Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwa kwenye mkesha wa Maulid katika viwanja vya Mnazi Mmoja usiku wa kuamkia leo. Kulia ni kaimu Mufti Sheikh Suleiman Gologosi.

Jioni hii mzee wetu mpendwa alikuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulidi katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini, na alipokuwa akihutubia alitokea mtu ambaye kila aliyekuwepo alidhani anataka kurekebisha kipaza sauti.


Kwa mastaajabu na mstuko wa wote alimshambulia Rais mstaafu na kabla hajaleta madhara walinzi shupavu wa Rais mstaafu walimdhibiti mtu huyo kwa kumpiga mtama na kumshikilia.


wakati tukienda mitamboni mtu huyo ambaye hajajulikana mara moja wala sababu iliyompelekea kufanya vile, alikuwa amepelekwa mzobemzobe kituo kitogo cha polisi cha daraja la salender kwa mahojiano. Alhaj Mwinyi hakudhurika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. Nasikia Mzee wetu alikuwa anasisitiza matumizi ya condom katika jamii ndipo huyo jamaa aliyemzaba kofi alipokereka kwa sababu yeye anataka tule tunda kavukavu.

    ReplyDelete
  2. Bro Michizi hakuna walinzi shupavu hapo. kama wangekuwa shupavu mzee wa watu asingezabwa kibao. inashangaza kuona mtu asiyejulikana anaweza kumkaribia mgeni rasmi (tena Rais mstaafu)wakati akitoa hutuba. huu ni udhaifu kwa vyombo vya usalama na viongozi wetu wadini pia. nasema viongozi wa dini kwasababu ninauhakika wanawajua vizuri waumini wao wa karibu.Kwa maana hiyo kudhani kuwa mtu anaenda kurekebisha mitambo wakati hata wao hawamtambui ni kitu cha kushangaza kidogo. Kingine ninahokiona hapo ni kuwa, Tanzania tumeanza kujisahau kwakuwa tunasifiwa (tunajisifia) kuwa ni kisiwa cha amani.Kwa hiyo tunafanya assumption kuwa watu hawawezi kufanya mabaya makanisani au misikitini.Tunakosea. Tuwe macho sasa, kila mahali lolote linaweza kutokea. Enzi zake mwalimu Nyerere (R.I.P)alitufundisha kuwa kila raia anatakiwa awe mlinzi wa Nchi yetu, tusitegemee askari peke yake.Unapomwona mtu humwelewielewi sehemu kama hii ni lazima umtilie mashaka na ikiwezekana adhibitiwe mapema.Na ndio maana JK akavamiwa jukwaani kule Mwanza. Pole Alhaji Mwinyi kwa yaliyokufika

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  3. Hii ndio fundisho kwa Fisadiz, yaani hiyo ni angalisho kwa akina Kikwete na wengineo.Maana ukiona rais mstaafu anapigwa kibao meble ya kadamnasi, haina tofauti na Bush kutupiwa kiatu, ni sawa tu.

    ReplyDelete
  4. Watu wameshachoka na ufisadi wanaamua kuzaba vibao tuu sasa.

    ReplyDelete
  5. Anasisitizwa njia za kujikinga na magonjwa Mtu anakasirika kwa kigezo cha dini,TUACHE UPUMBAVU ndugu zangu tutakwisha.

    ReplyDelete
  6. MTU ANATOA SOMO TUSISHE KWA UKIMWI WENGINE WANAKASILIKA SASA HII NINI?WADAU HILI SWALA HALIENDANI KABISA NA KITENDO ALICHOFANYA HUYO JAMAA SHERIA IKIFATA MKONDO WAKE HAKUNA WA KULAUMIWA
    MPILI

    ReplyDelete
  7. pole sana mzee wetu ruksa.

    binadamu hatuna hisani mangapi umewafanyia waislam leo kauli hiyo hata kama haikumpendeza mtu lakini jibu lake sio kumpiga kibao rais mstaafu.

    kwani kama kakoseam ziko njia ya kujibu kauli yake.hakuna uhalali wa kidini kuwa kibao ndio jawabu lake.

    huyo ni mhuni na hajui dini sheria kali ichukuliwe.

