
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akimzawadia zana za jadi za kabila la kimasai kiongozi wa operesheni ya kumata meli haramu Keith Govender.

Meli ya maharamia wa uvuvi iliyo kamatwa katika pwani ya maji kina kirefu ya tanzania ikivua bila kibali na imekutwa na shehena ya samaki tani zaidi ya 70 elfu.

JK akipokea zawadi ya kapelo toka kwa kiongozi wa meli inayoendesha operesheni ya uvuvi haramu katika bahari ya hindi, Keith Govender, leo Ikulu, Dar, alipowapokea ili kuwapongeza mabaharia wa meli hiyo iliyofanikiwa kukamata meli moja haramu. meli hiyo ilikamatwa juzi katika eneo la ukanda wa bahari wa uchumi, ambako maharamia hao walipoona vyombo vya operesheni hiyo waliongeza mwendokasi wa meli yao na kukimbia, lakini hawakufanikiwa na kukamatwa baada ya kutishwa kwa silaha. Operesheni hii imefanikiwa kwa kushirikisha nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambzo ni Kenya, Msumbiji, Afrika Kusini na Namibia, ambazo zimetoa wataalamu wake na vifaa kusaidia kudhibiti wizi huu.

JK akimpongeza Nwabisa Lutshete, mwanamama pekee baharia aliye katika meli hiyo ya kusaka wavuvi haramu katika hafla ilofanyika leo ikulu, dar
Je Kenya ni mwanachama wa SADC?
ReplyDeleteShukrani John Pombe Magufuli.
ReplyDeleteKama pia tungekuwa na umoja na moyo huu wa kuwakamata manahodha wa vyombo vya walarushwa na mafisadi basi nchi yetu ingekuwa bora sana na yenye maendeleo makubwa.
ReplyDeleteBILA MSAADA WA AFRICA YA KUSINI SIJUI TUNAWEZA KUJITEGEMEA KWA JAMBO LIPI?!SIFA YA NCHI NI UFISADI TU NA.......NCHI KAMA HAINA WENYEWE VILE WAVUVI HARAMU WANA VUA TU MIAKA YOTE HIYO.KWANI HATUNA JESHI AMA POLISI WA MAJINI KULINDA RASILIMALI ZETU???????????????
ReplyDeleteNafikiri hapo juu inatakiwa isomeke operesheni "...dhidi ya uvuvi haramu..." siyo "ya uvuvi haramu...". Halafu kabla hawajasifiwa sana wangeombwa wasogee kidogo pwani ya Somalia kule wakirudi ngangari wapewe nishani...
ReplyDeletelabda tujaribu
ReplyDeleteMELI YA UVUVI HARAMU,
MELI YA WAVUVI HARAMU
Inawezekana yote makosa kipi kiswahili sahihi kuhusiana na hicho kichwa cha habari?
miaka 50?wanavua?na hatukuweza kuwashika?tuna fish tani 70?na hii ni meli 1 tu so iyo miaka hamsini lets say meli 10 kwa mwaka 10x50=500ships +kila meli ilivua tani 100 za aina tofauti za samaki,so 500x100=50,000/tani
ReplyDeleteso mtauza ao TUNA FISH?
Yesu wangu!!aya maajabu wal'hahi,afu tuna askari sijui maji.
kenya sio mwanachama wa SADC,kwani iko kusini?wao wako na somalia ukoillions of money!!
sinilwaambia coast to coast on the way to tz sasa tumefika natumekamata na tutaenda pwani ya somaliland kupambana na pirate soon lakini waingie ktk jumuiya yetu kwanza au vp
ReplyDeleteMungu atuwezeshe kuendelea na hii operesheni uvuvi haramu. Isije tu ikawa nguvu ya soda.
ReplyDelete"MELI YA UVUVI HARAMU"vs"MELI YA WAVUVI HARAMU"
ReplyDeleteKwa kiswahili ninachokijua mimi, ambacho pia sijui ni kama fasaha ama la meli haiwezi kuvua bila kuwa na watu, katika hili ndiyo wavuvi. Hivyo, watu, ambao ndiyo wavuvi wanakuwa accused kufanya huo uvuvi haramu. Kwa hiyo kiswahili changu MELI YA WAVUVI HARAMU ndiyo sahihi, mnasemaje wadau.
Pompidou.
Langestrasse 7,
Rostock.
Germany
sentesi ya mwanzo inasema hivi " JK akipokea zawadi ya kapelo toka kwa kiongozi wa meli inayoendesha operesheni ya uvuvi haramu katika bahari ya hindi, Keith Govender, leo Ikulu" huo ni utata mkubwa sana michuzi!!! nadhani neno operation limekupiga chenga maaba yake. hapo una maanisha kuwa kiongozi huyo anaongoza uvuvi haramu wakati hiloo sio yeye anaongoza operation ya kuzuia uvuvi haramu. umeona tafauti ya maneno hapo?
ReplyDeletekiswahili sio kigumu ila uandishi mwengine unashangaza sana mimi naomba kuonyesha hii sentesi
ReplyDeletewalipoona vyombo vya operesheni hiyo waliongeza mwendokasi wa meli yao na kukimbia, lakini hawakufanikiwa na kukamatwa baada ya kutishwa kwa silaha.
hawakufanikiwa na kukamatwa? ni kiswahili kibovu? sasa kama hawakufanikiwa na kukamatwa mbona tunaambiwa kama walikamatwa?
Waswahili kwa ujinga,wamekalia kubishana na kukosoa lugha iliyotumika badala ya kutoa maoni...Ubabaishaji,watu wafanya uvuvi wa haramu na kutengeneza pesa nyie mmekalisha wowo zenu kubishana na kufikiria kufanya ngono tu!ACHA WAVUE TU SISI TUKO BIZE NA KUSAHIHISHA LUGHA ILIYOTUMIKA KATIKA KUTOA HABARI HII
ReplyDeleteMmETIA CHUMVI HAPO KAMA SI HAMIRA TANI 70ELFU HATA HIYO MELI YENYEWE haijafikisha hizo tani.
ReplyDelete