kocha wa taifa stars marcio maximo toka brazil akiwa na wakongwe wa soka ambao toka shoto ni kipa james kisaka, kipa juma pondamali na beki athumani chama.
kwa heshima na taadhima globu ya yamii inaanzisha mjadala wa kumjadili kocha maximo kwa nia ya kupata mawazo ya wengi baada ya kutolewa katika michuano ya CHAN kule ivory coast majuzi ambayo ndiyo ilikuwa ni kipimo tosha cha uwezo wake katika muda wa miaka miwili ya mkataba wake.
1. je, maximo amefanya kile alichokuja kukifanya?
2. mwezi julai mkataba wake unamalizika, je aongezewe ama aondoke?
3. kuna haja ya kuwa na kocha wa nje ama tubaki na wazalendo?
wakati ni kweli globu ya jamii inakaribisha maoni ya aina yoyote kuhusiana na mstakabali wa maendeleo ya soka nchini, si uwongo kwamba maoni yatayochafua hali ya hewa hayafai na hayatoona mwanga wa jua. hivyo mdau unaombwa utoe maoni bila jazba ama kashfa ili tujenge badala ya kubomoa.
-michuzi
Hi Bloggers,
ReplyDelete2. Kama nakumbuka vema, alitoa msimamo wake mwenyewe huko nyuma kuwa mwezi wa saba ni mwisho kwake na lazima aondoke. Tusije sababisha malumbano bila kujua msimamo wake kwa sasa.
Sasa Michuzi kama unaweza kumuuliza nini anawaza kwanza ndo tujadili juu ya yeye kuendelea kama yuko tayari kuendelea endapo tutaonyesha kumhitaji.
1. Mimi naona vijana wanapiga ball safi. Matokeo mazuri hayaji kama upepo, yanatafutwa na kutengenezwa. Hivyo tuko njiani kufuata maendeleo bora kisoka kama itakuwa aruta kontinyua. Hivyo naona alifanya kazi yake iliyomleta.
3. Kama Assessment itafanyika na kuonekana tunaye kocha mzalendo mwenye ujuzi basi hata mzalendo atafaa. Kama hakuna basi tuukubali ukweli kuwa tunahitaji kocha, wala hakuna miujiza. Kusema ukweli sijaona kocha wa kiwango cha makisimo, wote wana longolongo tu, Mtu kama Mziray ni kelele tu, mara kushoto mara kulia kweli sijaona msimamo wake.
Ni hayo tu kwa leo,
Sauti toka nyikani, Norway.
Kama anapenda kuondoka aondoke lakini mimi naona ametutoa mbali. Tulikuwa na makocha wengi wazalendo lakini hatukufika hatua hii na matokeo yake wachezaji wengi wazuri ambao leo tungekuwa tunajivunia japo wanacheza au walicheza soka ya kulipwa hawakutambulika mfano wangu binafsi ni Edibilly Lunyamila yule kijana angekutana na Maximo enzi zile tungekuwa tunajivunia hilo jina nje ya nchi. sasa umri umekwenda hawezi tena kucheza na akina Ngasa, umaarufu wake umeishia Tanzania, hakuna anaye muenzi
ReplyDeleteNadhani TFF ingemuongezea mkataba wa kufundisha vijana wadogo ili kuandaa vijana wa Timu ya Taifa kwani amefundisha watu ambao tayari vichwa vimesha ota kutu na sasa kuanza kupiga msasa ni kazi kwelikweli
ReplyDeleteSerikali imsaidie Kanali Kipingu katika mradi wake wa kuandaa vijana (vipaji) kwenye upande wa Soko basi wamlipe huyu Mbrazil awe mwalimu wa hawa vijana wapya kuandaa timu ya baadae. Hivyo apewe mshahara toka serikalini pesa ipo. kwani hataandaa kijana au timu moja ni vijana wengi watakao zaa timu nyingi na mashurhuri
ReplyDeleteMichuzi tusipoteze MUDA jamaa ni mtu mzima hivyo uamuzi anao mwenyewe.
ReplyDeleteHakuna kocha atakaye fanya miujiza kwa Tanzania we have to start from UMISHUTA NA UMISETA AGAIN
ReplyDeleteHaya maswali muuulize MUNGAI kwani ndio alijidai elimu haiendi na michezo matokeo yake ndo haya.
ReplyDeleteserikali irudishe michezo mashuleni bank nyingi zipo tayari kutoa sponsorship. MAXIMO ABAKI
MKATABA UONGEZWE AKIPENDA
ReplyDeletesioni alichofnya mziray wala kibadeni wala mkwasa
mjadala wako ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu
ReplyDeleteMaximo ni kama mwalimu wa darasa la saba.tunamshukuru kwamba alitutoa darasa la kwanza tukiwa bado hatuna ujuzi wa kusoma wala kuandika.sasa tunaingia sekondari kidogo angalau tunaweza kujivuna kwamba tunajua kusoma na kuandika.lakini tunahitaji mwalimu mwenye ujuzi zaidi ambaye ataweza kutufundishia timu yetu katika madarasa ya juu zaidi.Ushauri kwa TFF,itakuwa ni vizuri wakitafuta kocha mzalendo sasa,apelekwe kozi za ukocha nje kuongeza ujuzi ikifika julai hiyo apewe timu.
ReplyDeletemafunzo kwa kiswahili ni effective zaidi kwa aina ya mfumo wetu na mfumo wa ligi.wachezaji wanakuwa wakiwa hawana msingi mzuri wa ukocha.
ni hayo kwa leo
MADA YA LEO MZURIIII MICHUZI HUYU BWANA MAKSIMO ASEME ATAONDOKA ASISEME ATAONDOKA DAWA NI KUONDOKA TUU KWASABABU WEWE TANGU HUYU BWANA AJE HAPA NCHINI HATUJAPATA HATA KOMBE LA CHALLENGE BADO MNASEMA KIWANGO KIKUBWA KWELI JAMANI WADAU,SASA KILA AWALI ANAVUNJA KIKOSI INAKUWAJEEEEEEEEEEE...KAKA NGATUNGA
ReplyDeleteKaka Michuzi nafikiri huyo wa kwanza kushoto ni Sunday Manara "computer".
ReplyDeleteKatika kujadili inabidi tuwe na vigezo. Kuhusu kocha mzalendo tu "assume" kuwa atapewa support ya aina aliyopata Maximo ya fedha, uongozi wa nchi (kuanzia rais na bunge), wafanya biashara, TFF n.k. ndipo tuje katika mafanikio ya timu. Tusipozingatia haya tutakuwa tunalinganisha vitu ambavyo vina mazingira tofauti kabisa na makocha wa zamani tutakuwa hatuwatendei haki. Timu wakati ule ilikuwa haina hata fedha za kambi, viongozi wanahangaika kutafuta fedha, leo wanaweka kambi nje ya nchi. Hayo yalikuwa nia maelezo ya kuweka mjadala sawa ila nadhani Maximo kafanya vizuri kazi yake iliyomleta.
ReplyDeleteHello Bloggers,
ReplyDeleteMimi kwa mtizamo wangu tangu Maximo aanze kazi hata ule moyo wa kuiangalia timu yetu ya Taifa umerudi tena.Level of sponsorships vijana wanapata inajidhihirisha ni jinsi gani hata makampuni yanavyovutiwa na jinsi timu yetu ya taifa inavyocheza na matokeo inayoyapata.
