mtafiti na mhadhiri katika chuo kikuu cha south bank university 
cha london dk. hilderblad shayo aongea na globu ya jamii
 juu ya maswala mbalimbali ya kimaendeleo
 alipokuwa bongo kwa vekesheni pamoja na kazi ya 
kuendesha warsha kwa wajasiriamali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. Kisamvu kibichi.April 30, 2009

    Michuzi huyo MCHAGA anasema tu!kama ni mtu wa kurudi kwa NINI asirudi SASA nyumbani?????mwambie arudi kwao KISHUMUNDU ndio tutamuelewa!!!ukweli Mkuu wa NANIHI ""HATURUDI NG'OOO NYUMBANI!!!""HA!HA!habari ndio HIYO!!!HA!HA!

    ReplyDelete
  2. dokta peekee anayasema, wengine wako kimya utafikiri hawakusoma, hawipendi tz nini?

    ReplyDelete
  3. Wapiga KuraApril 30, 2009

    Hawa vijana Hususan

    John Mashaka
    Dr. Shayo
    January Makamba
    Ridhwani Kikwete

    Hii ni timu ya 2015, subirini. Hapa kuna jambo, na ni jambo la nguvu. Vijana Big up mie kura nawalatea, CCM Hoyeeee

    ReplyDelete
  4. good luck kwa mnaorudi, mkiweza kutokomeza rushwa na ufisadi let me know and I will catch the next flight to join you

    ReplyDelete
  5. baada ya ccm kulemewa na ufisadi, imewakimbilia Hawa vijana safi John Mashaka na kundi lake ili kujipanga kwa ajili ya 2015. Safari kati ya London new-York za Hawa vijana zimekuwa nyingi mno.Dr Slaa mjitayarishe kwa maana hii timu ya mashaka, shayo na January siyo mchezo hapa kuna vichwa

    ReplyDelete
  6. mhh jmk, jmk,wanasiasa bwana.

    ReplyDelete
  7. Huyu ana mpango wa kugombea ubunge jimbo gani?. Maana nimesikia "Chini ya uongozi wa Jakaya" zikiwa nyingi sana kwenye mahojiano, sound like a politician enh!, Ila una mawazo mazuri lakini ounguza politics kwenye kuyawakilisha.

    ReplyDelete
  8. Nimeipenda (interview). Huyu jamaa ana akili. Yuko deep. Na ana moyo. Hadi ananipa tumaini na moyo wa kurudi bongo kuanzisha mradi or something.. just to test the waters. Ni kweli kuwa Tanzania ni pazuri! Na pesa huko ndiko hasa iliko (hasa katika hiki kipindi cha recession huku Ulaya na US), it's just a matter of deciding (whether to go back and officially start your business or not).

    Asante mdau Dr Shayo. Lucky enough niko na wewe huku UK so I know how i can reach you.

    Kuhusu bwana Mashaka, sijamjua vizuri kwakweli kama yuko genuine or not. It's so ironic (and amazing infact) for the fact that I've been following all these debates between the 2 (Mashaka & Shayo), and i have watched all those Michuzi and Mashaka interviews, but till today, I haven't quite made my decision on Mashaka's authenticity. But I have only watched ONE Dr. Shayo's interview and I know what he is about and I was able to so easily connect with what he had to say!

    It's amazing!

    Well done Doctor.

    Mdau UK - representing Rock City.

    ReplyDelete
  9. naomba nimsifu dk. shayo kitu kimoja, ana moyo wa kujitangaza.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2009

    John Mashaka, Dr Shayo is the only bridge we have to see a different face of Tanzania.

    Vijana hawa wawili tuwaombeeni Mungu, Muda siyo mrefu watakuwa watu ambao historia itatuonyesha kwamba ni mibaraka toka kwa Mwenyezi Mungu

    Kila la kheri vijana wetu, Ibadilishaneni sura ya Africa

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 01, 2009

    swali langu ni hivi, hizi ndo kampeni zetnu? hii ni kwa sababu mashaka ameshachaguliwa kuwa rais 2015 kabla hajapigiwa kura. unaona wabongo tulivyo wajambo? Mashaka anaandika ground breaking articles ili kuturubuni na kujenga fan base ambayo sasa hivi ikekuwa kubwa mno, shayo naye ni yale ya mashaka
    kijana wetu ushauri mzuri tena wa kisomi. mungu na akulinde urudi kulijenga taifa letu. Nakuona na mwanaharakati J Mashaka kuwa ni vijana makini sana. Tunaomba huyu ridhwani naye aletwe ajumuike na wakina shayo akishindwa hawe mbali na safu yetu ya 2015

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2009

    comment please????

