FLAVA NITE ni usiku unaoletwa na madj wa ukweli toka katika familia moja wakiongozwa na dj BONILUV, Dj VENTURE na Dj MACKAY.
Wapenda burudani wamekuwa wakiimiss hii kitu toka La Taverna kuwa kwishnei na wenyewe wanasema ukifika BULLDOGS (masaki) meter kama 500 hivi kutokea international school ya masaki ni lazima ukubali.
ANGALIZO: DJ Bonny Luv aliyetangazwa kuwa atakwenda Marekani karibuni kwa ajili ya shoo kadhaa amesema yeye bado yupo Bongo na hana mpango wa kusafiri kwenda kokote hivi karibuni. Kwa mdomo mwingine BONNY LUV atakuwepo BULL DOGS kila Jumamosi kama kawa..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. jamani mbona nyinyi mpromota wa marekani mnatuyayusha mara ooh bon luv atakuwa EASTER PARTY DALLAS TX, mara ooh nah they didnt U 1& JT PRODUCTION TUNAMLETA WICHITA KS,SASA TUELEWE VIPI? MBONA ANASEMA HANA MPANGO NA USA? MDAU YOYOTE MSAADA ASANTENI!

    ReplyDelete
  2. Jamani Hiyo bulldogs haina kibao??? nimeitafuta mara kadha wa kadha mchana na usiku nimeshindwa kuitrace, msaada jamani,au kibao chake ni kidogo sana???? ahsanteni

    ReplyDelete
  3. kama DJ bon lov haji na sisi HATUJI KWENYE PARTY nyinyi mapromota inadidi muanze sasa kusema ukweli,na tiketi za ndege tulishaka.

    ReplyDelete
  4. Inaonekana huyu promota wa Marekani hana mpango. Je Bon luv atakuwa EASTER PARTY DALLAS TX? Au atakuwa BULL DOGS? Mbona amesema hana mpango wa kusafiri kwenda kokote??? Mapromota tuambieni ukweli.

    ReplyDelete
  5. NA DJ VENCHA MBONA HAPIGI!AU YEYE NI BONGO FLAVA TU

    ReplyDelete
  6. Mdau hapo juu, ukiwa international school masaki, unafata hiyo barabara ya haile sellasie road moja kwa moja mpaka unafika pale kuna george the dragon, unakata mkono wa kushoto unanyoosha moja kwa moja mpaka utaona kibao kikubwa cha savanna dry, kinaonyesha bulldogs iko mkono wa kulia ->->umefika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...