Zamani ilikuwa timu kama za Zambia,Senegal na nyinginezo wakija kucheza na Tanzania wanajua ah,hizo ni points za bure tu BUT these days timu zikija bongo au zikicheza na Tanzania wanaogopa wakijua vijana wapo vizuri n mpira wanaucheza.Program aliyoandaa Maximo ya soka la vijana pamoja na kuinua viwango vya soka itakuja kufanikiwa siku za usoni na sio lazima leo.Wachezaji leo hii kwenye ligi kuu wanajituma ili Maximo awaone waitwe kwenye timu ya Taifa.Discipline imeongezeka Taifa Stars na ujinga ujinga wa zamani kwenye technical bench haupo sasa hivi.You can actually tell the way timu inavyoendeshwa kuwa ni kisayansi.
Watu wengi wanajua kuwa kwa sasa ukiwa kwenye timu yetu ya taifa ni ajira tosha na you can use that time to make your mark.We have to admit that kwenye dunia ya leo,National Coaching ni kazi full time kama nyingine though kwa wale wadau wa Chelski watanikanusha BUT what I'm saying is a good coach utamjua kutokana na plans zake,technical ability awapo kwenye match pamoja na reaction anayopata kutoka kwa wachezaji.This guy amekuja kukiwa a language barrier kwenye timu yetu na yeye BUT look at what he did to the team pamoja na mental strength ya wachezaji.Nisieleweke vibaya hapo kwenye language barrier but imehamasisha vijana wengi watake kuichezea timu ya taifa kutokana na kitu watakachokipata from Maximo.
Hakuna kitu ambacho siyo negotiable under the sun.We can still convince him to stay and sign another contract that can even help him to fulfil his project.Pesa tunayo and instead of mafisadiz kuzikomba,zinaweza kutulipia coach atupe raha Watanzania kwenye hii dunia iliyojaa matatizo kila kukicha.Soka ni mchezo ambao humfanya mtu asahau matatizo yake kwa muda,and that is what we need - Happiness hata kama ni for 45 minutes.Mbegu inapopandwa jamani haioti hapo hapo,it will take some time BUT tumeanza kuona kijani kibichi kikijitokeza and let him finish his project tule result za mbegu.Kuna makocha wengi wa Kitanzania ambao wamesomea ukocha LAKINI track records zao zinaridhisha kwenye timu ya taifa?Tusimpe mtu a project only to test him "kama anaweza".Tufanye kitu kwa umakini na uangalifu.Kwa sasa ukipoteza pesa inauma sana kwa jinsi hali ilivyokuwa ngumu duniani pote,kwa hiyo tufungue macho na kuondokana na sera za chuki binafsi au U-SIMBA NA U-YANGA.Kama slogans za TFF ya sasa zilivyo - kuendeleza soka kwenye dunia ya sasa ya kisayansi na tecknolojia,basi ndivyo tunavyotakiwa.Watu wengi kama wanataka mtu abaki kwenye contract,negotiations huwa zinaanza mapema na sio usubiri mpaka mtu anakwambia kuwa anaondoka wiki ijayo ndio wewe unaonyesha nia ya kum-retain.That is a sign of insanity.Kama kweli we are determined to keep him,we should at least try to convince him to sign a new rolling contract now.Na pia tuwe wajanja kuwe na clauses ambazo zitatu-favor sisi mwishoni maanake sisi kwa wabongo kwa contracts....
Asante kaka Michuzi,
Mdau,Oxford.
maximo anatakiwa sasa kupicha makocha wengine tanzania iwe kama chelsea sio arsenal kila siku eti mwakani tunataka vikombe na kucheza kwenye mashindano makubwa sio kila siku anaandaa tuuu kwa sasa naona tunahitaji kocha kutoka europe na sio brazil, maana brazil hakuna makocha, makocha wazuri wote wanatoka europe ndio wanasomea ukocha wabrazil ni vipaji tuuu kama wakina mziray ndio maana wanaweza kuwafundisha wabrazil wenzao, na mpira stail ya mpira wa brazil ni tofauti na staili zingine ndio maana hata wachezaji wa brazil hawaonekani sana i meean hawangari sana europe kama wengine, tunatakiwa kucheza kwa nguvu
ReplyDeletenaona niishie hapoo nawezi kuandika sana halafu nikakosea bure i mean nikatoka nje ya topic
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, ameshaonyesha kuwa na imani na kuridhika na mafanikio ya Timu ya Taifa chini ya Maximo.
ReplyDeleteNakwakuwa ndiye anayemlipa mshahara na kuifanya kazi ya Maximo kuwa rahisi tofauti na walimu wengine waliomtangulia, ni imani yangu kuwa wapenda soka tumpende au tusimpende Maximo, ataendelea kuwa kocha wa Timu ya Taifa, labda yeye mwenyewe amwambie Mhe Rais J.M Kikwete, Basi!.
Pia naamini mahusiano ya kiutendaji ni mazuri kati ya Maximo, TFF, Baraza la michezo la Taifa ,Serikali kuu na wafadhili pia wadau wa soka, Je unamkumbuka PEPE aliyeletwa na FIFA,kama mtu wa ufundi ndani ya iliyokuwa FAT?
Aliondoka mwenyewe bila kuaga.
Kwa maana nyingine Maximo ni kama Arsene Wenger wa Arsenal.. matokeo ya uwanjani hayawezi kuathiri ajira yake hata kwa dawa!
Na endapo Maximo ataondoka basi mazingira mazuri yaliyomfanya apate matokeo mazuri ya kazi yake kwa kipindi chote cha ukocha wa Taifa, yapewe pia kwa mwalimu atakayekuja, awe mzalendo au mgeni hii itatoa uwiano sawa wa kuwapima kimafanikio.
Baadhi ya walimu walimtangulia kama, Msolla, Mziray. Magram,Msomali,Bendera,Kinanda nk, hawakuwahi kufanya kazi yao katika mazingira tulivu kama ya Maximo.
Mimi nadhani Maximo amejitahidi mno na anastahili pongezi. Kufutwa kwa michezo mashuleni nalo ni tatizo lakini kikubwa tuanze kuelimishana kuwa michezo ni ajira na zianzie hata majumbani wazazi wawaeleze watoto wao sio kuwazuia kucheza. Pia vilabu vyetu vya michezo vinatakiwa vianze kuwekeza kwenye watoto mashuleni ili kuibuwa vipaji vya michezo.Mwisho nawaomba watanzania kuwa uzuri wa kocha sio timu kushinda bali ni kiwango cha mchezo. Mbona timu kubwa za Ulaya nazo huwa zinafungwa? Tuwe tunakubali ukweli.
ReplyDeleteAongezewe muda, kwani kabla yake Taifa stars haijawahi kufanya miujiza kama ya sasa, anafaa sana maksio.
