Mh. William Geleja akisalimiana na Waziri Mkuu Mh Mizengo pinga. kati ni Mbunge wa Igunga Mh Rostam Aziz


Mpango wa serikali kutaka kuyanunua majenereta ya kuzalisha umeme ambayo yaliletwa nchini na Kampuni ya Dowans katika mkataba wake na kampuni feki iliyoumbuliwa ya Richmond hautokani na kulazimika kufanya hivyo bali hali halisi ya hali ya nishati nchini ndiyo inalazimisha serikali kupanga kuchukua hatua hiyo.




Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja alipozungumza na tovuti hii hapo jana kuelezea kile ambacho kinaonekana mgongano wa kimtazamo kati ya Wizara, kamati mbili za Bunge na hisia za makundi ya Watanzania.



Akizungumza nasi kwa kirefu Mhe. Ngeleja amejenga hoja kuwa suala la ununuzi wa mitambo hiyo halihusiani na masuala ya kifisadi kama wengi wanavyohisi huku yeye mwenyewe akisema kuwa "siyo wote mafisadi". Bw. Ngeleja alitumua muda mrefu kushawishi kuwa mpango huu ni mzuri kwa maslahi ya Taifa na kuna kila sababu ya kuangalia kwa ukaribu na kuubali.



Ni kwa kiasi gani ameweza au anaweza kushawishi uamuzi ni wawasikilizaji wetu wenyewe. Unaweza kusikiliza mahojiano hayo kwenye tovuti yetu hii au kwa kusikiliza kupitia tovuti yetu ya


http:/www.mwanakijiji.podomatic.com


ambapo unaweza kuyapata mahojiano hayo kwenye Itunes au Ipod yako.




Sikiliza wewe mwenyewe kama Mhe. Ngeleja amejenga hoja ya kukushawishi kukubali serikali inunue mtambo huu au ungependa serikali isiendelee nao.



Sisi katika tovuti yetu tutatoa msimamo wetu kwenye kijarida cha Cheche kitakachotoka hapo kesho.



Title: KLH News Episode: Mahojiano na Mhe. William Ngeleja kuhusu Dowans




Enjoy!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. 1. ngeleja, Dr Rashid wantuna wajinga kweli watanzania. Asanteni sana.
    2. Dowans ni ya wapi, Dowans ni ya nani? Hivi wewe ndugu msomaji ukiwa na mke mzuri au gari zuri, au ng'ombe mzuri si utapenda uonekane na ujulikane kwamba kile kitu chake kizuri ni cha fulani. Sasa mbona hawa wa Dowans wanajificha na haijulikani ni wa wapi, hata Ngeleja hajui lakini anataka kununua mitambo yao.Tumekwisha watanzania. Kama mwenye nacho anajificha na haijulikani anatokea wapi hii nisababu tosha ya kusema kitu chenyewe kibaya.
    3. Zito, pole kaka. Hoja za kijinga za wababaishaji na wewe umezikubali?? Hili ni doa amabalo hutaweza kulitakasa katika maisha yako yote ya kisiasa. Pole sana kaka. Walikupa shilingi ngapi maana siamini kuna nguvu ya hoja hapa?
    4. Serikali ya Tanzania itaacha lini kutoa kazi na kufanya biashara na vijikampuni uchwara vya mfukoni na vinavyoibuka ghafla kama uyoga hususan kufanya kazi maalum na serikali ya Tanzania- havikuwepo kabla ya kazi ya Tanzania haijajitokeza na vinapotea kazi ya Tanzania ikiisha? Richmond, Dowans ina historia ya muda gani na inatoka wapi na imewahi kufanya kazi wapi tena ndugu Ngeleja? Na je Richmond inafanya kazi wapi dunia hii sasa au ndiyo baada ya Mwakyembe kuitusua ndiyo basi tena? Ehe na wale makaburu eti walijidai wana uzoefu wa kuendesha makampuni ya nishati wako wapi sasa au vile vile kwishnehi?
    5. Rohoni mwenu mnajua hoja ya kununua Dowans ni ya kitapeli. Mtu amekushitaki alafu mnasema tununue mitambo yake. We Ngeleja na wewe Rashidi hivi katika maisha yako binafsi na kifamilia unaweza kufanya hivyo? Mtu kakushtaki umemwibia mifugo yake au mke wake alau unasema nataka kununua gari lake ili nitatue tatizo langu la usafiri. Kiama kipo jamani tena si lazima kiwe katika ulimwengu ujao, kinaweza kuibuka hapa hapa. Usitushauri kitu ambacho wewe huwezi kufanya.

