Nani anawaua watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, nchini Tanzania?
Kwa nini jamii hii inawindwa na kuuawa kikatili?
Na je hatua gani zinachukuliwa kuwalinda?
Haya ndiyo maswali ambayo najaribu kuyatafutia majibu katika blog hii. Jiunge na mimi Vicky Ntetema katika safari yangu ndefu ya kutafuta majibu kwa maswali hayo yote.
Nakukaribisha kuchangia kwenye blog hii kwa kutuma maoni yako na pia kuuliza maswali ambayo nitakujibu endapo yatakuwa chini ya uwezo wangu.
Karibu sana!
---------------------------------------------------
Glob ya jamii inapenda kuwa ya kwanza kumpongeza Da'Vicky sio tu kwa juhudi zake na weledi katika kupambana na janga hili la kitaifa, bali pia kwa yeye na BBC kuiongezea hadhi fani ya blog ambayo kwa mshangao na masikitiko makubwa hapa kwetu Bongo bado haijaingia akilini mwa wadau wengi kwamba ina umuhimu mkubwa katika jamii katika kupasha na kupashwa habari kama vilivyo vyombo vingine vya habari.
Uamuzi wako Da'Vicky wa kuendeleza libeneke nimeupokea kwa mikono miwili na natarajia wadau wengi wataungana nami kudiriki kusema kwamba uamuzi huu ulitakiwa uchukuliwe siku kibao zilizopita. Hata hivyo kuchelewa huko nina imani kulikuwa na sababu za msingi ambazo hazikuweza epukika.
Nikiwa kama mmoja wa wadau wakuu wa teknohama ya blog nachukua nafasi hii kuipongeza BBC kwa kufunua macho wadau wa habari kwamba kuna haja ya kuanza kuiangalia fani ya blog kwa jicho jipya. Kwamba wanaofaidika ni wachache kwa kuwa vifaa kama kompyuta na mtandao wa intaneti ni haba sidhani kama ni sahihi, kwani kwa uzoefu wangu teknohama inakua kwa kasi sana na watumiaji ni wengi kuliko inavyodhaniwa.
Isitoshe kuanzia mwezi Juni mwaka huu, ama miezi mitatu tu toka sasa, huduma ya fibre optic itayorahisisha na kukuza sekta hii inaweka bayana kwamba huko tuendako teknohama itashika hatamu. Hivyo si vibaya kujiandaa na mapema kuikumbatia kwani huduma ya teknolojia ya mawasiliano itazidisha kasi ya upatikanaji wa vifaa na matumizi yake kwani spidi ya intaneti itakuwa ya kufa mtu na itasambaa kila mahali.
Hapa namaanisha kwamba wakati umefika fani hii ya blog ianze kutambulika kama fani rasmi na sio kibwagizo, ukizingatia kwamba kuna wanaobeza ama wasiokubali kwamba blog ni chombo muhimu, kikubwa na cha lazima katika jamii kama vilivyo vyombo vyote vya habari vinavyoonekana kuwa ni rasmi.
Wakati ni kweli kwamba kuna blog ambazo katika jamii ni mwiba na shubiri kwa mpigo, lakini si uwongo kwamba takwimu zinaweka bayana kwamba si blog zote zenye mlengo huo. Kwa hesabu za haraka haraka utakuta kati ya blog takriban 100 za kiswahili zilizopo hewani, si zaidi ya tatu ambazo ni mwiba na shubiri kwa jamii. Haina haja ya mtu kuwa mwanasayansi kukanusha kwamba 'si samaki wote waliooza'.
Hivyo basi natumai wahusika wataanza kufunguka macho na mawazo (naongelea Bongo na blog za Kiswahili tu) kwamba fani hii ni muhimu katika nyanja ya habari na ina nguvu pengine kuliko baadhi ya vyombo vya habari vinavyotambulika kuwa ni rasmi. Takwimu za watembeleaji blog dhidi ya vyombo vingine inathibitisha haya, na hata haiingii akilini kwa nini Bongo tunakuwa wa mwisho kumaizi vitu vilivyo wazi kabisa kama hivi.
Ni ajabu kukuta kuwa hapa Bongo ni Daily News na HabariLeo tu vyenye blog kwenye tovuti zake (www.dailynews.co.tz) wakati wengine wanasuasua bila shaka kwa kuogopa kuhusishwa na blog zenye miba na shubiri.
Jamani tuamke, wenzetu (mfano ni huu wa BBC na pia vyombo vingine vya nje ikiwa ni pamoja na vya jirani zetu Uganda, Kenya, Zambia n.k.) wako hatua kumi mbele, sasa sie sijui tunamsubiri afande mnali aje (hahahaa, utani) ndio tuamke???
Sina nia ya kubeza mtu ama chombo chochote. Msisitizo wangu hapa ambao nitauvalia njuga hadi kieleweke ni kwamba naomba blog zitambulike kama vyombo rasmi vya habari kama ilivyo kwa vingine.
Na ikibidi, tena bila kuingiliwa uhuru wa kupasha na kupashwa habari, katika kuelekea huko kwenye kutambulika rasmi, blog ziingizwe kwenye orodha ya vyombo rasmi vya habari kwa njia yoyote inayostahili. Kumbuka pamoja na kupasha habari pia blog sio tu zinaweza kuwa chanzo cha ajira kwa jamii bali pia zitapanua wigo wa habari kwa kiwango cha juu.
