Mh. Profesa Mark Mwandosya (shati jeupe) akipiga simu kuomba msaada  muda mfupi baada ya ajali kutokea. Mbunge wa zamani wa Biharamulo Magharibi ndugu FAUSTINE KABUYE alifariki katika ajali hiyo pamoja na watu wengine wawili  sehemu za Kilosa mkoani Morogoro  iliyohusisha basi la RS investment likitokea Bukoba kwenda DAR. Habari ambazo bado kuthibitishwa zinasema basi hilo lilikuwa likiendeshwa na kondakta kwa mwendo wa kasi sana. Hayati Kabuye alikuwa njiani kuhudhuria mkutano mkuu wa TLP.
baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo
mmoja ya waliopoteza maisha
wasamaria wema wakisaidia majeruhi

Globu ya Jamii inatoa rambirambi kwa wafiwa katika ajali hii na pole kwa majeruhi. Wakati huo huo inaweka alama ya kujiuliza kwa nini hizi ajali hazikomi. Tatizo ni nini hadi ndugu zetu wanateketa namna hii kila kukicha? Kifanyike nini ili balaa hili lituame?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. bwana michuzi nafikiria ingekuwa vizuri kama wananchi katika basi wakati wanasafiri, dereva akiwa anakimbiza gari inabidi waungane na kupiga kelele kusema dereva punguza mwendo kama hatapunguza wampigie. Maana dereva anapokuwa anakimbia watu wamenyamanza yeye anaona ni poa kabisa.

    ReplyDelete
  2. Mungu awalaze marehemu mahali pema peponi. Amina

    ReplyDelete
  3. Kwanza kabisa inaonyesha ni jinsi gani wananchi walio wengi hawajui umuhimu wa maisha. Hatudhamini uhai wetu kabisa, na ndio maana tunawaachia madereva wakimbize magari au kuendesha pasipo na umakini.

    Ni wazi kabisa kuna watu wanashabikia mabasi yanayokimbia, na wanayapenda ndio maana hayo mabasi yanayosababisha ajali yanaendelea kuwepo. laiti wananchi wangesusia mabasi kama hayo kusingekuwa na biashara, na wamiliki bila shaka wangeliangalia hilo, ili kuajiri madereva makini.

    Pili, nadhani shukutuma ziende kwa mamlaka zinazohusika kwa kushindwa kudhibiti hizi ajali....kwa mtazamo wangu nadhani inabidi ifikie mahali kuwe na hatua kali, ikiwemo kuanzisha lesseni maalumu ya hawa madereva, ambayo itakuwa 'renewed) kila kipindi cha miezi 6 ili kuhakiki kuwa wanafuata sheria na maadaili ya udereva. kama kutakuwa na dosari ndogo tu basi leseni inyang'anywe.

    Hatua nyingine ni kuwapima akili hawa madereva, kuwapima kiasi cha pombe (mana ajali nyingine ni kwa vile madereva ni walevi), kuwapima kama wamepumzika vya kutosha...hii ifanyike kabla ya kila safari. Na jukumu hili wapewe wamiliki, ili kabla ya kumkabidhi dereva ufunguo ajaze form kuwa taratibu zote zimefuatwa, na ikitokea ajali ni uzembe wa dereva, basi huyo mmiliki au kampuni ifilisiwe ili kuwalipa watu waliopeteza maisha (ndugu zao) au majeruhi.....hii itakuwa ni maumivu kwa wamiliki na itasaidia wawe makini wanapo ajiri watu.

    Polisi pia wawe makini zaidi, sio kusimamisha magari tu, bali wafanye ukaguzi wakati gari likiwa safarini, ikitokea kuna hitilafu basi safari ifunjwe na uangaliwe utaratibu mwingine wa kuwasafirisha watu kwa gharama za mwenye basi.....We need to be serious....na ndio njia ya kuokoa maisha yetu.

