
wadau wapendwa hii sio postikadi ya pasaka bali ni taswira ya hali halisi ya libeneke la leo ambapo umeme umekuwa na kwikwi toka saa kumi hadi saa hizi saa tano na ushee hivi usiku. hivyo imebidi niendeleze libeneke kwa njia hii huku nikiomba chaji ya kompyuta (toka china hahahaa) isiishe na mshumaa usikatike maana umebaki huu mmoja tu, na maduka wamefunga, na pia kibatari hakina mafuta. dah! yaani noma kweli unaambiwa. bongo tambarare kweli hakyanani....sijui dowans itaanza lini kazi toba!
KAENI NA KIZA CHENU SI MNAMSAPOTI FISADI MNAFIKI MWAKYEMBE ANALETA UNAFKI WAKE WA KUISHINIKIZA SERIKALI ISINUNUE JENELETA KWA AJILI YA MASLAHI YAKE YA KUTAKA KUANZISHA KAMPUNI YAKE NA SERIKALI KUENDELEA KUPOTEZA MABILIONI YA PESA
ReplyDeleteDUH poleni sana michuzi,nadhani hii ni dalili tosha kwamba dowans inaanza kazi hivi karibuni LOL!
ReplyDeleteEndeleza libeneke nasie hatulali ayaa!
mafisadi sio watu..tayari wamewapa mlungura mafundi wa tanesco ili walazimishe kiza??
ReplyDeletehiiiiii sio miezi ya umeme wa mgao kwani maji mtela yapo bweleleeeeee!!
hii ni noma kwa JK kwani mwakani asije akahukumiwa kwa uzembe wa akina Rashid na timu yake ya Dowans!
POLENI SANA!!.
ReplyDeleteBONGO BADO NI TAMBALALE SASA JAMANI SI UTUMIE JENELETA MGAO UNAWENYEWE BWANA AU NDIYO UNAWASAPOTI KI SAIKOROJI??
NINATAMANI MUWASHITAKI HAO WATU WANAOENDESHA SHIRIKA LA UMEME TZ MAANA NAONA KAMA NI WABABAISHAJI WAKUBWA. AU WALIFOJI VYETI VYA ELIMU WALIODAI KUWA NAYO??.
Mr, michuzi karibu mwz kwani hakuna mgao wa umeme waala nini achana na rongorongo la dar joto kali na umeme wa mgao na juu yake
ReplyDeletehewa chafu kwa ajili ya msongamano na mara kiboko msheri.
watakuzeesha njoo ule sato na nembe achana na samaki chuchunge kazi kuchonga mdomo tu kama samaki chuchunge.
Maumivu ya kichwa huanza polepole...
ReplyDeleteWhaaaaaaaat?
ReplyDeleteThanks kaka Michuzi kwa kutuonyesha hali halisi ya nyumbani.
Be careful na mshumaa usijeunguza nyumba.
Jamani, Pole sana kaka and thanks for doing all this for us.
Thank you much!
kazi kweli! na wewe umejiunga katika mkondo wa kushinikiza mitambo ya dowans inunuliwe?!
ReplyDeletehahah! pole sana mdau kwani hiyo ni kali! sasa hifadhi hiyo chaji ktk laptop yako kwani hata kesho hautakuwepo...actually hautakuwepo kwa muda usiojulikana...! hahah! pole sana!
ReplyDeletePole sana ndugu yetu!
ReplyDeleteMi kwa kweli kila nikiangalia wenzetu huku ambavyo wanakimbia kimaendeleo,na hapo kwetu Tz ambavyo hakuna anayejali wala kufanya lolote huwa nasikitika sana. Mambo ya maana huyatilia mkazo na kuyatimiza hapo kwetu TZ ni aibu tupu kila mtu anajali aweke tumboni mwake, hakuna leo wala kesho. Siasa wanazopigwa wananchi ni nyingi sana kuliko matendo yenye kuleta maendeleo!
Mi kwa sasa najipanga niwawekee wazazi wangu solar pannel wapate angalau mwanga wa kuona na kucharge simu zao.
Inasikitisha sana tena sana, Mi nina miaka sita hapa nilipo sijawahi kushuhudia maji wala umeme ukikatika! Moto huwa unawaka mara kwa mara na matetemeko ya ardhi lakini serikali itahakikisha watu hawakai gizani muda mrefu hata kama kuna janga ni kubwa.
Watanzania tuwe serious basi! Yaani ni bla blaa tuu, hakuna hata mwenye uchungu. Labda kuwe na sera ya kufanya kazi masaa 24 kila sekta, halafu hao Tanesco waseme watu wasifanye kazi kisa hakuna umeme! Siku zote matatizo yapo, wameshatatua kiasi gani mbali na kupiga siasa tuu! Kila kukicha ni bora jana!
Watakuwa wameiba mafuta ya Transfoma. Adhabu wilaya nzima.
ReplyDeleteIla bongo kuna vikwazo, maji,umeme,luku, foleni za magari, dowans, EPA, Alex Stewart, IPTL, SUMATRA(Nauli za daladala). Tutafika kweli?