    Michuzi, wewe utapewa cheo gani?

    Ukuu wa wilaya Yombo vituka au Waziri wa habari?

    naona nawe humo kujitatayarishia 2015 !!!!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2009

    Dr Shayo kwa Publicity STUNT haujambo. Wewe na Mwanaharakati Yohanna Mashaka kama viongozi wa kesho, basi Tanzania itatangazwa kweli duniani

    Wewe Na Genius Yohanna Mashaka, nawavulia kofia, sasa kama mnafanya kila kazi wenyewe?

    Mkuu wa Wilaya Nanihii....
    Waziri wa Habari mtarajiwa 2015 atafanya kazi gani?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2009

    Waosha vinywa mnaniua, sasa ngoja na mimi niwaletee safu yangu ya uongozi 2015:=

    Rais Jonh Yohanna Mashaka
    Makamu January Makamba
    W-Mkuu Dr. Hildebrand shayo
    W-Habari Issa M. Michuzi
    M-Wilaya Nanii. Issa M Michuzi
    Balozi Issa M Michuzi

    ReplyDelete
  15. Sumaye (H-Town)May 01, 2009

    kama haya ndo mambo, mimi pia naenda kugombea urais. Shayo ameanza naye yale ya Joni Mashaka???? 2015 bado mbali wakuu. tulizeni bolli

    hii dunia imeharibika, watoto wa matajiri ndio wanaopewa super education, alafu wanakuwa super genius. angalia mashaka, angalia shayo, anagalia january.

    sisi watoto wa wala vumbi tutakaa siku zote kuota ndoto wakati wengine walishachaguliwa hata kabla kikwete hajamaliza muhula wa pili????

    mimi naacha kubeba boxi narudi kugombea urais na kikwete 2010 potelea mbali, mie nakuja bana baba yangu amelipa sana kodi tanzania

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 01, 2009

    Jifunze kusema Nchi,wacha mambo ya mgombani Nji Nji.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 01, 2009

    UBOVU WA WASOMI WA KITANZANIA NI KWAMBA WANAMUABUDU JOHN MASHAKA MNO. KWANI YEYE NDO KIPIMO CHA WATU WENYE AKILI TANZANIA NZIMA, MAN PULIZZZZ

    HATA SISI TUNABEBA BOXI NA TUMESOMA. BABA YANGU ANGEKUWA TAJIRI NA MIMI LEO NINGEKUWA WALL-STREET

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 01, 2009

    Baadhi ya mawazo ya kijana Dr Shayo ni ya msingi, na kama angeyafungia tu katika mipaka ya kitaalamu yangeweza kueleweka vizuri zaidi kuliko kuingiza siasa uchwara (zidumu fikra za mweyenkiti). Pili, na ni kwa bahati mbaya sana, inaelekea huyu kijana anaijua Tanzania moja tu (ya akina Ridhiwani Kikwete). Zipo Tanzania nyingi tu. Kama angekuwa makini, hata katika mahojiano mafupi kama haya angeweza kutuonyesha kuwa anafahamu sura mbalimbali za tanzania, lakini atajikita na hiyo ya akina RK!!
    Ni vizuri anapanga kurejea bongo, na nina uhakika baada ya mwaka mmoja ataweza kutoa maoni muafaka yanayoakisi bongo.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 01, 2009

    DR SHAYO YOUR SO HANDSOME JAMANI KUZIDI HATA HUYO CELEBRITY WANNA BE .............. GO SHAYO WEWE NDIO UWE RAIS. GO SHAYO GOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 01, 2009

    Nanukuu... "Chini ya uongozi thabiti wa rais Jakaya Mrisho Kikwete ameweka bayana misingi yote ya kuendelea, hamna nafasi ya sisi kukaa tukaanza kusema kuilaumu serikali' kila kitu kipo wazi ni namna gani ya mtu wewe binafsi unajituma"

    Ingratiating oneself to the powers? be wary of a sycophant..., they are always up to no good.

