Mbunge wa Jimbo la Karatu ( CHADEMA) Dk Wilbrod Slaa, akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Mbunge wa zamanai wa Jimbi la Biramulo Magharibi, Phares Kabutee wa TLP leo katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro
Baadhi ya viongozi wa Chama cha TLP Mkoa wa Morogoro wakiwa nje ya ukumbi wa Manispaa ya Morogoro kabla ya mwili wa Mbunge wao wa zamani wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Phares Kabuye kusafirishwa kwanda Dar na na kisha kusafirishwa kwenda Bukoba kwa mazishi
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta, ( kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Karatu, Dk Wilbrod Slaa (Chadema) na Hamad Rashid Mohamed, mbunge wa CUF na Kiongozi wa Upinzani Bungeni mara baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Bunge wa zamani wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Phares Kabuye wa TLP leo katika ukumbi wa Manispaa ya Morogoro
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sittaa ( watatu kutoka kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu ( wakanza kulia) kuhusiana na utaratibu wa kusafirisha mwili wa Marehemu Mbunge wa zamani wa Jimbo la Bijaramulo Magharibi (TLP) , Phares Kabuye, leo kabla ya kusafirishwa kuelekea Dar es Salaam tayari kupelekwa Bukoba kwa mazishi. Picha na mdau John Nditi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mungu ailaze roho ya marehemu Kabuye mahali pema peponi. Amin

    Huwa naumia sana nionapo watu wanakufa kwa sababu ya uzembe wa madereva. Inauma zaidi pale ninapona polisi wanashindwa kusimamia sheria za barabarani ipasavyo na badala yake wamekuwa wanasiasa badala ya kuwa watendaji. Hii inanitisha sana tena sana. sijui lini watu watatimiza wajibu wao????

    ReplyDelete
  2. May God rest the souls of the dead in peace!

    ReplyDelete
  3. Kwa sisi wana habari ambao tuliandika habari za Bunge miaka ya 1990-1993 wakati huo likifanyika Karimjee Mzee Kabuye alikuwa faraja yetu sana na mara nyingi alitununulia chai, huku akitufanyia mawasiliano na wabunge wengine ambao tulihitaji kuwahoji. Pumzika kwa amnani mzee wetu Phares

    ReplyDelete
  4. Mzee wa watu hakuwa na makuu ila alikuwa na machungu na nchi yake. Wakamuundia visa hata akawa anataka kuporwa ubunge. alipata ubunge si kwa kuhonga kwani hata angetaka kuhonga hakuwa na vijisenti vya kuhonga. Alipata ubunge kwa sifa zake za kuwapenda watu wake na nchi yake. haijatosha wamemuundia visa, visa vya kubuni tu. Pasi na visa na roho mbaya na husda waliyonayo wasiopenda maendeleo wiki hii angekuwa dodoma akihudhuria kikao cha bunge. Kumbe basi asingepanda basi ambalo urefu wa safari yake ya kutoka biharamulo usingemfanya dereva achoke na ampe kondakta (habari zinasema hivyo)aliyesababisha ajali ile. angewahi dar kutetea kiti chake cha umakamu mwenyekiti wa TLP. Pengine wamefurahi sasa maana jimbo litakuwa wazi rasmi. Yana mwisho haya.

    RIP mzee Phares Kabuye.

    ReplyDelete
  5. pole nyingi sana kwa rafiki yangu na mtumishi(familia)na Mungu akutie nguvu sana sana ktk wakat huu mgumu unaopitia,jikazi mtoto wa kiume!!

    ila jaman hizi ajali??uzembe gani huu?? ukipanda ndege vimeo! ukipanda mabasi speed ya kuua watu!!sijui tufanyeje

    Bwana ametoa Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe.

    mie

    ReplyDelete
  6. SIJAELEWA!!
    ni mbunge adi sasa umauti ulipomkuta au alikua mbunge uko nyuma??

    alikua anaenda bungeni dodoma na basi kweli???

    pliz nisaidieni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...