Wanasiasa wote matapeli, wana maslahi binafsi. Mh Warioba aliwahi kuuliza Bungeni, ni nani hajawahi kutoa rushwa. Wote walikaa kimya.
ReplyDeleteRASHID ALISHASEMA!!! HUO NI MWANZO TU WA KIZA KINENE! ANY WAY TUMESHAZOEA!
ReplyDeleteNATI
яNDUGU YANGU WA MARCH 21?2009 4,46 AM UMESEMA JAMBO LA MAANA SANA,SASA WATANZANIA TUWE SERIOUS,TUNAPIGISHWA SIASA HAKUNA LOLOTE WANALOFANYA!WATANZANIA TU MASKINI SANA NA HUTUSONGI MBELE,TUMERIDHIKA NA UMASKINI WETU NA KUDANGANYWA NA SIASA CHAFU ZA WANASIASA!TUANZE SASA KUWEKA NCHI MBELE NA WANANCHI WAKE NA SIO MTU MMOJA MOJA,YOTE HAYA MATATIZO YA UMEME NA MENGINE MENGI YANATOKEA KWA SABABU YA UBINAFSI WA WATU WACHACHE TU!!HAWA VIONGOZI WETU HUKU NJE HAWAJI???KWEA NINI HWATAMANI NA NYUMBANI KUWE NA MAANDELEO PIA KAMA KWA WENZETU!!NCHI ZA WENZETU TUNAKAA MIAKA YADI KUMI BILA KULALA KIZA NA MAJI PIA YA KUTOSHA UNATUMIA KADRI UWEZAVYO NA NI NCHI ABAYO HAINA MAJI MENGI KAMA SISI TZ!!HIVI TUNAAKILI KWELI WATANZANIA???KAKA MICHUZI UNACHOVUMILIA NI NN,HIZO TABU AMBAZO KWA VIONGOZI HAO HATUONI MWISHO WAKE?? VYOUNI HAPO TZ WANAFUNDISHWA NINI SASA AU NDIO HIZO SERA SA CCM ZA KIMASKINI NA KIFISADI,UKISEMA UKWELI WANAKUAMBIA UITAKII MEMA NCHI NA AMANI NA UTULIVU WAKE!YA NINI AMANI NA UTULIVU WA NCHI WAKATI KIFIKRA WANANCHI HATUNA AMANI??WATANZANIA TUFANYE MABADIRIKO NA MAAMUZI ILI TUENDELEE,LAZIMA TUANDAE MAISHA WA WAJUKUU WETU,KAMA SASA NINA MIAKA 20 HIVI BASI TUKIANZA KUFANYA MABADILIKO KIDOGO KIDOGO BASI WAJUKUU WETU WATAKUJA KUISHI KWENYE TANZANIA YENYE MAJI,UMEME,VYAKULA,MIUNDO MBINU BORA NK!!
ReplyDeletePost card ya Pasaka!!!! umeniacha hoi,teh teh teeeh
ReplyDeleteunaweza kutengeneza post card nzuri sana kwa picha hii hata hivyo.
Pole kwa mgao wa umeme though.
Koku
matokeo ya mechi ya premier league England leo 21/3/2009
ReplyDeleteFulham 2 ManUTD 0. Fulham walipata goli la kuongoza ktk kipindi cha kwanza baada ya Paul Scholes wa ManUTD kuunawa mpira ktk box na kula kadi nyekundu.
Fulham waliongeza bao la pili kipindi cha pili cha mchezo. Pia Wayne Rooney wa ManUTD alilambishwa kadi ya pili ya njano dakika ya 88 na kupelekea kupewa kadi nyekundu.
Matokeo hayo ya Fulham kuifunga ManUTD yanafanya ligi hii kuzidi kuwa tamu, maana sasa ManUTD itabidi wakaze buti ili kutimiza ndoto yao ya kuwa mabingwa.
wewe mtoa maoni wa kwanza mwenye matatizo ya kuelewa
ReplyDeleteSoma hii ni kutoka ippmedia
Mwambalaswa(MB) ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco, alisema kwa mfano, tafsiri inayokubalika ni ile inayotolewa na mahakama au wanasheria kwamba kama mmoja ana kampuni na zinashiriki katika zabuni moja iliyotangazwa, mhusika anatakiwa kisheria kutangaza maslahi yake mapema na kujitoa.
Alisema hakuna mgongano wowote wa kimaslahi kwa Dk. Mwakyembe katika suala hilo, isipokuwa kumekuwa na tatizo la uelewa.
Juzi Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alifafanua kuwa hakuna mgongano wa kimaslahi kwa Dk. Mwakyembe kuwa na hisa katika kampuni ya kuzalisha umeme kwa madai kwamba ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.
