Wole Soyinka

It is no longer a rumour.
It is official – not official official, but intellectual official.

You will get a notice/info of the JULIUS NYERER INTELLECTUAL FESTIVAL WEEK April 13th to 17th 2009 as early as next week.

Wole Soyinka is coming to give Nyerere Annual Lectures, 2009. His topic is: NEW IMPERIALISMS. Don’t ask me what it means – I keep my fingers crossed!

During the week we’ll have many stimulating events including celebrating NKRUMAH CENTENARY DAY and PAN_AFRICAN DAY.

Remember, the main mandate of the Mwalimu Nyerere Chair is to re-invigorate intellectual debates. The full programme will be circulated in this and other list servers, courtesy Chambi.

Issa G. Shivji
Mwalimu Nyerere Professor of Pan-African Studies
University of Dar es Salaam
P. O. Box 35091
Dar es Salaam
Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. it sound material and test honestly, this is the end result our leader and not thiefs should think of, DEAD BUT ALIVE.
    FUNNY , come to see how nany people will turn out on the material day.
    please make it posible, just as you read this post, tell your friends and enemies on the date of the occasion.
    Mungu ibariki tanzania,Mungu mbariki nyerere.

    ReplyDelete
  2. Sijui kama wakina Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Msekwa watahudhuria, safari hii!

    ReplyDelete
  3. Ni heshima kubwa kwa nchi yetu kutembelewa na Wole Soyinka, mwandishi wa kiwango cha juu kabisa duniani, aliyepata tuzo ya Nobel, mwaka 1986. Ameandika vitabu vingi: tamthilia, riwaya, mashairi, na insha, na bado anaandika sana.

    Soyinka amekuwa mstari wa mbele kutetea umoja wa Afrika. Kwa hoja makini zilizojikita katika utafiti, amesema na kurudia kuwa lugha inayofaa kutumiwa kama lugha ya Afrika nzima ni kiSwahili.

    Soyinka alishafika Tanzania, mwaka 1971. Katika maandishi na mahojiano yake, Soyinka amesema kuwa fikra na sera za Mwalimu Nyerere ni mfano wa kuigwa.

    Mimi kama mwalimu wa fasihi, ambaye nafundisha maandishi ya Soyinka pia, nasikitika kuwa, kwa ujumla, vitabu vya Soyinka havipatikani Tanzania: iwe ni Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara, Mbeya, Songea, Arusha, Mwanza au Dodoma. Nasikitika kuwa utamaduni wa kuvithamini vitabu na kuvisoma umefifia Tanzania. Nasikitika kuwa dhana iliyopo ni kuwa kusoma vitabu ni wajibu wa wanafunzi tu. Kwenye miji na vijiji zimejaa baa, lakini maduka ya vitabu hayaonekani. Na hata kama kuna duka la vitabu mahali, watu wananunua bia, si vitabu.

    Kuwasikiliza mabingwa kama Soyinka, au kusoma maandishi yao, ni namna nzuri ya kujielimisha, na kujipima ili tutambue wajibu tulio nao wa kujibidisha katika elimu. Tunakubaliana kuwa ufisadi ni adui wa nchi yetu. Lakini tukumbuke kuwa tulipopata Uhuru, tulitamka wazi kuwa ujinga ni adui yetu mojawapo.

    ReplyDelete
  4. kamwe hauwezi kumtaja mashaka bila kumtaja shayo na hauwezi kumtaja shayo bila ya mashaka. hao vijana wawili ndo tegemeo la tanzania dhidi ya mabadiliko, natumai siku moja nao watatuwakilisha jinsi nyerere alivyobakia moja ya historia kubwa katika bara la afrika. mm wakija kugombea ubunge au urais, kura nawapa kuliko kutupa kura yangu chooni na mafisadi wakina vjisenti