    waislam ilikuwa jamii iliyokuwa nyuma sana lakini mzee ruksa ndiye aliyewainua,misikiti mizuri yote imekuja kipindi cha ruksa,mashule kwa waislam ilikuwa marufuku kipindi cha nyerere, mzee ruksa akafungua milango ya elimu kwa waislam nao wakaanza kujenga mashule kwa nguvu yote ni kipindi cha ruksa.

    ni kiongozi ambaye ametumia muda mwingi kwenye ghafla au shughuli za dini na kutoa nasaha nyingi kwa waumini wake lakini mazuri yake yote hayaonekani ila kauli hiyo tu ndio aadhibiwe kiasi hicho?

    nachukua fursa hii kuomba radhi kwake mzee ruksa na familia yake yote kuwa kilichotokea sio uislam ni jazba za mhuni tu aliyetumia mazingira ya kidini kutimiza ujinga wake.

    naamini historia itamkumbuka ruksa kwa mchango wake kwa uislam Tanzania.Mwenyezi Mungu amlinde na mahasidi kama hawa.

    ReplyDelete
  8. MNAWAONEA WALINZI BURE,KWA STAILI HUYO KIJANA ALIYOKWENDA NAYO HATA ANGELIKUWA KIKWETE ANGELIZABWA TU,MAANA KWANZA ALIKWENDA PALE KAMA FUNDI MITAMBO,ALIINAMA AKAINUKA NA KUMZABA KIBAO,MSIWALAUMU WALINZI MNAWAONEA,HATA ANGELUKUWA NANI PALE AMGEFANYA ALICHIKUSUDIA KWA KUWA ILE SHEREHE HAIKUWA NA VITAMBULISHO VINAVYOWATAMBULISHA MAANDISHI AU MAFUNDI

    ReplyDelete
  9. Swali lakujiuliza ni kwanini mtu kama huyo aliamua kufanya kitendo hicho cha hatari? Ndio shukurani ya kumlipa mzee wetu huyu, kwa wema aliotutendea?
    Ni vigumu kupata jibu kwa sasa, kwasababu yupo chini ya usalama, lakini tukio kama hili linatufundisha kitu gani?
    Usalama wa viongozi wetu wastaafu unaangaliwaje?
    Yapo mengi yakujadili, lakini pia kuna haja ya kutoa mawazo, hasa viongozi wetu wanapohudhuria sherehe za kidini, kuhusiana na hotuba zao. Viongozi wengi wa kisiasa wamebobea `kisiasa' na wanapoalikwa mahali kama hapo wanatakiwa waangalie sana nini wanachokizungumza, je hakiwakwazi waumini? Je hakiwagawi waumini? Je imani zao zinakubaliana na nini unachotaka kuwaeleza?
    Swala kama la `kondomu' ni vyema wanasiasa wakaelewa `imani'za dini zinasemaje, na ni vyema swala kama hili likaongelewa kwenye viwanja vya siasa, kuliko kulileta ndani ya nyumba za ibada, kwani `utata' wake ni mkubwa.
    M3

    ReplyDelete
  10. Aisee nimesikitika sana... Nampenda sana Ali Hassan Mwinyi. Ana mawaidha poa, kweli ukimwi unatumaliza... sio siri, na sio mara ya kwanza Mwinyi kuongelea janga la ukimwi alishasema haka kagonjwa kamekaa pabaya sana tangu enzi zileeee, tujikinge wananchi sio swala la uislamu wala ukristo hapa ni facts and reality. Alamsiki.

    ReplyDelete
  11. Napenda kuungana na anonymous wa 5:10 am, kweli alichofanyiwa mzee mwinyi kinasikitisha. Mzee huyu ni mmoja kati ya viongozi wachache walio bega kwa bega na shughuli za waislamu toka alipokua rais hadi sasa. Siyo fair kabisa , tujifunze uvumilivu jamani, kila mtu ana mapungufu yake tukianza kuadhibiana hadharani hatufiki popote. Cha muhimu ni kuadress ishu aliyoisema mzee huyu, kweli kuna tatizo la ukimwi na kutovumiliana miongoni mwa wanajamii wa imani tofauti, nini kifanyike hilo ndilo jambo la msingi. Natoa pole kwa mzee mwinyi na familia yake pia.