    Asante sana Dk Hilbrendad Shayo

    na akaendelea... "Ukiwa umerudi hapa kwa nguvu zako kwa nia yako, nafasi ziko na kwa kweli hapa nyumbani pesa ipo bwana"

    With the population of 39 million people on the land, a country's GDP of $54 billions; Tanzania is at the bottom 10% of the world's economies in terms of per capita income. Yet a Tanzanian "scholar" confidently says "hapa nyumbani pesa ipo bwana".

    Ukweli ni kwamba, Hapa nyumbani pesa hakuna bwana, ingawa kuna wachapakazi hodari wachache wenye pesa, na wezi wengi sana wenye pesa.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 01, 2009

    sHAYO hERI WEWE NA mESIAH mASHAKA, sASA rIDWHANI ANAINGIAJE hUMU, AMEFANYA NINI tANZANIA? aU KWA sABABU NI MTOT WA rAIS??

    ReplyDelete
  22. Ng'ondoleMay 01, 2009

    Dr. Shayo asante kwa kutithibitishia kwamba wewe nifisadi mtarajiwa.

    Naona umetumia fursa hii kujikomba kwa Mkuu wa nchi na mwanae.

    Pia nina mashaka hiyo tenda ya Wizara ya Viwanda umeipata kupitia mgongo ya huyo bwana Rizwani.

    Itakuwa vema ukitubandikia hiyo research yako ili tuone substance, maana kuchomekea "demand and supply" kila mchumi hufanya hivyo. Ndio keywords za usomi katika fani ya Uchumi.

    Show us the money.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 01, 2009

    ukiashachanganya politics na academics unapata tabu, choose one, drop one. 'ooh chini ya uongozi wa JK'

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 01, 2009

    Anon wa May 01, 2009 1:06 PM

    Mbona unaongea pumba rafiki yangu?

    Kwani hao wawili uliowataja wameifanyianini Tanzania?

    Au kuja kuuza sura hapa na kuandika articles ndio mchango kwa taifa?

    Na je unamjua huyo Rizwani anafanya nini?

    Subiri basi na yeye wakati wake wa kuuza sura ukifika atakwambia kafanya nini.

    ReplyDelete
  25. Kimaro (MP) moshi vijijiniMay 01, 2009

    hi, inapendeza kuona vijana wa kitanzania kuwa na moyo wa kuridi nyumbani.

    Ukweli dr shayo ni kuwa ukirudi kwa kupenda bila kulazimishwa, maisha bongo ni mazuri tu. Ila lazima mtu akubali kuwa kuna kitu kinaitwa "transition period"

    Nimekuwa nikifuatilia sana debate ya hawa jamaa, kweli sasa ninaamini kuna kitu ndani ya hawa jamaa.
    Mtizamo wa dr shayo ni mwanzo tu, na ninaamini kuwa wapo vijana wengi tu ila wanaogopa kujitokeza.

    Ushauri kwa Dr. Shayo, utakapokuwa Tanzania, usichanganye siasa na profession yako.

    hii ndiyo njia pekee itakayokupa wewe nafasi ya kutimiza kile ambacho umekianza.

    Nilipitia kwa undani sana utafiti wako uliofanya, na nimeridhika na mtizamo wenu.

    Tatizo ni kuwa yale mliyoshauri yatafanyiwa kazi?

    ila kwa kweli ninafurahishwa na namna uliyoweka bayana mambo fulani fulani.

    Hongera Shayo safari bado ni ndefu lakini tutafika tuuuuuuuuu.

    Wanaochangia ati unajiuza na kujipigia debe ninaswali moja kwao wao wametoa mchango gani?

    ReplyDelete
  26. Peter MwakatobeMay 01, 2009

    Du, ama kweli nimeamini sasa vijana wameamua. Chngamoto hii ya dr. shayo ni nzuri.

    Ila wasi wasi wangu ni kuwa ukifika bongo ndugu yangu usijikite kwenye mambo ya siasa.
    Wewe fanya kazi
    Nafikiri ukifika tu hutapata shida ya kazi.

