
magari ya faya yakiwa eneo la tukio muda mfuoi baada ya moto mkubwa kuzuka na kuunguza nyumba tatu jioni ya leo sehemu za kinondoni moscow. chanzo cha moto hakijajulikana bado ingawa inahisiwa ni shoti ya umeme ambao siku mbili hizi umekuwa na kwikwi ile mbaya na vipindi virefu vya giza. haijatangazwa rasmi lakini redio mbao zinasema kwamba mgao ndio umeshaanza

askari wa zimamoto wakiwa kazini

majirani, wapita njia na waathirika wakiwa wanaangalia zimamoto wakifanya kazi yao. ishukuriwe moto umewaka mchana kweupe maana ingekuwa usiku ingekuwa balaa zaidi

askari wa zimamoto wakipambana na moto huo ambao waliweza kuudhibiti kabla ya kuchoma eneo lote hilo la kinondoni moscow

baadhi ya wathirika wa moto huo wakiwa na kiasi cha vitu walivyoweza kuokoa

askari wa ffu walitanda kila kona kuthibiti uhalifu wa aina yoyote

askari wa ffu akilinda nyumba zilizoungua kwa moto

kama ulikuwa hujui basi habari ndiyo hiyo, jeshi la zimamoto lina kinamama ambao wako bega kwa bega na kinababa kupambana na majanga ya moto