    Mdau, DSM.

    ReplyDelete
  12. LAKINI NA HUYU MSTAAFU WETU NAE KWANINI ALIHALALISHA NGONO (NGONO RUKSA)???? AAH AAH AAH POLE SANA BABU YETU.....

    ReplyDelete
  13. wewe anon 8.30 naona akili yako na yule kijana hazina tofauti nata chembe, aliyekwambia kwenye siasa ndio sehemu pekee ya kuzungumzia masuala ya ukimwi ni nani?? aliyekwambia kwamba haistahili kutumia kondom au kuna dini gani ilisema tusitumie kondom ni nani? hebu acha upumbavu!! tena huyo kijana anatakiwa ahasiwe kabisa, akitoka huko ana adabu. maana hao ndio wenye nao wanasambaza kwa kusudi wakisingizia dini!!. POLE SANA MZEE WETU! USIJALI HIZO NDIZO SHUKRANI ZA PUNDA!!!

    ReplyDelete
  14. Pole sana mzee hata mimi kimeninyoda.

    Kama huyo mwehu ana hasira sana, akampigane na wakurya huko tarime, kama hajatolewa meno. Africa wazee hawapigwi wala kutukanwa, huyo mtu ana laana. Wampeleke segerea huko akaolewe afundishwe kukata viuno. Bro Muchi tuwekee picha yake tumshambulie.

    Pili, hivi polisi/secret service/usalama wa taifa or whatever they are called.....hawana aibu kumshambulia mtu aliye kamatwa kwa mateke ya kichwa.......HIYO NI POLICE BRUTALITY.......inatumika sana bongo........ndio wanavyofundishwa huko chuo cha upolisi? Wanatia aibu......

    Pole sana mzee wetu Al Haj Ali Hassan Mwinyi.

    ReplyDelete
  15. Nina hakika mtu huyu ana matatizo, lazima atakuwa ni mgonjwa wa akili. Haingii hata kidogo kwa mtu yeyote kukubali kwamba Mzee wetu Alhaj Mwinyi anaweza kuwa na mahasidi wa kudiriki kufanya tendo kama hili tena mbele ya kadamnasi na wakati wa sherehe kubwa na tukufu kwa wa islam wote duniani. Pamoja na madai ya kukerwa na hoja iliyokuwa ikiongelewa na Alhaj Mwinyi huyu mshambuliaji bado inathibitisha kwamba ana walakini, kasoro kubwa ya afya yake, isije kuwa ni muathitrika sasa akaona "It was too late" kwake yeye kuzidi sikia nasaha za kujikinga, kumbe kinga hata kama ni muathirika unatakiwa kuwa muangalifu zaidi na ndipo hapo utakaporefusha maisha yako na kuokoa maisha ya wengine. Pole Alhaji kwa maswahibu haya na bado huyu kijana atafundishwa na dunia kama alishindikana nyumbani kwao. (dRU)

    ReplyDelete
  16. mimi wala sishangai nyie wenzetu mnajazba sana kama mnadiriki kujitoa mhanga ndo mshindwe kumchapa mtu makofi? pole sana mzee ruksa.

    ReplyDelete
  17. HAPA NDIPO PA KUANZI KUONA MAPUNGUFU YA KURANI TUKUFU AU MAPUNGUFU YA KUIELEWA. LAKINI MARA NYINGI WAISLAM WAMEKUWA WAKIAMUA KUCHUKUA SHERIA MKONONI KWA KISINGIZIO CHA KURANI BILA KUFUATA SHERIA ZA NCHI. ALICHOFANYA HUYO KIJANA KAFUATA KURANI INASEMAJE JAPO KAKOSEA SHERIA ZA NCHI.SIMLAUMU KWA UELEWA WAKE DINI YAKE INAMWELEKIEZA HIVYO.

    ReplyDelete
  18. ACHENI KUPOTEZA MUDA. ANGALIENI KURANI INASEMAJE MUUMINI AKIONA MTU ANAKASHFU DINI AU ANAPOTOSHA WATU.