ReplyDeleteNI BORA KAWAELEKEZA WASIO JUWA NA KUTAMBUA UTAWALA KATIKA KUENDESHA SOKA NA MICHEZO KWA UJUMLA,KIUWEZO HANA ZAIDI YA HAPO ALIPOISHIA SOKA BADO NI MBOVU NIDHAMU HAIJAKUWA YA KURIDHISHA KUKOSA KIKOSI CHA KWANZA MPAKA ATAONDOKA,HAKUNA HATA KOMBE LA MBUZI ALILOSHINDA(HATA CHALENGE CUP?)HATUJAFUZU CAN FAINALI MBILI NA KOMBE LA DUNIA TUKIWA CHINI YAKE ATAMBAE NA MISTARI HANA ZAIDI YA HAPO KAMA NI MWALIMU WA CHEKECHEA ALIPOMWACHA NGASA KATIKA KIKOSI CHAKE MWAKA 2007 MPAKA TUKATOLEWA NA MOZAMBIQUE ALITEGEMEA NINI? MPAKA WADAU WAKAMPIGIA KELELE LEO KASEJA HATAKI KUMRUDISHA MAKIPA WOTE WABOVU ANAPENDA MAJUNGU NA FITINA LAKINI NI MZURI KATIKA UTAWALA NI DIKTETA NAMUOMBA ASIJISIFU HAKUNA ALICHOFANYA KWA UUNGWAJI MKONO NA KUFIKIA HATUA ANAKULA WIRE DIRECT MPAKA IKULU ANAONGEA NA PREZDO UDHAMINI WA MAKAMPUNI MBALI MBALI KWA HALI NA MALI HATA UKIMPA MINZIRO TIMU ITATISHA BYE MAKISIMO MAZIMO WASALIMIE BRAZILI mulatofiddlers.maximo
ReplyDeleteValeu!Até mais tarde
Maximo amejenga umoja na uzalendo hasa kwenye soccer kitu ambacho mwanzoni watanzania wengi tulipoteza
ReplyDeleteAmetutoa mbali mpaka hapa tulipofika but safari ni ndefu sana ndio kwanza tuaanza yeye ndie atakaeamua kubaki ili kuendelea na programme zake ama kuondoka hilo ni uamuzi wake
Ila nasi watanzania tumejaa lawama sana na tunapenda mafanikio ya haraka haraka wakati uwezo bado upo chini
Wachezaji wetu wanalewa na sifa mpaka wanajitoa kwenye timu ya taifa labda awe kocha mwengine hili linanikumbusha enzi zile wachezaji wanaitwa timu ya taifa na wanakataa kuripoti lakini wanakwenda kucheza mechi za mchangani
Maximo tumpe Sifa yake na kama atataka kuendelea tumpe
Kama atataka kuendelea nadhani apatiwe timu,ila kama ataamua kuondoka tumwache aende.
ReplyDeleteLEO NIMEONA KITUKO UWANJA WA NDEGE DAR:NILIENDA KUWAPOKE STAAZ,MMH.Wachezaji Boban na Chuji wakatokea njia yao na kuwaacha wachezaji wengine na kocha wao wakiongea na media n.k Hii haikunifurahisha ni utovu wa nidhamu hata kama wana tofauti na maximo lazima wawe na nidhamu.Wengine waliobaki nawapongeza,walikuwa wametulia na kocha wao na walipendeza sana na suti zao.
Maximo ni kocha mzuri sana kwa Tanzania kwasababu:
ReplyDelete1. Amerudisha nidhamu katika timu
2. Amechangua kukua kwa Uzalendo.
3. Amjeenga timu bora na nzuri.
4. ana uhusiano mzuri na TFF.
Sasa ili tuzidi kukua kimichezo kocha Mtanzania hatakiwi kwa sasa hivi kwasababu:
1. Atarudisha mambo ya kizamani ya kuchagua majina na siyo ubora wa mchezaji.
2. Atakuja na Work Plan yake ambayo inaweza kukingana na Work Plan iliyopo ambayo ni Team work kati ya Tinoco na Maximo , kama umekuwa unafuatilia uteuzi wa Timu ya taifa utaona kila mara kuna wachezaji wadogo wanapanda/wanateuliwa kutoka kwa Tinoco kwenda kwa Maximo !!!!
3. Watanzania hawana bado Link na Makocha wengine duniani . Usimwone Maximo anaenda likizo mara kwa mara kwao ukadhani anapenda sana Brazil kuna A-B-Cs anaenda kupata kwa wenzake na kufanya analysis wapi amekosea na anaporudi anarekebisha.
Note: Kama England & Russia wote wamefikia pointi ambayo wanaona kocha wa kigeni ni bora iweje Tanzania.
Acheni longolongo Tanzania inahitaji uongozi huu huu uliopo wa TFF na Maximo. Sivyo tutarudi kulekule. Mpira siyo Siasa (blla blaaa).
Maximo na TFF hureeeeeeeee !
Hivi Michuzi wewe ndiye umeanzisha mjadala huu? Kweli hukupasa kuuweka kwa wapayukaji wa kwenye blog hii. Sisemi kwamba wote ni wapayukaji lakini kuna watu ambao vinywa vyao haviendani na akili zao. Kwa yule anayeangalia mpira wa sasa hivi wa Taifa stars atajua kuwa tuko mbali sana. Hawa akina Mziray, wapayukaji watupu, eti anaitwa Supper coach, mhhhh?? Hana kitu, mchangiaji mwingine anasema tupeleke makocha waende kujifunza, ina maana wakati amekwenda sisi tusimame tu? Wangapi wamekwenda na wamerudi na kufundisha mpira husiokuwa na kichwa wala miguu. Angalia sasa mfumo na uelewana walio nao sasa wachezaji wetu, kuna kipindi nilishaacha kuangalia mpira, lakini sasa unaona kandanda inachezwa na unaona pass inakwenda kwa mtu anayetakiwa, na bila ya ukali wa Maximo kwa wachezaji kusingekuwa na kitu. Nampa alama zote na mtujue katika mpira kuna kushinda na kushindwa. Timu ngapi zimetolewa kwenye CHAN, mbona hatuoni Nigeria, cameroun, Misri, Algeria etc. Tuache mambo ya kutona mbali aongezewe mkataba na muone mpira wetu utakapokwenda, hivi karibuni mtaona wachezaji wetu watavyokwenda nje kununuliwa kama njugu, Nsajigwa, Ngasa na vijana wengi watanunuliwa tu kwa kiwango chao kilichojengwa na Maximo.
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteTo be frank, I'm really proud of Maximo. Ametutoa mbali sana, Tanzania ilikua haijulikani hata kama ina timu ya soccer. Sasa hivi we're respected and admired. Maximo anaweza asiwe amefanya hayo yote mwenyewe but the fact remains the same, he has played a big part to bring back that spirit of soccer. Leo hii tunasimama proudly na kusema tunayo team.