bongo bado sana, eneo kama hilo inatakiwa watu wote wasiohusika na kuzima moto na uokoaji waondelewe.
ReplyDeletelakini wabongo tulivyo, hiyo ni sehemu ya kupeleka mpaka watoto wadogo. hivi huwa tunafaidi chochote kwa kufanya hivyo?
health and safety ni zero. najua wapo wataosema hayo mammbo ya kizungu, lakini ukweli ni kuwa uzembe wetu unatumaliza wenyewe - akifa mtu hapo kwa uzembe kisha tunaanza kuchangishana hela ya kukodisha FUSO!
MUNGU MKUBWA BALAA HILI LIMETOKEA MCHANA INGEKUA USIKU INGEKUA BALAA MAANA EFFECT INGEKUA KUBWA KUPITA MAELEZO VIBAKA NAO WABGEPROFIT
ReplyDeleteNCHI INAKAA KIZA KUTOKANA NA FISADI MMOJA TU MWAKYEMBE ANAESHINIKIZA SERIKALI NCHI IKAE KIZA KWA AJILI YA MASLAHI YAKE,KWA KUA YEYE HATOATHIRIKA NA KUUMIA KWETU
TUAMKE JAMANI HII MIJITU MENGINE YENYE ASILI YA KIFISADI TUSIIIPE MADARAKA
MIMI NIMESIKITISHWA SANA NA AJALI HII. UNAJUWA TUKO KTK KIPINDI KIGUMU CHA UCHUMI KISHA MTU UNAUNGULIWA NA NYUMBA UTAPATA WAPI HELA YA KUJENGA NYINGINE??
ReplyDeletePOLENI SANA WOTE MLIOKUBWA NA JANGA HILI.
SASA NALILUDIA SHIRIKA LA UMEME TZ. HAWA WAHUSIKA NA VIONGOZI WANAPASWA KUWAJIBIKA MAANA KAMA HAWANA ELIMU YA KUTOA HUDUMA ZA UMEME SI WAJIUZURU??
LEO TUKO KTK MWEZI WA TATU INAWEZEKANA VIPI WASEME KUNAMGAO WA UMEME WAKATI MALA YA KWANZA WALITUAMBIA KUNAMGAO WA UMEME KUTOKANA NA UKAME ETI BWAWA LA MTELA LIMEKAUKA NA SASA TUKO KTK MASIKA LIMEKAUKA VIPI?
SASA MGAO UKIANZA SASA HIVI TUNAELEKEA WAPI??
UZEMBE WA WACHACHE MNASABABISHIA WENGI UGUMU WA MAISHA.
Si bongo ni tambarare? si ndo mnasema hivyo kila siku...!! Unajua kuna kitabu cha zamani sana sijui siku hizi kimepotelea wapi. Aliyekiandika alikuwa mtu mwenye akili sana...Kinaitwa "UJINGA WA MWAFRIKA"...!! I'm looking for this book and enjoy the reality of african lives....!! Huu ndo Ukenge na ukarume kenge...badala ya kukimbia watu wanakuja kushangaa zima moto..wapi na wapi?
ReplyDeleteNyie ndugu hapo juu mnaokimbilia kuita majirani wa huyo mama wajinga kwa kusogea eneo lenye moto ni kwamba hamjui hali halisi ya maisha Bongo.
ReplyDelete1. Ujirani kwa hapa Bongo ni kusaidiana katika majanga. Ukifiwa majirani zako watakuja kukusaidia. Nyumba yako ikiwaka moto watakuja kukusaidia pia.
Msaada wenyewe ni kama vile kuanza kuzima moto kabla Fire Department hawajafika. Aghalabu Fire huwa wanachelewa kufika na sometime wakifika hawana maji, au wana maji lakini hayatoshelezi, au pump zao mbovu.
Hivyo kwanza kabisa Fire wakija wanakuta tayari majirani wameshaanza kazi ya kuzima moto, na majirani hao wataendelea kukaa stand-by ili kusaidia endapo FIRE itachemsha.
2. Katika eneo kama hilo vibaka huwa hawachezi mbali. Mwenye nyumba ukiwa unaokoa mali zako na kuziweka nje penye usalama ukiingia ndani kuokoa mali zingine huku nyuma vibaka wanabeba zile ulizotoa nje na kutokomea nazo.
Hivyo majirani wanakuja kusaidia kulinda mali zako. Pia wengine watakusaidia kuingia ndani na kutoa mali zako kama ukiwaruhusu.
Najua mnaangalia mambo kwa macho ya Ulaya. Mnasahau jinsi vile watu wanaishi hapa Bongo, especially maeneo yenye msongamano wa watu kama hapo Kinondoni Moscow.
Maisha ya kuchuniana kila mtu na 50 zake sana sana utayakuta Masaki ambako ni low density area. Ila high density area kama hapo Kinondoni Moscow moto ukiwaka kwa jirani yako unaweza ukaingia na kwako pia. Hivyo huwezi kucheza mbali kabisa, ni bora umsaidie kuuzima.
Ni hayo tu.
mdau wa March 21, 2009 3:39 AM,
ReplyDeleteUsichukie sana, wote hao waliokuja kushangaa zima moto hawana kazi. Wangekuwa na kazi wasingekuwepo hapo. Bongo Tambarareee!
