Kaka michuzi maoni yangu ya maswali yako matatu kuhusu kocha wa timu ya taifa ni kama ifuatavyo.
1. Je, maximo amefanya kile alichokuja kukifanya?
Jibu: Kwa maoni yangu maximo amefanya yale aliyotakiwa kuyafanya, nasema hivi kwa sababu ukiangalia uwezo wa timu yetu kipindi anachukua timu na jinsi timu yetu ilivyo sasa utatambua kuwa kocha huyu kafanya makubwa sana, timu yetu ilikuwa haijulikani wala kushiriki mashindano makubwa kwa muda mrefu lakini maximo kaiwezesha timu yetu kucheza CHAN. Pili ukiangalia wachezaji ambao maximo aliyonao leo katika kikosi chetu ni wachezaji ambao wengi wa makocha wazawa wasinge wapa hata nafasi ya kucheza timu ya taifa, wachezaji kama kigi makasi,juma jabu, mwinyi kazi moto, nurdin bakari, jerry tegete na ngasa.
2. Je, maximo aongezewe muda au aondoke?
Jibu: Kwa maoni yangu, maximo aongezewe muda, nasema hivi kwa sababu naona kuwa kuna uwezekano mkubwa wa maximo kufanya makubwa na timu yetu hasa pale atakapo endelea kukaa na kufundisha hawa vijana wadogo waliopo timu ya taifa hasa walio na miaka chini ya miaka 24 ambao wapo wengi. Watanzania wengi wanapenda mafanikio ya haraka lakini soka halipo hivyo, soka linahitaji muda, angalia Ghana ambao wameanda timu yao kwa miaka 5. Vilevile tatizo la Tanzania ni kutokuwa na academy za soka ambapo ni chimbuko la mpira…matatizo ya Chuji na haruna ni
kutokana na kutokuwa na malezi ya mpira toka udogo ndio maana wanabishana na kocha,….Ronaldo, maradona wameshawahi kutolewa nje na kocha au kutopangwa sembuse hawa vijana ambao wanapata kichwa na soka la simba na yanga?
3. Kuna haja ya kuwa na Kocha wa nje au tubaki na wazawa?
Jibu: Kwa maoni yangu kama maximo akibaki, tunahitaji kuwa na makocha watatu wazalendo kumsaidia ambapo kocha mmoja awe na kazi ya kuzunguka nchi nzima kutafuta vipaji vinavyochipukia, mwingine awe ni kocha wa makipa na mmoja awe wa physical fitness.
Nawasilisha….
Mdau Tini.



Uliyosema ni mazuri nakubaliana nawe kaka.uwezi kuchipukia dakika tano uwe bingwa inagitaji muda.na kweli ameifanyia timu ya taifa mazuri na sasa tunaeleweka africa kama tuna timu kamambe.na sio tulinganishane na ghana au other west countries but so fa tuko bomba na tutazidi ,kama tukitaka ushindi wa haraka hara na kutaka kumtimua kocha aliyesaidia nchi yetu kuwapa vijana wa soka nguvu mpya kazi mpya.labda wabongo wanataka kumleta mzee wenger au felix.hahah
ReplyDeleteMAXIMO ATENDEWE HAKI HATA KAMA TUMEMCHOKA TUKUBALI MAMBO MAZURI ALIYOTUFANYIA TUMUAGE KWA HESHIMA KWANI KUTAFUTA KOCHA MWINGINE NIMABADILIKO YA KAZI TU. HUYU MTU NI ANA ROHO YA KIUME KAZI YA UKOCHA HAPA NCHINI NI NGUMU SANA NIMEONA MARA NYINGI TAIFA STARS IKIFANYA VIZURI HUSIFIWA WACHEZAJI NA IKIFUNGWA MAXIMO HULAUMIWA
ReplyDeleteHata Mie nakubaliana na wewe ila mambo ya Ronaldo na Maradona yanakujaje kwenye Topic za Kuhusu Timu yetu ya Taifa tuongelee kuhusu Tanzania ndio kwenye Timu ya Taifa. wale hawana nizamu lazima wafundishwe nizamu mchezaji si mkubwak uliko Timu ya Mpira Nukta.
ReplyDeleteAchape mwendo haina jadala
ReplyDeleteWith due respect naona huu mjadala mheshimiwa balozi ni wako mwenyewe binafsi au wewe ni sehemu ya wanaomsakama Maximo.
ReplyDeleteMjadala umejadiliwa kwa kina mara mbili tofauti na maoni ya walio wengi wameoneshwa kuridhishwa na kazi ya Maximo. Sasa unapourudisha kila mara, unakuwa kamawale waamuzi waliohongwa wanajaribu kuitafutia timu ya ushindi ilhali hata kwenye penalti box hawafiki.
Haya endelea...ikibidi mpira wa kurusha ugeuze penalti.