    Haya ni maoni machache tu, mana nimeshaona magari mabovu, polisi analicheki then anamwambia dereva wafikishe hawa watu then report polisi...huuu ni upuuzi wa hali ya juu....tukitaka mambo yaende basi sheria must be strict...hakuna msamaha kwa kosa...na Abiria wakubali....mana sometimes Abiria ndio wanapiga kelele...kwa mfano Polisi akisema gari lina matatizo....basi utakuta watu wanataka wapelekwe hivyohivyo....ikitokea ajali basi ndio yanakuwa matatizo.....

    TATIZO: Watanzania wengi tunapenda ushabiki....na kufanya mambo ambayo hayana faida.....badala ya kuangalia matatizo.....hizi ajali kila siku zipo lakini watu wanashabikia mambo mengine yasiyo na direct impact to the society!!!!

    ReplyDelete
  4. anyway tusilaumu sana yote ni mipango ya mungu,tukisema sana tutakuwa tunakufuru ukizingatia jamaa wameanza safari toka Bukoba salama kwa masaa karibu 20 lkn wamekuja kupata ajali moro yakibaki masaa mawili au matatu wafike DAR,
    MAY GOD REST ALL IN PEACE.AMEN

    ReplyDelete
  5. The frequency of such accidents in bongo is frightening it would possibly help if public transport laws are reviewed and enforced
    There should for example be strict form of vehicle inspections like the MOTs in UK
    Driver fatigue laws to control working hours of drivers
    Driver logbooks
    Compulsory fitting of Speed Control governors
    A lot can be done
    Poleni sana ndugu na jamaa
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  6. mdau mwenye hotuba ndefu nakubaliana nawe hasa kwenye swala la leseni. tatizo rushwa.

    si mabasi wala malori ya bongo yenye tachograph ndo maana polisi hawajui kinachoendelea.

    safari ya bukoba-dar ni zaidi ya saa 24. lakini kuna dereva mmoja tu untegemea nini?

    pili, si SUMATRA wala wizara husika iliyo na kiongozi aliyewahi kutoa tongotongo angalau kujua jinsi nchi za wenzetu zinavyofanikiwa kuwabana madereva na kufuata kanuni za usalama barabarani.

    madereva wengi mtu akinunua gari, hanashida ya kujifunza ama kufanya mtihani ili dereva kamili. sheria kali zinasaidia kupunguza ajali. tatizo RUSHWA.

    HUYO MZUNGU ANA BAHATI KWELI BACK PACK YAKE IMENUSURIKA NAONA KAIGEMEA NA KICHWA CHAKE. PENGINE HAKOSI BIMA HUYO NA USIPOANGALIA DENI LITAMWANGUKIA MWENYE BASI.

    ReplyDelete
  7. Nadhani hamjasoma vizuri habari, afadhali huyo aliyekuwa anaendesha angekuiwa dereva no alikuwa ni kondakta ndugu zangu. Imefika kipindi mimi sielewi ni lini tutakuwa serious kwani the way tunavyoendesha maisha yetu ni kama sinema. We are not serous at all, individual level mpaka serikali. Ukipiga kelele kupinga uendeshaji mbovu abiria wenzio wanakugombeza, what do you do then?

    Ninaishi kimara mwisho, kituo cha polisi ni mita 20 toka kituo cha daladala. Lakini daladala zinashusha na kupakia zikiwa muda wote barabarani kwenye high way na no one cares. Mpaka siku lorry liuwe watu wote wa hiace ndio tutachukuwa hatua. Kama mjuavyo magari mengi mabovu hayana brakes na madereva huwa wanakuwa wamechoka so kuiparamia hiace ni kitu kidogo tu. Let's be serious wandugu hata sababu ya kufa kufa ovyo.

    ReplyDelete
  8. SIJUI PROF MWANDOSYA ILIKUWAJE AKAWEPO KARIBU NA HILO TUKIO LA KUSIKITISHALAKINI KWA KWELI JAMAA NI MTU WA WATU.SIJAWAHI KUKUTANA NAYE LAKINI THERE IS SOMETHING ABOUT HIM INANIAMBIA NI MTU WA KUAMINIKA NA WATU.

    USA 1

    ReplyDelete
  9. THIS IS VERY SADDENING I HAVE A SOLUTION FOR THIS TYPE OF PROBLEM FROM THE ENGINEERING POINT OF VIEW.
    1.A local or high government official must gather all citizens to look into all possible options available to decrease accidents.