    ReplyDelete
  19. kwanza pole sana mzee wetu, huyo kijana ana akili timamu na alikusudia alichokifanya ili tu kuwavurugia waislamu wanonekanike kuwa hawajui elimu ya kujikinga na ukimwi na usikute sio muislam kaja tu kwa nia ya kuharibu,anyway mimi nimependa sana mzee mwinyi alivyomsamehe bure kwani atachapwa bakora kubwa na mungu mwenyewe

    ReplyDelete
  20. ila watu tutalaanika kweli mzee wetu kama yule tena amejitahidi kuja kuhudhuria sherehe kama ile leo unamzaba kofi je angeanguka kwa kiwewe akafa jamani tumuogope mungu, na kama katumwa kweli wote watalaanika sana kwa sababu alichokizungumza mwinyi ni kitu cha kawaida kabisa ili kuokoa kizazi kijacho jamani kwa nini watu hawaelewi?

    ReplyDelete
  21. Kwa kweli ni kitendo cha kusikitisha sana kwani Mzee wetu hakukosea kutuasa. Walinzi walaumiwe walijisahau. Nampa pole mzee ruksa

    ReplyDelete
  22. hata mimi nadhani waislam hawajui uwezo mbaya walionao katika maamuzi unajitoa muhanga eti unaenda kwa mungu,mungu gani ua hawaelewi ukiua ni dhambi? sasa watapigana vibao na kutoleana maneno je mungu wao kazi yake nini kama wanajihukumu wenyewe duniani TAFAKARINI SANA

    ReplyDelete
  23. sijapenda ulinzi uliokuwepo!!!walinzi hawakuwa makini.the worst could have happened.

    ReplyDelete
  24. Yule Kijana ni Mshenzi na Mtovu wa Adabu kwa watu waliomzidi umri sawa na Babayake au Babuzake na kwa mtu aliyekuwa Rais wetu wa Nchi hivi karibuni tu!Alilifanya tendo lile akiwa na akili zake timamu na alitambua atahri zake!Inawezekana kabisa wapo wakorofi wachache(Islamic Fundamentalists/Extremists)waliomtuma akatende uhalifu ule kwa kumwahidi Kitita cha Fedha!Kwasababu alijua wazi baada ya tukio lile atakamatwa na kutiwa hatiani na mikononi mwa vyombo vya Dola!Na kwamba adhabu kubwa sana itamkabili hata kabla ya kufikishwa mahakamani na hatimaye kutiwa gerezani!Alikuwa na jeuri na ufedhuli wa aina fulani ambao hauji hivihivi tu,hadi mtu mwingine akutie Munkari ya kufanya uhalifu ule!Hawezi kudai kwamba Uislamu ndiyo uliomtuma afanye kitendo kile cha fedheha kubwa kwa Taifa na kwa Waislamu wote waliostaarabika!Mzee Mwinyi sote tunamfahamu kwa upole wake,unyenyekevu wake,kwa upendo wake na kwa mengine mengi.Hotuba yake ilijaa upendo,usia,maridhiano baina ya imani mbalimbali za kidini,kumcha Mungu na jinsi ya kujinusuru katika maisha yetu kwa kuchukua tahadhari mbalimbali katika maisha!Kama vile Mzazi atakavyo wahusia wanawe na wajukuze!Alifanya kosa gani akastahili kufedheheshwa kiasi kile mbele ya kadamnasi ya waumini wa Kiislamu?Kuzabwa Kofi na kijana mdogo kabisa aliekosa Adabu na Fikara za Ustaarabu!Aliwezaje kutenda ushenzi wa aina ile bila ya woga mbele ya watu wazima,viongozi wa dini na nchi kwa kisingizio cha kuchukizwa na ushauri wa Mwinyi kuhusu jinsi ya kujinusuru na maradhi ya ukimwi?Huyu sio Uislamu ndiyo ulomshinikiza kufanya Ushenzi ule!Uislamu haufundishi Utovu wa Nidhamu na kukosa adabu kwa Viongozi wa Nchi na Watu waliotuzidi umri!Uislamu ni dini ya amani na inayofundisha ustaarabu wa hali ya juu!Huyo Kijana lazima ASULUBIWE hadi ashike Adabu ili liwe Fundisho kwa vijana wengi hapa nchini.Hii inatukumbusha tena kwamba MaRais Wastaafu lazima wapewe ulinzi wa kutosha popote pale iwe makanisani au misikitini!Dunia hivi sasa imechafuka mno.Kila aina ya uchafu kutoka nje umekuwa ukitiririka na kuingia katika nchi yetu.Bado Watanzania hatujafikia hatua ya kuwazaba Viongozi wetu wa nchi hadharani kiasi kile hata iwe kwa visingizio gani! Tukio hilo lazima lilaaniwe na kila Mtanzania na kila aliyestaarabika.Huyo Kijana pamoja na wenzake wote waliomtia Munkari hata akathubutu kutenda uhalifu ule lazima washughulikiwe ipasavyo ili matukio kama hayo yasije yakatokea tena hapa nchini.Mzee Mwinyi tunakuomba radhi sana tena sana kwa Utovu huo wa Adabu kutoka kwa huyu kijana wetu hayawani aliyekosa adabu na hata chembe ya ustaarabu!Tutamshughulikia ipasavyo!

