Hatimaye kampuni ya Development Entrepreneurship Community Initiative (DECI) inayoendesha shughuli za upatu ambazo haziruhusiwi kisheria, imesalimu amri na kukubali kuwa imekuwa ikivunja sheria za nchi, imefahamika. Kwa mujibu wa tangazo la kampuni hiyo lililotolewa jana katika vyombo mbalimbali vya habari, Deci ilieleza sasa ndiyo inafanya jitihada za kusajili shughuli zake ziendane na sheria zilizopo. 

“Menejimenti ya Deci inapenda kutoa taarifa kwa wateja wake kuwa kampuni inachukua jitihada zote muhimu kuziweka shughuli zake kwa mujibu wa taratibu, ziendane na sheria na taratibu zilizoko,” lilieleza tangazo hilo. Tangazo hilo lilitolewa wakati Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, akisisitiza msimamo wa Serikali kuwa kampuni hiyo haina sifa za kuendesha shughuli za kibenki ambazo kisheria ilipaswa kupata kibali cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kabla ya kuanza kufanya shughuli hizo. 

Kampuni hiyo inayodaiwa kuendesha mchezo wa ‘Vuna Kutokana na Mbegu Uliyopanda’ unaofanyika katika mfumo wa Piramidi, ambao unadaiwa uliwahi kutumika kuchukua amana za watu nchini Kenya na kupotea nazo, imekuwa ikifanya kazi zake kwa kutumia mgongo wa dini bila kufafanua kwa undani shughuli zake. 

habari kamili


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. JAMANI WATANZANIA TUAMKIA,VITU KAMA HIVI TUNAVITOLEA MENO NA KUONA NI VYA MZAHA KUMBE WANANCHI WA CHINI NDIO WANALIA,VIONGOZI HUWACHUKUI MIKOPO,KAMA HITU KAMA HIKI KIMESHAWALIZA WATU KWA WATANI WA JADI INAKUWAJE WATU WANAANZISHA KITU KAMA HIKO WATU WAPO KIMYA KWANZA HAO VIONGOZI MPAKA SASA WANATAKIWA WAWE NDANI KWA KUVUNJA SHERIA KWANI UKIVUNJA SHERIA NI LAZIMA UTUMIKIE ADHABU ,ILA KWA UZEMBE WETU HAO JAMAA TUTAKUTANA NAO MITAANI KAMA KAWA,HII NI SAWA KWELI?

    ReplyDelete
  2. WIZI MTUPUUU... WAJINGA NDIO WALIWAO.... WA TZ BADO TUMERARAAAA..

    ReplyDelete
  3. Wadau labda kuna kitu cha kisheria hapa ambacho mimi sikijui. nijuavyo mimi kama mtu au kikundi cha watu wanafanya shughuli yoyote kinyume cha sheria(kwa mfano kuuza dawa baridi badala ya pombe kali), Serikali mara moja huchukua hatua ya kufunga shughuli hiyo na pengine wahusika kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Sasa kama Waziri wa fedha, BOT na CMSA wote wanatuambia kuwa DECI inafanya shughuli zake kinyume cha sheria, nini kinashindikana kwa Serikali kuwachukulia hatua DECI kwa kukiuka sheria za nchi? nakumbuka miaka ya tisini watu walishawahi kuanzisha kitu kama hiki na wakawaingiza watu mjini huku serikali ikiangalia. Baada ya watu kuwa wameshaumia ndipo wajitia kuingilia kati.Mimi nataka kuamini kuwa kuna jambo linaendelea hapa ambalo Mkulo analijua ila sisi wananchi bado hatulifahamu. Naomba yeyote anayefahamu kwanini hawa jamaa hawachukuliwi hatua atufahamishe

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  4. B KimbacheApril 11, 2009

    Nimesikitishwa kuona hawa Viongozi wa dini maaskofu wa makanisa ya Pentekoste wakitumia jina la Kanisa na heshima waliyonayo ya ukasisi kama silaha ya kujenga uaminifu na kukubalika katika jamii kwa kufanya biashara za kitapeli na haramu ambazo zinawa deceive wananchi masikini na wasiokuwa na Elimu ya biashara na utambuzi ambao ungewapa mangamuzi na kuelewa hapa wanapigwa changa la macho, wakiwa wanaelewa kabisa kwamba biashara wanayoifanya haina uhalali.