Mambo ya kocha mzalendo hayana nafasi katika ulimwengu wa soccer. Timu nyingi sana duniani zinafundishwa na makocha wasio wa nchi zao. Hii ni business just like any other business. Hao makocha wazalendo watoke nao wakatafute kazi nje ya nchi. Wazungu wanasema "don't change a winning team", kama tumeona tumepiga hatua kubwa ki-soccer, why on earth would we change the coach (winning team)? Hao wanaomponda Maximo embu waseme wazi walichofanya kukuza timu yetu? Mbona walikua hapa toka miaka miiingi na hakuna chochote? Kama wako juu watoke kwenda nchi nyingine kufundisha, walipwe kisawasawa. Najua kuna nchi nyingi sana wanatamani sasa kutunyang'anya Maximo coz wana-appreciate kazi yake aliyofanya Tz. Na kwa vile hii ni biashara na ni competition hata dau watalipandisha maradufu kumvutia. Maximo ndo aamue anachokitaka but for us (Tanzanians)"we're dying to have him here."
wadau, Maximo ndio mwenye kauliya mwisho, kama anataka deal ya kufundisha Taifa Stars, ata-apply kazi TFF wakitangaza, kama hataki kazi bila shaka itabidi tusonge mbele, Maendeleo ni mabadiliko, hivyo ili tuendelee lazma tukubali kubalika , inapofika suala la kubadili kocha isiwe kinyume, mafanikio aliyotupa yanaridhisha, sio mubaya tukitoa fursa hiyo kwa mwalimu mwingine,
ReplyDeleteHata hivyo, muhimu zaidi sio kocha wa National Team, wanasoka wa TZ wanahitaji kuelimishwa zaidi kuhusu Proffessional Football, Competitive Football na mambo ya discipline ya kandanda, hapo kandanda letu litapiga hatua kuliko ilivyo sasa ambapo wachezaji wetu wanacheza mechi ngumu wakicheza against Simba,ama Yanga ama kidooogo Mtibwa.
Hivyo competetive mentality yao ipo chini sana.
Ni hayo,
Mdau
Nelspruit
tatizo watanzania tunataka mafanikio ya chapchap. Moja ya weakness ya wachezaji wa timu ya Taifa ni kufikisha pasi kwa mlengwa, sasa kwakweli sijui kama hili ni la kufundishwa na kocha wa Taifa au mwalimu wa michezo primary. Kuna wanamichezo wiki tatu baada ya olympics ya China walianza kujifua kwa ajili ya olympics ijayo 2012, sasa kama sisi baada ya kucheza kwenye matuta ya viazi kwa miaka yote hio tunategemea vikombe vimiminike tutakuwa tunajidanganya. Kwakuwa Tinoco kaondoka, Massimo apewe timu ya vijana under 21 na hio ndio iwakilishe Taifa.
ReplyDeleteTATIZO kikwete ameaufanya mpira siasa akiamini kuwa utatufanya tusahau ahadi zake lukuki...
ReplyDeleteMungu si athumani ,ndio maana pamoja na ujuzi na kiwango alicholeta maximo tumekosa kushinda hata kombe la mbuzi chini yake unlike kina kayuni,marehemu kinanda au mziray na kakakuona yao....sijui tatizo lipo wapi ...kenya wamefika mbali juzi na kocha mzalendo ..jana tu ndio wamepata kocha toka scotland....
sisi kwa kifupi ndio hivo MUngu hatupi kwa kuwa anajuwa kina kikwete wanataka kutumia mpira kutusahaulisha mattatizo.......wakati michezo sio siasa.
otherwise maximo kajitahidi ..tumekosa tu bahati!!!!..na kama tunapima mafanikio kwa achievement sijui tusemeje!!!!
Maximo alisema anafikiria kuondoka ili ampishe mtu mwingine aje na mawazo mbadala ya kuiwezesha Tanzania kusonga mbele zaidi.
ReplyDeleteHivyo suala ni vipi tutasonga mbele, ni kwa kutafuta kocha au mfumo wa kuibua wachezaji wazuri.
Maximo ameifanya kazi yake vizuri kwa kuweza kushawishi wachezaji wawe na 'mentali' ya kuwa wanaweza kuzifunga timu 'bora' na pia kupata timu ulaya kama wakifuata mafunzo yake kwa umakini.
Pia Maximo amekuwa kama 'Sir Alex Ferguson wa ManUTD' ktk ushawishi kwa wadau kuipatia misaada lukuki timu ya Taifa toka kwa Serikali kuu, taasisi kama mabenki na watu binafsi kwa kutaja wachache.
Maximo hakuburuzwa wala kuyumba kimsimamo, na klabu mbili kubwa za Tanzania, au na wachezaji wenye 'majina' au watu waojiona kuwa ni 'wasemaji' wa soka Tanzania. Maximo amebeba majukumu yake kama kiongozi wa kweli ambapo akishindwa anakubali na akishinda pia anakubali.
Sasa basi kwa kuwa Maximo ana ondoka, Kocha anayekuja inabidi atizamwe kwa mazuri na mapungufu ya Maximo. Mambo mazuri niliyo ya bainisha hapo juu ni mazuri ya kuzingatia ktk mchakato wa kumrithi Maximo.
Mwisho kama Yanga wangekuwa na kocha kama 'Maximo', Al Ahly ya Misri ingekuwa ina kosa usingizi, labda wachezaji 10 wa Yanga wa Maximo wawe kama Chelsea, ambapo uzoefu walio nao Chelsea wawe na kocha au la wanaendelea kutisha.
Pengine Maximo angeombwa na Yanga na serikali, wasaidiane na Kocha wa Yanga ili kupanga mikakati ya kuingoa Al Ahly, kwani Yanga pia ni timu ya kupeperusha bendera ya Tanzania ktk ulimwengu wa soka.
Mdau
Rocky
Jijini London.
KWA MTAZAMO WANGU KAIFIKISHA MBALI TANZANIA KISOKA, KWANI HUKO NYUMA ILIKUA BWELELE HATAISIKIKI,NA HATA IKICHEZA ILIKUA TIMU ZILE ZA KUFUNGWA, LAKINI KWA SASA ANGALAU, UTASIKA IMESHINDA MECHI HII, HII IMETOKA SALE, ANGALAU, NI KOCHA ALIYEINUA TIMU,
ReplyDeleteWadau, ingawa nimechanganya mambo. Naomba mwenye kufahamu ilipo SANITARIAM CLINIC, nataka kumwona Dr Isack Ndodi. Huyu Dr alikuwa anahojiwa saaana Channel Ten. Mara ya mwisho alisema yuko Mwembechai, nimefika pale, kibao anachosema kipo kuelekeza alipo, sikioni. Tafadhali! Just write here, I will read.
ReplyDeleteHana Uyanga na Usimba, Makocha wenyeji huleta hizo za Uyanga na Usimba matokeo yake hugawa timu.
ReplyDeleteABAKI
Hapa sioni maana ya kuongelea mate na wino upo, kama kweli nyie ambao hamjamkubali Maximo mnajua kipimo cha soka, Tanzania ni ya 103 kwa ubora wa soka duniani kati ya wanachama 201 wa FIFA!! na hii ni tumeshuka point 11 baada ya kutolewa CHAN, na mkumbuke hapo kabla tulikuwa wapi? Hiki ndo kipimo sahihi cha kuwa soka la Bongo limekua na sio kingine!
ReplyDeleteMaximo kama anataka kuendelea apewe nafasi, na kama hataki basi tuletewe mwingine wa nje mwenye CV nzuri ila kwa kweli hawa wabongo hawana lolote, watarudi kule kule simba na yanga!!