    ReplyDelete
  25. MICHUZI TOA HII.

    POLE SANA MZEE RUHUSA.
    NIMESIKITISHWA SANA KWA KITENDO CHA KUMZABA RAISI WETU.
    MWINYI NI MWANA SIASA COMENTS ZAKE ZINAWAHUSU WATU WOTE WAKRISTO, WAISLAMU,HINDU,WAPAGANI,MALAYA,WASENGE NA KADHALIKA...
    JAMAA ANAMTIZAMO MDOGO SANA,KAMA UJUMBE HAUKUUSU JAZIBA YANI?
    WAMPIGIANI? MZEWETU? ACHENI SIASAKALI?
    NA WEWE ANOY WA UK ATI UNASEMA KWANINI POLISI WAMEMDUNDA HUYO JAMAA! HAPA SIO UK HII NI BONGO .

    MWAKUMBUKA???...HOTUBA ZA ALHAJI. NAIGA ANAVYOONGEA...NI UTANI TU.

    VILEVILE
    NDUNGU WANANCHI NAPENDA KUTOA DUKUDUKU LANGU KUHUSIANA NA HUYO JAHILI ALOTAKA NITOA ROHO MSKITINI, NIMEMSAMEE NAJUWA ALIKUWA NI IBILISI TU KAMPALIA,WAJUA TENA UKIPALIWA NA PUNJE

    VILEVILE
    NATAKA KUTOA ONYO KUWA WABAYA WANGU KUWA MI NDO ALHAJI MAKOMANDOO WANGU NI SHABABI MSIJE KICHWAKICHWA.

    VILEVILE
    NATAKAKUWAKUMBUSHA KWAMBA
    CHOKOCHOKO MCHOKOE PWEZA ALHAJI HUTOMWEZA.

    VILEVILE
    NASIKITISHWA SAANA KUONA WAFANYA KAZI WA SERIKARI WANAISHI MAISHA YA KIMASIKINI, UTAFIKIRI UKOLONI YAANI ZILE ZAMA ZA UTUMWA BADO ZIPO. KWANZIA LEO HII, MIE KAMA JEMEDARI AMRI MKUU WA MAJESHI BARA NA VISIWANI NAWAPA RUUGHHSAA KUNUNUA MAGARI NA KUJENGA MAJUMBA MAZURU MUISHI NYIE NA FAMILIA ZENU, KWANI BABA WATAIFA ALITUAMBIAAA UCHUMI TUNAAOOO ILA TUMEUKALIAAA.

    VILEVILE
    WANAZUONI NA WANAFALSAFA WALOBOBEA WALISEMA SHURTI MTU ARUHUSIWE KULA APATE AFYA YA KUFANAYA KAZI AKIENDA NA NJAA KAZINI LAZIMA TU ATADOKOA,
    BAADA YA KUONGEA NA MKE MKUBWA MAMAM SITI TUMEFIKIA MUAFAKA KUWA RUGHUSA KULAAAA MKISHIBA KAFANYENI KAZIIII.
    MI SINA HIYANA KAMA ALOPITA KULA PEKEYAKE.
    ZIDUMU FIKRAZE NA ZANGU.
    ASANTENI SANA.

