Habari yako mdau,
nimependezwa sana na mjadala kuhusu hii DECI, kinachoniuma ni kuwa watu wenye kuaminiwa ndo hao wanawapoteza wananchi! Kama kweli hiyo DECI inafanya kazi halali na mtirirko wake ni sahihi,kwa nini wasitoe ripoti yenye kuonesha mtaji wao uko vipi na wanawezaje kuzungusha fedha za watu hata wakatoa faida ya zaidi ya asilimia 150% kwa miezi minne tu.
Ni kawaida yetu sisi waongozwa kuamini jambo hata ukweli wake ukihitaji elimu ndogo tu kuufumbua,wale maaskofu walichotakiwa kufanya ni kwenda wizarani(fedha),au kuwaona wataalamu wa uchumi wawashauri kabla hawajaanza kuwakusanya wanachi pale PTA na kuanza Kuimba nyimbo za injili.Hivi wananchi hatujui tu malengo ya hawa viongozi wetu wa dini?Yatakuwa yaleyale ya wale jamaa zangu wanaotaka kwenda Ulaya Kuhubiri Bila ya kuwa na ticket ya ndege wala Visa,ni imani gani basi hizo,au mnataka yawakute ya kibwetere ndo mseme ooh kumbe tulikwa tunapotea?
Kinachouma zaidi ni kwamba wataalamu kama kina Prof.Lipumba-mtu aliyebobea kwenye uchumi anafafanua vizuri,lakini ndo kwanza unasikia eti maelfu ya wananchi leo wamejiunga DECI.Niwakumbushe tu wananchi wenzangu hakuna maisha ya mteremko kihivyo duniani,basi watu wasingefanya kazi,ni kiasi cha kuuza kitu cha thamani ulicho nacho then unaenda kupanda DECI,baada ya miezi minne aaaah mavuno tu.Sidhani kama kuna kitu hicho duniani zaid ya vile ilivyotokea katika kizazi cha Adamu na Hawa na kile kizazi cha musa na wana wa Israel!
Ushauri wangu ni kwamba wananchi waelimishwe vizuri,na hata watafitiwe data kwa nini huo mpango wa DECI ni batili.Kwa kuanzia mimi nawarushia hii link,mdau wape watu wajionee wenyewe.
http://en.wikipedia.org/wiki/Pyramid_scheme
Nawasilisha mdau!


Sawa wajinga ndio waliwao!!! si mmekwisha twambia? na hata hivyo hapa tulipo hatuwezi kujinasua!
ReplyDeleteDECI imeanza miaka mitatu iliyopita, mbona hamkutushtua? sasa hivi baada ya Mheshimiwa Simba na Mabenki Matano yalipoungana nanyi mnaibuka kusema.
Subirini tutakapotapeliwa na kuja shtaki serikalini ndipo Mseme!!!
Waote hamna maana si DECI si ninyi. kama mnatupenda mbona hamkusema huko mwanzo?
Mbona walipoanzisha UPATU wake wa wakubwa, na hakuna hata moja iliyofanikiwa, hakukuwa na tahadhari wala baada ya watu kutapeliwa hakuna hatua zilizochukuliwa.
Hii kwa kuwa inagusa walala hoi, ndio mnaona kwa nini nao wapate mfanane?
Ninavyoelewa mimi "Hakuna mapenzi hayo ya kumuokoa Mlala hoi katika Hatari hata siku moja' toka lini?
Mnachoweza kufanya kwa nguvu zote ni pale mlala hoi anapodhulumiwa au kupoteza chake "Kutomjali wala kumfuatilia" Hivyo subirini kitokee hicho ambacho tunakitegemea, hatutoshangaa.
Mwana-DECI kwa saana tu.