    2.The solution should include electronic equipments to monitor highspeed vehicles it must also include personel officers being placed every reasonable distance along all major highways accross the country,it must also include punishment for everyone bus drivers,bus owners and everyone in between if they violated any law conversion.

    3.As an electrical engineer i am willing to cooperate with anyone in the government willing to obtain these equipments.I will provide my expertise advice in expertise quality in comparison to prices.

    4.About laws any financial fines imposed on these senseless and dangerous citizens should go to good courses such as provide income for all these personels and cover the cost of equipments and should also help construct more hospitals and schools.That way no one will afford to be irrational and unsafe when operating a vehicle.

    WE CANNOT BE LAID BACK WHILE OUR PEOPLE ARE GONE OVERSENSELESS AND SELFISH ACTS!!!

    i can be reached at kambizambo@yahoo.com

    ReplyDelete
  10. lorry liuwe watu wa hiace wote? kwani hukusikia ya Monduli watu 23 waliokufa kwenye hiace jumamosi fulani mwaka sikumbuki, wamejenga kamnara na hakuna la zaidi. nana aangalie sheria wakati waangalia sheria wao wana usafiri wao na kama wanaenda mbali basi ndege zipo, na wao ndio wamiliki wa baadhi ya mabasi na wavunja sheria wakuu kwa kwa kutowalipa mishahara madereva na makonda eti wale mezani kwao! mambo mengine hata si ya kujadili kwani yanaudhi sana utadhani nchi inaendeshwa na watu wa nchi ya kufikirika.Pole kwa wafiwa na majeruhi.

    ReplyDelete
  11. Hemed KagobeApril 25, 2009

    kusema ukweli hili swala la ajali za kila kukicha nchini Tanzania mimi binafsi linanisikitisha na kunihuzunisha sana kwani linachangia sana kupoteza nguvu kazi ya Taifa, nipo masomoni nje ya nchi, binafsi nimekuwa na mawazo nikirudi Tanzania nianzishe Kipindi kuhusiana na swala zima la ajali hizi za kila siku. imefikia hatua, mtu mwenye afya na ambaye ni tegemezi katika familia fulani anakufa gafla au kulemaa kwa ajali na akiacha familia au ndugu ambao walikuwa wanamtegemea wakipata tabu zaidi, mfana leo Bwana michuzi ukisema unaenda Iringa au Mbeya inabidi uende unasali njia nzima,kwa jinsi gani usafiri ulivyo kuwa si salama. sasa basi hili swala la ajali tuungane watanzania wote tulipige vita, kwani linaepukika kwani ni uzembe tu ndio unaofanyka. ni bora mtu apate ugonjwa atakufa taratibu atapangilia vitu vyake. ila ajali mtu na nguvu zako unakwenda kazini,mkutanoni,kusalimia wazazi, au ndugu na jamaa,au katika shuhuli mbali mbali za kimaisha unajikuta unapata ajali gafla na kufa au kulemaa. hili swala watu tuamke na tulipige vita kwa nguvu zetu zote. nimekaa miaka 4, hapa ugenini ila ajali ambazo nimesikia au kuona ni chache sana na hazi cost maisha ya watu.sababu watu wapo makini sana barabarani, hivyo basi watanzania tuungane kupiga vita swala hili.

    ReplyDelete
  12. THIS IS A BIG SHAME TO US TANZANIANS.WE ARE APROXIMATELLY 50,000,000 PEOPLE AND CANNOT DO A SINGLE ACTION ABOUT IT,WE ARE WAITING FOR BARACK OBAMA OR UNITED NATIONS OR A GROUP OF FEW SCIENTISTS OR SOME WHITE PEOPLE TO COME AND COORDINATE A MEETING AND HELP US SOLVE THE PROBLEM OF USALAMA WA BARABARANI.

    WE ARE VERY LOUSY ,UNACTIVE,UNDETERMINED GROUP OF PEOPLE.