    ReplyDelete
  2. Huyu benson mwakyanjala au mwanakijiji au lula mwana nzela kwenye raia mwema ni mtu mmoja anabadili majina tu,

    anatumiwa na MBOWE kuisakama serikali ya jk.kila kitu hakifai yeye yuko DETROIT mambo yake ya uhamiaji hayajaa vizuri anasubiri msamaha wa obama kwa illegal migrants ili aweze kuja nyumbani,

    anataka tugombane wakati yeye yuko kiguu juu marekani.

    kwanini asimuhoji MBOWE anayemfadhili kumfungulia hizi website na kukidhamini kijarida za cheche kwenye nia ya kuichafua serikali ya jk tu.

    amuhoji MBOWE juu ya kifo cha chacha wangwe kwa kusema kuwa Chadema ni chama cha wachagga na pia wabunge wa viti maalum wote wametoka kilimanjaro na ndugu au wapenzi wa viongozi waandamizi wa chadema kama ndesamburo ana mtoto wake anaitwa lucy kapewa ubunge bila kikao chochote cha chama, komu ambaye ni mkurugenzi wa fedha mchagga kampa mkewe anna komuu ubunge,

    Mwanakijiji wewe umeondoka umeona bongo haifai sasa tuache na bongo yetu acha kutugombanisha.

    kamuhoji tajiri yako Mbowe kwa kula ruzuku za Chadema kwa vile wewe umelipwa dola elfu mbili za website?

    pia wewe si ndiye kila siku unaikandia michuzi blog mbona unaleta ujinga wako kwa michuzi hapa hapa? hata jina la jamii forums mmeiba BRAND ya michuzi yenye slogan ya blog ya JAMII.

    Naomba waziri anayehusika kuwapiga stop mawaziri kufanya mahojiano na mtu asiyejulikana au anayeficha jina lake kila mara anatumia majina ya bandia.makala zake ni chuki na sumu kwa serikali tu.
    Mswahili wa JF.

    ReplyDelete
  3. Wadau, ingawa nimechanganya mambo. Naomba mwenye kufahamu ilipo SANITARIAM CLINIC, nataka kumwona Dr Isack Ndodi. Huyu Dr alikuwa anahojiwa saaana Channel Ten. Mara ya mwisho alisema yuko Mwembechai, nimefika pale, kibao anachosema kipo kuelekeza alipo, sikioni. Tafadhali! Just write here, I will read.

    ReplyDelete
  4. Watanzania wenzangu, naomba tukubaliane kuwa si kila jambo ni ufisadi. najua kuwa tumeshagonwa na nyoka kwa hiyo hata tukiona unyasi tunashituka. suala la mitambo ya umeme ni suala muhimu sana. hii ni mitambo majeneleta ya kuzalisha umeme iliyoletwa kwa lengo la kuongeza mgw 100. kununua mitambo mipya ya namna hii ni usd 86 milioni na kununua hii iliyopo ni kalibu 55 usd milioni. tanesco wanaidai kampuni hii kalibu 8 milioni usd. wakinunua na kutoa deni itakuwa kama 48 milioni usd. hapa ni kuwasha tu mitambo na kufanya kazi. ikiwa italetwa mipya itachukua kama miaka 2 kukamilika na kuifunga, hii ni kwa mujibu wa taarifa za magazeti. sasa jema ni lipi maana taifa siku chache zijazo litatumbukia katika giza zito la umeme. hivyo tusubili miaka miwili ili tupate mitambo kama hiyo ama tuwashe mitambo hiyo na tuwe na umeme?
    Mimi nina amini kabisa kuwa hata hao mnaopinga mitambo isinunuliwe mtakuwa wakwanza kulaani mtakapo kuwa gizani. kama wataalam wametuhakikishia kuwa mitambo itafanya kazi kwa muda mrefu, basi tuungane na tanesco ili waweze kuinunua mitambo hii. tusijiingize katika siasa zitztumzliza na tutakuwa wa kwanza kuoneshana vidole.

    ReplyDelete
  5. ROSTAM AZIZ ndani ya kundi, dah!!!
    Ama kweli kuuvunja mtandao ni sawa na KURUDISHA JINI KWENYE CHUPA

    ReplyDelete
  6. Serikali ya Kikwete isijaribu kununua hiyo Mitambo Ya Dowans hata kama ni kwa Robo Ya Bei Yake Halali!This will have Devastating Political Consequences on his political career!Ikishanunuliwa na serikali wapo watakao jisifu kwa majigambo,kwamba,"Kiko wapi sasa,tulipoiagiza sisi mitambo hiyo ya Dowans kwa dharura,mlituona sote hatuna akili,mkatushutumu kwa matusi na kjeli za kila namna eti sisi Mafisadi,wabaya wetu wakashinikiza hadi Mawaziri kuachia ngazi,sasa kiko wapi?Mbona sasa mmeshika adabu na mmeamua kuinunua kuhofia Giza (ambalo halitakuwepo f.y.i)".Je,bado mnayo jeuri ya kuendelea ktuita sisi Mafisadi? Sijui utajibu nini!Mitambo hiyo acheni kabisa,imesha ingiwa Najisi!Huko ni kuhalalisha Uhalifu.Na hilo likipata baraka za serikali,basi utawala wa Kikwete utaingia Doa ambalo hakuna atakaye weza kulifuta!Na huo ndio utakao kuwa Wimbo Wa Kampeni za Uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu Ujao!Wake Up Kikwete!Wajinga wana angalia Matumbo yao tu,hawana lingine!They Dont Care whats gonna happen to this country or to Kikwete's political future!Hatuyahitaji hayo ma Mitambo ya Dowans!Kama ni Giza wacha Lije!Tumeishi miaka mingapi bila ya Dowans?Nani huyu anayetaka kutuzuga na kutugeuza sote wajinga kiasi hicho?Kick Ngeleja out of the Ministry,he is an "Eye - Sore"!Mitambo hiyo ikinunuliwa tutajua ni Kikwete aliyeinunua,na siyo mtu mwingine!Hapata kuwepo kusingiziana tena kwamba ni kosa la Waziri Mkuu,"yupi?"