    Tumesikia kuwa kampuni hii ya Development Entrepreneurship Community Initiative (DECI) inayoendesha shughuli za upatu ambazo haziruhusiwi kisheria, imesalimu amri na kukubali kuwa imekuwa ikivunja sheria za nchi, imefahamika. Huu ni unafiki mkubwa wanajifanya sasa wamegundua kuwa wamevunja sheria za nchi, kana kwamba hawakufahamu tangu awali, wameona maji yamewafika shingoni ndio maana wanajifanya kukiri.

    Inasikitisha kuona wanazidi kuwapotosha wananchi masikini wasiokuwa na uelewa kwa kutambua “wanapigwa changa la macho” kwa kusema “Menejimenti ya Deci inapenda kutoa taarifa kwa wateja wake kuwa kampuni inachukua jitihada zote muhimu kuziweka shughuli zake kwa mujibu wa taratibu, ziendane na sheria na taratibu zilizoko,” huu ni utapeli ambao utawafanya wananchi waamini kuwa biashara hii inauwezekano mkubwa wa kuendelea kwa kufuata taratibu za kisheria, hapa hamna kitu kama hicho kwani ni biashara ambayo haitambuliki kisheria ni haramu, ni upatu , ni utapeli ni serikali gani itakayokubali kuirasimisha? Kwa hiyo wananchi na wateja wafahamu fika kuwa huu ndio mwisho wa DECI habari ndio hiyo, ujumbe umefika.

    Pia insikitishwa kuona kuwa kuna baadhi ya watu wanadhani hatua inayochukuliwa na serikali dhidi ya Deci ni wivu dhidi ya mafisadi wanaomiliki PRIDE huu ni muono finyu na kutotaka na kuwa na uvivu wa kuchambua na kufikiri, hili ni tatizo letu watanzania hatuoni mbali tunafikiria wakati uliopo bila ya kujali in a long run ni nini kinaweza kikajiri. Serikali inania ya dhati kuhakikisha hakutakuwa na madhara makubwa yanayoweza kutokea mbeleni, haya yaliyojitokeza sasa yanatosha. Tunakubali pengine Serikali imechelewa kuchukua hatua zinazostahili ili kulinda taratibu za kisheria, na kuokoa mali za wananchi wake, hata hivyo imeonyesha nia ya kuhakikisha taratibu zinafuatwa.

    Biashara hii ya mfumo wa piramidi sio ngeni imeanza zamani sana miaka ya 1800 na muasisi wake ni Little Dorrit. Watu wanaendelea kuifanya kwa kutumia majina mbalimbali miaka ya sasa mfano DECI , PONZI na kadhalika.
    Haina hii ya biashara ilikuwa inafanyika sana nchi za Ulaya na Amerika na imeshapigwa marufuku kwani ni haramu.

    "Kupanda na Kuvuna" ni biashara ya mfumo wa "Pyramide scheme" kama inavyoitwa Kiingereza Pia inaweza kuitwa "Ponzi scheme" ambayo ilisambazwa na na muhuni mmoja mu Italy, kwa jina Ponzi akiendeleza sera zile zile za muanzilishi L.Dorrit.

    Ni biashara haramu kutokana na mfumo wake ulivyo kwani sio biashara ambayo inaweza kuendelea(unsustainable)kwani inalipa marejesho kwa mpandaji kutokana na fedha zinazolipwa/zitakazolipwa na wapandaji wengine, na huyu mpandaji wa awali halipwi marejesho kutokana na faida inayopatikana kwa kufanya hii biashara, hapa inamaana hamna biashara inayofanyika kama ni faida basi ni fedha zinazolipwa na wapandaji wanaofuata.
    Kam kuna biashara inafanyika tunaomba hawa baadhi ya maaskofu wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania watuambie ni biashra gani wanafanya inayoweza kuleta faida kubwa kiasi hicho.

    Ili Mradi huu uweze kuwa mradi endelevu(sustainable) unahitaji wapandaji wapya kila siku zinavyoenda ili zipatikane fedha zinazoweza kuwalipa wapandaji wa awali kitu ambacho hakiwezekani kwani itafikia mahali hakutakuwa na wapandaji wapya na mara nyingi mradi huu unashindwa kuendelea kwani serikali ya nchi husika huwa zinaingilia kati kwani ni mradi haramu unakiuka taratibu za kifedha, kimaadili na ni utapeli uliojificha mtu wa kawaida huwezi kugundua na ndio maana wanachama wa DECI masikini wamechachamaa wakiangalia faida walizozipata haiingii akilini mwao unapowaambia huu mradi kwa siku za usoni utashindwa kuendelea kusimama hawaelewi na kuishambulia Serikali kwamba imeshindwa kuwasaidia na hivyo iwaache watu waliojitokeza kuwasaidia kwa kuwapunguzia umaskini.