Tanzania inatakiwa ijitowe katika mashindano yote ya kimataifa kwa miaka kama mitatu hivi. Fedha zote amabazo zingeligharamia maandalizi na safari, malipo ya makocha, malipo ya wachezaji na gharama zote za miaka mitatu hiyo zielekezwe katika kuinua kiwango cha mpira. la muhimu sana ni viwanja bora vya timu zote za daraja la kwanza na la pili, elimu kwa makocha wa timu zote, vifaa vya mazoezi (sio mpira, viatu na jezi tu) ya kujenga miili ya wachezaji wetu na kuimarisha stamina zao. vifaa bora vya matibabu, huduma bora za matibabu. ni muhimu timu zote zipigwe jeki ili kuinua viwango vya mafunzo na mazoezi ya wachezaji wao. si sawa tu kukaa na kungoja wachezaji waitwe kucheza timu ya taifa wakati taifa halisaidii kujenga na kuimarisha hao wanaotaka walitetee taifa.
ReplyDeleteNakaribisha ubishi
yani huyo maximo aende tuu kwao..kafanya kazi nzuri kuifikisha timu yetu hapa ilipo sasa. Lakini ameanza tabia za ajabu ajabu..angekuwa professional asingekua anaweka mabifu na wanamichezo tena anawaweka wenye vipaji vyao na viwango benchi..kwa hilo amechemka..angewaacha watu wacheze halafu mambo mengine baadae.Tunataka kuwaona vijana wetu wakiendeleza vipaji na sio kuwekwa benchi tuu kwa sababu ya huyo kocha wao..akapumzike tuu naona amechoka!!!!
ReplyDeleteThanks.
Ni kweli kuwa kiwango cha soka cha sasa kimechangiwa na mambo mengi, na kimoja wapo ni rais kikwete na serikali yake kwa ujumla kwa motisha na uamasishaji wa hari ya juu. lakini ni ukweli kuwa maximo anatufaa sana na kwa sasa hakuna kocha mzalendo anayefaa kufundisha timu yetu ya taifa. Mziray, kibadeni, kayuni na mkwasa kwa sasa hawawezi kabisa kuiletea mabadiliko timu hiyo. zaidi tutashuhudia majungu tu.
ReplyDeleteLabda kidogo mtu kama julio, akipelekwa shule kwa muda iwe uk ama ujeruman anaweza. ni kwa vile anaweza kuhamasisha vijana na kukubalika.
Mheshimiwa balozi Naomba nitoe mchango wangu kwenye mada hii. natumaini kila mmoja atakubali
ReplyDeletekwamba jitihada zote za kuinua mpira Tanzania zimeanza very late na kwa pupa sana without proper analysis, may be because was a President order. Washikaji level ambayo kila mmoja Tanzania anaiota ni lazima iwe na vitu viwili muhimu. let me expalin one after another.
The first component ni WACHEZAJI. Mheshimiwa balozi wachezaji wa kitanzania wanakuwa wamejiandaa au waliandaliwa toka lini kuwa wachezaji wenye mafanikio? let me tell you this, Mchezaji wa kitanzania mpaka anamaliza darasa la saba hajui kama anaweza kuwa mchezaji, anaanza kuhisi hilo akifika form two au three hapo ni miaka 15 au 16, lakini akiweka mkazo kwenye soka anadrop kwenye masomo na hapo conflict na familia inaanza, baba atamkataza mtoto wake apunguze mpira
akazanie masomo (That by itself affects at large SAIKOLOJIA ya mchezaji) "I PUT IT IN CAPS TO EMPHASIZE"
mpaka muda huo mchezaji hajaanza kufundishwa mpira (ANAJIFUNDISHA) akimaliza form four anaanza kucheza Ukonga Rangers, one season then AFC Arusha two season and then simba/yanga na ndio national team wanamuona hapo tayari ana umri wa miaka 26 au 28. mfano ni Godfrey bon wa Yanga ana umri sio chini ya 35 sasa ( I know him) lakini kaonekana lini?na mpaka anaonekana anakuwa tayari anavuta bangi za kufa mtu, kwa sababu ya kukosa muongozo wa kulea vipaji vyao na kujua madhara ya madawa wanayotumia michezoni. Labda sasa nitoe comments zangu, what can be done?
1. Nafikiri and i am real conviced kwamba sasa Mpira uwe ni displine inayojitegemea kama ilivyo kwa walimu, Doctors, Engineers. Tatizo ni kwamba mzazi sasa hivi hawezi kumuacha mtoto wake aache shule acheze mpira tu, hata mimi sitaweza ila kama kuna mifumo bora, kwamba there is chances of
success in football/sports, tutapeleka tu watoto wetu. Sijawahi kusikia Steven Gerald, paul scholes, beckham, Essien, Adebayor, Nani and Ronaldo kama walipita other displines halafu wakachepukia kwenye mpira. Najua walijikita kwenye mpira since utoto. THAT IS THEIR TAALUMA. Wanasaikolojia wanaweza kutusaidia, but as far as i know kitu anachofundishwa mtu utotoni from 8 to 15 hakitoki. (Muangalie Scholes anachofanya au Giggs, yale walifundishwa utotoni jamani)
2. Iam sure there is no limitations kwa watu kuwekeza kwenye michezo including kuanzisha sports academies. kama hizi zingefanikiwa could have been better kwa soka letu. But hapo hapo policies contradics serikali inataka kila mtoto lazima aende shule kupata elimu ya msingi, sina hakika kama
serikali inaweza kuelewa kuhusu hilo. Lakini Steven Gerald alijoin Liverpool at the age of 8 years. Lakini hizo ni changamoto ambazo ambazo wadau na serikali wanatakiwa wakae kuzijadili. Mbali tu ya kuwa na elimu mpira lakini mchezaji anatakiwa kujua ni aina gani ya mazoezi yanatakiwa, na kwa muda gani, chakula gani, mapumziko gani. Hivi hawawezi kuvijua kama watakuwa wanasoma shule ya msingi Kalobe Mbeya, lazima wawe kwenye academy maalum ya michezo.Mengi, Bakhresa, Mohamed Dewji and Manji changamkieni tenda hii, waachieni simba na yanga na matatizo yao.
3. Walimu wa kufundisha hawa watoto nao kwanza watengenezwe, Nchi yetu has good diplomatic relationship na developed countries, those people may assist us technically kama sisi tutashindwa kusomesha wataalamu wetu, mbona waCuba walileta wataalamu wa kulea vipaji kwenye ndondi.
Mheshimiwa balozi kama hutaiweka kapuni hii, ntakuletea part two yake ambapo ntaongelea serikali ifanyeje.
