

bosi wa masoko wa tbl david minja (pili kulia) akiwa na meneja wa kilaji cha kilimanjaro lager oscar shelukindo (pili shoto) na wadau katika maandalizi ya kili music awards wikiendi iliyopita

pamoja na kuwa mwanamuziki mkongwe na kilimanjaro band wana njenje, keppy kyombile pia ni fundi mitambo mahiri wa sauti katika matamasha mbalimbali, akiwa mtaalamu wa makonso ya aina zote. aghalabu humkosi kwenye matamasha toka ya ziff na sauti za busara kule zenj na yote yafanyikayo dar.

mabingwa wa kushuti video na tv wa 2eyez production wakiwa na vyombo vya kisasa vya kwao na vya digital art productions huwa makini na kazi zao

majukwaa hupambwa kwa ustadi na huvutia pia kwa mapambo na taa za kisasa

kila kitu kinatengenezwa hapahapa bongo

muziki wa nguvuna vikorombwezo kibao vya kisasa vipo bongokwa shoo ya aina yoyote ile. huu mzigo ambao uko full nondo ni wa prime time promotions ambayo pamoja na sauti pia wana jukwaa ka kisasa linaloweza kutumika hata na wacko jacko

juu na chini ni ukumbi wa diamond jubilee hall kabla ya hafla ya kili music awards

Bongo kweli tambarare lakini BILA UMEME TUTAFIKA KWELI?????
ReplyDeletemtoamaoni wa kwanza huna jema??bongo tambarareeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteJUST ONE WORD-"FANTASTIC". ILA NA BARABARA NAZO NA MITAA IWE KAMA HIVI, LOL.
ReplyDeletena parking ziwe hivi hivi
ReplyDeletesecurity
valet parking
na sura za tabasamu kwa wahudumu wanaokaribisha watu
kuna watu wabeba mabox ulaya na marekani wanaboa, kila kitu cha bongo wanaponda. wanatia kinyaa, nyumbani ni nyumbani, hta ikiwa unakaa chini ya mti. East or West, home is best
ReplyDeleteTusikasirike inatakiwa miundo mbinu kwanza na sio vinginevyo!
ReplyDeleteBONGO TAMBARARE TOKA ZAMANI . YATEGEMEA POSITION YAKO KIMAISHA KWA WAKATI HUSIKA .
ReplyDeleteduh! video mixer kwenye sherehe ahaaaa kumbe ndiyo maana video za kibongo ni vichekesho...!
ReplyDeleteSHELUKINDO UPO HABARI YA MIAKA MINGI?NAONA UPO TBL KWA MBELE,TULIKUWA WOTE AGUMBA COMPUTER MIAKA YA 200-2001.PALE JENGO LA USHIRIKA,TUPE NAMBA YAKO BASI TUKUSALIMIE RAFIKI.UKEREWE
ReplyDeleteWe anonymous wa 11.06 a.m unayetaka namba ya Shelukindo, si umeshaambiwa ni yeye ni meneja wa Kilimanjaro Lager hapo TBL? Basi piga simu TBL umwulizie utampata ! Sio lazima aweke namba yake kwenye hii blog ya jamii !
ReplyDelete