    Kwa mtizamo wangu utakuwa "hot cake"

    Ila ombi usiingie kwenye siasa mdogo wangu. Hata ukisahuriwa kupewa kanafasi ka kuingia kwenye mbio za ubunge usijikite huko

    Nafikiri huu ni ushauri mzuri tu ninakupa kama mtu ambaye nimeona vijana wa namna yako wakiwa wanaishia kwenye majukwaa na michango yao kutokutambuliwa.

    Hongera kijana kwa ujasiri wako
    kusoma kwako ndani na nje ya nchi ni manufaa kwa taifa la tanzania

    Mungu akubariki
    mungu aibariki tanzania

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 01, 2009

    HABARI BWANA MICHUZI,

    ---HUU SI USENENE, BALI NI UKWELI----

    TUNAFAHAMU KUWA HUWA UNACHUJA COMMENTS ZA WADAU...SASA ILE COMMENT YA MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI ZA MUAJIRI WAKO (TSN) NA WALIPA KODI NAONA UMEAMUA KUINANA..MAWAZIRI NA WATENDAJI WENGINE WA SERIKALI WAKITUMIA MAGARI NA RASILIMALI NYINGINE ZA UMMA, NYIE WANA HABARI NDIYO WA KWANZA KUPIGA KELELE WAKATI NYIE HIZO KAMERA NA VITENDEA KAZI VINGINE MNA JINUFAISHA NAVYO...

    USHAURI WA BURE.....TOA KABISA HII POST HAPA AU LA BARUA YA WAZI INATAYARISHWA KWENDA KWA WAZIRI WA HABARI WAKUCHUNGUZE KWA MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI ZA NCHI KWA KUJINUFAISHA KIBINAFSI....HAPA KWENYE BLOG UNA WADHAMINI WANAOKULIPA KUWEKA MATANGAZO YAO, WOTE HAO PAMOJA NA WEWE MNAWEZA KUPITIWA NA MKONDO WA SHERIA...

    TOA HII VIDEO NA ZINGINE ZILIZOPITA (MALI YA TSN) HARAKA IWEZEKANAVYO...

    ASANTE

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 01, 2009

    BWANA MICHUZI na DR SHAYO:

    Jamani hiyo ripoti kwani ni Siri?! Au tunahitaji kutoa fwedha ili tuione? Kama kweli hii ripoti ipo tuisome basi, tuwekeeni hapa katika mambo ya uwazi ili tuisome tufaidike jamani.
    Au mnabania tu na mnakaa kujitangaza kisiasa??!!

    Mazungumzo ya Dakika Saba nzima DR Shayo hakuweza hata kutoa mfano mmoja kutoka Ripoti yake hiyo ila kamtaja JMK mara zaidi ya Tano hadi mtoto sasa sijui hayo ndio majumuisho ya ripoti ama vipi?!

    Kwa kweli ili umsifie mtu inabidi uone kazi yake sasa hapa sijui kwa nini tunamsifia mtu... Watanzania tuwe macho jamani tutabaki hivi hivi kusifia bila kujua..watu wanakula vya kwao.

    Shauri yenu, Mmeshaambiwa "Kuweni Macho"

    Eee Mola utuepushe na wajanja!
    Mzawa

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 01, 2009

    Naomba watanzania hasa sisi tujiitao wasomi tuwe makini katika yale tusemayo. Tukidiriki kumpa mtu sifa au changamoto, basi tuwe wazi ili tumsaidia mlengwa. Sijaona usomi wa Dr. Shayo kama ajulikanavyo ktk kutatua matatizo ya uchumi Tza. Kuna wasomi wengi TZA na ambao ni very effective. Waswahili wasema, "chema chajiuza na kibaya chajitembeza." Namuonea huruma Shayo kwani wasifa apewao hapa ktk blog ni kama mabezo kwa makala aandikazo, zenye mtiririko hafifu, lugha ya kubabaisha, na kujitangaza kama mtaalamu wa uchumi kutoka South Bank Univ. Tukiwa UK, USA, au popote, tujue tumetoka wapi.There are a lot of clever people back home, they are venerable in what they are doing, and we have to be grateful for their contribution in keeping up with hard times in Bongo.I don't believe that Dr. Shayo is aware of his weaknesses in public and economic affairs. Uplifting Kikwete in his interview, shows how naive he is with regard to the current economic and political situation in Tanzania. JK is doing fine, but you don't have to mention his name repeatedly when you are making your economic or political strategies in Tanzania. At any rate, we are born different and our differences make us what we are. Dr. Shayo can deliver something to us, but he should do that with caution because not everything he says makes sense. "Tanzania kuna pesa bwana" that can be true, but it can also be rubbish with the proportion of Tanzanians who earn less than a dollar a day. Good luck Dr. Shayo, but remember a latin adage, 'Nemo dat quod non habet' (you cannot give what you don't have). Rgds, Mlahabwa, UK

