwa internet ni sehemu ya watu wasio na kazi kupoteza muda na kuangalia picha za Ngono na kuchat mambo ya kijinga jinga na kuandika kwenye maforuma yasiyo na kichwa wala miguu, kuhusu wakayaita maisha ya watu.

    Wakafanya kila juhudi kuziua forum zote, wakaitafuta JAMBOFORUMS sana, upelelezi ukawekwa kila kona, baadaye wakawadaka vijana wawili na kuwaweka sero kwa kuwa waliwatuhumu kuwa wahusika wa huu mtandao. Wananchi wakaja juu, vyombo vya habari viakaungana kucondem swala kukamatwa kwa hawa vijana. Walipoona pressure kubwa wakasema huu ni mtandao wa kigaidi.

    Walipokuwa wamekosa ushaihidi wa ugaidi unaofanyika katika forum hiyo, na kama ni ugaidi, ugaidi gani utafanywa wazi wazi namna hiyo? Wakabadirisha hoja waksema mtandao umekuwa ukiandika habari za uongo ambazo hazijathibitishwa, wanataka waone habari za kweli. Sisi wnengine tukaona wamekosa Point, kwani wamelazimishwa kuchukua kila kinachaonikwa hapo jamvini? kama wanaona kuna habari zisizo za kweli wanaplatform za kukanushia hizo habari, wana wizara na kurugenzi zinazohusika na habari, kwanini wasikanushe? Na kuieleza dunia ukweli?

    Sasa leo hii amekuja kiumbe mwingine, huyu anajiita ZeUTAMU, duuu, Huyu tofauti na hao kaka zake waliomtangulia yeye habagui, hachagui, atakaye mzika hamjui. Maana yeye ili mradi ni picha imefika mikononi mwake inaruka hewani, kazi ya wadau wake kuchambua mchele na mawe. Akajiita anaendeleza uhuru wa kutoa maoni.

    Wakati dada zake ze utamu waliwashambulia watu wa tabaka la wenye pesa, walio kwenye madaraka, yeye haangalii usoni, uwe na cheo kikubwa au mkulima wa Sumbawanga wote mnapandishwa mbele ya hakimu, na hakimu anaangalia pande zote mbili, watu wanarusha mabaya na mazuri juu ya mtuhumiwa. Kitakachokuuwa hapo ze utamu, ni umaarufu wako uko mkubwa kiasi gani, na wanamna gani? Kama kuna tufununu kidogo tu kuwa ulilala na Fulani, mara ulikuwa umelewa siku Fulani na kuna mmoja kati ya baraza la mahakama hapo wanahabari zako wanalia na wewe, habari zako zinawekwa kwa herufi kubwa bila editing, kwa uwazi kwa kutaja kila kitu na kila kiungo kilicho mwilini kuelezea hiyo habari.

    Wale wale waliokuwa maarufu kwa kuwachambua wenzao wa tabaka la Juu, tabaka la wenye hela, tabaka la watawala kwa kuchangia kwenye magazeti, redio na forums, wakawa wapo kwenye hatari ya kuwekwa kwenye tanuru la moto wa hukumu ya zeUtamu.

    Wameaanza kuhaha, wameanza kukimbia huku na huko wanapwayuka jamani ze Utamu, ze Utamu, hatendi haki, anakaba mpaka kwenye Penati, wamezama kuomba masaada wa kusaidiwa, jamani tunakufa tusaidieniiiiiiiiii,.
    Tulipokuja kuwauliza kuna nini? tukasikia, amekuwa akfuatilia maisha binafsi ya watu. Maisha binafis ya watu ndio yepi? Je Wema Sepetu, Latoya, Richard, Edward Lowassa, Rostam Aziz, Salama Jabir, na wengine wengine mliowatundika kwenye redio, magazeti na Forums zenu hawana maisha Binfsi?

    Sisi wengine wenye akili zetu tunadhani ZeUTamu anapigwa vita kwasababu amekuwa tishio la kuwaumbua hata wale waliodhani wako safe, kwani wao waliona hawako katika tabaka la watawala wala watu wenye fedha nyingi, wakajua wapo salama wao kazi kuwajadili hao wenzao. Sasa ZeUtamu amekuwa tishio,.