By Mwakalebela (Sio wa TFF)
Kuendelea kuwepo au kutokuwepo huo utategemea uamuzi wake mwenyewe Maximo kwanza kabla ya kitu kingine chochote!Na hata akiombwa akakubali arefushe mkataba wake,nashauri kwamba apewe nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja tu,tuone atatufikisha wapi zaidi.Kumpa zaidi ya mwaka mmoja kuna athari zake.Baada ya mwaka mmoja akifanya vizuri zaidi basi atapewa mkataba wa miaka miwili zaidi hadi hapo matokeo yatakapo anza kufifia.Maximo ni Kocha ambaye hana Mbwembwe za Ufahari kama Makocha wengine wenye majina makubwa hapa Duniani.Mimi ule "u simplicity" wake ulinivutia sana japo mwanzoni nilikuwa na wasiwasi naye sana kuhusu uwezo wake kama Kocha.Swali la kujiuliza ni kwamba,je,katika kipindi chake Maximo,timu yetu ya Taifa Stars imepiga hatua yoyote kimaendeleo kwenda mbele? Jibu ni NDIYO.Bado haijafika pale tulipopataka.lakini,angalau sasa Taifa Stars imebadilika.Imebadilika kimchezo na Kisaikolojia pia.Bado yapo mapungufu,lakini hayo yatapungua hatua kwa hatua.Nilichukizwa sana na kauli ya Kocha Mziray pale alipokosoa mfumo wa uchezaji wa 3-5-2 aliokuwa akiutumia Maximo kwenye mashindano ya hivi karibuni kule Ivory Coast!Na kudai kwamba mfumo ule ulikuwa unaua nguvu za mawinga na ushambuliaji.Sikukubaliana na wazo lake hilo.Kwa maumbile madogo na vimo vifupi vya wachezaji wetu huo mfumo ndio uliofaa zaidi kwa timu yetu katika baadhi ya mechi.Mfumo wa uchezaji sio "Static".Na mara nyingi unatakiwa uanzishwe na wachezaji wenyewe kwa wenyewe kwa kadri kasi ya mchezo itakavyo badilika.Kwa hilo nilimuona Mziray kama mbabaishaji.Maximo ni Kocha mzuri siyo sana sana lakini ni Mzuri.Hana Makuu,hana Mbwembwe,Hana Majigambo,Ni Msikivu na Mvumilivu sana.Kwa kweli amejifunza mengi sana katika kipindi hiki kifupi na amebadilika sana katika Ukocha wake.Mwanzoni sikuupenda ukocha wake.Lakini kwa kadri siku zilivyo songa mbele,Maximo amezidi kuwa Kocha Bora zaidi na zaidi.Tukiamua kumtema tutakuwa tumewekeza kwake KWA FAIDA YA WATU WENGINE.Labda yeye mwenyewe aseme,BASI SASA IMETOSHA,anahitaji kupumzika au akabadilishe mazingira ya ufundishaji.HAPO HATUTAKUWA NA HAKI YA KUMLAZIMISHA.---tonnie--
ReplyDeleteMichuzi acha usenene wako, kwa kusema amefuatwa na nchi mbalimbali ila kipaumbele anaipa Tanzania na hivyo abaki, tumpe tena miaka kama minne hivi ili aiunue vipaji vya vijana umepiga chini maoni yangu. Sasa nakwambia hivi kama wewe unamtazamo wako kila mtu ana wake na hukuwa na haja ya kuleta mjadala huu hapa, watu tunapoteza muda na nguvu kuchangia wewe unachukulia kiurahi tu yaani unapiga chini. Poa tutaenda kule "we dare to talk openly" nawe si unakujua endelea na blog yako ya picha kwani hutaki analysis wewe.
ReplyDeleteWadau wengi waliotangulia hapo juu wamesema kweli kabisa. Maximo has nothing to do with anything. Ni sawasawa na mtu kutokwenda shule halafu Maximo anakuja kufundisha elimu ya watu wazima, halafu unategemea kushindana na vijana wadogo ambao wako fit and strong.
ReplyDeleteNa sio mpira wa miguu tu ni michezo yote, turudi nyuma kwenye mashindano ya shule za msingi, na angalau mpaka seconadary na vyuo kama ingewezekana. Kuwa na vituo vya michezo vya mitaani, miaka hiyo tulikuwa na vitu kama mbio za jogging, diocese, ymca etc.
Na mwisho kabisa yanatakiwa maslahi mazuri kwa wanamichezo. Maanake katika nchi zetu shule ndio kila kitu mambo ya michezo utakuja kuzeeka vibaya. Wazazi wengi watakazania watoto wao masomo na sio kuendeleza vipaji vyao na wako sawa kwenye hilo.
Tukumbuke tena jinsi yule kocha mzungu miaka hiyo ya zamani alivyoweza kuitengeneza Yanga from yosso na timu kama TP Lindanda zilivyokuwa na vipaji vya wachezaji. Wizara ya michezo na utamaduni ilitakiwa iwe na mkazo katika kugundua na kuendeleza vipaji ikibidi hata kama ni kutoa scholarships kwenda shule za seconadary.
For Maximo au hata angekuwa kocha yoyote mwingine sidhani kama kuna miracle angeweza kufanya, this is the furthest we can reach at this point. Labda tungeweza kufanikiwa to the second round and that was it!
kWANZA KABISA LAZIMA TUELEWE HUYU KOCHA KAJA KWA NIA YA KUENDELEZA SOKA NA KWELI TUMEONA ANGALAU KIDOGO SOKA LA NCHI YETU LIMEBADILIKA TOFAUTI NA HAPO MWANZO SASA HIVI UNAWEZA KUONA ZINAPIGWA PASI HATA SABA WAKATI ZAMANI ILIKUWA BEKI AKIPATA ANABUTUA MBELE,KWA MAANA HIYO KWA KIPINDI HICHI ALICHOKAA AMEJITAHIDI SANA MAXIMO,NA HASA UKIZANGATIA HAWA WACHEZAJI ALIYOWAKUTA HAWAJAANDALIWA,NINA MAANA WAMETOKEA KATIKA TIMU ZA MICHANGANI HAWAKUPATA MAFUNZO MAZURI YA KIMPIRA,KWA HIYO NI VIGUMU SANA KUWABADILISHA ILI WAWEZE KUCHEZA SOKA LA KUELEWEKA.KWA MAONI YANGU MAXIMO AONGEZEWE MUDA NA MAENDELEO YA SOKA YETU YATAKUWEPO KUTOKANA NA MPANGILIO ULIOKUWEPO HIVI SASA WA KUENDELEAZA VIPAJI VYA WATOTO KATIKA MICHEZO.
ReplyDeletewatu mnaandika mibarua mireeefu km hotuba?mnamshinda ata michu,,aya
ReplyDeleteabaki asibaki ni juu yake na rais..
ila Tz makochaz tunao???
majungu?
ivi timu ya zamani Tz zilizokua zinatamba nani alikua anazifundisha?waje hao
Suala la kutokushinda mimi sioni kama ni tatatizo. Taifa stars walicheza mchezo wa kiwango cha cha juu kabisa.
ReplyDeleteSasa hicho kiwango sijui waliwezaje kukifikia kama siyo kwa jitihada za mwalimu wao Maximo.
Sikubaliani na wadua wanaopendekeza uwezekano wa kupatikana kwa makocha wazalendo, kwani hao ndiyo chanzo cha malumbano na migogoro kati soka letu.
Maximo ni mwalimu mzuri sana, watanzania wanatakiwa wampe ushirikiano mzuri ili aweze kuifikisha timu yetu ya taifa mahala pazuri.
Mada hii imenifanya nihisi kuchangia hapa. Nakumbuka mwaka 1998 tulishiriki michuano ya awali ya kuwania kucheza fainali za CAN huko Misri,na timu yetu ilishika nafasi ya mwisho kwenye kundi la sita kama ifuatavyo
ReplyDeleteGROUP 6
Team Pts W D l GF GA GD
Togo 10 3 1 2 9 5 +4
Congo DR 9 3 3 1 6 5 +1
Liberia 8 2 2 2 5 8 -3
Tanzania 5 1 2 3 5 7 -2
Ambalo Tanzania ilikua na nafasi kubwa ya kufuzu,kama kwa atakaye kumbuka ni kwamba mechi mbili za mwisho tulisheza ugenini ,ya kwanza dhidi ya Congo DR ambapo tulishawakamata hadi ndani ya dk ya tisini tulikua mbele kwa goli moja na refa aliongeza muda takribani dk 7 hivi na dk ya 95 DRC wakapata penalt iliyozaa bao la kusawazisha,tukatoka sare 1-1.