    ReplyDelete
  30. Hata kama ugenini ni kuzuri lakini nyumbani ZAIDI.
    Nyumbani ni nyumbani hata kama kichakani.
    Haya mambo ya kutoamini mazuri yanayotokea ama .
    yatatokea nyumbani kwetu Tanzania ni ya kizushi.
    Maneno ya shayo ni mazuri!!
    Kitakachotuinuwa watanzania ni kilimo bora,Ubunifu wa hali ya juu.pendo wa dhati kati yetu ambao utaleta imani.
    K MMBANDO

    ReplyDelete
  31. Mlokole wa UKMay 01, 2009

    Dr. Shayo.
    I concur with most of your opinions about investment opportunities. One thing, though: dual nationality. Why bring up the ramifications of prosecuting someone with dual nationality? You can sue me if I have broken the law. Whether as a British or Tanzania is immaterial.
    I cannot wait to hear your objections to dual nationality for Tanzanians. Other nations existed without such anxieties of nationalities.

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 01, 2009

    Learning has not liberated a man if all he learns to want is a certificate [page 29] on his wall, and the reputation of being a ‘learned person’— a possessor of knowledge. For such a desire is merely another aspect of the disease of the acquisitive society - the accumulation of goods for the sake of accumulating then. The accumulation of knowledge or, worse still, the accumulation of pieces of paper which represent a kind of legal tender for such knowledge, has nothing to do with development.

    Mdau
    USA-1

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 02, 2009

    Loooooh mthomi dk shayo, ukivunja sheria popote utashitakiwa kwa sheria za mahala pale "rules of the land". na kama kuna makubaliano ya mshitakiwa kuhamishwa "extadition" hii itategemea makubaliano ya serikali husika, kwa hiyo kukwepa/kutokuweza kwako kujibu swali inaonyesha kwamba huna "substance"

    Maoni yangu binafsi kuhusu uraia wa nchi mbili ni kwamba, ni chini ya asilimia mbili ya watanzania wanaoweza kupata uraia wa nchi za magharibi, na karibu asilimia zote za wa-magharibi wataweza kuupata uraia wa Tanzania kama wakiutaka. Mtanzania wa kawaida wa Chamwino au Bagambaakabo hatofaidika na hili, ingawa kina Chenge wachache watafaidika sana.
    Uraia wa nchi mbili utasababisha "trillions of loop holes" to be exploited by wazungu, kiuchumi, kiulinzi na usalama, na hata kiutamaduni. Mtanzania mwenye uraia wa marekani hana faida yoyote zaidi ya wepesi wa kusafiri duniani na kufanya biashara, lakini m-marekani mwenye uraia wa tanzania atakuja kuwa rais wetu baada ya vizazi vichache sana, na hasa ukizingatia sisi tunaabudu wazungu, wahindi na waarabu.
    Mawazo yangu ni kwamba, kwa manufaa ya watu wachache (chini ya 2%) yasitufanye tukaiweka nchi yote katika hatari ya kuporwa. Kumbukeni, sisi bado ni taifa changa sana (we are not an established nation yet) kwa hiyo sidhani kama kuruhusu mianya kama hii ni kitu kizuri kwa muda.

    This is just my opinion and everybody has got their own, I suppose.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 02, 2009

    MICHUZI NA HUYU SHAYO KWANI SINGLE???MIE NIMEMPENDA....

