DAVID MATTAKA

MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA (ATC) DAVID MATTAKA AMEKANUSHA UVUMI ULIOTAPAKAA JIJINI DAR LEO KWAMBA AMEJIUZULU WADHIFA WAKE HUO.

AMESEMA  SASA HIVI KWA NJIA YA SIMU KWAMBA YEYE BADO NI MFANYAKAZI WA ATC  KAMA MKURUGENZI WAKE NA HAKUWA AMEJIUZULU NA WALA WAO HANA. ALIKUWA AKIHOJIWA NA REDIO ONE KATIKA KIPINDI MAALUMU CHA HABARI ZA KUVUNJIKA.

MATTAKA AMESEMA HUENDA UVUMI HUO UMEKUJA KUFUATIA KUTEULIWA KWAKE KATIKA KIKOSI KAZI (TASK FORCE) ILIYOUNDWA KARIBUNI NA SERIKALI KULIANGALIA NA KULIUNDA UPYA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA NA KUKAMILISHA KAZI HIYO KATIKA KIPINDI CHA MIEZI SITA.

AMESEMA KWA KUWA WANAOUNDA KIKOSI KAZI HICHO WATATAKIWA WAFANYE KAZI HIYO KWA MUDA WOTE (FULL TIME BASIS), NA KWAMBA ALIONGEA NA MENEJIMENTI YA ATC KWAMBA KAZI ITAPOANZA ITABIDI MMOJA WA VIONGOZI WA SHIRIKA HILO  AKAIMU NAFASI HIYO HADI KAZI HIYO ITAPOKAMILIKA.

MATTAKA KASEMA KWA VILE KAZI YA KIKOSI KAZI BADO HAIJAANZA BASI YEYE BADO NI MKURUGENZI MKUU WA ATC, KINYUME NA UVUMI ULIOENEA KUELEZA VINGINEVYO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jamaani hivi wenye kujua kiswahili fasaha habari zilizovunjika ni sahihi ? au? mi naona si sawa hapo wangetumia neno katisha habari au habari zilizokatishwa si habari zilizovunjika naomba Misupu uiweke hii hewani ili wadau waijadili

    -Mdau

    ReplyDelete
  2. Hivi kaka yangu unado twit? kama hufanyi basi fungua one...This is the next big thing now....na wewe ulivyo na magnet ukifungua utapata washabiki wengi sana......I love it.....hata Obama anatwit...hahaha seriously masenator na congress people wengi tu wanafanya hii .....go to www.twitter.com.... I hope to find you there

    ReplyDelete
  3. Misupu, naomba uweke hii habari watu waijadili, wasome hiyo habari hapo chini toka gazeti la rai halafu watoe maoni kwa vile sidhani kama yaliyosemwa hapa ni sahihi TRLinapewa mzigo ambao si wake! kama kuna watu wamekufa kampuni kama hizi hulipa fidia tu kwa kutumia bima.
    sasa swala la wao kuwa waokoaji linakuja vipi? hivi tumesahau ya kuwa haya majukumu yanapaswa kuwa ya vikosi vya uokoaji jamani? nani asiyejua jinsi watanzania wanayzopenda kulalamika haswa wafanyakazi wa Railway ili hali wana-subotage kampuni nani asiyejua katika treni hizi controllers hutia hela mifukoni yaani hukusanya nauli halafu hawatoi risiti na huwa mstari wa mbele kutaka nyongeza ya mishahara, nani asiyejua wafanyakazi hawa huiba kuanzia mafuta hadi mataruma ya reli! Jamani tukitaka kuendelea tujue kuna kufunga mikanda pia hamna cha dezo dunia hii hii kuwa na malalamiko mengi juu ya menejimenti sidhani kama kila kitu ni sawa ukiacha matatizo madogo madogo kama kupeleka engine India lakini kuna hisia kuwa wafanyakazi wa Railways hawakutaka muwekezaji kwa vile walijua ataziba mianya ya ufisadi wao! Hii Tanzania yetu sasa fisadi kuanzia juu mpk chini!
    Hebu tujiulize ni mfanyabishara(muwekezaji) gani leo hii katika dunia hii ya capitalism yuko tayari ku-invest katika franchise hambayo haina retuns? tuache midomo mimgimimgi! wmacontroler wanaihujumu kampuni huku wakilalamika ndo maana makusanyo hayajitoshelezi kuendesha kampuni naomba zile sheria kali juu ya wahujumu uchumi zirudishwe jamani maana taifa linaelekea kubaya ufisadi kila mahali!

