Na Ripota wa Globu ya Jamii, Helsinki
Timu za Watanzania za FC BONGO ya Finland na KILIMANJARO ya Sweden zitachuana rasmi siku ya Jumamosi tarehe 27.6.2009 katika viwanja vya Finnair Stadium Helsinki Finland.
Timu hizo ambazo zilichuana kwa mara ya kwanza mwaka jana huko Stockholm na Kilimanjaro wakabahatika kuwafunga Fc Bongo mabao 4-3 kwa taaabu.
Inasemekana kuwa Fc Bongo walichukiwa sana na
uamuzi wa refa kuwapa bao la nne vijana wa kilimanjaro kwa mpira ambao ulikua ushatoka nje, pia baada ya mpira kuisha wakapewa pilau dume bila ya nyama kiasi hata wageni wengine walikwamwa na pilau kavu na kupata huduma ya kwanza.
Habari kutoka Helsinki zinasema kuwa Vijana wa Fc Bongo wanajinoa vibaya sana ili kulipizia kisasi watani wao hao wa jadi kutoka nchi ya jirani. Habari zaidi zinadatisha kwamba safari hii benchi lao la ufundi litaongezewa nguvu na kibabu kimoja kutoka Lamu, nchini Kenya, ambacho kinawasili usiku huu.
Kocha na Mlezi wa Fc Bongo Abdalla Ezza (hahaha sasa anaitwa Hiddink) ameahidi kuwapa fundisho kubwa la kandanda kwa wageni wake hao wa Kilimanjaro, anaamini kikosi kilichoenda stockholm mwaka jana kilikua hakijatimia kwani wachezaji wake (Key Players) wengi hakuweza kusafiri nao kwani walikua ndio kwanza wamerudi makazini kutoka kwenye likizo zao za summer na hawakuweza kupata ruhusa makazini.
Nao Kilimanjaro wakizidi kujiamini kuwa wataweza kuwanyamazisha wenyeji wao huko Helsinki. Ripota wa Stockholm ameshuhudia timu hiyo ikijifua kisawasaw na kocha wa timu anayochezea Mohamed Athumani Machupa.
Habari zaidi kuhusu mechi hiyo tembelea website ya kilimanjaro hapa http://fckilimanjaro.snabber.se/
Kiama chao kinawasubiri hao Kilimanjaro, Watakoma ubishi mwaka huu, na biriyani ya mbuzi tutawalisha.
ReplyDeleteMmechi mbona mwezi wa sita na umeandika jumamosi hii?
ReplyDeleteWalete hao kilmanjaro tuwatoe hangover za botini
ReplyDelete