
ACP Kalinga (wa pili kushoto) akimkabidhi SSP Protas mfano wa hundiya Milioni 40. anayeshuhudia kushoto kabisa ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa Bw. Stephen Kingu.
Vodacom Tanzania hivi karibuni ilikabidhi zawadi za pesa taslimu zenye jumla ya shilingi Milioni 80 kwa washindi wawili wa Droo ya Tuzo. Rioba Nchunchulia Mwita (pichani chini) ambaye ni mkulima wa Nyamongo Tarime alikuwa mshindi wa Millioni 40 wa mwezi Desemba 2008 wakati SSP Pudensiana Protas (pichani juu) ambaye ni Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mwatex Mwanza yeye alikuwa mshindi wa Milioni 40 wa mwezi Januari 2009. Zawadi zote hizi zilikabidhiwa na ACP Kalinga ambaye ni Kaimu Mkuu wa Polisi Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...