    Na Mwandishi Wetu

    Kampuni ya Reli Nchini, ambayo hapo zamani kabla ya kuondolewa mikononi mwa serikali ilikuwa moja ya mashirika yaliyojijengea heshima kubwa miongoni mwa Watanzania, ikisafirisha mamilioni ya watu na mamilioni ya tani za mizigo kila mwaka, sasa inachungulia kaburi.

    Kabla ya kuuzwa na kugeuzwa jina, TRC ni shirika lililokuwa likimilikiwa kwa asilimia 100 na serikali na linamiliki mali ambazo awali zilipata kuwa sehemu ya Shirika la Reli la Afrika Mashariki (EARC), likitoa huduma Kenya, Uganda na Tanganyika na huduma za usafiri wa treni nchini kwa sasa zinatolewa pia na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

    Miundombinu ya reli ya TRC kutoka mashariki hadi magharibi mwa nchi iliwekwa enzi za utawala wa wakoloni wa Kijerumani wakati Reli ya Kati inatoka Dar es Salaam hadi Kigoma na kuna nyingine kutoka Tanga hadi Arusha. Ya kaskazini – kusini inatoka Korogwe hadi Morogoro ikiunganisha zile nyingine. Njia kuu ya reli ina matawi zaidi, moja likielekea Ziwa Victoria huku ile ya kutoka Tanga ikiunganisha na maeneo ya kaskazini mwa Kenya, japo kwa muda imekuwa haifanyi kazi.

    Unganisho jingine la njia mbili hizo lipo Kidatu, ambapo reli ya TAZARA inakutana na tawi hilo.

    Mauzo ya Shirika hilo, yalifanywa mwaka 2007 na ndipo kampuni ya Rites ilipofanikiwa kupata mkataba huo kutoka Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC). Mkataba wenyewe ulisainiwa Septemba 3 mwaka huo huo ukitakiwa kuanza Oktoba mosi, 2007.

    Kifo cha kampuni hiyo, kimetokea vibaya na kuvunja misingi yote ya thamani ya Mtanzania iliyowekwa tangu kuasisiwa kwa taifa hili. Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, baada ya treni ya kampuni hiyo kupata ajali Jumapili hii, wamiliki wa kampuni wamesikika wakiombolezea mabehewa yake, bila hata kujali kuuliza idadi ya abiria waliofariki au kupata majeraha katika ajali hiyo.

    Ujinga huo ambao Mwalimu Nyerere aliuita unyama wa kibepari, ulimhudhi hata waziri mwenye dhamana ya usafiri na usafirishaji nchini, Waziri Dk. Shukuru Kawambwa, aliyesikika kwa hasira akisema: “nyie Wahindi mnawadharau Watanzania hata kwenye tukio hili mnafika mmechelewa.”

    Hawakuchelewa tu, bali pia walileta mtaalam wa kuangalia kiwango cha uharibifu wa mabehewa siyo kiwango cha majeraha waliyopata abiria wake.

    Kwa maneno yake mwenyewe, Kawambwa alisema: "Ninyi (TRL) ni wazembe sana na wapuuzi... mnajali maslahi yenu kuliko maisha ya binadamu. Haiwezekani mumtume injinia kuja kuangalia usalama wa treni badala ya kuangalia namna ya kuokoa maisha ya abiria wanaokufa baada ya kubanwa kwenye behewa," alisema Dk. Kawambwa ambaye naye pia ni mhandisi.

    Huu ni mfululizo wa matukio yasiyo ya kuridhisha kwenye kampuni hiyo tangu kuingiwa mkataba wa uendeshaji 2007; kuanzia mkataba mbovu, kushindwa kuwekeza vilivyo, wafanyakazi kutojua hatima yao, TRL kutaka kung’oa kipande cha reli na kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi.

    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipata kueleza kushitushwa na aina ya mkataba ulioingiwa kati ya Serikali na wawekezaji wa kampuni ambayo sasa inaonekana kutojali utu wa wateja na wadau kwa ujumla.

    Menejimenti ya TRL mwanzoni mwa wiki ilimchefua Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa pamoja na wananchi wengine, kutokana na uamuzi wa kumtuma mhandisi kwenye eneo la tukio ya ajali ya Machi 29 mwaka huu mkoani Dodoma kuangalia usalama wa treni badala ya kutuma watu kuokoa abiria na kuangalia jinsi ya kuondoa maiti kwenye mabehewa.

