Kaka Michuzi kwanza shikamoo.
Pole kwa libeneke la kuijenga jamii na ahsante kwa kutupa taarifa na habari za nyumbani kila uchao.
Napenda kuwajulisha wadau kuwa leo ni mwaka mpya wa Kiirani unaojulikana kama Nauruzi au mwaka koga. Jana saa tisa na dakika 13 mchana, uliingia mwaka mpya wa 1388 wa Kiirani wa Hijiria Shamsia. Mwaka mpya huu kwa sherehe na sikukuu ya siku 15!
Napenda kuwajulisha wadau kuwa leo ni mwaka mpya wa Kiirani unaojulikana kama Nauruzi au mwaka koga. Jana saa tisa na dakika 13 mchana, uliingia mwaka mpya wa 1388 wa Kiirani wa Hijiria Shamsia. Mwaka mpya huu kwa sherehe na sikukuu ya siku 15!
mashule na maofisi hufungwa na kuna likizo ya wiki mbili. Siku ya leo ambayo inasadifiana na kuanza msimu wa machipuo (spring season) husherehekewa na watu wote wa Iran na baadhi ya nchi zenye utamaduni wa kifarsi kama Afghanistan, Pakistan, Tajikistan, Azerbaijan na nchi nyingine za Asia Kusini.
Watu huvaa nguo mpya, hutembelea ndugu na marafiki na kufunga safari ya kutembelea miji na maeneo mbalimbali. Kwa mila na desturi za Waiirani siku ya Naouruz kwa hakika ni siku ya ukarimu na urafiki. Waliogombana hupatana na walio mbali hupigiana simu huku wale waliotengana wakionana tena.
Miongoni mwa desturi ya mwaka mpya wa Kiirani ni kuwa pamoja familia wakati muda wa mwaka mpya unapowadia. Kila nyumba hutayarisha meza yenye vitu 7 vinavyoanza na herufu "s" ya kifarsi. ( picha nimeattach hapo juu)Vitu hivyo ni Sib=Tufaha, Samanuu= uji wa ngano, Sumak= fuu, Serker= siki, Sombol=maua, Sekkeh= sarafu za dhababu (gold coins) na Sir=kitunguu thomu.
Katika meza hiyo huwa pia na picha ya familia, kitabu kitukufu cha Qur'ani, makomamanga, mayai yaliyopambwa na samaki aina ya goldfish kwenye kibakuli cha kioo. Pia huweka majani ya kijani ambayo ni ishara ya kuanza msimu wa machipuo na kioo ambacho wanaamini ni ishara ya mwanga na nuru.
Usiku wa mwaka mpya watu hula wali kwa samaki. Nawatakia kheri na fanaka wale wote wanaozungumza kifarsi(kiajemi) na wote walioko Iran. Mwaka mpya mwema kwa wale wanaoujua.By the way mwaka koga wa Zanzibar unahusiana na mwaka mpya wa Kiirani. Historia inasema kuwa, mwaka koga unaosherehekewa kila mwaka Makunduchi Zanzibar ulianzishwa na Wairani waliotokea Shirazi, Iran miaka ya nyuma na kuhamia Zanzibar.
Pia Rais Obama pia ametuma ujumbe kwa mara ya kwanza Iran na kuwapongeza Wairani kwa kuanza mwaka mpya huo, suala ambalo linaonekana kuwa ni katika jitihada za kuboresha uhusiano na pande mbili ulioharibika muda mrefu.
Habari zaidi nenda
/ap_on_go_pr_wh/obama_iran
Nawakilisha
Ni mimi mdau wa Tehran.
Ahasante sana mdau mwenzetu kwa kutuelimisha. Hii ndiyo faida ya blog na wanaojitolea kama wewe kuelimisha jamii. Nakutakia mwaka mpya wenye baraka tele na afya njema.
ReplyDeleteElias - Kinshasa.
Well written and educative inf. Imejipanga, inavutia msomaji, inatoa ufafanuzi, haichi mashaka pia. Big up
ReplyDeleteShurani kwa maelezo ya hitsoria ya mwaka mpya wa Iran.
ReplyDeleteSalam kwa Watangazaji wa Radio Irani idhaa ya KiSwahili hasa da WaridiPoleJeusi.
Duh
ReplyDeleteAsante sana mdau,Ujumbe mzuri unaelimisha na umeuandika hata asieelewa ataelewa ,
Big up
SHUKRAN DADA WARIDIPOLEJEUSI,KWA KAZI NZURI SANA YA KUELIMISHANA.
ReplyDeleteNilikuwa sijui kabsaa asili ya mwaka koga, Ingawa kwetu huufanya kila Muharram , twavaa nguo mpya na kukoga Baharini.Nikijua tu ni mila za Washirazi wa Afrika ya Mashariki.By the way sio tu Makunduchi , bali Pwani yote ya Africa Mashariki kwenye watu wenye asili ya Kishirazi(Afro-Shirazi).Nimeyakuta haya Mombasa, Malindi, Lamu, Kiunga , Raskamboni mpaka huko juu Kisimayu(kisima cha juu jamani).
ReplyDeleteAhsante kwa kuelimisha jamii, mungu akubariki sana
ReplyDeleteNdugu Mdau,
ReplyDeleteHappy Mwaka mpya wa Iran,
Iran inaonea sana wananchi wake, hasa wasichana, inaendeshwa kinguvu. Tafadhali rudi nyumbani kwa sababu hailipi kabisa kuishi huko. wairani wengi wanakimbilia Canada kama wana uwezo au Dubai kutokana na kutokuw ana uhuru. Sisi wairani tuliozaliwa bongo tunashukuru sana kutokaa huko, madada zetu wan uhuru. Serikali ya Iran inafuata siasa kali ya kislamu ya kishia na watu hawana uhuru, nadhani unajua kila kona kuna askari na huwezi hata kupata denda kokote.
Pia, tuna habari zote ulizoziandika katika internet sasa, dunia imekuwa ndogo.
Mpaka hapo serikali ya Iran itakuwa kama ya enzi za shah, basi hao kina Obama ni maneno tu, wabunge wao wanatawaliwa na Israel, ambaye ni adui wa Iran. Sioni njia yoyote wataelewana leo au kesho wakati Iran inataka bomu lake kama wayahudi. Maneno ya White House ni porojo tuu.