    Wengine wamesema awe anaweka piha za watu walio uchi tu, kwani kila Fisadi wa Ngono anapiga picha za Uchi? Alafu kwani kupiga picha za Uchi ni kosa? Kwa mujibu wa nani? Kwa hiyo kama tunakubaliana kuwa Uzinzi na uasherati ni tatizo acha wote tuliopiga picha za uchi na za kwenye Nguo tuwekwe mbele ya haki tuhukumiwe sawa sawa na matendo yetu. Uzinzi ni uzinzi, uasherati ni Uasherati kwa namna yoyote ile uwe na Nguo uwe umevua.

    Ze Utamu nayo imekuja kama Vyombo vingine vilivyokuwa vimekuja, nayo itapita tutakuja kuioona fashion nyingine kama Jerry Springer, Cheaters zikija Bongo hivi karibuni, Tutashangaa kuwa ilikuwa nafuu ya ze Utamu, kwani yeye aliweka picha hata huwezi kuthibitisha kama ni kweli yanayosemwa. Na ze utamu washabiki wake ni wale wanaotembela internet tu,fikiria naweka kipindi change cha cheater EATV, wangapi watakiangalia ukilinganisha na zeUtamu? Hizo zinazokuja zitakuwa mbaya zaidi maana zitakuwa na motion, sauti na picha nzuri, Tutasemaje???

    Huu ndio Utandawazi, lazima tukubali, dunia haijatulia inazunguka na kila kukicha kunavichwa vimefikria jambo jipya. Jiwekeni tayari ku-cope na mabadiriko haya. Ishi maisha yako ambayo hayatakufanya uguswe kwa vikashfa kashfa visivyo na kichwa wala mikia. Kubadiri wasichana na wanaume tumelihalarisha limekuwa ni jambo la kawaida sana kwenye jamii zetu sasa hivi, kiasi kwambe mtu kutembea na wasichana sita saba tunasema hayo ni maisha yake binafsi….

    Utamu atakufa tayari nimesikia kuna http://www.zemnato.blogspot.com kuendeleza kazi pale atakapoishia ZeUTamu,,,, kazi ipo kweli kweli… Mpaka tukafike,….. Sijui.
    KuMbo

    ReplyDelete
  6. duhh michuzii ze fulanazzz.....

    ReplyDelete
  7. Michuzi, sasa hiyo ni sahani au sinia? Aisee...nadhani ulisubiri kwa hamu huo msosi...Halafu hiyo fulanazz ndiyo imechoka sana...time to retire!!

    ReplyDelete
  8. DU! BRO MICHU BASI HUACHIII HATA HARUSINI PIA HUISAHAU HIYO ZE FULAZZZZZZ..... NA HIYO TABIA YA KUTUONYESHA MINUSO IISHE MWENZIO NNA MWAKA SIJAITIA MDOMONI HIYO PLAU KISHA UNALIBEBA SINIA ZIMA PEKE YAKO?SIKU NYENGINE UKIALIKWA NIJULISHE ANGALAU NA MIMI NIJE KUFAIDI KIDOGO MAANA CHA SHUHULINI NI KITAMU SANA

    ReplyDelete
  9. Hiyo picha ya pili hakuna hata mmoja aliyevaa suiti inayomtosha. Ukauzu mtupu.

    ReplyDelete
  10. Duh, brother michu mie hiyo ze fulanazzz tu. kwa kweli ulichagua kitambulisho bomba cha blog yetu ya jamii. Endeleza libeneke mithupu, maarusi jaman kila la kheri.

    ReplyDelete
  11. haki ya nai vile,,iyo sinia tuu yan udelele wantoka apa,lote ilo lako?

    za fulanazzzz idumu milele!!

    ila michu mbona uwa wapenda sana kulia ktk sinia??

    ReplyDelete
  12. mmh michu mate yamekutoka mwana,,nimependa ilivyokuwa simple,hongereni saaaana

    ReplyDelete
  13. my wife wa michuzi hebu tafuta fulana nyingine za my husb wako

    ReplyDelete
  14. Nimependa sana picha ya bibi harusi na familia yake,
    WANAWAKE WAMEVAA MAVAZI YA HESHIMA!!!!!!!!!
    Hongera sana !
    Mdau Ughaibuni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...