    Baada ya mfululizo wa malalamiko kutoka kwa wafanyakazi, wateja na hata maofisa wa Serikali ya Tanzania kuhusu mfumo wa uendeshaji wa wawekezaji hao – Rites Ltd, sasa inaelekea kuna mkato wa tamaa kutokana na ajali ya treni iliyoua watu saba, kujeruhi kadhaa na kuharibu mali, huku viongozi wa TRL wakionekana kutoshitushwa wala kutojituma haraka eneo la tukio kufanya kazi ya uokoaji.

    Maofisa wa TRL walichelewa kufika hivyo kwamba Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alifika saa mbili kabla yao, wakati wao ndio walitakiwa kufika mapema kuokoa. Hisia zilizojengeka, na zinazoelekea kuaminika sasa ni kwamba wawekezaji hao wa TRL wanawadharau Watanzania na ikiwa hivyo ndivyo, hakuna haja ya kuendelea na mkataba wao.

    Ajali hii mwaka huu, imetokea kwa treni ya abiria kugongana na ya mizigo kati ya Igandu na Gulwe mkoani Dodoma, umbali unaokadiriwa kuwa wa kilomita 11 kutoka eneo ambalo mamia ya watu walipoteza maisha yao katika ajali ya mwaka 2002.

    Kazi ya kutoa miili ya abiria waliofariki dunia kwenye ajali hiyo ya treni iliyokuwa inatoka Dar es Salaam kwenda Kanda ya Ziwa, ilionekana kuwa ngumu, ikabidi mashine zitumike kukata mabehewa.

    Majeruhi walipelekwa katika Hospitali ya Mpwapwa kwa matibabu, watatu kati yao walipatiwa matibabu na kuruhusiwa na wengine walikuwa wakiendelea na matibabu. Waziri Kawambwa alisema ugumu wa kazi hiyo unatokana na vifaa duni vilivyotumika kukatia vyumba vya mabehewa. Kampuni kubwa kama hii, kutokuwa na vifaa vya maana maana yake ni nini?

    Serikali ya Tanzania iliingia mkataba wa miaka 25 na Rites Ltd, ambapo imechukua asilimia 49 ya hisa za TRL na Rites asilimia 51 kwa ajili ya kuendesha reli yenye urefu wa kilometa 2,700 iliyorithiwa kutoka kwa wakoloni.

    Tayari imeundwa kampuni mama – Reli Assets Holding Company (RAHCO) kusimamia utekelezaji wa mkataba huo na kufanya tathmini ya utendaji, ikiwa ni pamoja na kusimaia uwekezaji katika miundombinu ya reli, huku Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Ardhini na Majini (SUMATRA) ikitakiwa kuratibu mambo.

    Itakumbukwa jinsi mkataba huo uliosainiwa na Mkurugenzi wa TRL, Sudhir Kumar na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya RAHCO, Agnes Bukuku na baadaye kuzua malalamiko kutoka kwa wafanyakazi ambao hawakuwa wameambiwa hatima yao ingekuwaje. Walizuia uzinduzi wa safari za treni jijini Dar es Salaam.

    Mbali na ubovu wa mkataba husika, mwekezaji kushindwa kutoa fedha walau za mishahara kwa wafanyakazi mara kadhaa, TRL ilifikia mahali pa kuamua kung’oa kipande cha reli ambacho ni mali ya walipa kodi wa Tanzania, lakini wakazuiwa na kupewa karipio kali na Rais Jakaya Kikwete, aliyesema wawekezaji hao waelewe kuwa ni wanahisa tu katika kuendesha usafiri na kuwekeza, wala si kunyofoa miundombinu.

    Zipo tetesi za kuletwa mabehewa mabovu kutoka India na nyingine zikidai kuna vifaa vilikuwa vihamishiwe India pasipo Serikali ya Tanzania kujua. Picha za mabehewa yaliyohusika katika ajali ya Jumapili, zinatia shaka kama mabehewa hayo ni imara au ubabaishaji mtupu.

    Wachunguzi wengi wa mambo ya biashara, wanapendekeza kuwa hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuendelea kuwavumilia wawekezaji wa aina hii ambao hata Waziri Mkuu Pinda ameshasema uwekezaji wao ni mbovu, upitiwe upya na Serikali na yenyewe iendeshe shirika hilo kubwa kama zinavyofanya nchi nyingine tajiri na masikini. Hiyo ni kutokana na unyeti wa usafiri huo na pia usalama wa nchi na watu wake.

    Pamoja na ubovu wa miundombinu ya reli, ilitarajiwa kwamba kuingia kwa Rites nchini kungesaidia kukwamua hali hiyo kwa kukarabati maeneo yote mabovu, kuongeza vichwa vya treni na kuleta mabehewa mapya, hivyo kwamba safari za bara zingeongezeka, ikizingatiwa kwamba ndio usafiri unaotumiwa na watu wa kipato cha chini walio wengi nchini.

