bosi wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba 
akitangaza msaada wa kompyuta mashuleni

KAMPUNI ya simu za mkononi kupitia mfuko wa msaada Vodacom Foundation imezindua awamu ya pili ya msaada wa kompyuta katika shule za sekondari vijijini.

Msaada umedhaminiwa na Vodafone na Vodacom Foundation na zaidi ya kompyuta 60 zitatolewa kwa shule sita nchini.

Mkuu wa Vodacom Foundation, Bi Mwamvita Makamba amesema kwamba nia ya kutoa msaada huo ni kuziba pengo lilipo katika tecknolojia ya habari na mawasiliano kati ya shule za mijini na vijijini.

“Awamu ya pili ya mpango huu itagharimu 48m/- (pauni za uingereza 25,000) na mikoa ambayo itafaidika ni pamoja na Tanga, Mara na Visiwa vya Unguja na Pemba”, amesema.

Shule za sekondari ambazo zitapatiwa msaada ni pamoja na Utaani (Pemba), Hamamdi (Unguja), Soni na Korogwe (Tanga) na Serengeti na Musoma mkoani Mara.

Kwa mujibu wa Bi Makamba, Vodafone and Vodacom Foundation ilizindua mpango wa kutoa msaada kwenye shule za sekondari baada ya masomo ya kompyuta kuingizwa kwenye mtaala wa elimu ya sekondari.

Amesema kuwa baada ya kuanzishwa masomo ya kompyuta shule nyingi za vijijini hazipati vifaa hivyo kama ambavyo zinavyopata shule za mijini.

“Kutokuwepo kwa uwiano baina ya shule za mijini na vijijini kunaweza kusababisha madhara baadae kwa wanafunzi watakaoendelea na masomo ya juu kutoka vijijini na tunajaribu kusaidia kuepusha hilo”, amesema.

Mpango huu ni sehemu ya msaada wa Vodafone Group Foundation kwa nchi za Afrika na katika awamu ya kwanza kmpyuta 184 zilitolewa kama msaada kwa shule nane katika mikoa minne.

Vodacom Foundation inashirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika kutambua shule ambazo zinastahili kupata mnsaada wa kompyuta kwenye maeneo mbalimbali ya nchi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. bi makamba kumbuka na kioa mingine nje ya tanga please... vodacom inatumiwa na wananchi mikoa yote ya ta

    ReplyDelete
  2. michuzi, nadahni ms. makamba anatumia nafasi yake vibaya kwani misaada mingi ya vodacom foundation anaipeleka pwani hususan tanga. akumbuke kwamba mtandao wa vodacom unatumiwa na wananchi mikoa yote ya tz. aache siasa awe proffessional

    ReplyDelete
  3. Bi Makamba samahani, eti wewe umesha olewa, una mchumba au vipi?

    ReplyDelete
  4. PENDELEA TANGA BWANA, WAACHE WASEME.Pele vitu vizuri kwetu.

    ReplyDelete
  5. Mwamvita is kinda hottt!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. anony 2:44 pm unayeuliza kama kaolewa usiguse hapo kama mshua wake umbeyana maneno kibao wakati ni mwanamme itakuwaje huyo binti yake?

    ReplyDelete
  7. binti KAOLEWA NA ANA MTOTO MZURIII (rangi-rangi)

    dada umependeza sana,umewiva na kazi yako unaijua,unatuhamasisha kuwa watoto wa kike wanaweza na wako juuuuuuu!!

    kip the gd work babe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...