    VILEVILE
    LETENI BENZI LANGU NIONDOKE MIDA YA KUFTURU HII.

    HAHAHAHAHAHAHA NILIPENDA KISWAHILICHE. PAMOJA NA KUMKANDIA MZEE RUGHSA YEYE NDO ALITUTOA USHAMBANI
    ENZI ZA MCHONGA HURUSIWI KUWA NA TV .
    MWINYI ALIWAPENDA WATANZANIA NDO MAANA AKAWARUHUSU KUALA MPATE AFYA YA KUCHAPA KAZI.

    WE MISS YOU MZEE.

    ReplyDelete
  26. Kama Uraisi siku hizi ni pamoja na kukubali kuzabwa kofi au kurushiwa viatu, sijui dunia hii tunaelekea wapi, kwa kweli...

    Pole sana Alhaj Mzee Mwinyi kwa huo mshtuko! Na huyo kijana lazima akapate fundisho.

    ReplyDelete
  27. Kwakweli mwinyi alikua raisi mzuri aliyeelewa matatizo ya wananchi na aliyependa nchi yake na wananchi wake. ruksa ile ilibidi kw amda ule lasivyo tungeachwa nyuma kama cuba hiyo ni wakati ulimlazimu tusimlaumu. huyo mtu ana unchungu wake maisha magumu anataka kumtolea hasira mwinyi. na hao askari huwezi kuwalaumu mwinyi ni mtu yule very relaxed hana cha kuogopa watu sio kama mke wa kikwete hata akienda kwenye harusi anadance bodyguard wake pembeni mpaka anachekesha hivyo na maaskari wa mwinyi wako relaxed hawakutegemea lolote baya kumtokea

    ReplyDelete
  28. JAMANI HUYU MTU SI KWAMBA HANA AKILI....PENGINE NDO MAFUNDISHO HAYO YA DINI YAMEMUIINGIA HASWAA DONT USE CONDOM...PILI MASHULE KWA WAISLAAM HAIKUWA MARUKFUKU ENZI ZA NYERERE?????? MDAU UMECHEMSHA...KAMA ULISHINDWA SHULE NI WEWE NDIO MAANA NDUGU ZAKO WENGI MBUMBUMBU

    ReplyDelete
  29. Shambulizi hili sio kwa Mzee ruksa tu bali ni kwetu sote na kwa taifa letu.

    ReplyDelete
  30. MAKOSA MAWILI:
    1. MZEE ALITAKIWA AIJUWE HADHIRA, UKIENDA KWENYE VIWANJA VYA DINI yeyote USISEME MANENO YANAYOPINGANA NA maandiko YA DINI HAYO WALA viongozi WA DINI HIYO.

    2. HADHIRA: HAIKUWA VUMILIVU, JAPO UBAYA WA UVUMILIVU NI KULEA KIVUMILIWA.

    ReplyDelete
  31. ninyi woote mnafahamu dini inayokataza zinaa katu katu, na mnafahamu inayokataza ado ado.

    Isilamu na Katoliki hawataki kuhubiri condomu kwani kufanya hivyo kunapingana na maandiko katika amri ya "usizini" japo inaokoa maisha ya wazinzi.

    Hivyo ni kazi ya serikali na NGO kuhimiza watu watakao kufanya tendo hilo, wavae ngao.

    ReplyDelete
  32. Mzee umri umeenda, hekima inaanza kupungua. Watu wanasherehekea mtume we unahimiza kitu cha kumpinga mtume huyo. Unategemea nini?

    Si kosa saana maana akifika mia, kila mtu huwa sawa na mtoto wa miaka 10. Ndo maumbile yetu, wala haitakiwi kukasirika.

    ReplyDelete
  33. Mbona kondomu zimehubiriwa saana na watu bado wanakufaa? Hapa tatizo inaweza isiwe kondomu bali hiyo mia ya kununulia kondomu.

    ReplyDelete
  34. Mzee alichanganya dini na siyasa.