    NITAJIKOMBA MPK NIMPATE...SI UNANIONA EEEEEH???WEWE NDIO SHAHIDI WANGU...MIE NDIO WA KWANZA KUMFATA....BASI BAADAE WATU WATAANZA WENYEWE NDIO WA KWANZA...AAAAAAAAAAAAAGHHHH

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 02, 2009

    mbona hutoi comment za watu,nimekua nikiandika comments lakini unanibania,wewee michuzi blog yako inapokea comments za kuwasifia magaidi na mafisadi.
    FISADI MKUBWA,wewe ni Papa namba 6,na Shayo ni Papa namba 7.
    Wizi mtupu,msomi gani anasifia uozo.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 02, 2009

    Michuzi naona maoni yangu umeamua kuayachikichia!!! Democrasia ni pale watu wanapokuwa na uhuru wa kutoa maoni bila uoga ili mradi hawavunjii wengine haki zao.
    Maoni yangu kuhusu shayo ni kuwa, Yeye ameamua kutafuta cheap popularity. anayoyasema ni hadithi za abunuasi, means hayatekelezeki. Angekuwa amesomea biashara angejua tatizo liko wapi kwa wafanyabiashara wetu kufanya hizo biashara za mboga ulaya!! Ametumia methodology gani yakinifu katika kuanisha na kung'a mua yote aliyoyasema? Ametmimia theories na amabzo zinakubalika ulaya lakni hapa Tanzania the same theories hazifiki mbali. Mwisho clip ni fupi amesema amekupa dose nzima iweke hapa ili tuichambue vizuri.
    Nyongeza ya mwisho mbona misifa kibao kwa kikwete? je emeoniesha ni faida gani tutazipata baada miaka ya mbeleni ambazo ni jitihada za kikwete na sio mfumo mzima wa biashara Duniani kubadilika?? Je Huyo mtoto wa kikwete ndiye mpiga debe wake kwa baba yake??
    Amevamia anga za watu. Kuwa Southbank siyo tija.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 02, 2009

    na mimi pia nanukuu... "kwa kweli watu wa viwanda na biashara wameridhishwa na utafiti tuliofanya, na kuna nafasi nyingi sana za biashara wa za opportunities"

    wadau nitafsirieni hii "kuna nafasi nyingi sana za biashara za opportunities"

    ReplyDelete
  38. Christina KilangoMay 02, 2009

    ndugu wadau
    mnaotaka report za huu utafiti swali langu ni kuwa mtazisoma?
    Zipo report nne
    ya kwanza page 250
    ya pili page 96
    ya tatu page 79
    ya nne page 144

    kifupisho cha report hizo ziko katika gazeti la the guardian la 26/04/09 ukurasa wa 24 na 25

    kazi kwenu, jamani mchango wa Dr. shayo ni changamoto.

    hivi wabongo mnataka mpewe nini mridhike? aliposema kuna opportunity za biashara ni kuwa uwezo wa kuuza nje ya nchi bidhaa za kitanzania upo sasa sijui wadau wa blog hii mnataka mpewe nini?

    mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi duniani ni changamoto kwa wafanyibiashara wa kibongo kuchangamkia biashara, na tusilaumu tuuuuuuuuuuu bila sababu

    Dr. shayo mimi binafsi ninakupongeza kwa jitihada zako. wapo watu wasiopenda maendeleo yako na jitihada zako. songa mbele mwanangu jitihada na juhudi zako zitaonekana siku moja.

    hao wanaokuambia eti unatafuta popularity, wao wamefanya nini? Angalau wewe na huyu mashaka mmekuwa mkitoa changamoto hata kama ni nadharia.

    huyu aliyechangia kuwa unasifia uozo anashindwa kuelewa kuwa kila pahali hapa duniani kuna wachache ambao siku zote wanataka kuvuruga mambo, ina maana alitaka wewe useme nini?

    shayo katoa hadithi za abunuasi, wewe umetoa nini?