    Mbali ya idadi kubwa ya wasafiri wanaotegemea usafiri huo, reli ni nguzo muhimu ya maendeleo ya nchi yoyote duniani na hasa kwa usafirishaji wa mazao ya biashara. Tangu tupate uhuru, reli ndiyo ilikuwa msafirishaji mkuu wa mazao kama pamba, kahawa na katani kutoka mikoa ya ziwa kwenda pwani kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi.

    Lakini kwa bahati mbaya, usafirishaji wa mizigo hiyo unapita katika kipindi kigumu kutokana na kutoaminika tena kwa usafiri wa treni.

    Hata wasafiri wanaojikuna na kupata nauli wamekuwa wakiishia kulala kwenye vituo vya treni, maana hata baada ya kuingia Rites na Shirika la Reli Tanzania (TRC) kubadilishwa jina na kuwa TRL, hali imebakia hiyo na wakati mwingine kuwa mbaya zaidi. Hali hii ikiendelea kwa miaka 25 ya mkataba wa uendeshaji wa TRL, wadau wengine wa usafiri huo wataona kwamba serikali waliyoichangua haiwatendei haki.

    Mazungumzo ya kuwapatia Rites mkataba huo yalikuwa yakifanyika enzi Basil Mramba akiwa Waziri wa Miundombinu, na alinukuliwa akisema kwamba mazungumzo yalichukua muda mrefu kwa sababu Rites walikuwa wakisubiri kupata idhinisho kutoka Serikali ya India inayomiliki Rites kwa asilimia 100.

    Rites inasemwa kuwa na miradi mbalimbali 35 katika nchi 13, hasa katika sekta ya usafirishaji wakati TRC ndilo lilikuwa shirika kubwa zaidi katika usafiri wa reli, kwa safari za ndani na nje ya nchi, ikiwa ni treni za watu na mizigo pia kwenda nchi jirani kama Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Waziri Mkuu Pinda, alionyesha wasiwasi wake juu ya kuwapo udanganyifu katika mkataba wa ukodishaji wa TRC Rites alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa TRL, kuhusu Serikali kuingilia kati mgogoro katika kampuni hiyo na kuikopesha Sh bilioni 3.6 ili iweze kuwalipa mishahara ambayo wafanyakazi walikuwa wakiidai.

    Pinda alisema licha ya kuwapo taarifa zinazotofautiana kuhusu mali ya kampuni hiyo, hali halisi inatia shaka iwapo mwekezaji huyo ana uwezo wa kuiendesha kwa ufanisi uliotarajiwa. Alisema tangu TRC ikabidhiwe kwa wawekezaji, ilionekana kwamba walishindwa kufanya kazi hiyo ipasavyo na matokeo yake malalamiko kuwa mengi.

    “Hapa kama kuna udanyanyifu… nimekuwa nikijiuliza nani kamdanganya nani? Ingawa TRL ina mambo ya kulaumiwa, lakini na sisi tumewadanganya. TRC ilisema imeacha vichwa 92, lakini wakati wa kukabidhiwa kulikuwapo vichwa 55,” alinukuliwa Pinda akisema. TRL imekodi injini 15 kutoka India zinazodaiwa kugharimu Sh 600,000 kila siku kwa kila injini, hata kama zisipofanya kazi.

    Ama kweli Journalism in Tanzania inaenda kubaya mbali na uchochezi, it lacks content analysis sijui editor yuko wapi kwenye gazeti hili

    ReplyDelete
  4. Mambo ya Task Force ya nini si basi aende huko ili atoe nafasi kwa mtu anayeweza ongoza ATC vizuri?

    ReplyDelete
  5. Yaani ATCL iko mahututi halafu anachukuliwa CEO wake akasaidie kuifufua NIC iliyoko ICU?? Mimi nafikiri Bw. Mattaka hapa wenzako wamekupiga changa la macho, wamekusogeza pembeni kidiplomasia tu!

    ReplyDelete
  6. Am disappointed!

    ReplyDelete
  7. Tuwe wakweli, tatizo la mashirika yetu ni uongozi. Mbona sisi hatutaki kuwa wakweli kwamba viongozi wanaposhindwa kazi wakae pembeni na wenye uwezo wachukue.
    Kwani haya mashirika yanashindwa kutengeneza faida. Nimeenda kwenye jengo la ATC utafikiri ni gofu, everything is completely obsolete. Kwanini, kwanini?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...