Kipimo Hiki Cha Maximo Ni Kinaonyesha Ni Njinsi Gani Watz Wanarizika Mapema: Huu Ugonjwa Wa Maximo Ndio Tulionao Hadi Kwa Wanasiasa Wetu Au Viongozi Kisa Mkuu Wa Mkoa Katujengea Daraja Basi Hata Kama Anaharibu Poa Tu Mkoa Una daraja. Maximo Kweli Kafanya Kile alichoweza Ila Zaidi Ya Hapo Tusitegemee Mengine : Mkija Na History Kama Hizo Makocha Wangapi Wamewezesha Timu Za Taifa Lakini Ikifika Kung aatuka wanaanza Kwa Hio Mdau Usitulazimishe Kumkumbatia maximo Wakati Hata Huko Alikotokea Ana History Hio Ya Kuziwekea Tu Timu Msingi....MAXIMO TIMES OUT BRO WEE BACK NA BIASHARA ZAKO ZINGINE TU BONGO MAANA KUNA TETESI JAMAA TAYARI KASHANUNUA NA NYUMBA NA ANA BIASHARA FLANI
ReplyDeleteMaximo ni Coach mzuri na mwenye mapenzi na watanzania, for some reason ameweza kujichanganya na kujua namna ya kuishi na watanzania.
ReplyDeleteWachezaji wanatakiwa kuwa na nidhamu kwa Coach hilo halina ubishi. Kazi nyingi zinakutaka uweze follow directions and once. Fikiria madaktari, marubani, askari na professional nyingine wacheze chini ya viwango tutaumia.
Still issue ni kukuza vipaji tokea level ya primary and secondary schools na pia timu za watoto za mitaani. Na pia malipo mazuri kwa wachezaji kwani nini faida ya kucheza mpira wakati utakuja kufa masikini? si bora uende shule utafute kazi za maana?
Ni vizuri tuwe na wataalamu wa nje kama Maximo pamoja na mambo mengine waweze pia kuchangia programs za kuinua timu za watoto.
MAXIMO NA EL BASHIR WASHIKE USUKANI
ReplyDeleteNakubaliana na mdau TINI nafikiri maswali na majibu ni msimamo wa wengi ingawaje si uamuzi kwa kuheshimu wanoangalia kinyume cha kubakia kwa MAXIMO.
Ni kweli tunao waalimu wengi wazuri
nchini wana uhuru kujitokeza-TFF na kuomba nafasi ya kutoa mchango wao wa utaalamu,lakini hatuhitaji mwalimu toka nje wakati kiwango chetu bado cha Taifa hakijafikia lengo la Kimataifa
Wachezaji ingawaje si wote hawajajuwa kuwa mmojawapo wa mchezaji wa kimataifa ni nidhamu na mchezo wa maelewano kama wachezaji wa pamoja ndani na nje ya mchezo.
mickey@mail-online.dk
DENMARK
Yeye mwenyewe anajua amefikia mwisho wa uwezo!!!
ReplyDeleteMaximo sio kocha ni gogoro.RIO FERDINAND anavuta bangi ana amekulia maisha ya Peckham kwa wahuni au ghetto.lakini fergusson anajua kuwa na wachezaji wenye tabia tofauti hivi sasa ni captain wa manchester na makombe yote anakabidhiwa yeye.maximo hajui hata role ya captain wa timu.
ReplyDeleteGallas ni mvuta bangi na alimpiga van pas na silvester lakini WENGER akayamaliza matatizo kiutu uzima wote wanacheza.kama Boban angepigana na Nsajingwa kesi hiyo angeepata looser maximo ingekuwaje?
watanzania wengi wanaujua mpira hawamtaki maximo ndio maana walithubutu kumpiga mawe challenji 2007 Tanzania.
analipwa pesa nyingi wakati uwezo hana.
kuwa kocha ni kuleta makombe nae kasema kuwa kaja kujenga msingi kama kajenga basi aondoke.
hakuna mzalendo kocha anaweza kushirikiana na maximo labda awe zezeta.
wachezaji kam Rooney walikuwa watovu wa adabu lakini makocha wanaojua kazi zao wamewapa mawaidha na sasa ni ASSET kwa timu na mataifa yao.
MAXIMO AONDOKE.wanaosema abaki ni wale makuwadi wake wa kumtafutia wanawake. kama anataka kubaki alipwe dola mia tano kwa mwezi.CV yake mbovu.
MTAKUWA MNABADILISHA MAKOCHA KILA SIKU,ICHUNGUZWE, TATIZO NI MAKOCHA AU TIMU NZIMA KWA UJUMLA KUANZIA HUKO JUU HADI CHINI. HALAFU ULIVYOSEMA ETI KUWA NA MAKOCHA WATATU, HUU UTAKUWA WIZI TU HAMNA LOLOTE, TIMU ITAFILISIKA NA VIPAJI KUFA!!
ReplyDeleteIkumbukwe kuwa timu ya taifa ni organisation by itself na Maximo ni MD au maneja kiongozi,na ili kuwe na ufanisi huyu atakiwa aongoze kwa miaka miwili tu zaidai ya hapo hana la ziada kiongozi as expert kwanini? zaidi ya hapo atataka kujifunza mambo mengine kuhusu Tanzania akitumia kisingizio ameshaisaidia timu ya taifa hivyo ile efficiency itapotea tusidanganyike, mkataba umeisha kama hakuna mtanzania wakuchukua nafasi yake lete mwingine...lets open our eyes
ReplyDeletetuonyeshe picha za jengo la yanga na uwanja wa kaunda inaendeleaje?
ReplyDeleteRon -- US