    ReplyDelete
  35. HAPA NDIO INADHIHIRI KUA MWINYI NI MBUMBUMBU KIDINI KWELI KABISA NI KOSA KALIFANYA HANAHAKI YA KUHALALISHA KITU AMBACHO NI HARAM HATA KUKIKARIBIA LICHA YA KULIFIKIRIA VIPI AHIMIZE MAMBO YA KIYAHUDI BRAVO KIJANA.SIKU YA MAULIDI YA RASUL (SAW) NI KUELEZA SIFA,HISTRY,MIUJIZA YA MTUME SI KONDOM.

    ReplyDelete
  36. Watu wengi hapo juu wanaishia kusononeka na kuhuzunika lakini wanasahau uwanja huo haukuwa kwa ajili ya kuhubiri sera za serikali na ngo yake bali sehemu ya ibada.

    ReplyDelete
  37. hao waislam waliompiga kijana wote wanadhambi kijana angepigwa mpaka akafa ingekuwa safi sana mana peponi kimoja tena angekuwa amekaa karibu na maswahaba.

    duh amekosa chance ya pepo masikini hiyo ndo inaitwa JIHAD kufa kwa kumtetea mwenyezi mungu na mtume wake.

    kweli kabisa ndugu muheshimiwa ulipitiwa kabisa.umesahau ulishasema sukari imeingia utamu?

    sasa cha muhimu kijana hasifungwe au itakuwa kasheshe kubwa jamani msalieni mtume jamani msitoe comment za kijana afungwe

    hii itakuwa vita jamani.
    baina ya serikali na waislam.
    haya yangu macho.

    ReplyDelete
  38. sasa hata kama kimemuuma ndio aamue kumpiga kofi raisi wetu tuliempenda jamani, mimi nimeudhika sana hapa nadhani ningekuwepo hata mie ningechangia kumpa kibano huyo mpumbavu na ushamba wake. hasira huko huko usituumizie mzee wetu jamani, alafu mzee wa watu kwa kuonyesha hana ubaya na mtu bado alikuwa amesmile tu, nimejisikia vibaya sana, na afungwe huyu jamaa sio chizi wala nini ni mkorofi tu na maisha yamemshinda

    ni hayo tu wadau

    ReplyDelete
  39. Mie personally nampenda sana mwinyi, ni mtu mwema sana na ameonewa tu hapo, tafadhalini watu inabidi mgrow up acheni ujinga, mambo gani hayo hata kama hukubaliani na mtu ndo umpige kofi?
    na afungwe huyo taahira

    ReplyDelete
  40. We ukivaa kondomu basi ukimwi utapitia kwenye vidonda vya mdomoni au vidoleni, ndo maana bado twafa.

    ReplyDelete
  41. Ya kwanza imebaniwa.. Sasa sijui niliandika nini kibaya au hii globu na yenyewe ishaingia luba? Mzee Ruksa kaonewa.. Muda wa kuoneana haya umepita tunakwisha jamani... kama hamtaki Mzee Ruksa awaambie muache ngono msimkaribishe kuongea. To me, huyu Mzee ni Jasiri na inabidi tumjengee statue kuuubwa pale mjini kwa yote aliyotufanyia. Mungu amlinde Mzee R.

    Mdau Boston, US

    ReplyDelete
  42. BADO MZEE MWINYI NDO KIPENZI CHA WENGI ANAONGOZA MPAKA SASA AKIFUATIWA NA KIKWETE

    ReplyDelete
  43. wadau wooote mlosema dini yake inamruhusu,NI KWELI KABISAAAA

    ndo matokeo ya kufundishana madrasat kuwa so critical,mujahidina,kufia dini ndo uku!!utafikiri wao hawafanyi ngono tena zembe.
    me nimeona sawa tu icho kibao kama Bush tu
    YAAN DINI INARUHUSU TENA KAANDALIWA ******AKIFA
    tukisema jaman ivi wanausalama/viongozi hamwoni jinsi mijadala ile ya kukashifu dini zingine tena kwa jazba ndo matokeo yake ayo,yan awa frustrated guyz wako wengi tu kwenye "nyumba za ibada"

    michu usibane

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...