    ReplyDelete
  13. Kwa muda wote niomsikia marehemue sijawi kusikia jina FAUSTINE bali PHARES KASHEMEZA KABUYE sasa wewe michuzi hili la faustine umelitoa wapi? Au unakumbukumbu za marehemu faustine rwilomba? Halafu wewe anony unayesema kuhusu kondakta kuendesha sioni cha ajabu hapo kama kampuni hiyo inautaratibu wa kuwa na madereva wawili wakipokezana kazi zote utawahukumu tu kwa sababu abiria mmoja alikaguliwa tiketi na dereva ambaye hakuanza safari? Dereva aliyeanza safari akipakia mizigo au akibadilisha tairi iliyopata pancha na abiria alipandia njiani baadaye akamwona ameshika usukani ni sawa akidai utingo anaendesha gari?

    ReplyDelete
  14. Poleni mliofikwa na kuguswa na ajali hii! Mheshimiwa Kabuye si alikuwa anasubiri rufaa ya kesi ya Uchaguzi!! Mungu awarehemu!

    Watanzania hatujui thamani ya maisha. kama mdau alivyosema tunaishi kisinema zaidi kuliko uhalisia. Licha ya ufukara unaotuzingira bado tumeruhusu kuingia gharama za kijinga kabisa za kupoteza nguvu kazi kwa vifo na ulemavu, usiseme hasara ya mali.

    Watz twaishi maisha ya aibu kwa ktosimamia taratibu tulizojiwekea kwa usalama wa maisha yetu. Hebu waulize polisi au SUMATRA, leseni ngapi zimefutwa kwa kukiuka sheria za usalama barabarani?? utaambiwa hakuna hata moja licha ya ajali za kutisha zinazojirudia. Kwa nini hatuigi nchi za wenzetu wanavyodhibiti ajali kwa kutumia sheria (faini kali, kunyang'anywa leseni, kifungo)bila kujali hadhi ya mhusika. Jana nimesikia mchezaji wa Chelsea John Obi Mikel kazuiwa kuendesha gari kwa miezi 15 kwa kuendesha gari akiwa kalewa. Sie tunadhani RUSHWA na bla bla ni BORA kuliko maisha ya watu.

    Siku tukiruhusu sheria na taratibu halali kuongoza maisha yetu, ndipo tutakuwa na haki ya kudai kuwa tu-wastaarabu kama wenzetu wayapao maisha ya watu thamani, vinginevyo tutaendelea kuwa wanyama tutembeao kwa miguu miwili na kutenda kama vivuli vya binadamu. AIBU SANA!!
    Mungu na atusaidie

    ReplyDelete
  15. Madereva wa bongo wamezoe barabara mbovu period. Kabla ya kuwekewa lami ajali zilikuwa ni nadra sana. angalia njia za dar-arusha, dar-tanga, dar-mbeya kila leo ni ajali tu. Lakini hii ya mwanza na ile ya kwenda kwa mkuu wa zamani wa nji Mkaahapa ni mara moja moja sana.
    suluhisho hapa ni mabasi kupangiwa muda wa kufika vituo vikubwa na hapa tusiwategemee polisi maana hawana maana. Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu wakishirikiana na tanroads waweke kamera zitakazo kuwa sehemu kama vile mizani ilivyo zitakazo kuwa zinarekodi wakati basi linapoanza safari likiingia na kutoka kati ya miji mikubwa njiani. Mfano kama basi linatakiwa kufika dodoma saa tano likafika saa nne mmliki atozwe faini ya kufa mtu ikibidi hata basi auze.

    ReplyDelete
  16. Pumbavu kabisa!! nasikia hasira yakutisha, swala la madereva wa bongo lisipopewa umuhimu watatuuuwa wote, mpaka msafara wa rais na mkuu wa polisi na maafande mbuzi wa bararani wapate ajali mbaya kama hizi ndio hiyo nchi itatia akili kuzingatia umuhimu wa sheria za barabarani, kondacta anaendesha gari????????

