Halo kaka michuzi naomba plz ukipata muda utuwekee hii picha ni pale Daraja la Nduruma Arusha ambalo baada ya kuwa chanzo cha ajali kibao sasa yamewekwa matuta ya kufa mtu na gari zimeshika adabu kidogo...
--
Meshack c.Maganga
Tumaini university
www.pichanamaishatz.ning.com
meshackmaganga@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mh, mbona sasa ninaona njia zetu za kutatua matatizo hazieleweki, hivi unapoweka matuta hapo, hawaoni kuwa ndiyo kitakuwa kituo cha majambazi kuteka magari? au wataweka askari 24/7?

    ReplyDelete
  2. Hongera kwa viongozi wa Usalama Barabarani mkoani Arusha kwa kuchukua hatua hiyo muhimu iliyokuwa inasubiriwa na wengi. Watu tumechoka na ajali za kila siku; watoto wengi wanabaki yatima, wake na waume wanabaki wajane, na maisha hayana tena thamani nchini mwetu kwa sababu ya wazembe wachache. Trust me man, that's the way to go, mwenye haraka, aanze safari yake mapema. The next step, Traffic department wafanye kazi na Insurance compananies ili madereva wanafanya AJALI kwa UZEMBE wapandishiwe bei za BIMA zao maradufu. Hii itawafanya madereva waheshimu sheria za barabani, na maisha ya Binadamu kwa ujumla. Kuhusu hoja kwamba majambazi watafaidika na hatua hii, natumaini kikosi cha polisi na traffic, ambavyo vyote vipo chini ya WIZARA moja, wanatambua suala hili na ni jukumu lao kulipa kipaumbale. Lakini kusema kwamba tuwaachie hawa madera wasio na nidhamu kuendelea kuua watu will be a crime againts humanity.Statistics shows that 80% of our road accidents are caused by driver error, intoxication, and other human factor, human factor!!!
    Its bout time we hold our drivers accountable.
    Mdau-Quebec

    ReplyDelete
  3. Nashukuru sana kwa kuwekwa matuta hayo.Nilishashuhudia ajali moja maeneo hayo ambayo iliua watu zaidi ya kumi papo hapo.Afadhali kuwe na foleni na raia wawe hai.

    ReplyDelete
  4. Bora maisha ya watu waokolewe. Haraka ya nini?

    Hata hapa USA wakiweka matuta na vizuizi vingine ajali zinapungua. Panga 'extra time' kwa ajili ya safari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...