Ndugu Michuzi,
kupitia mtandao huu wa jamii,ninapenda kuwatangazia watanzania wote katika jiji la Dallas na maeneo yote ya Marekani kwamba, Kanisa la Umoja litakuwa na ugeni mkubwa kutoka nyumbani Tanzania kuanzia tarehe 1.5.09.
Kwaya ya Azania Front Cathedral kutoka D.S.M itakuja kumsifu Mungu katika jiji la Dallas.Tunaomba kila moja atakae soma tangazo hili amjulishe mwingine.Kanisa la Umoja ni kanisa ambalo limeanzishwa na linaendeshwa na watanzania pamoja na watu mbali mbali wanaozungumza lugha ya kiswahili.
Mpaka sasa kanisa hili limeshaleta waimbaji mbali mbali katika jiji hili la Dallas kama Cosmas Chidumule, Rose Muhando, Mkasa junior,Mfalme Daudi na watumishi wengine wengi kutoka nyumbani.
Mwisho tunapenda kuwakaribisha watu wote katika ibada zetu siku za jumapili kuanzia saa kumi na mbili kamili jioni mpaka saa mbili kamili. Kumbuka kuna mafundisho maalumu ya watoto.
Anuani:
12727 Hillcrest,
Dallas
Teaxs 75230
Simu:
214 554 7381,
682 552 6402,
817 875 4764,
469 2791762.
Karibuni sana.
Mnaonaje safari ijayo muwaalike wasabato masalia,maana ni karibu mwaka sasa wanasubiri zali kama hilo.
ReplyDeleteKwa aliyetuma hiyo habari nafikiri haiko sahihi, mimi nikiwa ni miongoni mwahao wanakwaya sisi tumepata mwaliko toka kanisa la kilutheria la Oklahoma City kupitia mwanakwaya mwenzetu aliyerudi toka huko Oklahoma. Naomba kurekebisha hilo.
ReplyDelete