    ReplyDelete
  17. Mungu azilaze roho za marehem peponi.
    Naungana na wachangiaji wote, niliwahi kusafiri Dar-Iringa nilikoma maana dereva aliendesha ovyo, nikajaribu kupiga kelele kumuomba apunguze mwendo,

    abiria wenzangu wote ndo kwanza waliniangalia kwa dharau nakukonyezana eti huyu nae sie twawahi shuguli zetu kama unaona hujaridhika ungekodi la peke yako.

    Inasikitisha sana kila kukicha ndo wimbo huo huo ajali. Mamlaka zinazohusika wangesimamia hata suala la kila bus kuwa na mikanda, itokeapo ajali angalau kunakuzuia majeruhi kwa kiasi fulani.

    Sijui hadi ajekufa nani ndo sheria ziwekwe. Abiria jamani tuwe na umoja kumshambulia dereva pindi atakapoendesha ovyo.

    ReplyDelete
  18. Michuzi hizi picha zinatisha. Uwe unaweka onyo kwanza kwenye picha kama hizi. Manake wadau tutaanza kuota ndoto mbaya

    ReplyDelete
  19. Kwa maoni yangu ni RUSHWA!! Kama unaweza pata leseni halali kwa 'njia haramu' unategemea nini?Kuendesha gari ni dhamana anayopewa dereva juu ya maisha ya watu(abiria na watumiaji wengine wa barabara). Tunawapa watu dhanmana ya maisha yetu si kwamaba wana uwezo unaostahili bali ni kwa kuwa wana pesa inayostahili!!Tunatia aibu, lakini thats the choice we have made ourselves!!
    R.I.P. the victims.
    Pompidou.
    Athens.

    ReplyDelete
  20. Patrick Nhigula "magazeti"April 25, 2009

    Haya, wazee sijui kama watu Tanzania wana kumbukumbu juu ya ajali ambazo zimeua kuanzia Waziri Mkuu mpaka wananchi wa kawaida. Waziri mkuu Sokoine alifariki kwa ajali ya gari akitoke Dodoma Bugeni, Waziri mdogo Salome Mmbatia, Wabunge wawili sasa, na Maziri kadhaa wameusika na ajali kama Kapuya, Muhidi Fadhili, na Chenge ambaye ameua watu wawili. Mwasiasa Mkongwe Diwani alifariki kwa ajali ya gari kongwe dodoma. Mimi ninafikiri viongozi wa Tanzania sasa hawa interest na issue ambazo haziusiani kama watatengeneza pesa. Pili, wengi wao hawana elimu ya public policy na hawana elimu ya Public issue. Tatu, Mzumbe and Chuo Kikuu sasa ni lazima waanzishe taaluma ya kufindisha watu watakaokuwa viongozi wanatakao angalia matatizo ya jamii. Nne, wabunge wetu sidhani wana staff waliosoma professional degree kuwasaidia kuandika proposal juu ya matatizo na kuandika policy na ku-table kuwa bill and pass kuwa law. Hivyo, bunge ofisi sasa badala ya kununua magari ya wabunge na kuongeza posho, ni wakati wa kuajili personal assistances wa wabunge wenye elimu ya juu ya nyanja za maeneo yote ya social issues....

    ReplyDelete
  21. Nilipishana na hiyo basi 75 km from Morogoro, sina hakika lakini ilikuwa saa moja kasoro 10 au 15, hizo ni kama 180 km kutoka Dodoma, Most prob ni kuwa wakitokea bukoba walilala Dodoma. Kisheria walipaswa kuondoka saa 12.00 lakini kimahesabu jamaa ni ama waliondoka Dodoma saa 10.30 au mapema zaidi, au waliunganisha usiku kucha ndo maana dereva alichemsha akamwachia konda.
    Mvua ilikuwa imenyesha na lami ya Moro-Gairo inateleza sana. La kujiuliza ni JE, ni mabasi mangapi yanayosafiri umbali mrefu yana madereva wawili ?????? Bukoba Dar ni zaidi ya km 1200 au masaa 16 ya mwendo!!

