ALI KIBA AKILAKIWA NA MC JUDY MARA BAADA YA KUTUA NAPOLI
ALI KIBA AKIJIDAI NA FULANAZZZ YA SEE WEAR
ALI KIBA AKIWA NA PROMOTER RICKY J.G BONDO 
ALI KIBA AKIWA NA MSANII MPYA WA KIZAZI KIPYA BONGO FLAVA ANAEISHI ITALY MAVUMBI, AMBAYE KATIKA SHOW ALITOKA NA SINGLE YAKE "UHAKIKA" feat:SARA SEE ,SINGLE YA MAVUMBI ITASIKIKA HIVI KARIBU KATIKA REDIO STATION HUKO NYUMBANI NA EUROPE. 
CEO WA SEE WEAR ,ALI KIBA,SARA SEE,MAVUMBI NA LADY JUDY KATIKA PICHA YA PAMOJA MARA BAADA YA KUWASILI NAPOLI JANA 
MAUA KWA ALI KIBA
WADAU KIBAO WA NAPOLI WALIJITOKEZA KUMLAKI ALI KIBA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. I like this, flowers for our artist! Sio mnapiga mapicha tuu, you have to show them some love and embrace the fact they are superstars!

    ReplyDelete
  2. EEee bwana huyu " MAVUMBI" ana uhusiano na sheikh Mkuu wa mkoa wa Tabora "Sheikh Mavumbi" wa pale mabatini karibia na Tambukareli.

    Big up kama ndiye maana si lazima mtu urithi kazi ya baba/babu yako.

    ReplyDelete
  3. İNATİA MOYO , KEEP İT UP ALİ KİBA

    ReplyDelete
  4. Mmmh mwaka wako ali kiba.

    ReplyDelete
  5. UGHAIBUNI KOTE TUNAKUFAGILIA ALI KIBA MWENYE WIVU AJINYONGE TU

    ReplyDelete
  6. picha ya juu kabisa, wote wameziba macho na mikofia wanaonana kweli?

    ReplyDelete
  7. USHAURI WA BURE KWA ALI KIBA NA WASANII WENYE KUPATA KIPATO CHA KUELEWEKA, NENDENI SHULE HUKU MNAFANYA MUZIKI WENU, KWANI KAZI YENU NI NGUMU SANA NA PESA MNAZOPATA HAZITOSHI KUSTAAFU WAKATI MNA UMRI HUU MDOGO. IGENI MFANO WA MWANAfa, MIKE-T, C-PWAA, NK....MSILEWE NA SIFA, WANAWAKE NA STAREHE ZA MUDA MFUPI, NADHANI MIFANO HAI MMEIONA KWA BAADHI YA WASANII WENZENU KAMA MR NICE NK, KUPOROMOKA NI RAHISI SANA KAMA HUNA KIZINGITI CHA ELIMU AU MALIGHAFI ZA KUWEKEZA.

    NI HAYO TU.

    ReplyDelete
  8. RUDI NYUMBANI INATOSHA, SOMA KAMA ULIVYOAMBIWA NHAPO JUU. MTOTO HUSHOKI KUPAYUKA.

    ReplyDelete
  9. wadau kibao? nimehisabu na numba niliyopata siamini inakubalika kama ni kibao

    ReplyDelete
  10. Ali K, unazidi Kuwa HOT, Come back to Washington,Dc.NAKSHI NAKSHI,NICHUM BASI.I Love your Music.Hongera.

    ReplyDelete
  11. Mimi napenda kuuliza machache tu hapa kuhusu huyu ali kiba na bongo flava yake. Hivi yeye anapiga chombo gani vile??? na hii miziki ya bongo flava mbona wanafani hiyo(siwaiti wanamuziki maana najua hawajui hata kupiga chombo kimmoja) mbona nyimbo za zinafanana fanana?? au ndo wanaprove kuwa bongo kila mtu mwanamuziki.....hata kama hajui kuimba au apigi ala yoyote?? jamani kama alivyosema mdau hapo chini nendeni shule.

    ReplyDelete
  12. KAMA WEWE UMEAMUA KWENDA SHULE NENDAAAA,MUACHENI MTOTO WA WATU, KACHAGUA KAZI YAKE KUWA MWIMBAJI MUACHENI, NDO ANAPOPATA RIZIKI YAKE KAMA AMBAVYO WEWE"ULIYESOMA" UNAVYOTUMIA ELIMU YAKO, SHULE SIO YA KILA MTU,WANGAPI MAMILIONEA AU WANA MAISHA MAZURI NA HAWAJUI HATA KUANDIKA, LEAVE HIM ALONE, HATERS!!

    ReplyDelete
  13. Jamani mnaambiwa kupanga ni kuchagua.

    Elimu haipatikani bure. Kwa hiyo mwenzetu kachagua apige myuziki kwanza ... labda akizichanga kiasi fulani ndio anaweza kufanya mambo mengine ikiwemo kutafuta elimu atakayoona inamfaa.

    Wabongo tusikariri kwamba muziki sio dili. Kuna watu wakiona mtu kawa msanii wanaona kapoteea, halafu wao wakiwa wanapiga buku ndio wanajiona wamepatiiiia.

    Maisha hayana formula bwana.

    ReplyDelete
  14. ivi italy kuna JUA KALI ivo picha #3

    kiba umetalii,umesafisha jicho!!safi sana for being sooo exposed to tht world!!

    promoterz safi sana kuwakumbuka watoto wa bongoland-home kwakweli kuliwaza watu uko kwenye box za kufa mtu

    kisamvu,nyanya chungu,tembele lipo?

    ReplyDelete
  15. teheteheteheee, mudogo wangu ari kiba kipu iti apu. ila nakupa ushauri wa bure kamna kaka ako, ebooo. hiyo mihela unayopata kwenye shoo zako hebu nunua begi jingine, wee vipi, sio unakuja uraya na begi ra shule, ebooo, henoheeno, wazimu kitu gani.
    the living legend.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...