    ReplyDelete
  7. Mimi nashangaa kwanini watu wanaogopa kukosolewa! naamini kama mtu hataki kukosolewa ni kutaka kuficha udhaifu wake kiutendeji.
    Tukirudi katika mada ya Dawons, kusema ukweli ni kichekesho hasa kwa wale walioweza kusoma gazeti la Mwanahalisi la leo tarehe 04-01-09, kuhusu hali halisi ya maji katika mabwawa yetu ya Kidatu na mtera kuwa ni nzuri sana.
    Hapa kinachoonekana ni WIZI mtupu wa Idrisa rashid ambae pia ni mshirika wa Rostam kibiashara na kibaya zaidi inaonekana kijana Zito Kabwe tayari amenasa ktk mtego huu ambao utamfanya asaulike katika orodha ya mashujaa wa Tanzania kwa kukubali kurubuniwa na Rostam.sote twajua Idrissa ni Fisadi, kumbukeni mgao wake wa dola 600,000 toka kwa fisadi Chenge kama mgao wake wa RADA!!!

    Mungu Ibariki Tanzania ya Mwalimu Nyerere.

    Mangi wa K'koo

    ReplyDelete
  8. Naungana mkono na Anonymous 4:46 AM.Cahdema ni chama cha kichaga na kwa hiyo ni hatari kwa nchi hii tena hatari sana. Lakini hapa tuzungumze ya Ngeleja na Rashidi na utapeli wao.Ikibidi kuongea ya Chadema na ukabila basi tuweke nafasi nyingine thread togfauti na tulichambue hilo peke yake.Michuzi anzisha hiyp thread basi ya Chadema na ukabila na tuanze kuchangiya. Ukweli wa mambo chama pekee chenye sura ya kitaifa ni CCM- lakini duh! si maskandali hayo na ulafi huo na utapeli.Inaeleke kila chama tulichonacho kinatuweka pabaya kwa namna yake wananchi wa Tanzania.

    Anonymous 9.39 AM- chonde chonde ndugu yangu tusianze kuleta tabia ya kutoheshimu sheria kwa sababu eti wakubwa walisinzia na hawakujua watanzania wanataka umeme kiasi gani na wakaitumia kujishipisha na kukwapua mali ya umma. Jamani ndugi zangu nchi hii na tuliyo wengi wanyonge tunahitaji utawala wa sheria maana mkubwa ana njia nyingi ya kujilinda kama hakuna sheria.Hatuwezi kukubali eti Rashidi kasinzia hakujua watanzania watataka umeme kiasi gani kwa hiyo anataka kununua mitambo ya Dowans kampuni ya swaiba wake Rostam.Hivi President wa uchina alipokuja alikuwa wapi kwa mfano asipendekeze msaada wa majenereta?? Na viongozi wote wengine ambao wanapita hapa ambao wana uhusiano mzuri na Tanzania je sekta ya nishati inapewa priority au haipewi ili tununue umeme Majenereta ya Dowans Rostitamu? Kuvunja sheria ya ununuzi ni kubariki utapeli wa Ngeleja/ Rostam/Rashid.nai hajui wote wamioja hawa na Ngeleja kaingia siasa akiwa ametoka VODACOM ambako Rashid alikuwa Mkuriugenzi Mkuu na Rostam bado ni shareholder mkubwa tu na Godgather wa Ngeleja kisiasa ni Rostam. Rostam kamwingiza Ngeleja siasa. Tunajua. JK anatakiwa kuisafisha sekta ya nishati inanukla rushwa usanii na utapeli. Acheni longolongo eti itakuwa chipa.......... JK safisha sasa la sivyo 2010 ndiyo hivyo tena...............

    ReplyDelete
  9. Michuzi nakuomba sana kwa heshima ya blogu yetu, usiweke picha ya Rostam humu. Leo nakuachia lakini ukirudia navunja kompyuta.

    ReplyDelete
  10. amenichekesha sana mchangiaji hapo juu wa 8:56 PM, sasa ukivunja computer nani ataingia hasara!! cafee au computer yako! Du!!!!

    ReplyDelete
  11. SERIOUSLY

    NAUNGANA NA ANNON APO,,MICHUZI MWISHO NA MWANZO KUMBANDIKA ROSTAM AZIZI UMU BLOGUNI,KM NI WAO NA MTANDAO WAO KIVYAO

    usituchafulie hewa umu ndani wal'hahi!!!
    alaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...