Afisa Habari wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania,wa pili kutoka kushoto Matina Nkurlu akiwa na walemavu wa ngozi(Albino)wakionyesha ujumbe wao kwa jamii ya kitanzania kwa kutumia mabango katika viwanja vya chuo cha ushirika Moshi wakati wa mbio za kili marathoni mwishoni mwa wiki. Vodacom imekuwa mstari wa mbele kusaidia walemavu wa ngozi kwa misaada mbalimbali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hawa jamaa wanatia huruma sana wanavyoteseka katika nchi yao.Ngozi zao adui mkubwa ni jua.bado kuna watu wanaajiri wa2 hawa katika kazi ngumu na katika jua.Yawezekana hawajui madhara wayapatayo katika jua bali elimu muafaka ikitolewa itasaidia sana kuwakoa hawa ndugu zetu na madhara ya kukaa katika jua au kufanya kazi katika jua kwa muda mrefu

    Mangi wa K'koo

    ReplyDelete
  2. swali:
    albino ni lugha gani?zeruzeru ni lugha gani?

    ni hayo tu

    ReplyDelete
  3. We anon 4:43pm muliza swali! albino ni lugha gani?zeruzeru ni lugha gani! we nadhani ni mtu mzima mwenye akili zako zinazofikiria na kuchambua mambo na kutafakali! hapa bwana kinachoangaliwa ni ujumbe yakwamba umefika! usilete mada za luga wakati! we mwenyewe unawaona na mabango! KWA UFUPI HATUITAJI MADA ZA LUGHA! TUNAITAJI UJUMBE NA UMETOLEWA KWA HAWA NDUGU ZETU.

    ReplyDelete
  4. Anon wa pili. soma hii

    Albinism (from Latin albus, "white"; see extended etymology, also called achromia, achromasia, or achromatosis; not to be confused with albedo) is a form of hypopigmentary congenital disorder, characterized by a partial (in hypomelanism, also known as hypomelanosis) or total (amelanism or amelanosis) lack of melanin pigment in the eyes, skin and hair (or more rarely the eyes alone). Albinism results from inheritance of recessive alleles. The condition is known to affect mammals (including humans), fish, birds, reptiles and amphibians. While the most common term for an organism affected by albinism is "albino" (noun and adjective), the word is sometimes used in derogatory ways towards people; more neutral terms are "albinistic" (adjective) and "person with albinism" (noun).

    ZERUZERU ni kiswahili ila neno hili linaoneka kuwa na ukali kama vile ukisema "Mama amezaa" inakuwa bora ukisema "Mama amejifungua" au mtu "kilema" unasema "asiyejiweza". Hapo inatumika tafisida.

    ReplyDelete
  5. Anyway tuwasaidie ndugu zetu zeru zeru lakini mimi binafsi sijafurahishwa na uamuzi wao wa kukisigina kiswahili chetu na kukacha jina la "zeru zeru" wakaamua kujiita "albino"

    Je asili ya hilo neno "albino" wanalielewa?

    ReplyDelete
  6. matina vipi wewe,naona umekuwa bosi huko...haya bwana mimi ni mdau mwenzako wa Minnesota/Iowa ni salaam tuu na baridi huku inapiga sawasawa!

    ReplyDelete
  7. Mimi nafikiri ni bora na sawa kabisa kuwaita hawa ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi kwa jina la Albino.Ni jina linalotambulika na kukubalika Kimataifa.Hili la kwetu zeruzeru lina ukakasi ndani yake na limekuwa likileta hisia za ubaguzi na unyanyasaji katika jamii.Fulani akimwita mwenzake Zeruzeru huyo,mara nyingi linabeba hisia za kumdhalilisha na kupunguza thamani ya utu wake katika jamii kana kwamba vile mtu huyo hafai na hana uwezo wowote wa kuchangia katika maisha yake mwenyewe na katika maendeleo ya jamii.Ubaguzi huu au kuwanyanyapaa huku kwa Albino hakukuanza Jana,bali ni mazoea ya muda mrefu sana katika jamii ambayo hatimaye yalikuja kuzoeleka na "kuhalalishwa" na makabila mengi kama vile ni jambo jema na la kawaida bila ya wao kutambua kwamba tendo hilo lilikuwa ni uhalifu mkubwa sana katika jamii.Polepole tuanze kulisahau hili jina la Zeruzeru na kulizoea zaidi jina la Albino.Lakini mada muhimu zaidi hapa ni kuangalia jamii ifanye nini katika kuwapa ndugu zetu wa Albino huduma maalum za kiafya na lishe bora ili wasiathirike zaidi na athari za mionzi ya jua,uwezo mdogo wa kuona vizuri,jinsi ya kuzihudumia nywele zao ili zisichukize,na jinsi ya kulinda ngozi ya mwili dhidi na mionzi yz jua,baridi kali na ukame,na kutotembea pekupeku bila ya viatu au makubazi.Muhimu zaidi ni kuhakikisha kwamba kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule basi anapata fursa hiyo ya kusoma bila ya ubaguzi wala manyanyaso.Wazazi waelimishwe kutowaficha watoto wao maAlbino majumbani mwao kwa kuhofia lawama na shutuma kutoka kwa ndugu wa karibu na jamii iliyowazunguka.Pia tuchukue tahadhari katika kupunguza uwezekano wa kuzaa watoto wenye ulemavu wa ngozi kwa "sababu za kurithi mapungufu hayo kutoka kwa wazazi wao",hilo linawezekana kabisa.Tusiyakimbie matatizo kwa kutafuta njia za mkato bali tuyakabili kwa ujasiri na umakini mkubwa.

    ReplyDelete
  8. Albino ni neno la kigeni, sijui ni lugha gani. Hawa wanaitwa zeruzeru. Kama kawaida yetu, cha kigeni ndo kilicho bora, na ndo maana wanataka kuitwa albino.

    Jeno sahihi ni zeruzeru.

    ReplyDelete
  9. Hawa ndugu zetu walemavu wa ngozi lazima tuwajali ndugu zanguni haina haja ya kuwatenga na kuwaua kwani ni binadamu kama watu wengine,Big up Matina ni vizuri sana kuwapa moyo kijana big up again!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...