    ReplyDelete
  22. Phares Kabuye (alitanguliwa ubunge) amefariki dunia siku chache baada ya Anatory Choya (kumfungulia mashtaka ya kufutwa kuwa mbunge)kutanguliwa uDC juzi ! Yote ya Mungu.Japo mengi. What a concidence of events?RIP

    ReplyDelete
  23. Kaka Michuzi, kila ukitoa habari ya ajali nimekuwa nikisema na leo narudia kusema "ili kukomesha tatizo la ajali za Barabarani, wasababishaji wa jali za barabarani wahukumiwe kama wahalifu wengine wa makosa ya Uuaji"

    ReplyDelete
  24. Hibi Kikwete ana muda gani madaakani? Mbona hachakaliki kama mwenzie siku mia tu lakini mambo si haba.

    Hivi hawezi kuweka sheria kali kuhusu haya mabasi? Ingekua wenye mabasi wanachukuliwa hatua kubwa au kufilisiwa. Ninauhakika wangeajiri madereva wenye ujuzi. Kila siku ni ajali na maisha ya watu yanaponyoka bila sababu. Agggghhhhhh.

    Raisi sikia kilio cha watu. barabara wala sio mbaya ila madereva ndio hawafati sheria.

    RIP

    ReplyDelete
  25. Wakati mwingine sisi abiria ni wajinga. Ilikuwaje wamwachie Konda aendeshe hilo basi? Mtasema Mungu alipanga lakini wakati mwingine mnachosha Mungu na hizi sababu zisizo na maana. Kama hamjijali hata Mungu mwenyewe hatojali. Kinachotakiwa ni pindi abiria watakavyoona dereva anahatarisha maisha yao basi wamshushe na kumpa kibano cha nguvu hii itarekebisha tabia zao.
    Pia, inakuwaje dereva mmoja akabidhiwe basi kutoka bukoka mpaka Dar pekeyake? kungekuwa na angalau madereva wawili ili kuondoa uchovu wa kuangalia lami.
    Inatakiwa wenye mabasi washitakiwe kwa kuwa wanaharibu maisha ya watu kwa sababu za tamaa zao binafsi. Kuna watoto sasa hivi hawana wazazi kwa sababu za uroho kama huu, na kama wakishitakiwa na kufilisiwa kwa sababu ya kusababisha upotevu wa maisha ya watu watatengeneza akili na hawataruhusu huu uhuni.
    Mwanga wa milele uwaangazie, wapumzike kwa amani...........

    ReplyDelete
  26. Tunamalizwa na mambo mengi watanzania! Mafisadi wanatumaliza, Ukimwi unatumaliza, Malaria inatumaliza, Umaskini ndio huo! Sasa madreva naona nao wamejidhatiti kuwamaliza abiria wao! Maskini katika picha namuona Mzee Kabuye akiwa kalaa pale chini kifua wazi katika dakika zake za mwisho!
    Madreva wengi ni watu ambao maisha yao ni ya duni kiasi kwamba hawatofautishi maisha na kifo! Hawezi kujasli maisha ya watu wengine kama yeye haoni umuhimu wa kuishi. Madreva wetu ni watu duni sana! angalia familia zao kama wanazo!

    ReplyDelete
  27. hivi vyombo vya usalama barabarani mnafanya kazi gani? mnajisikia raha sana kupokea mshahara mwisho wa mwenzi wakati watu wanapoteza maisha kila siku?

    linchi langu ila nalichukia sana hasa kupokuja mambo ya ajali

    ReplyDelete
  28. Tatizo hapo linaanzia mbali sio tu swala la konda kuendesha au basi kuwa na dereva mmoja. Kitu kinachotumaliza sisi ni adui RUSHWA. Wadau wametoa maoni mazuri tu ila hayo wayasemayo hayatekelezeki kwa kuwa RUSHWA inatawala ktk kila hatua. Dereva akikamatwa kwa kuendesha mwendo wa kasi hilo si tatizo, anamalizana na askari hapo hapo na safari inaendelea. Mwenye basi hafungiwi leseni ya biashara kwa kuwa anajua kula na wahusika. Watanzania tufumbue macho, RUSHWA ni adui mkubwa sana na ndiye anaetumaliza huko barabarani sio hao makonda. Tukifanikiwa kupunguza RUSHWA kama si kuimaliza basi hayo yote walosema wadau yatawezekana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...