Alisema kuwa ni jambo la kawaida kwa wabunge kuwa katika kamati mbalimbali hata kama wanafanyabiashara zinazofanana na masuala yanayoshughulikiwa na kamati zao.
hamna conflict of interest hapo na rostam asimuite mwakyembe mmbaguzi ukienda kwenye kampuni za wahindi viongozi wote ni wahindi. lazima atutetee sisi wabatu rostam angekua analipenda taifa hili asingefanya hayo
mdau uk
WEWE MBEBA MABOX UNAEJIITA MDAU WA UK INAONESHA NI JINSI GANI USIVYOFUATILIA DATA!!NYINYI NDIO WATUMWA WA KIMAWAZO MPAKA LEO HII MSIO NA UCHUNGU NA NCHI YETU NA NDIOMAANA MPO TAYARI KUISHI KITUMWA HUKO BADALA YA KURUDI NYUMBANI KUJENGA NCHI.
ReplyDeleteHIZO HABARI ZA IPP MEDIA KILA MTU KAZISOMA NA KAMA HUJUI KWA TAARIFA YAKO HAYO MAGAZETI YA IPP NI MASHABIKI WAKUBWA WA MWAKYEMBE NA NDIO MAANA HAWAKUANDIKA MAHOJIANO YALIYOFANYIKA KATI YA WAHALILI NA SLAA,KAMA YALIVYOFANYA MAGAZETI MENGINE.
PIA WAMEANDIKA KINAFKI MAHOJIANO KATI YA LIPUMBA HAWAKULIANDIKA KAMA ILIVYO MAHOJIANO HAYO HAWAKUZUNGUMZIA KUHUSU MASLAHI KAMA WALIVYOFANYA MAGAZETI MENGINE WALICHOFANYA WAO IPP KUANDIKA HABARI ZA HOTUBA YA RAISI TU WKT LIPUMBA ALIZUNGUMZA MENGI
KWELI KABISA KESI YA NYANI HUWEZI KUMPELEKEA NGEDERE NI SAWA NA HII KESI YA ROSTAM UMPELEKEE MWAKYEMBE WKT WOTE MAFISADI KILA MMOJA ANATETEA MSLAHI YAKE MATOKEO YAKE SISI WANYONGE NDIO TUNAOUMIA.
ReplyDeleteHUWEZI UKAMPA TUME MFANYABIASHARA AU KUTUNGA SHERIA ZA NCHI MFANYABIASHARA KWA MASLAHI YA NCHI BILA YA YEYE KUTETEA KWANZA MASLAHI YAKE.
NISAWA KABISA NA UGOMVI WA MWAKYEMBE NA ROSTAM NI WA KIMASLAHI WANATUDANYA SISI TU WOTE WACHAFU WAKUBWA.
KWANINI BAADA YA KUGUNDUA KUA RICHMOND NI KAMPUNI YA KIFISADI WASIISHAURI VIZURI SERIKALI KWA KUNUNUA MITAMBO YAKE BADALA YA KILA SIKU KUKODI NA KUPOTEZA VEZA ZA WALIPA KODI NA NDIOMAANA AKAONA DILI KUANZISHA KAMPUNI YAKE MAANA YEYE SI NDIO YUPO JIKONI ANAJUA MASLAHI YA UMEME.
HAWA WATU BUNGENI SASA HIVI WAMETENGENEZA KAMBI KWA HIYO WASITUCHANGANYE WAKAENDELEA KUITAFUNA NCHI YETU.
MAGAZETI NAYO YAMEJENGA KAMBI AKIYAMUNGU WENYE UZALENDO NA NCHI NI WACHACHE MNO UKILINGANISHA WALIOKUA NA UZALENDO NA MAKABILA NA MASLAHI YAO BINAFSI.WANANCHI MPAKA VIONGOZI WAO WOTE SAWA TU NA NDIOMAANA NCHI KILA SIKU MASKINI KWA UPUUZI KAMA HUU.
UTAKUTA MTU ANAMTETE ROSTAM AMA MWAKYEMBE KWA MASLAHI YAKE BINAFSI EITHER KWA UKABILA AMA VIJISENTI NA KUSAHAU MASLAHI YA NCHI.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Ni pale tu tutakapoacha UBINAFSI ndipo mambo yote yatakaponyooka.
ReplyDeleteMe nawashangaa saana nyie watanzania mnaolalamika kuhusu umeme...Oooh Kibatari.......Ohh giza...Utamaduni wa Muafrika ni nini? Me nafurahia sana ninapowasha kibatari ndani kwangu kwani inanikumbusha utamaduni wa muafrika kabla hatujaingiliwa na Wakoloni..Yani najihisi raha ndani ya roho..
ReplyDeleteNyie mnafurahia mnaenda sehemu za makumbusho kuangalia mambo ya zamani wakati hata nyie wenyewe wakati fulani mnaweza mkajibadili kwa muda mkafanya vitu kama vya zamani...Angalao jikumbushieni Uafrika sio kufuata Modern technology tu. Wahenga cha kale dhahabu...ndio hicho kibatari sasa..
Mmang'ati Original
huyojamaa anayeweka matokeo ya mechi za FA huku ni umeme kwakwe ulikatika akachanganyikiwa au naye ni fisadi?
ReplyDelete