    Tuweni watu wa kudhamini michango na juhudi za mtu.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 02, 2009

    wewe christina kilango namna gani wewe? yaani wewe umeona kusoma kurasa 250 ni kazi kubwa sana? Watu wanatak kuona "substance" katika kilichoandikwa. Shayo mpaka hapo hajatoa mchango wowote, na watu wanafanya biashara kati ya uingereza na tanzanaia miaka nenda miaka rudi, na kama kuna "opportunity" yoyote mpya ambaya ameigundua aiweke kwenye huo utafiti wake na atuonyeshe hapa. Mpaka hivi sasa kitu kipya hapo ambacho watanzania walikuwa hawakijui ni hizo "nafasi za biashara za opportunities"

    Ebo! Muda wa kuja hapa na "superficial knowledge" kisha kujifanya kujua mambo umeshapita na watanzania wa leo wana uwezo wa kuchanganua mambo. Utafiti kukubaliwa na wizara ya viwanda na biashara haitoshi kwetu sisi kwani hata ununuzi wa "rada" kanjanja za Chenge, Kikwete, Mkapa,na Sumaye pia ulifanyiwa utafiti na utafiti wake ulipitishwa na wizara za ulinzi na mawasiliano. Lakini angalia jinsi "rada" zilivyotutia hasara.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 02, 2009

    Ndugu wadau, lazima kuwepo na pande zenye maoni tofauti pale watu wanapochangia hoja ambazo zina manufaa au zaweza kuleta matatizo katika jamii. Kuwa critical kwa Dr. Shayo ni kitu chema na lazima kiwepo kwani TZA ya leo sio sehemu ya kuongea kitu ukadhani kitapokelewa ki-imla. We need critical realism or any approach that will help us to discern substance, kama alivyoongea mchangiaji mmoja. Siasa ya leo lazima iondokane na kasumba ya kumpigia mtu kura au kumuunga mkono kwa sababu ana sura mzuri au anatoka kijijini kwetu, kama mdau mmoja anayemnadi Dk.Shayo. Alichoona kwa Shayo ni kwamba ni handsome na labda single kwa hiyo anaweza amfae. Huo ni mchango na mtazamo wake, wengi tunamshangaa hata hivyo, kwani we are discussing issues that may impact public interest and not individual whims. We need to go through the report before we make any judgments, at the same time, I am trying to google Dr. Shayo, but to my surprise, he doesn't seem to be anywhere in academic journals in his area of interest. Mjomba, umepublish wapi? Kama ulikuwa unafundisha UDSM, unaanza kufanya niwe na mashaka na kile kitolewacho pale Mlimani, na kama hapo South Bank Univ. una darasa, lazima kuwauliza wameona nini kwako. It is possible that you are still offering tutorials to undergraduates, which is not nothing. On the other hand, if you really want to be somebody in politics or government in Tanzania, you better brace yourself in many ways. You have a long way to go if this is your desire, because TZA ni ya wasomi na sio mbumbumbu kama zamani. So much so, I don't disapprove your efforts in research, what I want to know is the extent your research answers what you are keen to establish in your research. It is possible that your cohort and you at SBU have discovered something of interest, please, post the links here, don't refer us to Mzalendo or Majira where we will read a summary of your eulogy rather than academic and practical implications of your research. Yule mdau asemaye report ina page 500 au zaidi, asikonde, kwanza kama report ina page nyingi kiasi hicho ni dalili ya kwanza kwamba ina hitilafu. Hiyo sio report tena, we need an executive report, something suitable for carrying out plans as he is desirous to do. Ndugu amka hapo ulipo! Mlahabwa, UK

    ReplyDelete
  41. Asha KiwiaMay 02, 2009

    Hi
    wadau
    acheni kuweka malalamiko humu.
    nilikuwa na bahati ya kukutana mdau mmoja akanionyesha summary that seem to be OK.

    Cha kushangaza ni kuwa mtu akitoa maoni mnasema ni mwanasiasa, jamani uanasiasa unatoka wapi hapa? Acheni kutoa misimamo isiyokuwa na manufaa kwa jamii

    Ninamshangaa huyu mtu anajiita christina Kilango hizo page kazitoa wapi, kwani that is not true.
    Hii inaonyesha wazi ni kwa kiasi gani watu wanakurupuka na kuchangia vitu vya kupotosha kwenye hii blog

    Jamani angalieni, mtabakia mkisema huyu "siye mtoto wa yule seremala"?

    Kazi kwenu

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 03, 2009

    Nafikiri uraia wa nchi mbili tusiuharakishe kwa sasa. Tukiukubali kichwa kichwa wakenya wote watakimbilia bongo na kutwaa ardhi chap chap.
    Tuangalieni mbali zaidi au tusubiri na kuendelea kutafakuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...