Nimalizie kwa kuipongeza tena BBC kwa kumruhusu Da'Vicky kuanzisha libeneke na kutoa rai kwamba huu uwe ni mfano wa kuigwa na waandishi wa habari wa vyombo vyote. Vicky Ntetema ameonesha njia kwamba inawezekana kabisa kwa waandishi kuanzisha libeneke la aina moja ama nyingine ya mada mbalimbali kama ambavyo yeye alivyochagua ya albino.
Kunahitajika libeneke la aina mbalimbali kama vile elimu, wanawake, watoto, ajira, utamaduni na michezo, uchumi na fedha, miundombinu na kadhalika. Orodha ni ndefu na walio katika libeneke kwa sasa hawatoshelezi kukidhi mahitaji. Mwenye macho asikie na mwenye masikio aone.....
-Michuzi



MESSAGE TO MASHAKA....!
ReplyDeleteMICHUZI KWANZA KABHISA NINGALI PENDA KUKUSUKURU KWA KUIWEKA HII MADA HADHALANI BIRA UOGA. MIMI NAANZA KWA KUSEMA MASHAKA NILIMWAMBIA BILA UOGA NI UJINGA KUENDELEYA NA KUTUPA HABARI ETI KURETA KANYA BOYA NI MADHALA MAKUBWA KWA UCHUMI WA NCHI YETU NIKAFANIKIWA KUMJIBU KITAALAMU NAZANI WENGI WALIYAONA WAKAKUBALIANA NAMI NA WENGINE WAKAYAPINGA. SASA UNAONA HATA WEWE UMEONA UMUHIMU WA HAWA NGUDU ZETU KUISHI KAMA SISI. SASA MASHAKA TUPE MWANGA NINI KIFANYIKE SIYO TUU KUTUPA MAMBO YA KANYA BOYA NA CHINA. LETE DATA ZA MAALUBINO BWANA CHINA WANAOTAKA KWENDA KUNUNUA KANYA BOYA HIYO NI JUU YAO UCHIMI WETU HAUTAKUFA KWA SABABU YA KANYA BOYA ILA MAENDELEO HAYATA PATIKANA KAMA JAMII MOJA ITAENDELEA KUONEWA NA KUPUKUTIKA, MASHAKA UNAWEZA KUNIJIBU KAMA UTAPENDA LAKINI KUANDIKA KINGELEZA CHA KUKALILI KWENYE VITABU VYA YULE MUTUNZI JAMES HARDLEY CHASE SIYO KIPIMO CHA USOMI KISWAHILI NI LUGA YA KUJENGA TAIFA NA UCHUMI WETU NI UTI EWA MGONGO. ASANTE BLOTHER MICHUZI KWA JUHUDI NA MAARIFA. NI MIMI EX MUZUMBE CHUO KIKUU CHA MUROGORO MUZUMBE.
Ni kweli Chuzzi(singular),Michuzzi(plural),tunakumbushana tu lugha wkati huu wa Breakfast!Naungana na wewe katika kumpongeza Vicky kwa jitihada zake hizo,naamini zitazaa matunda na zita ongeza miwashawasha miongoni mwa vijana wetu katika kufungua Blog za nguvu zitakazo endeshwa kitaalamu zikiwa na masuala muhimu na ya msingi kuhusu maisha ya kila siku ya jamii.BADO LIPO PENGO KUBWA SANA katika nyanja hii ya kupashana habari kwa sekunde moja tu kwa njia ya Blogs!Its a very effective mass communication tool!Its a tool against poverty of the mind!INFORMATION IS POWER!No doubt,information is still a very expensive commodity.But thru the Internet,Blogs have made this horrible task of seeking a multitude of information which you would otherwise have to buy daily and weekly newspapers at great expense to access,now you can do it at a tap of the finger!It may still be a bit of a problem to most us living in the remote rural areas,BUT ATLEAST for now THERE IS AN EASIER AND MUCH MORE FEASIBLE ALTERNATIVE than anyone would have thought of in the most recent past!So,Vicky congratulations for the courage to show the way!Bado tutataka wasomi wetu na wale wote wenye ujuzi maalum (specialised skills)wafungue Blogs zao,iwe kupitia Michuzi which will be a lot easier thru one window!or each on his or her own,fine!Zipo Fani nyingi sana.Tunachohitaji ni "serious blogs for the serious minded",na siyo Blogs za Kitoto!Blogs sio kitu cha kitoto,zinasomwa ulimwenguni kote na watu wa rika mbalimbali na wenye upeo wa kufikiri wa ngazi zote kuanzia kina sisi hadi maprofesa katika fani zao.KWA WENZETU WATANZANIA ambao wako mbali kabisa na nyumbani,walioko Ughaibuni,Blogs ni nija pekee na ya uhakika kwa kupata habari za matukio ya huku nyumbani,na pia ni njia pekee kwao kuweza kutuma habari na ujumbe kwa ndugu,jamaa na marafiki walioko huku nyumbani na kupata majibu ya haraka sana kwa gharama nafuu sana.Jitokezeni zaidi lakini kwa nia njema.Wasomaji hawakawii kuziponda Blogs zilizojaa Utumbo,Majungu na Fitna,Matusi na Ufisadi!The Choice is Yours!,,,,,yrs,tonnie,the only!
ReplyDeleteAibu tupu yaani watu wameanza kutafuta umaarufu binafsi kutengeneza jina katika suala hili la kusikitisha?!!Njaa mbaya sana....!
ReplyDelete