yaani, hata siku mmoja sijaamka na kusema nimekosea stepu kuja ulaya.....upuuzi wa watu uko vile vile. maji na umeme hola...yaani, hutataendelea milele. Kazi kwenu, mimi natesa hapa.
ReplyDeleteUlaya oyeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!
Bongo ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!
BRA ZIMEUNGUA NYUMBA ZENYEWE MBOFUMBOFU BORA WAJENGE MPYA
ReplyDelete*Michuzi, "magari ya 'faya'"?.. hizi kwikwi za kiswahili ukiziendekeza, unakiharibu..
ReplyDelete*Shukrani ziwaendee woote walioshirikiana kupunguza tafrani na hasara kutokana na janga hili..
*hapo wengi wameona mabaya tuu..na kila mmoja lawama tuu..lakini kuna mazuri, japo mawili..1. FFU kufanya kazi ya kulinda kwa umakini..wakipiga raia twawashia moto hapa wanastahiki pongezi.."mnyonge mnyongeni...". 2. Zimamoto wa kike, kumbe wapo?..warembo..yaonekana wengine hawakwenda kushuhudia janga..tehe tehe!..
*Kwa wadau wengine kama mnajua ntashukuru maelezo yenu, "Kinondoni Moscow"..kwa nini ikaitwa 'Moscow'...kumbuka kuna Morocco pia..UZENG
nyie wabongo wote mnaocheka shida za nyumbani ni wajinga kabisa watumwa wa hiari nyie mimi niko ulaya pia lakini naumia sana na nawaza hata niingie kwenye siasa ili niweze kupambana na ufisadi na kuwasaidia watanzania wengi wanaoishi kwa tabu sana,sasa nyie mnawacheka badala ya kuweka mikakati pia jinsi ya kuisaidia nchi yenu,watanzania tulio nchi mbalimbali duniani tungeweza kuichalenge serikali yetu tukiwa hukuhuku kama tungekuwa na umoja naupendo na nchi yetu,sio kukaa tu na majungu.
ReplyDeletewe ulosema ujinga wa mwafrika nahisi wewe utakuwa mjapani ,mchina au mzungu yaani haao jamaa kushangaa hapo nini kinaendelea ni kosa mpaka ututukane mbona osama alipolipua twin tawa Ny wazungu kibao walikuwa wanashangaa kinachoendelea acha ujinga ,
ReplyDeletekimenisikitisha hao madada wa zima moto ni watoto wa mjomba waliopewa kazi kiundugu waone hawako fit kabisa kupambana na moto.
Tunshukuru MUNGU hakuna aliyepotenza maisha au kujeruhiwa. Pole pole tutafika.
ReplyDeleteMNAJUA NINI NDUGU ZANGU?TUSIWASHANGAE SANA HAWA WATUMWA WA KIMAWAZO.UNAJUA NYANI NI NYANI HATA UMVISHE SUTI ATABAKI KUA NYANI
ReplyDeleteMSHAMBA NI MSHAMBA HATA UMKUTE NEW YORK.
ETI LEO UNAITUKANA NCHI YAKO KISHA WATU WANASHANGAA
MBONA HAUKUITUKANA U.S.A WAMAREKANI WALIVYOJAZANA KWA MSHANGAO KUONA JENGO LA WORLD TRADE CENTRE LILIPOKUA LINAUNGUA
TENA WAO NDIO WALISHANGAA NA KUDUWAA KWELIKWELI KULIKO HATA HAO KWENYE PICHA MAANA WAO WALIKUA WANAZANI MAJENGO YALE YAMEJENGWA NA MUNGU NA HATA SIKU MOJA HAYATOKUJA ANGUKA
TUSIWALAUMU HAWA NDUGU ZETU WENGINE WASHAMBA ASILIA WAMEZALIWA KTK FAMILIA ZENYE USHAMBA NA UTUMWA WA ASILI INGAWA HUJIONA BORA.
HAWA SI NDIO WALE WENYE KUUTUKANA USWAHILI WAO NA LUGHA YAO YA KISWAHILI NA KUKITUZA KINGEREZA
TUSIILAUMU TANESCO TUWALAUMU WANASIASA MAFISADI KWA KUWACHEZA SHERE WATANZANIA KWA MASLAHI YAO BINAFSI
MAFISADI HAWA MWAKYEMBE NA ROSTAM WANALIFANYA TAIFA LISAFE KWA MASLAHI YAO BINAFSI
1. Jiji la Dar halina budi kuendelea toka pale alipotuacha mkoloni na kujenga Fire stations nyingi zaidi. Maybe 1 station for every 1,000 buildings.
ReplyDelete2. Tangu lini wanawake wakawa fire fighters jamani. Kituko gani hichi? Tunaleta mchezo mpaka kwenye vitu serious? Life is not a rehearsal jamani - it is a performance. Lets be serious.
Maskini dada wa watu, yeye mwenyewe asipokaa vizuri moto utamuwasha mwenyewe.....I hope she performs differently from the looks.....
ReplyDelete