    ReplyDelete
  5. Mbele wa 7:04 am alipaswa kufahamu ni kitu gani kilicho "uwa"maduka ya vitabu hapa nchini kuanzia miaka ya themanini mwanzoni!Analalamika kwamba ajabu utaona watu wanajali sana kununua Bia kuliko Vitabu,mabaa na vilabu yako mengi lakini maduka ya vitabu ni machache!Eti,watanzania wamepoteza utamaduni wa kujisomea vitabu!Kajiuliza,kinachosababisha kuwepo kwa hali hiyo hapa nchini ni nini?Je,Mbele kapita katika maduka ya vitabu hapa nchini na kuona bei kubwa ya vitabu mbalimbali?Wangapi wenye uwezo wa kununua vitabu hivyo,iwapo mlo mmoja tu kwa siku ni tatizo kubwa kwake? Hao anao waona wakinywa Bia kila siku ni wateja walewale,sio kwamba soko limekuwa likiongezeka!Litaongezekaje kwa bei ya shs.1,400/= kwa chupa moja ya bia ya nusu lita?Wasomi wengi hapa nchini hawachapishi vitabu kutokana na vikwazo mbalimbali,hususan vinavyo tokana na gharama kubwa za maandalizi ya vitabu hivyo na uchapishaji!Serikali imeweka mbele sana "Kodi katika kila kitu"bila kutumia akili na busara kwamba sio vyote vinavyo stahili kutozwa Kodi nyakati zote!Kodi au Mzigo wa Kodi unapokuwa ndio chanzo cha kuzorotesha tija na ufanisi katika maendeleo na ukuaji uchumi,basi serikali itakayo ng'ang'ania mfumo uleule wa Kodi uendelee,ujue kwa hakika kwamba haiko pamoja na wananchi au walipa kodi wenyewe!Tumesha poteza miongo mingi sana kwa kubishana sana kuhusu hata hili jambo dogo lakini muhimu sana la kutotoza kodi vitabu na machapisho mbalimbali maalum kwa kutoa elimu na kupunguza ujinga!Lakini jitihada zote hizo zilikuwa sawa na "Kumpigia Mbuzi Gitaa!".Muziki wake ndio huu ambao sasa tunaucheza!Uhaba wa Vitabu na watu kupoteza kabisa hamu ya kujisomea vitabu!

    ReplyDelete
  6. Mbele wa 7:04 am alipaswa kufahamu ni kitu gani kilicho "uwa"maduka ya vitabu hapa nchini kuanzia miaka ya themanini mwanzoni!Analalamika kwamba ajabu utaona watu wanajali sana kununua Bia kuliko Vitabu,mabaa na vilabu yako mengi lakini maduka ya vitabu ni machache!Eti,watanzania wamepoteza utamaduni wa kujisomea vitabu!Kajiuliza,kinachosababisha kuwepo kwa hali hiyo hapa nchini ni nini?Je,Mbele kapita katika maduka ya vitabu hapa nchini na kuona bei kubwa ya vitabu mbalimbali?Wangapi wenye uwezo wa kununua vitabu hivyo,iwapo mlo mmoja tu kwa siku ni tatizo kubwa kwake? Hao anao waona wakinywa Bia kila siku ni wateja walewale,sio kwamba soko limekuwa likiongezeka!Litaongezekaje kwa bei ya shs.1,400/= kwa chupa moja ya bia ya nusu lita?Wasomi wengi hapa nchini hawachapishi vitabu kutokana na vikwazo mbalimbali,hususan vinavyo tokana na gharama kubwa za maandalizi ya vitabu hivyo na uchapishaji!Serikali imeweka mbele sana "Kodi katika kila kitu"bila kutumia akili na busara kwamba sio vyote vinavyo stahili kutozwa Kodi nyakati zote!Kodi au Mzigo wa Kodi unapokuwa ndio chanzo cha kuzorotesha tija na ufanisi katika maendeleo na ukuaji uchumi,basi serikali itakayo ng'ang'ania mfumo uleule wa Kodi uendelee,ujue kwa hakika kwamba haiko pamoja na wananchi au walipa kodi wenyewe!Tumesha poteza miongo mingi sana kwa kubishana sana kuhusu hata hili jambo dogo lakini muhimu sana la kutotoza kodi vitabu na machapisho mbalimbali maalum kwa kutoa elimu na kupunguza ujinga!Lakini jitihada zote hizo zilikuwa sawa na "Kumpigia Mbuzi Gitaa!".Muziki wake ndio huu ambao sasa tunaucheza!Uhaba wa Vitabu na watu kupoteza kabisa hamu ya kujisomea vitabu!