    Maaskofu wa umoja wa makanisa ya Pentekoste wanavyoendelea kutetea ninashindwa kuwaelewa, watetee basi kisomi mbona hawajasema mpaka sasa wanafanya biashara gani? mbona hawajasema kama DECI ina akaunti? tumesikia tu account zimefunguliwa kwa majina binafsi, hapa inaonyesha ni kwa jinsi gani hii biashara inavyoendeshwa kienyeji, na ni ya kitapeli. Maaskofu ninavyofahamu mimi ni watu wanaokuwa na busara, hekima na uelewa wa hali ya juu, niashangaa hapa ni kwa nini wameweza kulogwa na watu wachache walioleta wazo la kufanya huu mradi kwa kutumia jina la kanisa na wao kukubaliana nao bila ya kugundua kwamba huu ni utapeli, hapa napata wasiwasi pia uwezo wao wa kuelewa mambo.

    Kwa mara ya kwanza nilisikia jina la DECI 2008 miezi ya katikati kutoka kwa mama yangu mdogo ambaye alipanda fedha alinishawishi nami niweze kupanda, kabla sijafikia uwamuzi nikawa najaribun kumdadisi ili nipate maelezo ya ziada baati mbaya akawa anashindwa kunipa maelezo ya ziada jinsi Deci wanavyoendesha shughuli zao, hivyo nikachukua uwamuzi wakutafuta mawasiliano nao, nikapata namba ya simu pamoja na anuani ya mawasiliano pepe. Cha kushangaza basi nimepiga simu kama mara kumi kwa siku tofauti tofauti hamna hata siku moja simu ilipokelewa,nikaandika email kwa kuwaeleza nimekuwa interested kujiunga na upandaji ila nina kosa maelezo ya kutosha kufahamu ni kwa jinsi gani wanaendesha shughuli zao na ni jinsi gani ninaweza kujiunga na kunufaika, email zangu zote tatu hazikujibiwa, ya nne nikawaandikia kuwakosoa jinsi wasivyoona umuhimu na kutoa kipaumbele katika swala zima la mawasiliano,hawakujibu.

    Kuanzia hapo nikaanza kuwa na muono hasi juu ya hawa jamaa, na kujiuliza ni kampuni gani makini inayoshindwa kujibu hoja na maswali ya wateja wake? nikaona hawapo organised na kuona ni matapeli tu, kingine kilichonishangaza ni huu mfumo wao wakuvuna fedha kwa kwenda kuchukua ofisini kwao, kwa nini wateja wasiwekewe kwenye account zao? hapa kuna kasoro wanakwepa nini? wanakwepa mahesabu yao yasionekane bank?

    Mwisho kabisa sidhani kama ni busara serikali kwa kupitia JK na Waziri Mkuu (kama wenyewe walivyowaomba), wawasaidie kurekebisha mfumo wa uendeshaji biashara yao, na wala sio kufungiwa.Hapa hamna swala la kurekebisha au kurasimisha, hapa swala ni kuivunja na wananchi walipwe fedha zao that is it, Pia waanzilishi washitakiwe kwa mujibu wa sheria zilizopo. Mfumo wa biashara ni wa kipiramidi huwezi kurekebisha chochote, labda kama watatuzibitishia mfumo wa uendeshaji sio wa kipiramidi hapo Serikali kwa kutumia wataalamu wake inaweza kuangalia mfumo bora jinsi ya kuendesha shughuli zao.




    Na, B. Kimbache
    Kilwa Kipatimu
    benedictkimbache@yahoo.co.tz

    ReplyDelete
  5. Jamani!?

    i)Tangazo la DECI limetolewa na nani na wapi?

    Nukuu toka kwenye link aliyotuwekea Michuzi:

    "Kwa mujibu wa tangazo la kampuni hiyo lililotolewa jana katika vyombo mbalimbali vya habari, Deci ilieleza sasa ndiyo inafanya jitihada za kusajili shughuli zake ziendane na sheria zilizopo." HabariLeo, Gwiji la Habari Tanzania. Jumamosi Aprili 11, 2009.


    ii)Huyo au hao "MENEJIMENTI" waliotoa tangazo hili kwa niaba ya DECI ni pepo, mapepo, mtu au watu?