Mechi ya pili tulikwenda Monrovia,Liberia huku timu ikiwa choka mbaya posho hamna,timu ikalala goli moja.Kama timu ingekua na motisha ya kutosha ikiwa na udhamini na kuungwa mkono kama ilivyo sasa na uhakika tungeenda Misri.tena na kocha mzalendo.
Hivyo kwa mazingira yalivyo sasa hivi Marcio Maximo alikua na kila support ya huhakikisha timu inafanya vyema zaidi ya hapo mlipoona katufikisha.
Pia nimesikitika kusikia kwamba jamaa ameanza kuwagawa wachezaji hasa kwa taarifa nilizozisikia kuhusu kujitoa kwenye timu ya Taifa kwa Athuman Idd, na Haruna Moshi, hatua ya kuanza kujenga makundi kwenye timu ni mwanzo wa kuharibu timu na kuleta matokeo mabaya.
Kwa maoni yangu jamaa amefanya alilofanya anastahili kusifiwa kwa alichofanya ila aende zake na wala asiongezewe mkataba.
We need a more professional coach if we are to climb higher in FIFA ranking,and kutawala East Africa na Africa.
Mdau Sijajua
Wa TAndale kwa Mtogole.
Tufanye lolote lile lakini tusiweke kocha Mtanzania kamwe, sisi hatuko serious na hatujui kushindana wala kupanga, ni Uswahili tu.
ReplyDeleteMaximo sio KOCHA NI TEKINISHENI TU.ALIYEKUZA MPIRA WETU NI JK SIKU ALOPOKWENDA MWANZA NA BURKINA FASSO MAXIMO ALIKUWA NA WIKI MOJA NA TIMU YETU IKASHINDA.
ReplyDeleteANALETA WADHAMINI KWA TIMU YA TAIFA SIO MAXIMO WATANZANIA TUKO ULIMWENGU GANI?NI JK.NCHI ZOTE ZILIZOPIGA HATUA KIMPIRA AFRICA NI NGUVU ZA MARAIS. MFANO ZAMBIA LIPOKUWA KAUNDA ANA PENDA MPIRA KIWANGO CHAO KILIKUWA JUU.
CAMEROUN KINA SONG NA ETOO WANARIPOTI KWA RAIS WAO BEYA.
MAXIMO MUONGO LEO ANASEMA WATANZANI WAKIMUHITAJI ATABAKI. SABABU HANA PA KWENDA.NAAMINI TUMUACHA UTASIKIA NI KOCHA AZAM. HANA UJUZI WA KUMSHINDA PHIRI MZAMBIA LABDA TU TUNABABAIKA NA JINA BRAZIL.
KILA SIKU ANASEMA KAJA KUJENGA MSINGI KAMA KAJA KUJENGA MSINGI AONDOKE KWANI MSINGI TAYARI TUNAO.
TIMU YA TAIFA INASHINDA KWA HAMASA ALIYOITENGENEZA JK.
MCHEZO WA TAIFA STARS NA ZIMBABWE UTAJUA KABISA MAXIMO HAMNA KITU.
ALIPOTOKA IVORY AMEKUJA NA MPYA ETI SASA ATAUNDA KIKOSI CHA VIJANA TU HATAKI WACHEZAJI WAKUBWA ANATAKA WADOGO JEE KWANINI ASICHUKUE HAO WADOGO KABLA YA KWENDA CHAN?
HUWEZI KUMUWEKA NJE CHUJI MTU ALIYEWAPA TAABU CAMEROON.KAMA ANGECHEZA CHUJI TUSINGEFUNGWA MECHI NA ZAMBIA KIZEMBE.
JK TUNAKUSHUKURU LAKINI MTU SASA HATUFAI AMESEMA KAJA KUWEKA MSINGI NDIO KAZI YAKE SIO KULETA KOMBE.MWALIMU KAZI YAKE KUTENGENEZA NA NIDHAMU LAKINI HUYU BWANA KILA DAKIKA ANA BIFU NA WACHEZAJI.AONDOKE.KWA MATUNZO WANAYOPATA STARS HATA MBARAKA WA ASHANTI ANAWEZA KUTULETEA KOMBE LA DUNIA. MAXIMO NI LOOSER,MBABAISHAJI.
MDAU KISIJU.
Jamani eehh, tutapiga kelel sana kwa sababu timu yetu haikusonga mbele. Kama Zambia wasingerudisha na tukashinda ni wazi Wa-TZ mngemsifia Maximo. Lakini kwa sababu tumetolewa basi oooh hafai. Hebu tutoe mawazo nini kifanyike.Angalieni kabla hajaletwa nchini kufundisha Taifa Stars nchi yetu ilikuwa wapi kisoka na angalia alipoanza kufundisha timu yetu imeweza kumenyana na vigogo vya soka barani Afrika na hatuwi kapu la magoli kama zamani.
ReplyDeletehivi mmesikia jana alivyosema ?anataka kuunda timu upya kwa kuondoa wachezaji wasio na nidhamu(by the way kutokuwa na nidhamu kwake kuna include kumchallenge kwa chochote kwa ajili ya kujenga).mankumbuka timu aliyo anza nayo kipindi kile alivokuja.akaunda timu mpya ikaenda brazil training..katikati hapa anaunda unda unda timu upya.anaunda tena ijumaa.nyie muendekezeni kama mnavoendekeza mambo mengine ya ovyo kama ununuzi wa Genereta za dowans,mikataba mibovu kama ATCL,TRL...endeleeni tu
ReplyDeletekama mimi ningekuwa Maximo, kwa hatua niliyoifikisha Tanzania, ningeondoka kwani tayari nishavuta mshiko wa kutosha USD 15,000/= kwa mwezi ndani ya miaka miwili!!!!!
ReplyDeleteThen ningejipeleka South Afrika nikachukue mshiko pia mpaka end of 2010 then narudi Rio de Janeiro ,Brasil kupumzika.
Sisi waTZ ni wagumu sana kuwa sehemu ya mafanikio, Mafanikio sio kitu rahisi Lazma mtu ufanye kazi sana,jasho litoke,ubomoe,ujenge upya,uingie gharama zinazoepukika na zisizoepukika hapo ndio utapata mafanikio endeleveu. Falsafa ya Maximo inapita njia inayofanana na hiyo lakini WaTZ tunataka matoke mazuri within no time ,
Tunajilinganisha na wakenya wenye MATHARE SOCCER VILLAGE inayojulikana Ulimwengu mzima wa kandanda.
Maximo, unangoja nini, tambaa zako, sisi wazalenda tunaoheshimu mchango wako tutakukumbuka tu kama tajiri Abrahimavic anavyomkumbuka the "special one" kwani kwetu sisi waTZ ukiondoka ndio tutaona na kukubali mchango wako,
Mzalendo, Rombo Bar, Tabata Mawenzi
Mjadala huu umeleta maoni tofauti ya wapenda maendeleo katika uongozi na Utendaji wa kuinua kiwango cha timu ya Taifa Stars.
