mwanamichezo bora wa mwaka wa jumla kwa mwaka 2008 mary naali akipeana mikono na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo (taswa), boniface wambura, huku mgeni rasmi waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais (muungano) mh. muhammad seif khatib (pili shoto) na mwenyekiti wa yanga imani madega wakiwa pembeni. hii ni katika hafla ya kila mwaka ya taswa ya kutoa tuzo kwa wanamichezo bora ilofanyika usiku huu hoteli ya kilimanjaro kempinski. pamoja na kombe kubwa  na cheti mary alipokea pia kitita cha shilingi laki sita. washindi wa kila mwezi walipata kombe, cheti na laki mbili unusu kila mmoja
mabosi wa tbl walikuwapo kuhakikisha udhamini wao wa hafla hii iliyofana sana haiendi kombo. nao walifurahi kama sura zinavyoonesha.
mgeni rasmi mh. muhammad seif khatib akitoa nasaha zake. pembeni yake ni mwenyekiti wa taswa boniface wambura
mwenyekiti wa taswa boniface wambura akiongea na kadamnasi
mc wa shughuli hii hakuwa mwingine ila anko deogratius rweyunga wa itv na radio one
meza kuu
mgeni rasmi mh. muhammad seif khatibu na kamati kuu ya taswa akiwa na mshindi wa jumla mary naali na wachezaji wa yanga athumani idi chuji (shoto mbele) na juma kaseja (kulia chini) aliyemwakilisha mussa hassan mgosi ambao waliiibuka katika tatu bora.
mgeni rasmi akiwa na washidi 12 wa tuzo hizo
meneja wa uhusiano wa tbl maneno mbegu (shoto) akimtuza athumani iddi kwa kuwa mchezaji bora wa mwezi  desemba 200
 makamu wa pili wa rais wa tff ramadhani nasibu akimkabidhi tuzo mchezaji bora wa mwezi novemba 2008 mcheza tennis  chipukizi mkunde iddi
mwenyekiti wa yanga imani madeha akimkabidhi tuzo mwanamichezo bora wa mwezi oktoba 2008 mary naali ambaye pia aliibuka kuwa mshindi wa jumla baada ya kuwa mwanamichezo pekee aliyeipatia medali bondo mwaka 2008 kwa kushinda medali ya fedha katika michuano ya jumuiya ya madola huko india
mshambuliaji hatari wa yanga boniface ambani akipokea tuzo toka kwa  afande meja mbuge wa jkt
binti wa hayati grace daudi  mcheza netiboli wa jeshi stars akipokea tuzo toka kwa mwenyekiti wa baraza la michezo afande iddi kipingu kwa kuwa mwanamichezo bora wa mwezi agosti
meza kuu ikiungana na wageni waalikwa kutoa heshima ya dakika moja kumkumbuka hayati mwananetiboli  hayati grace daudi
mwanamichezo bora wa mwezi juni 2008 aliteuliwa kijana mcheza gofu hodari amani saidi ambaye alipokea tuzo toka kwa katibu mkuu wa zamani wa fat michael wambura
mshambuliaji hatari wa timu ya kagera sugar mike katende akipokea tuzo ya mwanamichezo bora wa mwezi aprili 2008 toka kwa afisa uhusiani wa nmb na makamu mwenyekiti wa chaneta mh. shyrose bhanji
dennis mallya akipokea toka kwa naibu mkurugenzi wa michezo mama yasoda kwa niaba ya mwanariadha jumanne tulway aliyekuwa mwanamichezo bora wa mwezi machi 2008
katibu mkuu wa tff frederick mwakalebela akimkabidhi tuzo mwanamichezo bora wa mwezi februari 2008 ambaye ni bingwa wa judo toka zenji masoud amour
mwanamichezo bora wa mwezi januari 2008 bondia francis miyeyusho ambaye anapokea tuzo yake toka kwa afisa uhusiano wa benki ya stanbdard chartered na miss tz 1999 hoyce temu
kiongozi wa taswa akielezea namna washindi wa tuzo walivyopatikana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hapa nilimpo nimechanganyikiwa hivi hizi zawadi ni za 2008 au 2009

    ReplyDelete
  2. Braza Michuzi,hv huyo Ramadhan Nassib si alipaswa aachie ngazi baada ya timu yake ya Villa Squad kushuka daraja?Au Tenga na wenzie wameamua kuleta ushkaji?

    ReplyDelete
  3. wewe mchangiaji wa pili umeona wapi hiyo kanuni yako kuwa nassib anapaswa kuachia ngazi kwa vile timu yake imeshuka daraja?

    ReplyDelete
  4. UBAGUZI WA KIJINSIA-TANZANIA SPORTSMAN OF THE YEAR AWARDS...WANAWAKE JE?

    ReplyDelete
  5. Jamani huu ni uvaaji gani kwenda kwenye award? hamuoni zile award za FIFA wachezaji wanavaaje siku wakiitwa kupokea award zao? TUBADILIKE, hapo palikuwa ni dhifa na kuna mavazi ya Dhifa bwana

    ReplyDelete
  6. KWANI HIZI NI TUZO ZA WANAUME PEKE YAO?

    KWA NINI JINA LISINGEKUWA "SPORTSPERSON OF THE YEAR" BADALA YA "SPORTSMAN OF THE YEAR"??!!!

    WANAWEZAJE KUMPA MWANAMICHEZO MARY NAALI TUZO INAYOSEMA SPORSTMAN OF THE YEAR 2009??

    ReplyDelete
  7. big up masoud amour wa zenji!!!

    ReplyDelete
  8. We mbogela unazingua tu, ushasema award za FIFA, hizi ni award za TASWA. Unaiga kila kitu, yatakushinda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...