    Nukuu nyingine:

    “Menejimenti ya Deci inapenda kutoa taarifa kwa wateja wake kuwa kampuni inachukua jitihada zote muhimu kuziweka shughuli zake kwa mujibu wa taratibu, ziendane na sheria na taratibu zilizoko,” lilieleza tangazo hilo.
    HabariLeo, Gwiji la Habari Tanzania. Jumamosi Aprili 11, 2009.

    iii)Kama ni mtu au watu majina yao ni kina nani? Na wana wadhifa gani katika DECI?

    Wakati mwingine kwa habari kama hizi hata ukijitahidi vipi kufumba fahamu na domo lako unashindwa.

    ReplyDelete
  6. Jamani hivi hawa viongozi wa kanisa wanaoitetea DECI mbona wanakwenda kinyume na maandiko. Na kwa kufanya hivyo wanawapotosha wakristo wengi. Lakini na wao wakristo wanapotaka serikali iwasaidie kuilinda DECI ni kisingizio tu. Serikali inawasaidia kwa kuwahamasisha waanzishe SACCOS. Michezo kama hiyo ya kupanda na kuvuna kwa haraka haiendani hata kidogo na kanuni ya maisha. Yote kwa sababu watu wengi ni wanapenda short cut na raha na starehe. Enyi viongozi wa kanisa na waumini tubuni na someni maandiko.

    1 Tim 6: 10; ..shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha..ukiitamani hiyo utafarakana na imani na utajichoma kwa maumivu mengi.

    Waebrania 13;5; Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, SItakupungukia kabisa wala sitakuacha kabisa.

    Methali 13:11; Mali ilyopatikana kwa haraka itapunguka, bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa

    Mhubiri 5:10;Apendaye fedha hatashiba fedha wala apendaye wingi hatashiba nyongeza

    Inatia uchungu kuona Watanzania ni wavivu wa kufikiri. Hawa maaskofu ambao hata elimu yao ya biblia inatia shaka ni mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo.

    ReplyDelete
  7. 1.Nafarijika sana kuona walio wengi kwenye globu yetu wana uelewa wa utapeli wa pyramid scheme kama DECI- ni wachache sana waliotetea DECi katika hii globu. 2.Nasikitishwa na kutoelewa kwa wananchi wenzetu wengi amabao baadhi wako tayari kupeleka pesa DECI mpaka leo.
    3.Cha kutisha zaidi ni ukimya wa serekali kwa miaka mitatu na kushindwa kwake kusitisha uharamu huu. Je ni kwa sababu enzi za Tibaigana kina mama wa wakubwa waliawaliza kina mama wenzao na na ponzi scheme kama hii wakashtakiwa na Tibaigana akaingilia kati kulizimisha swala hili kwa kusimamia waliolizwa kufidiwa badala ya kusaidia mashitaka mahakamani yafanikiwe? Au ni kwa sabau kwa mara nyingine tena kuna mikono wa wakubwa humu ndani ya DECI- nina wasi wasi kwa maanahivi karibuni gazeti moja la kila siku hapa TZ (Mtanzania Aprili 5) linalomilikiwa na mbunge mwenye tuhuma za ufisadi limediriki kutetea DECI?
    4.Natamani maelezo mengi yaliyotolewa katika hii globu yangeweza kuenezwa kwa njia ya radio kwa maana nadhani ni teknolojia amabayo walio wengi walioingia huu mkenge wanaimudu na ni njia nyepesi ya kufikisha taarifa haraka.
    5.Aidha wingi wa washiriki katika DECi imeonyesha udhaifu wa sera za fedha ya seriklai yetu kukidhi utashi wa karadha, mikopo kwa gharama wanayoweza kuimudu. Benki zetu zinatoa riba ndogo mno kwa wale wanaoweka pesa benki ukilinganisha na riba ya juu wanayotoza kwa wakopaji na serikali imekuwa inaliangalia hilo tu bila kufanaya lolote.Sana sana serikali kumekuwa na mahela ya Kikwete ambayo wajanja wamejikopesha wenyewe na walengwa kwa kiasi kikubwa wamekosa. Nadhani kazi ya serikali ingekuwa rahisi zaidi kama ingeingilia na kupanga toafauti ya riba ya amana (deposit) na kukopa isiwe kubwa mno, kwa njia hiyo wengi zaidi wangeweza kumudu kukopa kutoka vianzo vya fedha halali na rasmi na ingekuwa vigumu zaidi kwa matapeli kuingia soko la fedha.
    6. Mwisho inatisha zaidi kwamba viongozi wa kiroho wanadiriki kutetea utapeli. Mungu kweli atusaidie nchi hii!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...