ReplyDeleteKila mtazamo wa maoni ya wote waliyochangia yaheshimiwe,lengo ni moja kuleta maendeleo ya hali ya juu kwa Taifa.
Kitaifa "Stars" imejipatia msingi, lakini "kimataifa" bado tupo nyuma kabisa na mwendo mrefu saana kufikia kiwango cha hali ya juu.
MAXIMO "IS AND STILL WILL REMAIN AS THE ONLY SOLUTION FOR THE FUTURE OF TAIFA STARS" kama tunataka kuiona "TAIFA STARS" inayoelewana na kucheza kama timu moja katika mashindano yote ya kimataifa.
Ni kweli kuna waalimu wengi ndani ya nchi na nje ya nchi kama watoaji maoni walivyopendekeza, lakini ubadilishaji wa mwalimu hautoleta maendeleo ya haraka zidi ya kuzalisha "mchezaji pekee mwenye sifa zote za kiubinafsi" bila ya kuleta ushindi kama timu moja tunayotaka kuijenga.
Tunayataka maendeleo ya kimataifa wanaohusika kwa sasa "MAXIMO NA MSAIDIZI BUSHIRI" wapewe mkataba mpya wa miaka mitano,kuweka malengo ya TAIFA STARS katika "WORLD CUP" ya mfumo wa pili baada ya South Africa yatakayofanyika 2014.
mickey@mail-online.dk
COPENHAGEN-DENMARK
We Anony wa 9:37pm;Mdau wa Kisiju , hata kumbukumbu nzuri huna. Mechi ya mwaka juzi tu umeshasahau ilichezwa wapi. Burkina faso ilicheza na Stars, Dar es Salaam na sio Mwanza.Afu unataka kina Chuji nao wakaripoti kwa KJ. Kwa hiyo ndio mpira utapanda ??! Watu wengine bwana Mnatafuta kwa nguvu watu waanze kuosha hapa..!
ReplyDeleteMaximo ni mzushi hana kitu.aondoke period.
ReplyDeleteJK hatumtaki mtu wako na jeuri unampa wewe.TFF wote hawamtaki ila wanasemea pembeni.wanaogopa ajira zao.ila maximo ni zigo.
Tarehe March 04, 2009 11:05 AM, Mtoa Maoni: Anonymous umelonga na ninanukuu 'hata wachezaji wa brazil hawaonekani sana i meean hawangari sana europe kama wengine, tunatakiwa kucheza kwa nguvu'. Pitia hii listi. Pitia vilevile listi ya waliopata kuwa wanasoka bora wa Ulaya ama wa Dunia, huenda ukaona kitu:
ReplyDelete1. Ronaldo de Lima
2. Ronaldinho Gaucho
3. Roberto Carlos
4. Robson de Souza aka Robinho
5. Romario de Souza Faria
6. Ricardo Izecson dos Santos Leite Kaka
7. Alexander Pato
8. Adriano
9. Cicinho
10. Blumer Elano (huyu ndiye aliibeba Man City chini ya Erikson na kuifanya Man City ifanye vizuri kuliko siku za kabla ya kufika kwake. Mark Hughes amekuwa akimwacha benchi. Man City inajitahidi isishuke daraja sasa hivi).
Hapo nimeacha wachezaji kama Dida, Cafu, Vagner Love, Careca, Bebeto, Edmundo japo walisikika vya kutosha. Vilevile nimeacha wachezaji kama Deco, Marcos Senna walioamua kuchukua uraia wa mataifa tofauti ilipofika wakati wa kuchagua timu ya taifa ya kuchezea.
Michuzi brother.
ReplyDeleteMimi ni mmoja wa watu wanaopenda kufuatilia kiundani, na kwa maana hii huongea na Maximo. Nakuomba Brother ukiwa kama muandishi wa habari uandae mjadala wa kwa nini soka ongozi kwa letu liwe maala lilipo. Nipo tayari kushirikiana nawe kwenye hili.
Kuhusu Maximo, hatuwezi kumuachia kila kitu, kwani soka ni mafunzo, Vifaa, na Mazoezi ya kutosha ikiwa ni pamoja na michezo ya Majaribio amabayo hii nafikiri ni swala la TFF na Uongozi wetu wa Michezo nchini ikiwa waziri wa michezo ni muhusika mkuu si tu Soka bali kila Mchezo. Tatizo Viongozi wetu wanakuwa wana SIASA KUPINDUKIA na kazi HAZIFANYWI.
Wenzetu wana vitengo vya kuangali a Afya ya Mchezaji hadi mchezaji. Uzito wa Mchezaji kama Defenda na Lishe yake therefore ni muhimu kuwa determined, kama kweli tunataka Matokeo Mazuri. Sisi Mchezaji anakula Kama Miss!!! alafu tunategemea awezi kumudu wachezaji kama wa West Africa ama Central n.k ama akacheze Ulaya?!
By definition Nguvu ama energy ni "a thermodynamic quantity equivalent to the capacity of a physical system to do work; unapokuwa kwenye Michezo kimashindano unatakiwa kupambanisha Energy zako na za Adui wako, mfano kuwania mpira kwa kuruka , kufukuzana kama Mabeki na forward n.k. Sasa ndugu yangu fikiria kama utakuwa na Nguvu kidogo na Mazoezi kiduchu kuna aja ya kutafuta Mchawi? Hatuna wataalam wa Psychologia, watu wetu wamesoma shule za kawaida ambapo hawakufundishwa Mbinu mbadala za kupambana na Matukio , yaani sababu za kuwa tulipo tusimuachie Maximo tu. Haya ni mawazo yangu....
Mwisho kabisa nasema Roma haijajengwa KWA SIKU MOJA. Themistocles
JOSE MOURINHO ANASEMA FOOTBALL IS ABOUT WINNING THE TROUPHY(MAKOMBE) SASA MAXIMO KAFUNGWA HADI NA SOMALIA KWENYE CHALLENJE.MIE NAONA ANAPOTEZA PESA ZA KODI YETU HANA JIPYA NA AMEKUWA MSWAHILI HIVI SASA.MTU WA MAJUNGU NA FITNA. KISA ANA NGUVU ZA RAIS.
ReplyDeleteAONDOKE WANAOMTAKA WAANZISHE TIMU WAO WAMUWEKE.
Sasa ni muda muafaka kuwapatia makocha wazalendo kuifundisha timu yetu ya taifa na tuwalipe vizuri na kuwapatia ushirikiano kama ambavyo tumefanya kwa Maximo. Pia napendekeza tubadilishe utaratibu wa kupata wachezaji wa timu ya taifa. Utaratibu unaopendekezwa ni kila mkoa kupewa jukumu la kutafuta angalau mchezaji mmoja toka kila mkoa ambaye atakuwa ndiye mchezaji bora toka mkoa husika. Pia inapendekezwa wachezaji wetu wa timu ya taifa wawe wanalipwa mshahara wa angalau shilingi milioni moja kila mwezi na tuwakatie bima ya maisha.
ReplyDeleteSalaam
Josephat
Dar es Salaam