Hayati Michael Uledi
Na Martha Mtangoo, Dodoma
MWANDISHI wa habari wa Magazeti ya Mwananchi mkoani hapa Michael Uledi (40), amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Mirembe alikokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa za kifo cha Uledi zilitolewa jana na Mke wa marehemu Agness Mzola nyumbani kwake. Uledi ambae kifo chake kimesababishwa na kuugua kifua kwa muda mrefu (TB) alizaliwa mnamo mwaka 1969 katika Kijiji cha Buigiri wilaya ya Chamwino, alisoma katika shule ya msingi Buigiri 1977-1983 na baadae mwaka 1986 alijiunga katika shule ya Sekondari Chidya wilaya ya Masasi ambako alimaliza kidato cha nne mwaka 1989.
Mwaka 1990 alijiunga na shule ya sekondari ya Moshi kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita ambako alihitimu mwaka 1992 na baadaye kujiunga katika mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa mkoani Mara ambako alihitimu na kisha alikwenda Jijini Dar es Salaamu ambako alifanya kazi katika makampuni ya watu binafsi kwa kipindi cha miaka miwili.
Uledi alijiunga na MAMET kwa ajili ya kozi ya Uandishi wa Habari kwa muda wa miezi mitatu na alipomaliza alijiunga na kampuni ya IPP mwaka 1998 ambapo alipangiwa kituo cha Dodoma akiwa ni Mwandishi wa magazeti ya Nipashe, Guardian pamoja na Radio One.
Marehemu alijiunga na chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini mwaka 2001 hadi 2003 ambapo alimaliza Shahada ya juu ya Mipango na Maendeleo Vijijini na kufanya kazi kwa muda mfupi katika shirika la Viwanda Vidogo mkoani Dodoma (SIDO) na baadae alihamishiwa katika kituo cha kazi Mtwara.
Mwaka 2004 hadi 2006 alifanya kazi katika Benki ya Exim katika wilaya ya Masasi akiwa ni Meneja Msaidizi wa Bank na baadae alijiunga na kampuni ya uchapishaji magazeti ya TSN, Mkoani Morogoro akiwa mwandisahi wa habari wa gazeti la serikali la Habari Leo.
Januari mwaka 2007 alijiunga na kampuni ya Mwananchi Communications kazi aliyoifanya hadi mauti yanamkuta.
Uledi ameacha mke na mtoto mmoja na taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa arehemu Nkuhungu mjini hapa. Mmwili wa marehemu unatarajia kusafirishwa leo kwenda Kijijii kwao Buigiri kwa maziko.
Wakati huo huo Chama cha waandishi wa habari za bunge (BUPAT), kimesema kuwa kimepokea kwa maskitiko makubwa taarifa za msiba huo.
Mwenyekiti wa chama hicho Lauden Mwambona amesema kuwa chama chake kimepata pigo kubwa kutokana na kuondokewa na mchapakazi na mtu ambaye alikuwa na mahusiano ya karibu na wenzake.
Uledi alikuwa ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama cha waandishi wa habari za bunge BUPAT ambapo alichaguliwa Juni 13,2008 na umoja wa waandishi wa habari za Bunge katika kikao cha kwanza cha uundwaji wa chama hicho ambapo alikuwa akiwakilisha mkoa wa Dodoma.
-----------------------------
Globu ya Jamii kwa niaba ya wadau wote inatoa mkono wa rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mpiganaji Michael Uledi ambaye mchango wake katika fani ya uandishi tutaukosa.
Mola aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu
Amina

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kifo cha Michael Uledi kimenistua sana!. Marehemu alisaidia sana maendeleo ya mchezo wa mpira wa wavu mkoani Dodoma miaka ya 90, kwa kuandika habari za michezo mingi ya ndani kama wavu, kikapu, pete, mikono,pia Umitashumta na Umiseta, huku wengi wa waandishi wa michezo wakati huo walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi kwenye mpira wa Miguu.

    Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi pia faraja kwa ndugu na jamaa wa marehemu Michael Uledi

    ReplyDelete
  2. Ni habari ya masikitiko na huzuni kubwa kwa waliomfahamu marehemu uledi. kwa kweli ni pigo kubwa sana kwa wana Dodoma wenzangu. Mungu akuweke mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana wafiwa, kifo cha Uledi ni pigo kubwa kwa taifa na kwa familia yake. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Ameen.

    ReplyDelete
  4. R.I.P kaka Uledi.Poleni sana wafiwa Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  5. kwa tuliomfahamu imetusikitisha ,alikuwa mtu wa watu na alipenda kushauri bila ya kuombwa Mungu ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi. Poleni wote mlioguswa na msiba huu. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMEN

    ReplyDelete
  6. R.I.P Komrade UlED.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...