    ReplyDelete
  7. Kazi nzuri Prof. Shivji na wengine kuleta kichwa hiki. See you there!

    ReplyDelete
  8. ndo nani uyu bwana??soyinka?

    ofkoz kodi za nchi hii wal'hahi huwezi fanya +ve things,,,asa sie wafanyakazi ndo kabisaaaa pesa yoote waishiwa kuliwa VAT,EWURA nk

    anyway tutafika tuuuu!!

    ReplyDelete
  9. Profesa Shivji, Naomba umkumbushe mgeni wako mazuri na mabaya pia ya Nyerere. Nakukumbusha kuwa raia wa Tanzania walikuwa hawana haki yoyote chini ya Mwalimu na wengi walikufa njaa.

    Kama mfanyabiashara enzi za uhai wake, wazazi wangu walipokonywa mali zao kutokana na siasa ya kijamaa. Dukani kwangu wananchi wanalilia sabuni na unga kwa resheni. Sukari na mchele nilikuw anapata magunia mawili kwa mwezi kutoka ugawaji.

    Nategemea mgeniw ako atagusia matatizo kama hayo tuliyopata sio kumfagilia tu.

    Shukurani Balozi Michuzi kwa kunipa nafasi hii.

    ReplyDelete
  10. Kuna swali gumu la kujibu kuhusu legacy ya Nyerere.

    Nyerere alisema kwamba ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

    Halafu tena akaendelea mbele na kupora mali za Wahindi na Wazungu.

    Je hiyo ndio siasa safi na uongozi bora?

    ReplyDelete
  11. Wole Soyinka anayajua mabaya na mazuri ya Mwalimu na Ujamaa, hebu soma maneno yake mwenyewe haya:

    "On the one hand, Ujamaa was evolved from certain principles of traditional social organization which had emerged through cultural evolution. On the other hand, violence was done to this obviously organic process by uprooting cohesive communities, relocating then in comparatively modernist villages where social amenities and access to centralized organs of development could be provided. The effect of this on the existing cultural security, itself a non-negligible factor and agent of productivity, was underrated. We are speaking here of a quantity beyond sentimental attachments. Century old and tested modes of production were abruptly interrupted; the results was, even in Nyerere’s admission, not the developmental model it was expected to be. Let me add by the way that I was, and still am, a believer in the basic philosophy of Ujamaa; indeed, I eulogized it in a poem. That aspect of interrupting, in such artificial way, the cultural cohesion of a community was however, one which remained for me, frankly, troublesome" (Wole Soyinka's 'Culture, Memory and Development' 1992: 205)

    ReplyDelete
  12. Mdau Chambi Chachage ahsante sana kwa kutuletea kitabu cha Soyinka kilichogusua Ujamaa na Nyerere.

    Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ndio iliyotutia katika umasikini mpaka hivi leo. Nyerere aliweza kuendesha nchi kama kijiji chake bila ya kujali haki za Watanzania ili mradi anachokitaka kinafanyika. Tukakopa Uchina na Urusi ili wananchi walishwe. Vijiji vikafa na watu wakafa na vijiji vyao kwa kulazimishwa kuhama na kuishi pamoja.

    Japokuwa alikuwa hana makubwa, lakini hajaishi maisha ya kimasikini kama vile ya wanaujamaa wenzake kama akina Fidel Castro. Na hata Castro, amejenga nchi yake, daktari wa kila aina wapo na watu hawajafa njaa.

    Ningependa kweli kujua faida ya miaka zaidi ya 20 ya udikteta wa Nyerere Tanzania ili niweze kuwa na pointi za kumfagilia.

    Wenzake Cuba, China na Vietnam wana viongozi wa kijamaa au walikuwa na viongozi wa kijeshi (Brazil, Chile) lakini sio wa kijamaa lakini wamejenga nchi zao na wako mbali zaidi yetu. China ni uchumi mkubwa wa tatu duniani, Brazil wa nane. Je, wasomi wa Nyerere hapa, nilikuwa naomba kujua vipi Nyerere katusaidia kuiendesha nchi na kasaidia nini kuifanya Tanzania katika maendeleo hata kwa nguvu.

    Ahsante Balozi Michuzi kwa nafasi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...